Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zatakiwa kuendelea kusimamia ugatuaji madaraka

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) Hawa Ghasia.

…………………………………………
GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE -ARUSHA

NCHI  wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zimetakiwa kuendelea kusimamia ugatuaji wa madaraka kwa umma  ili  haki iweze kutendeka  na kuwezesha kuwepo kwa utawala bora kwa nchi hizo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) ,wakati akizungumza katika  uzinduzi wa baraza la viongozi wakuu wa serikali za mitaa la Afrika Mashariki lililofanyika mjini Arusha.

Alisema kuwa, endapo nchi wanahama watasimamia vizuri ugatuaji madaraka  utawezesha kwa kiasi kikubwa sana kuondokana na changamopto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kutokuwepo   kwa  matumizi mabaya ya rasilimali .

Ghasia alisema kuwa, kuanzishwa kwa baraza hilo kutasaidia kwa kiasi kikubwa  kuwa kitu

kimoja ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha utendaji wa Serikali za Mitaa na utekelezaji wa dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa Umma kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu katika kanda ya Afrika Mashariki.

 Alisema kuwa, kuanzishwa kwa baraza hilo litawezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali katika utendaji kazi ndani ya serikali za mitaa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Ghasia  alizitaka nchi hizo wanachama kuhakikisha kuwa zinawajengea uwezo viongozi wake ili waweze kuwa na maamuzi sahihi yanayayoendana katika nchi hizo ili kuweza kuwa kitu kimoja na kudumisha ushirikiano katika nchi hizo.

 Aidha Waziri huyo alichaguliwa kushika nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo kila nchi wanachama watapata fursa ya kuchagua mwenyekiti mwingine kila mwaka.

 Naye Mwenyekiti wa ALAT Tanzania ambaye pia ni Meya wa jiji la Mwanza , Didas  Masaburi alisema kuwa,baraza hilo litasaidia viongozi wa serikali za mitaa kupata nafasi za kushiriki vikao vya ndani ambapo hapo awali vilikuwa haviwashirikishi ,hivyo kuwafanya kukosa haki zao za msingi.

 Masaburi alisema kuwa,kupitia baraza hilo ni muda muafaka sasa kwa serikali za mitaa kupata maendeleo ya kiuchumi katika kuhakikisha kuwa watu wanaweza kushiriki katika maamuzi mbalimbali ya serikali za  mitaa.

 Aliongeza kuwa,baraza hilo ni chombo cha kuwawezesha viongozi wa serikali za mitaa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki waweze kubadilishana mawazo ambayo yataweza kutatua changamoto zinazowakabili .

 ‘Kwa kweli umefika wakati sasa wa kuhakikisha kuwa tunakusanya nguvu zetu pamoja ili kuungana na kuwa kitu kimoja na hatimaye kuweza kushughulikia changamoto mbalimbali mbalimbali ili kuhakikisha hazitakuwepo tena’alisema Masaburi.

 Masaburi aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa wanawajengea uwezo serikali za mitaa ili kuwa na uwezo wa kuongoza watu na kuweza kuboresha utendaji kazi katika idara mbalimbali na hatimaye kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na baraza hilo.

 

admin

Got something to say? Go for it!