Archive for June 12th, 2013

Hakuna mchezo kabisa, Tuzo za filamu za steps kufanyika Jumamosi!!

1Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba (mwenye koti) akizungumzia udhamini wa kampuni yao katika tuzo za Steps Movie Award zilizopangwakufanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl. 3 (2)Meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus akionyesha moja ya tuzo zitakaotolewa kwa wasanii sikuya Jumamosi kwenye ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, kulia ni  Mwakilishi wa kampuni ya Steps Solar, Johnson Mwamba.

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya usambazaji wa filamu Tanzania ya Steps Entertainment limited Jumamosi  itatoa tuzo kwa wasanii, Watayarishaji, Waongozaji, na wadau mbalimbali waliopo katika tasnia ya filamu Tanzania.
Mratibu wa tuzo hizo, Carlos Johns Silondwa alisema kuwa tuzo hizo zitafanyika kwenye ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza na zitawahusisha zaidi wasanii wanaofanya kazi na kampuni yao tu.
Silondwa alisema kuwa kutakuwa na vipengele nane ikiwa pamoja na Filamu Bora ya Mwaka, Kampuni iliyotengeneza filabu bora, msanii anayependwa na watu ndani na nje ya mwisho, msanii bora chipukizi, muigizaji bora wa kike, muigizaji bora wa kiume, muongozaji bora wa filamu na mwandishi bora wa filamu.
Silondwa alisema kuwa wameandaa tuzo hizo kwa lengo la kuanzisha tuzo hizo ni kuleta ushindani na kukubali mchango wa wasanii, watayarishaji na wadau wote kampuni inatumia fursa hii ya kuwatambua na kujali mchango wa wasanii katika ukuzaji wa filamu nchini Tuzo ni kichocheo kitakacholeta ushindani unaoweza kujenga tasnia ya filamu na kujenga ajira kwa jamii kubwa.
Alisema kuwa tuzo hizo zimezingatia michango mbalimbali kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa mbele katika kutangaza tasnia ya filamu ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali, pia kutakuwa na tuzo za heshima kwa waliotangulia kuitambulisha tasnia ya filam u Tanzania.
“Tunaamini kuwa tuzo zitakuwa kichocheo kikubwa cha kukuza tasnia ya filamu kuongeza ushindani katika kutengeneza filamu Bora, hadithi nzuri zinazoelimisha, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania lugha ambayo imekuwa ikukua kila siku kwa kupitia filamu za kitanzania zinazopenyeza na kuvuka mipaka ya nchi,” alisema Silondwa.
Alisema kuwa wanaarajia kuwa na Tuzo kubwa zitakazoshirikisha wadau wote kwa baadae, na kuwa ni moja kati ya moja ya kampuni wadhamini wa tuzo zenye mlengo wa kimataifa, mwaka huu kampuni imeandaa tuzo hizo pasipo kuwatumia wadhamini wa nje ya kampuni ikipata udhamini kwa kampuni ya Steps Solar pekee

TTCL ILIVYOSHIRIKI MAONESHO KATIKA VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA

IMG_0096Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi akipata maelezo kutoka wa Josephine Mwakapugi kuhusu huduma zipatikanazo katika simu za kiganjani za TTCL “SMART PHONE”
pamoja na punguzo kubwa la bei ya Intarnet kwa simu zenye waya na zisizotumia waya “wireless”.
  IMG_0101Waheshimiwa wabunge wakipata maelezo kuhusu mkongo wa taifa wa mawasiliano. m IMG_0115 IMG_0118Naibu waziri wa Nishati na madini Mheshimiwa Steven Masele akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kupata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na TTCL. IMG_0120

JAJI BOMANI ASHAURI KUPIGWA KURA ILI KUABAINI MFUMO WA MUUNGANO

index

NA BELINDA KWEKA – MAELEZO,DSJ

MWANASHERIA  Mkuu wa Serikali  mstaafu, Jaji Mack Bomani ametoa wito wa kupingwa kwa kura ya maoni kwa wakazi wa Tanzania Visiwani ili kuona kama wanahitaji mfumo gani wa Muungano kabla ya kuendelea na mchakato wa sasa wa rasimu ya Katiba  mpya .

Akizungumza na  waandishi wa  habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO , Jaji Mack   Bomani  alisema  anaipongeza tume ya Jaji  Joseph   Warioba kwa kazi nzuri na pia kwa mapendekezo yake juu ya  Muungano  wa Tanzania.

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo  Jaji  Bomani  alitoa historia fupi juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo ameeleza kuwa muungano huo ulipendekezwa na hayati Sheikh Abeid  Amani  Karume na hayati Mwalimu  Julius  Nyerere, ambao walikutana mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari, mwaka 1964.

