MBUNGE VITI MAALUM CHADEMA AWAOMBA WALIMU KUTOGOMA

MBUNGE wa viti Maalum mkoa wa Dar  es Salaam, Philipa Mturano (Chadema), amewaomba walimu nchini kutogoma katika kufundisha wanafunzi kwa kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuliangamiza taifa.
 
Mturano alitoa kauli hiyo juzi, wakati akikabidhi vyeti katika mahafali ya tano kwa wahitimu wa kidato cha nne kwenye Shule ya Sekondari Magnus iliyopo Chanika nje kidogo ya jiji la Dar esSalaam.
 
Alisema kitendo cha kuwakosesha elimu vijana ni sawa na kuliandaa taifa kuwa  la wahalifu amabapo madhara yake ni makubwa kwani watakapoa kufanya vitendo vya uhalifu hawatachagua wa kumdhuru.
 
“Wakati huo watamdhuru kila mtu wakiwamo walimu wenyewe kwa vile  elimu yao itawelekeza kutumia nguvu walizojaaliwa na mwenyezi mungu kwa ajili ya kukaba watu na kuwapora mali zao.
 
“Mimi mwenyewe ni mwalimu kitaaluma ninachoongea huenda msinielewe ila tusifanye migomo itakayowathiri watoto wetu katika maisha yao ya badaye na kwa kuwa sisi ndiyo tumeifikisha nchi hapa ilipo basi tuwape elimu bora ili waweze kuitoa katika hali ya watu kukosa thamani katika nchi yao”alisema Mturano.
 
Aliongeza kuwa walimu ni miongoni mwa watu waliochangia kuwepo kwa serikali iliyopo madarakani hivyo kama wataona malengo yao ya kazi yanakwamishwa na serikali wanapaswa kuiadhibu kwa njia nyingine na siyo ya kuwadhulumu watoto haki ya kusoma.
 
Aidha Mturano alitoa wito kwa wanafunzi waliyohitimu kujitambuwa, wafahamu kufeli siyo mwisho wa malengo yao ya kielimu na kimaisha kwa kuwa fursa zipo nyingi za kujiajiri, kuajiriwa kama watakuwa na nidhamu katika maisha.
 
Awali Mkuu wa Shule hiyo, Leonce Kayagwa, alisema shule yake inakabiliwa na changamoto mbali mbali miongoni mwa hizo nipamoja na kukosekana uzio unaozunguuka shule hiyo, hali inayosababisha kushindwa kuwadhibiti wanafunzi watoro wa vipindi.
 

Changamoto nyingine ni pamoja  na kukosekana kwa kisima cha maji katika shule hiyo na ukosefu wa dawa kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wakati wa dharura.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!