WILAYA YA MUHEZA INA MTANDAO MKUBWA WA UVUNAJI MISITU KIHOLELA

MKUU wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu amesema kuwa wilaya hiyo inamtandao mkubwa wa uvunaji wa misitu, ukiwashirikisha viongozi wa idara ya misitu na wenyeviti wa vijiji.

  Akizungumza na Fullshangweblog mwishoni mwa wiki Mkuu huyo wa Wilaya, alisema vitendo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kasi kubwa uharibifu wa mazingira. 
 Mgalu alisema kuwa hali ni mbaya sana ya uvunaji misitu katika wilaya ya hiyo, kutokana na wenyeviti wa vijiji na maofisa watendaji wa kata na vijiji kushiriki katika mtandao wa uvunaji miti ya kupasua mbao kiholela, huku wakijua upigwaji marufuku, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa.
 
Alisema inasikitisha pale wenyeviti na watendaji wakitoa vibali, viongozi wakishiriki kuharibu mazingira kwa kuvuna miti kiholela kwa ajili ya tamaa ya kujipatia kipato hata kama njia wanazotumia zina madhara katika jamii.
 Mgalu alisema kuwa wilaya hiyo yenye misitu mingi hivi sasa imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa maji kutokana vitendo vya uvunaji wa misitu kitendo kinachosababisha mabadiliko ya tabianchi hali inayochochea ukame na  ukosefu wa mvua za kuaminika.
 “Mtu anakamatwa na mbao nyingi katika lori harafu anapigwa faini ya 400,000 na gari linaondoka anakwenda kuuza na kupata faida ya Milioni 5 ama 10”alisema Mgalu.
 Mgalu alitoa onyo kuwa sehemu itakayobainika kuwa kumevunwa miti mbalimbali ikiwemo ya mbao haramu ofisa mtendaji wa sehemu hiyo atachukuliwa hatua za kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Alisema kuwa agizo la mkuu wa mkoa huo kuzuia uvunaji miti ya mbao liko palepale, agizo hilo pia linawahusu hata wale watu wanaomilikiki mashamba yao binafsi.
 Kikao hicho cha Kamati ya  Ushauri ya Wilaya ya Muheza  kiliwahusisha maofisa watendaji na wanasiasa.

 (DCC).

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!