SAID MECK SADIK AZUNGUMZIA ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amevipongeza vyombo mbalimbali vya habari vinavyoendelea kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa ya watu na makazi na kuongeza kuwa hivi sasa wananchi wana uelewa mkubwa juu ya zoezi hilo na wako tayari kuhesabiwa.

 “Navishukuru sana vyombo vya habari kwa kazi nzuri za uhamasishaji wa watu kushiriki katika Sensa ya watu na Makazi japo vipo vichache sana vinavyoendesha mijadala ya kuipinga”

 Amesema maandalizi ya zoezi hilo kwa mkoa wa Dar es salaam yamekamilika licha ya kuwepo kwa  malalamiko na madai ya baadhi ya makarani wachache kutolipwa fedha za mafunzo jambo ambalo amesema mamlaka husika zinalifanyia kazi kwa kuhakikisha kuwa ukamilishaji wauhakiki na uthibitisho wa majina yao unakamilika leo.

 “Kwa upande wa jiji la Dar es salaam wengi wameshalipwa fedha zao na kwa  wale wachache ambao madai yao yanashughulikiwa nawahakikishia kuwa watalipwa kwa kuwa fedha yao ipo” amesisitiza.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!