Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia,January Makamba amesema kuwa taasisi za dini hapa chini zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na kuisaidia serikali kwa kutoa ufadhili mbalimbali wa elimu kwa jamii yenye uhitaji pamoja na kuhubili amani.
Makamba aliyasema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za kidini na utamaduni zinazoadhimishwa kila mwaka na dhehebu la dini ya wahindu wa jamii ya kilala kutoka jimbo la kusini nchini India,ambao wanaasili ya kiasia waishio hapa nchini, kwa kutoa shukrani wakati wa mavuno .
Alisema kuwa sherehe hiyo inamanufaa makubwa hapa nchini katika kuwaunganisha watanzania kiutamaduni ,kiimani na wenzao wanaotoka madhehebu ulimwenguni katika kudunisha amani,ambapo alieleza kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa taasisi za dini hapa nchini,itaendelea kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo kwenye vifaa mbali mbali vinavyokuwa na manufaa kwa wananchi ili kuweza kuwasogezea maendeleo.
Aidha alizihakikishia taasisi hizo kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ikiwa ni pamoja na kuheshimu imani ya kila dhehebu bila kuingilia na kuzitaka taasisi hizo kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani kupitia Nyanja mbalimbali .
Naye msemaji wa chama cha Arusha Meru Maalayelee Assiociation(AMMA),Prem Cheriam alisema kuwa AMMA imeanzishwa hapa nchini miaka 6 iliyopita ikiwa na lengo la kuwaunganisha waumini wa dini hiyo ya wahindu na wenzao waishio hapa nchini na nje ya nchi.
Alisema lengo la ni kumshukuru mungu kwa kutoa sehemu ya mavuno yao kwa kuisaidia jamii kama shukrani yao kwa mwenyezi mungu kwa kufoa sadaka na kwamba mwaka huu wameamua kusaidia katika Nyanja ya elimu kwa kufadhili wanafunzi 7 kusoma masomo ya kompyuta nje na ndani ya nchini.
Prem alisema kuwa mpango huo utawanufaisha zaidi wanafunzi wasio na uwezo ambao wanalelewa kwenye vituo vya watoto yatima na kwamba AMMA imeahidi kujenga bwawa moja kwenye shule moja wapo ya msingi katika jiji la Arusha litakalosaidia kuwaimarisha vijana kimichezo ya kuogelea .
Katika sherehe hizo watu mbalimbali walihudhuria wakiwemo wabunge wa Mikoa ya Arusha na Manyara na viongozi wa ngazi mbali mbali serikalini pamoja na wenzao wa jamii hiyo kutoka mataifa mbalimbali na kwamba sherehe hizo zilipambwa na kunakshiwa na vikundi mbalimbali vya utamaduni na sanaa kutoka Nchi ya India .





