VIONGOZI WA CCM WATAKIWA KUSIMAMIA KERO ZA WANANCHI

                                                                                                                                                                                                            NA GLADNESS MUSHI

VIONGOZI mbali mbaliwa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya  kata
,vijiji na vitongoji   wametakiwa kushughulika na kero za wananchi na
kuhakikisha kuwa wanazitatua kwa muda muafaka ili wananchi wao waone
umuhimu wa chama na serikali .

Hayo yalisemwa  na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya arumeru Bw
Langaeli Akyoo alipokuwa akihutubia  wananchi  katika mkutano wa
hadhara wa chama cha mapinduzi uliofanyika kijiji cha ngyeku kata ya
kikatiti wilayani a rumeru.

Alisema kuwa kwa sasa ufike muda viongozi wasionekane kuwa wamepewa
uongozi kwa ajili ya kustarehe na badala yake wajikite zaidi katika
kusikiliza matatizo ya wananchi wao kwa kuwa uongozi wao ndio kimbilio
la wananchi  kwa kuhakikishwa wanawasikiliza yale wanyohitaji.

Alieleza kuwa ili wananchi waweze kukiamini chama  cha mapinduzi ni
vema viongozi hao wakadili na matatizo mbali mbali yaliyoko ndani ya
jamii husika hususan kuwatatulia kero ya  maji kwa kuwa viongozi hao
wao ndio suluhisho la wananchi .

Alifafanua kuwa kwa sasa hakuna tena haja ya kutafuta wa chawi
wanaosababisha ccm kuchukiwa  bali viongozi watambue kuwa wenyewe ndio
wasababishaji  kwa kuwa hawafuatilii ipasavyo kutatua kero
zinazowakabili wananchi wao

“Ninawaagiza madiwani , wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha
mnafuatilia  kero hizo ,tusitafute wachawi wanaosababisha CCM,
kuchukiwa wakati wachawi ni nyie wenyewe”alisema Akyoo.

Mbali na hayo akyoo akielezea mafanikio ya serikali ya ccm katika
kijiji hicho cha ngyeku alisema kuwa ni pamoja na kufanikiwa kujenga
shule ya sekondari ngeku,zahanati pamoja na barabara iliyotengenezwa
kwa mradi wa TASAF.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!