Jaji Bomani   aliongeza  hayati  Karume  alipendelea nchi mbili kuungana  na kuwa  nchi moja , lakini hayati  Nyerere  alisita  kidogo  kwa kuogopa kwamba ingeonekana Zanzibar imemezwa na Tanganyika na pengine kuleta maasi Zanzibar hivyo kupendekeza kuundwa mfumo wa muda mfupi wakati mfumo wa kudumu ukifanyiwa kazi.

“Suala la Muungano  ndilo  suala kubwa kuliko yote katika  mchakato  wa Katiba mpya.  Niliwahi kuto ushauri nao ni kwamba ifanyike kura ya maoni ya wananchi hasa Zanzibar  kama wanautaka muungano au la na kama wanautaka uwe muungano  wa mfumo gani ? Mpaka sasa maoni ambayo yanasikika ni maoni ya viongozi mara Zanzibar ijitoe kwenye muungano mara tuwe na muungano wa mkataba,” alisema  Jaji Bomani.

Akijibu maswali aliyoulizwa  na waandishi wa habari ,Jaji Mack Bomani amesema katika uundwaji wa Serikali tatu anaamini utaweza kumaliza migogoro inayojitokeza mara kwa mara hasa upande wa Zanzibar kuogopa kumezwa. “Woga  wa gharama za mfumo wa Serikali tatu hauna msingi.Inategemea Serikali hizo unazifanya vipi.ipo mifano mingi mno duniani ya miungano ya mfumo mbalimbali,” alisisitiza.

Pia ameongezea kuwa kama kutaundwa Serikali tatu basi iwe Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.

Akiongezea kuhusu katiba mpya amesema “kwa maoni yangu si lazima kazi hii ya katiba iishe kabla ya 2015, tupate muda wa kutosha ili tuweze kupata katiba ya kueleweka na kukubalika na kila mtu”.

TANAPA YAKABIDHI TUZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA USIKU HUU

2Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Musa Juma kutoka gazeti la Mwananchi  mfano wa hundi  ya shilingi milioni moja na laki tano aliyoshinda baada ya kuandika makala nzuri ya kutangaza utalii wa Tanzania   katika tuzo inayoandaliwa na shirika la hifadhi za taifa TANAPA kwa waandishi wa habari wa Televisheni, Redio na Magazeti katika hafla ya kukabidhi zawadi  kwa washindi watuzo hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Hiltop Hotel ya mjini Iringa, hafla hiyo imefanyika baada ya mkutano wa siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA katika  ikiwa na kauli mbiu ya Jukumu la Vyombo vya habari Katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za taifa uliomalizika leo , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA 3Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Albano Midelo wa Gazeti la Dira tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 4Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Alex Magwiza wa TBC tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 5Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi David Azaria wa Sahara Media  tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 7Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali alioongozana nao katika hafla hiyo kutoka kulia ni Adam Swai Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Iringa,Theresia Mahongo Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,James Lembeli Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili na kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 8Mhariri wa habari Chanel Ten Esther Zelamula akitangaza mmoja wa washindi katika hafla hiyo kulia ni Lesara Kabongo Afisa Utalii TANAPA na kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA Pascal Shelutete. 9Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Eliya Mbonea wa  gazeti la Rai tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 10Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi David Rwenyagila wa Radio Five tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 11Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Antonio Nugas wa Clouds Media  tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 12Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki  akimkabidhi Mwandishi Lilian Shirima wa TBC  tuzo  aliyojishindia baada ya kuandika makala iliyozungumzia vyema masuala ya utalii , kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Ndugu James Lembeli na katikati ni Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi. 14Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za TANAPA mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao kutokana na ushindi wao.

1Kikundi cha ngoma cha Mkwawa Magic Site Cature Troupe kikitumbuiza katika hafla hiyo. 4 Lesara Kabongo Afisa Utalii TANAPA kulia na kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA Pascal Shelutete pamoja na maafisa wengine wakiwa katika hafla hiyo. 5Jaji mkuu Dr. Ayoub Rioba akitambulisha majaji wa shindano hilo Majaji wa shindano hilo  kulia ni Beatrice Kessy na kutoka kushoto ni Jack Meena na Tuma Abdallah 6Wahariri mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo. 7Meneja uhusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akitangaza utaratibu wa hafla hiyo 11Baadhi ya wahariri wakifurahia jambo katika hafla hiyo 12Baadhi ya wahariri wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.

MKUTANO WA WADAU WA UHAMASISHAJI WANANCHI KUJIUNGA NA NHIF,CHF NA TIKA WAFANA PWANI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, akihutubia katika mkutano wa wadau wa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya mkoani Pwani leo.
 
Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akielezea mikakati mbalimbali ya kuboresha mfuko huo nchini

 

Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani,Andrew Mwilungu akiwakaribisha wadau kwenye mkutano huo muhimu wa uboreshaji sekta ya afya kwa wananchi kujiunga NHIF,CHF pamoja na TIKA mkoani
Humba akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza kwa nasaha zake alizozitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa wadau ambao ulihudhuriwa na watendaji wakuu wa kutoka wailaya zote za mkoa huo wakiwemo na wabunge.
Mbunge wa Kibiti, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Pwani, Abdul Marombwa akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa hotuba yake pamoja na ujio wa NHIF  mkoani humo.
Baadhi ya wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani, wakiwa katika mkutano huo. Kutoka kulia ni, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Ahmed Kipozi na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu
.
Baadhi ya wadau wakihudhuria mkutano huo.
Mmoja wa wadau wa mkutano huo akihudumiwa na maofisa wa NHIF
Viongozi wa NHIF, CHF wakiwa pamoja na wadau kwenye mkutano huo
Ofisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Kisinga (kulia) akiratibu mkutano huo. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee na Mratibu wa NHIF Mkoa wa Pwani, Andrew Mwilungu.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo

MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHURI

Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati
yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya
Jamhuri  hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB
imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao
umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
 Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB  kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka
kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote
zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
 Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.

FLAVIANA MATATA FOUNDATION STATIONERIES …….COMING SOON!!

FLAVIANA MATATA FOUNDATIONS

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

IMG_0386Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge waBunda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Utatibu, Mhe. Stephen Wasira. Bngeni Mjini Dodoma Juni 12, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  IMG_0442Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Bungeni mjini Dodoma Juni 12, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMG_0468Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na bunge wa Viti Maalum na Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni12, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMG_0507Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Southern Highlands yaMafinga Iringa waliotembelea Bunge Juni 12,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMG_0514 IMG_0573Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 12, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IMG_0577 IMG_0582Wanachuo wa Chuo kikuu Cha Mtakatifu John cha Dodoma wakifurahi kusalimiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 12, 2013.(Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)

KIINGILIO MECHI YA STARS, IVORY COAST 5,000/-

images

Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.

 

Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.

 

Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.

 

Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili kabla ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.

 

Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.

 

Utaratibu katika mechi hiyo utakuwa kama ilivyokuwa katika mchezo wa Simba na Yanga, ambapo hayataruhusiwa kuingia uwanjani isipokuwa kwa yale yatakayokuwa na sticker maalumu kutoka TFF.

KIKOSI CHA IVORY COAST KUWASILI JUNI 13

Ivory_CoastMsafara wa timu ya Taifa ya Ivory Coast (The Elephants) wa watu 80 wakiwemo wachezaji 27 unatarajiwa kuwasili nchini kesho (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.

Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri, na itachezeshwa na Charef Mehdi Abdi kutoka Algeria.

Kikosi hicho kitawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 2.50 usiku na kitafikia hoteli ya Bahari Beach iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajia kuondoka saa chache baada ya mechi hiyo.

Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Abdoul Razak, Akpa Akpro Jean-Daniel Dave Lewis, Angoua Brou Benjamin, Arouna Kone, Aurier Serge Alain Stephane, Bamba Souleman, Barry Boubacar, Boka Etienne Arthur, Bolly Mathis Gazoa Kippersund, Bony Wilfried Guemiand, Cisse Abdoul Karim, Diarrassou Ousmane Viera na Dja Djedje Brice Florentin.

Doumbia Seydou, Gbohouo Guelassiognon Sylvain, Gosso Gosso Jean-Jacques, Kalou Salomon Armand Magloire, N’dri Koffi Christian Romaric, Sangare Badra, Serey Die Gnonzaroua Geoffroy, Sio Giovanni, Tiote Cheik Ismael, Toure Yaya Gnegneri, Traore Lacina, Ya Konan Didier, Yao Kouassi Gervais na Zokora Deguy Alain Didier.

Taifa Stars iko kambini hoteli ya Tansoma tangu iliporejea kutoka Marrakesh, Morocco ambapo leo na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri. Ijumaa itapumzika, na itafanya mazoezi ya mwisho Jumamosi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili.

Makocha wa timu zote mbili (Taifa Stars na The Elephants) watakutana na waandishi wa habari Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF kuzungumzia jinsi walivyojiandaa kwa mechi hiyo.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATUNUKUIWA CHETI NA SHIRIKA LA VIWANGO LA KIMATAIFA(ISO)

ISO..3 Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor pamoja na Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi wakionesha cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) kwa wana habari jana katika ofisi za kiwanda cha bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.  ISO....6Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) mara baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam.  ISO...4Meneja mawasiliano ya ndani wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza jambo katika mkutano na wana habari jana jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor

ISO...5 ISO..1Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO)   akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor

OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUPITIA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA, YAKABIDHI MSAADA WA KOMPUTA KWA KITUO CHA MAFUNZO YA KOMPYUTA CHA CHWAKA MJINI UNGUJA (CHWAKA COMPYUTER TRAINING CENTER)

001Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhi sehemu ya Compyuta 15, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu, kwa Kituo hicho cha Chwaka Computer Training Center. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula. Picha na OMR

002Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la chwaka wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kusini Uguja, (hayupo pichanio) wakati alipokua akizungumza baada ya makabidhiano hayo, alipomwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Bilal.Picha na OMR 003Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji (kulia) akikabidhiwa sehemu ya Compyuta 15, na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw. George Mulamula, ambapo Mkuu huyo wa mkoa wa Kusini unguja, alizikabidhi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya jimbo la Chwaha Bw. Muhammed Ali Selemani, kwa niaba ya Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kwa ajili ya Kituo cha Chwaka Compyuter Training Center, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Mhe. Makamu Dkt. Bilal kwa kituo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kwenye Kituo hicho. Kulia ni . Kushoto ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis. Picha na OMR 004Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslih Haji, akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Chwaka mara baada ya makabidhiano ya Computer 15, ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Makamu wa Rais Kwenye Kituo cha Chwaka Computer Training Center. Kulia ni  Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Chwaka Bw. Muhammed Ali (kushoto) ni Shekha wa Shehia ya Chwaka Bw. Msaraka Pinja na Mtendaji Mkuu wa Sayansi na Teknolojia Bw George Mulamula. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Juni 11, 2013, kituoni hapo. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA UJERUMAN ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

 

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus Peter Brandes, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake, nchini. Picha na OMR 2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Klaus Peter Brandes, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake nchini. Picha na OMR

Vyuo vya ukunga vyatakiwa kusajiliwa

images

  NA MAGRETH  KINABO- MAELEZO

BARAZA la Uuguzi na Ukunga Tanzania limetoa agizo kwa mtu, kikundi au taasisi inayoendesha  mafunzo ya uuguzi na ukunga bila kuwa  na kibali kufunga mara moja.

Aidha baraza hilo limewataka wamiliki wa vyuo  hivyo, wafuate taratibu zinazotakiwa ili kuhakikisha vyuo vyao vinasajiliwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msajili wa  vyuo hivyo kutoka katika baraza hilo, Lena Mfalila wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari- MAELEZO jijini Dares Salaam.

Alisema baraza hilo ,linafanya kazi chini ya sheria inayoitwa ‘The Nursing and Midwifery Act’ ya mwaka 2010 namba 1 ili kuhakikisha kuwa huduma za  afya inayotolewa kwa umma ni bora na salama.

“Kuanzia sasa baraza halitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wle wote watakaokiuka agizo hili, ni vyema  tukazingatia wito wa kutii sheria  bila shuruti,” alisema  Mfalila.

Aliongeza kuwa kuanzisha  mafunzo ya uuguzi bila kibali cha mamlaka husika, ambayo ni baraza hilo ni uvunjaji wa sheria. Hivyo katika sheria  ya baraza hilo kifungu namba 41 kinaeleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu,taasisi,kikundi chochote kitakachokiuka sheria hii.

Akifafanua kuhusu kifungu hicho, Afisa Muuguzi Mkuu –Kitengo cha Mipango na Fedha alisema , Andrew Kapaya alisema sheria iko wazi kifungu cha 41 sehemu ya  nane inatoa  adhabu kwa mtu atakayekiuka kuwa   atatoa faini ya sh.milioni tatu au sh. milioni tano au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Hata hivyo Mfalila alisema wana mpango  wa kuanzisha utaratibu mpya wa kufanya kazi kwa pamoja yaani wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wa kitengo hicho, baraza hilo na   Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)  ili kuhakikisha vyuo vya taalauma hivyo vimekidhi masharti ya usajili.

Baraza hilo limewataka wananchi   kuacha kuandikisha vijana  wao katika vyuo ambavyo vinaendesha mafunzo kinyume na utarati bu kwa kuwa wale wote wanaohitimu katika vyuo  hivyo hawatambuliwa na baraza hilo na hawatasajiliwa kama wauuguzi wa wakunga hapa nchini na duniani kote.

UJUMBE WA PLO YA PALESTINA WAKUTANA NA KINANA

1Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose, akimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid, baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Kiongozi huyo na ujumbe wake Jehad Abu Znead (kushoto) na Saleh Raafat (wapili kushoto), wapo nchini kwa mwaliko wa CCM.(Picha na Bashir Nkoromo)
2Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid, baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Kiongozi huyo yupo nchini kwa mwaliko wa CCM. (Picha na Bashir Nkoromo). 3Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid (wapili kushoto) katika mazungumzo maalum yaliyofanyika kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa HKT ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Wengine, Watatu kushoto ni Balozi wa Palestina nchini, Dk. Nasri Abujais. (Picha na Bashir Nkoromo).

4Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid (wapili kushoto) katika mazungumzo maalum yaliyofanyika kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa HKT ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Wengine, Watatu kushoto ni Balozi wa Palestina nchini, Dk. Nasri Abujais. (Picha na Bashir Nkoromo).

