TWANGA YAREJEA TOKA ZIARANI IRINGA NA MBEYA.

Wakali wa Muziki wa Dansi wa  hapa Bongo African Stars “Twanga Pepeta” imerejea jijini Dar es salaam mara baada ya kumaliizika kwa ziara ya maonyesho katika mikoa ya Iringa na Mbeya.

Ziara hiyo ilikuwa ni ya siku tatu kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 14-09-2012, Jumamosi tarehe 15-09-2012 na Jumapili 16-09-2012 ambayo ilisababisha Bendi kutokufanya maonyesho katika siku hizo kama ilivyokuwa kawaida ya Twanga Pepeta.

Wiki hii Twanga Pepeta itaendelea kukonga nyoyo za mashabiki  wake kama kawaida katika kumbi za Club Billicanas siku ya Jumatano, Alhamis watakuwa New Club Maisha Oysterbay, Ijumaa watakuwa  Free Time Resort Ukonga, Jumamosi watakuwa Mango Garden Kinondoni na Jumapili watamalizia kwa onyesho la mchana Leaders Club Kinondoni na usiku watakuwa Mzalendo Club Millenium Tower.

Pia kwa wiki hii Bendi inataraji kuitambulisha nyimbo mpya ya Badi Bakule inayoenda kwa jina la “Mwenda Pole Hajikwai”  ambayo itakuwa ni nyimbo mpya ya SITA ya Twanga Pepeta mara baada ya kuzindua albamu ya 11 ya DUNIA DARAJA.

 Nyimbo nyingine mpya  ni “Shamba la Twanga”  iliyotungwa na Grayson Semsekwa,” Walimwengu hawana jema” uliotungwa na Jumanne Said au J4 lapova, “Mapambano ya Kipato” iliyotungwa na Mwinjuma Muumini, “Ngumu Kumeza” ya Mirinda Nyeusi na “Nyumbani ni Nyumbani” iliyotungwa na Kalala Jr. 

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!