Mbelgiji Tom Saintfieti atimuliwa yanga kutokana na mwenendo mbaya wa timu

Saintfiet akisaini mkataba na Yanga Julai mwaka huu, kulia ni mwesigwa na kushoto ni Seif Ahmad ‘Magari’
………………………………………
KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mbelgiji Tom Saintefiet ameteua wachezaji 18 kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya JKT Ruvu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, safari hii akimchukua mshambuliaji Jerry Tegete na kumtema Said Bahanuzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Mbelgiji huyo alisema anaelekea kukatishwa tamaa na wachezaji wake hivi sasa juu ya viwango vyao.
Alisema hata kufunga penalti, hivi sasa imekuwa ni tatizo na mazoezini jana akiwajaribu kwa penalti wachezaji wake, kati ya mastaa wake sita, waliofunga ni wawili tu. “Yaani hata kesho siombei nipate penalti, maana sijui kama tutaweza kuitumia vizuri,”alisema Mtakatifu Tom.
Aliwataja wachezaji aliowateua kwa ajili ya mechi ya kesho, ambayo itakuwa ya tatu tangu kuanza kwa Ligi Kuu ni makipa; Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan,  Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika.
Aliwataja viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Rashid Gumbo, Shamte Ally na Simon Msuva, wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na Hamisi Kiiza na ambao hawamo kwenye programu ya kesho ni kipa Said Mohamed, mabeki Nsajigwa Shadrack, Job Ibrahim, viungo Frank Domayo, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Assega, na Issa Ngao wa Yanga B anayekomazwa kikosi cha kwanza na mshambuliaji Said Bahanuzi.
Yanga imeambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za Ligi Kuu, awali ikilazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Huo ulikuwa mchezo wa pili Saintfiet anafungwa Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic.

Katika mechi hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico ya Burundi. 

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

One Comment on "Mbelgiji Tom Saintfieti atimuliwa yanga kutokana na mwenendo mbaya wa timu"

  1. Bosco Akilei says:

    Tafadhali, Siyo Mtakatifu Tom, bali sahihi ni Thomasi Mtakatifu !

Got something to say? Go for it!