POLISI WANUFAIKA NA USHIRIKIANO WA POLISI WA BAVARIA,UJERUMANI

1Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer  akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati wakiwa katika kikao cha pamoja na maafisa wa Polisi Makao Makuu.Bw.Sommer yupo katika ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) 2Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer  akimkabidhi zawadi  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati  wa ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi) 3Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer  akiangalia jinsi ya uendeshaji wa mafunzo katika Gym ya Polisi iliyopo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

…………………………………………………………..

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limefaidika kwa kiasi kikubwa na ushirikiano uliopo kati yake na  chuo cha Bavaria cha Ujerumani  katika Nyanja za mafunzo, vifaa na polisi jamii jambo ambalo limewezesha maboresho ya jeshi hilo kuendelea vyema na kutoa huduma inayostahili kwa wananchi.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria cha Nchini Ujerumani Wolfgang Sommer alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na baadhi ya  vikosi vya Jeshi hilo kujionea mafanikio ya Polisi jamii pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa kuimarisha usalama wa raia na mali zao hapa nchini.

Akizungumza katika ziara hiyo Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja alisema ushirikiano baina ya chuo hicho na polisi umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata mafunzo ya jinsi ya kuimarisha mkakati wa polisi jamii pamoja na jinsi ya kuboresha mitaala katika vyuo vyetu vya polisi.

“Ujerumani ni moja ya nchi zilizoendelea sana duniani hivyo na sisi kupitia maboresho yetu tuna mambo mengi ya kujifunza ili kuendana na usasa unaohitajika katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika nyanja ya usalama”Alisema Kamishna Chagonja.

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria cha Ujerumani Wolfgang Sommer alisema majeshi ya Polisi hivi sasa duniani yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuibuka kwa wahalifu wenye kutumia mbinu zilizoendelea hivyo Polisi wana wajibu wa kujifunza kwa kasi mbinu hizo.

Bw.Sommer alisema Polisi kote duniani wapo katika maboresho hivyo kwa siku zijazo majeshi hayo yataimarika katika kupambana na uhalifu na lengo la ziara yake ni kujifunza mbinu zinazotumiwa na polisi wa Tanzania katuika kukabiliana na uhalifu.

Katika ziara hiyo alitembelea Kikosi cha matengenezo ya magari ya Polisi ambacho kwa kiasi kikubwa kilifadhiliwa na Serikali ya Ujerumani mwaka 1994, Kikosi cha Mbwa na farasi, Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA), Kikosi cha Polisi Anga pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

RECOGNITION AND TACKLING OF THE CURRENT ELEPHANT POACHING CATASTROPHE IN TANZANIA

Picture1

BY DR. ALFRED KIKOTI (WORLD ELEPHANT CENTRE PROJECT)

Tanzania’s elephant population declined from 109,000 elephants in 2009 (TAWIRI) to the current estimate of less than 70,000 elephants in 2012.  That is at a rate of more than 10,000 elephants a year.  Estimates are that currently, 30 elephants are killed per day or 10,950 elephants will be killed in 2013. If this slaughter is allowed to continue unabated, the last of our elephants will be killed in seven years time, the year 2020. 

This wanton decimation of the country’s elephant herd will impact on the national economy (declining tourism revenues and diminished employment prospects) and the country’s reputation as a beacon of conservation in Africa.

Today’s situation is even more serious than the 1970’s to 1980’s wave of poaching, which led to Operation Uhai.  Like with operation Uhai, the GoT needs to act immediately and wilfully.  A national response as serious as Operation Uhai is needed now to defeat the well-organised and well-armed poachers and criminal gangs operating in the country.  Strategic Objective 3 (Law Enforcement) of the existing Tanzania Elephant Management Plan 2010-15 needs to be fully implemented.

Poachers need to fear that there is a high chance of arrest and conviction, but equally important is the demonstration of political will and the increased use of intelligence to identify and arrest the ivory traders in the country who are driving the poaching.  Greater security is needed at all potential exit points from the country to seize ivory. 

Simultaneously, we need to address the root cause of the current poaching vis a vis the demand for ivory from south-east Asia (especially China, Philippines, Japan and others) and the current high price of ivory.  Poachers will continue to be easily recruited from Tanzanian villages until the price comes down, which is unlikely to happen until demand reduces. To save Tanzania’s elephants, the GoT must apply more pressure on its partners in Beijing, Manila, Tokyo, Dubai and the other known points of transit and sale and delivery.  These governments need to be pressured to ban the domestic ivory trade and / or the shipment of ivory across their territories and through their ports.  Common strategies are needed to combat the trade.

In the long-term, Tanzania has the capacity to successfully protect its elephants, as it did throughout the 1990s and early 2000s. In the short-term however, western donors and governments must step up rapidly to assist Tanzania, by-passing lengthy bureaucracy to provide the extra funds, expertise and equipment required to defeat elephant poaching. And, the police and judiciary must apply the effective laws that exist.

