BAADHI ya wateja na wafanyakazi wa ofisi za jiji wilayani Ilala, afya zao ziko hatarini kupata maradhi ya mlipuko kutokana na choo cha hoteli iliyomo katika jengo hilo kufurika hadi kutiririsha kinyesi nje.
Wakizungumza na Fullshangweblog jijini Dar es Salaam jana, miongoni mwao walisema wanastaajabishwa na hali hiyo ya hatari ikiendelea kwa
zaidi ya miezi mitano bila kutafutiwa ufumbuzi.
Mmoja wa wateja hao, Khamisi Khalfan alisema kutokana na uchafu huo kukithiri na kuhatarisha afya zao baadhi yao wanatarajia kuacha kwenda kujipatia huduma katika hoteli hiyo.
Alisema tatizo hilo linafahamika hadi kwenye ofisi za wakubwa lakini inatia hofu kuwaona viongozi hao wakikaa kimya kama vile hawana taarifa za uchafu.
Akifafanua zaidi, alisema kuwa yeye ni mteja wa muda mrefu na amekuwa akifika mara kwa mara katika hoteli hiyo hivyo anauhakika na hayo anayoyazungumza.
Vilevile aliwashutumu waendeshaji wa hoteli hiyo, kwa kitendo chao cha kufanyabiashara katika mazingira machafu kama yale kitendo ambacho huenda kikawapunguzia wateja ambapo kuwapata tena itawawia vigumu baadaye.
“Unajua hiki choo tangu kuanza kufurika ilikuwa mwenzi wanne ambapo hata mkurugezi mwenyewe wa jiji alifika kujionea hali hiyo lakini hajachukua hatua”alisema khalfan.
Alisema Agosti mwaka huu, Mkurugenzi aliwahahidi waendashaji hoteli hiyo kuwa ofisi yake ingelifanyia kazi hara tatizo hilo lakini hadi leo bado halipatiwa ufumbuzi.
Alipoulizwa msemaji wa jiji kuhusu suala hilo, Makwembe, alisema niko kwenye ziara ila hebu waulize wenye hotel hiyo, mkataba wao unasemaje.
Naye kiongozi wa hotel ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alikiri kufurika kwa choo hicho, lakini hakuwa akijua mkataba unasemaje iwapo choo kingefurika nani angehusika kukifanyia usafi, zaidi alisema asubiriwe mkurugenzi wa hoteli hiyo.