MKUTANO WA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA TANAPA WAENDELEA MKOANI IRINGA

1Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Allan Kijazi akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa washiriki wa mkutano wa  wahariri wa vyombo vya habari na TANAPA unaofanyika kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo mjini Iringa ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Maada mbalimbali zinawasilishwa leo ikiwa ni pamoja na Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi, Miradi ya ujirani mwema na Ulinzi katika mbuga.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA 2Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Mubnge wa jimbo la Iringa mjini Mchunagji Peter Msigwa akitoa mada  katika mkutano huo wakati wa majadiliano kuhusu utalii katika hifadhi za TANAPA kulia ni Mkurugenzi wa Tanapa na Kushoto ni Dr. Ayoub Rioba na mstari wa nyuma  kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli na kushoto ni Meneja uhusiano wa TANAPA Bw. Pascal Shelutete. 3Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli  akizungumza katika mkutano huo unaoendelea mjini Iringa leo 4Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Mzingira na Maliasili Ndugu James Lembeli  akisisitiza jambo wakati akichangia mada katika mkutano huo unaoendelea leo. 5Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima  Ndugu Charles Misango  akiuliza swali katika mkutano huo 6Dr. Ayoub Rioba akiendesha majadiliano katika mkutano huo 7Mwandishi wa habari Antonio Nugas kutoka Radio Clouds kushoto akiwa pamoja na washiriki wengine katika mkutano huo. 8Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo. 9Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo. 10Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali za mkutano huo.

PELLEGRINI AKUTANA NA VIBOSILE VYA MANCHESTER CITY KUWEKA MAMBO SHWARI KABLA YA KUTUMBUKIA!!

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com

Kocha mtarajiwa wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini amekutana na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Txiki Begiristain pamoja na mkurugenzi mkuu Ferran Soriano ili kuweka sawa baadhi ya mambo kabla ya kutangazwa rasmi kurithi mikoba ya kocha aliyetimuliwa klabuni hapo Roberto Mancini.

City wanatarajiwa leo hii au kesho kumtangaza Pellegrini  kuwa bosi mpya wa miamba hiyo ya soka nchini England baada ya kukubaliana ana kocha huyo wa zamani wa klabu za Malaga na Villarreal za nchini Hispania.

Usiku wa jana, City walithibitisha kumsainisha mkataba winga machachari wa Sevulla, Jesus Navas kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 14.9

Baada ya kusaini City, Navas mwenye umri wa miaka 27 alisema ” Manchester City ni timu inayonifurahisha sana, nafikiri ni wakati wangu muafaka kuifanyia makubwa”.

Kocha mpya wa City, Pellegrini anatarajiwa kufanya mazungumzo na wachezaji Carlos Tevez, Gareth Barry na Joleon Lescott ili kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.

City watasafiri kwenda Afrika kusini, Hong Kong na Helsinki kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England pamoja na michuano mingine barani Ulaya.

Incoming: Manuel Pellegrini will join Manchester City in the coming days Bosi Mpya: Manuel Pellegrini anatarajiwa kujiunga na City siku chache zijazo
New boys: Jesus Navas (above) and Fernandinho (below) have already joined City this summer Mashine mpya: Jesus Navas (juu) na  Fernandinho (chini) tayari wameshajiunga na klabu ya Manchester City kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu nchini England
New boys: Jesus Navas (above) and Fernandinho (below) have already joined City this summer

 

MAMA SALMA KIKWETE AKIWA NEW YORK KUPOKEA TUZO MAALUM

IMG_6374Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais wa Afrika wakati wa hafla ya ukaribisho iliyofanyika katika ukumbi wa UN Millenium Hotel huko New York nchini Marekani tarehe 11.6.2013.  Mama Salma yupo nchini humo kwa ajili ya kupokea tuzo maalum ya Millenium Development Goals; Women Progress Award. Wengine katika picha ni Mama Constancia Mangue Nsue de Obiang, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea, Mrs Nana-Fosue Randal, Mwanzilishi na Rais wa Voice of African Mother’s Inc.akifuatiwa na Mrs Denise Nkurunziza Bucumi na Mwisho ni Madam Traore Mintou Doucoure, Mke wa Rais wa Mali IMG_6401 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Mali Madam Traore Mintou Doucoure wakati wa hafla ya ukaribisho iliyofanyika huko New York tarehe 11.6.2013. IMG_6656Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mwanzilishi na Rais wa Shirika la Voice of African Mother’s Inc.la nchini Marekani Mrs Nana-Fosue Randal wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wake wa Marais kutoka barani Afrika watakaotunukiwa tuzo ya Millenium Development Goals itakayotolewa tarehe 13.6,2013. IMG_6692Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na wake wa Marais wa Afrika wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika katika ukumbi wa UN Milenium Hotel tarehe 11.6.2013. Wengine katika picha ni Mke wa Rais wa Mali Madam Traore Mintou Doucoure, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de Obiang na wa mwisho ni Mwanzilishi na Rais wa Shirika la Voice of African Mother’s Inc la nchini Marekani Mrs Nana-Fosue Randal. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye tafrija  akiongozana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de ObiangMke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye tafrija akiongozana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de Obiang

WIZARA YA AFYA YATOA SEMINA KWA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MATUMIZI YA DAWA ZA KINGA TIBA DAR ES SALAAM

SONY DSCKaimu Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Neema Rusibamayila 
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akifungua mafunzo kwa wanahabari kuhusu umuhimu wa kutumia dawa za kinga, tiba ambazo zitaanza kutolewa bure juni 22 hadi 27 mwaka huu na wizara hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza kupitia mpango wa taifa wa kutokomeza magonjwa ambayo yalikuwa hayajapewa kipaumbele (NTD’s). Kulia ni Mratibu wa Taifa wa magonjwa hayo, Dk. Upendo Mwingira
SONY DSCMmoja wa wanahabari akichangia mada SONY DSCMratibu wa Taifa wa magonjwa hayo, Dk. Upendo  Mwingira,akitoa mada kwenye semina hiyo

SONY DSCOfisa Miradi wa NTD’s Dk. Edward Kirumbi akitoa mada kwenye semina hiyo 007Mratibu wa Elimu ya Afya Dr.Theodore Tigahwa akitoa mada yake.
SONY DSC

Wanahabari wakiandika taarifa mbalimbali za semina hiyo SONY DSCWatoa mada katika semina hiyo kutoka Wizara  ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya
 pamoja na wanahabari waliohudhuria semina hiyo  ya siku moja

  (Na Philemon solomon wa Fullshangwe)

Wizara ya afya na ustawi wa jamii kupitia Mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyo kuwa yahapewi kipaumbele, imeendesha warsha ya siku moja iliofanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu jijini Dar es salaam jana, kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini Kuhusu ugawaji wa dawa za matende na mabusha katika mikoa ya Dar es salaam na mwanza.

Akifungua warsha hiyo kaimu mkurugenzi kinga wa wizara hiyo Dr. Neema Rusibamayila amesema kuwa, ugonjwa  wa Matende, Ngiri, Minyoo ya tumbo, Kichocho, Trakoma na usubi kwa muda mrefu yamekuwa hayapewi umuhimu unaostahili kama magonjwa mengine na wadau wa afya hapa nchini, jambo linalofanya yaendelee kusambaa katika mikoa mbalimbali na kuiathiri jamii.

Aidha Dr.Neema amesema kutokana na magonjwa hayo kuwa tishio kubwa katika jamii, wizara hiyo mkupitia mpango wake wa kudhibiti magonjwa hayo imeandaa mkakati wa kuyatokomeza hapa nchini ifikapo mwaka 2020.

Kwa upande wake mratibu wa taifa wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyosahaulika Dr.Upendo Mwingira amsema endapo jamii itapata elimu na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mpango huo, ni dhahiri kwamba magonjwa yatakomezwa na kubakia kuwa historia.

Wizara ya afya na ustawi wa jamii kupitia Mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyo kuwa yahapewi kipaumbele, imeendesha warsha ya siku moja iliofanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya binadamu jijini Dar es salaam jana, kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini Kuhusu ugawaji wa dawa za matende na mabusha katika mikoa ya Dar es salaam na mwanza.

Akifungua warsha hiyo kaimu mkurugenzi kinga wa wizara hiyo Dr. Neema Rusibamayila amesema kuwa, ugonjwa  wa Matende, Ngiri, Minyoo ya tumbo, Kichocho, Trakoma na usubi kwa muda mrefu yamekuwa hayapewi umuhimu unaostahili kama magonjwa mengine na wadau wa afya hapa nchini, jambo linalofanya yaendelee kusambaa katika mikoa mbalimbali na kuiathiri jamii.

Aidha Dr.Neema amesema kutokana na magonjwa hayo kuwa tishio kubwa katika jamii, wizara hiyo mkupitia mpango wake wa kudhibiti magonjwa hayo imeandaa mkakati wa kuyatokomeza hapa nchini ifikapo mwaka 2020.

Kwa upande wake mratibu wa taifa wa mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyosahaulika Dr.Upendo Mwingira amsema endapo jamii itapata elimu na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mpango huo, ni dhahiri kwamba magonjwa yatakomezwa na kubakia kuwa historia.

REDD’S MISS KINONDONI 2013 WATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR

 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
 Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
 
Warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari. 
Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd’d Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
  Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.

Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd’s Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala  na kufanya usafi.

Warembo hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).

Harambee hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.

Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.

CCM YAPATA UGENI KUTOKA PALESTINA

 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO,

 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat (Kushoto). Wapili kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini  Dk. Nasri Abujasir.

Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizingumza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuanzia saa 3.30 asubuhi hii, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

CRDB YADHAMINI KONGAMANO LA WASOMI WA VYUO VIKUU NCHINI

Meneja wa Biashara wa benki ya CRDB tawi la
UDOM, Danford Muyango akitoa mada 
kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la UDOM, Emmanuel Chaburuma akifafanua jambo kuhusu kongamano hilo. 
 Rais wa AISEC Tanzania, Frank Mushi
 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu  UDOM, Lulu Molel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo. 
 Baadhi ya wanafunzi wakionesha vipaji vyao 
Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.

Mkurugenzi wa ulinzi na usalama CHADEMA Wilfred Lwakatare apata dhamana

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akiingia katika chumba cha ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kupata dhamana katika kesi yake inayomkabili ya kula njama ya kutaka kumzuru kwa sumu Mhariri wa gazeti la wananchi.
 Wilfred Lwakatare akiwa na furaha pamoja na wakili wake baada kupata dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mshtakiwa wa pili katika kesi inayomkali akiwa amerudi rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
Wakili wa Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara akiwa katika picha ya pamoja na mteja wake Wilfred  Lwakatare pamoja na wadhamini wake muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na mahakama leo.
Baada ya kupata dhamana safari ya kuelekea uraiani ilianza.
 Lwakatare akipandishwa katika Pickup.
 Akiwashukuru wanachama na wafuasi wa chama chake.
 Msafara ukiondoka katika maeneo ya Mahakama.
 Wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya Mahakama ya Kisutu.
Ulinzi pia ulikiwa mkali

HATUA YA TATU LIGI YA MABINGWA KUCHEZWA JUMAMOSI

Biharamulo-FC

Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zitachezwa Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) wakati za marudiano zitachezwa Jumatano ya Juni 19 mwaka huu.

 Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana (Juni 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za michezo iliyopita na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwemo mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars na Machava FC ambayo haikuchezwa.

 Machava FC ambayo ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi kwa mabao 2-0 inaendelea katika hatua ya tatu kwa vile haikuhusika katika kukwamisha mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia mchezo huo kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa kinyume na maelekezo ya Kamati ya Mashindano ya TFF. Kamati katika kikao chake cha awali iliekeleza kuwa mechi zote za RCL zitachezwa makao makuu ya mikoa isipokuwa kwa Morogoro ambapo timu ya Techfort FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa CCM Mkamba mjini Ifakara.

 Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza raundi hiyo ni Friends Rangers ya Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi, Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo SC ya Mbeya, Machava ya Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe, Polisi Jamii ya Mara na Stand United FC ya Shinyanga.

 Wakati timu nyingine zimefuzu kwa kushinda mechi zao za raundi ya mbili, Njombe Mji imeingia hatua hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano mdogo wa kufungwa (best looser) katika hatua ya pili.Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo; Kariakoo vs Friends Rangers, Machava FC vs Stand United FC, Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia nyumbani.

 Vilevile Kamati ya Mashindano imeagiza Kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars vs Machava FC, Mwijage Rugakingira wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja wa Mgambo badala ya Uwanja wa Jamhuri kinyume na maelekezo ya TFF aondolewe kwenye orodha ya makamishna.

 Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao nao walikwenda Mpwapwa badala ya Dodoma Mjini wamepelekwa Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kutokana na tukio hilo.

 Kamati ya Mashindano imekumbusha kuwa RCL ni mashindano yanayosimamiwa na TFF, hivyo maelekezo yoyote kuhusiana na mashindano hayo pia yatatoka TFF na si mahali pengine popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa hana mamlaka ya kubadili uwanja.

 Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.

MTEMVU ATOA MSAADA WA SH. MIL. 3.5 KWA VICOBA NA ULINZI SHIRIKISHI

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivikabidhi vikundi vitano vya Kuweka na Kukopa (VICOBA, kila kimoja msaada wa sh. 500,000 na kikundi cha ulinzi shsirikishi sh. 500,000 za kutunisha mifuko hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akikumbatiana na mmoja wa wanachama wa kikundi cha Vicoba cha Tuyangatane waliofurahi kupatiwa msaada wa sh. 500,000 za kutunisha mfuko wa kikundi hicho.
Wanachama wa Tuyangatane wakifurahia kupata hundi hiyo.
Mtemvu akikipatia kikundi cha Vigoba cha Tumaini msaada wa sh. laki tano
Kikundi cha Tupendane kikipatiwa laki tano
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kulia, akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 Mweka Hazina wa Kikundi cha Saccos cha Pambazuko, Sophia Said, kwa ajili ya kutunisha mfuko wao, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivipatia pia kiasi kama hicho vikundi vingine vitano.
Mtemvu akimvisha filimbi Juma Mlanzi ambaye ni miongoni mwa walinzi shirikishi  56 waliohitimu mafunzi ya kijeshi. Pia walikabidhiwa vyeti.
Juma Kambona akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wa pili kulia, akimpatia cheti Mwanaisha Gea ambaye amekuwa miongoni mwa vijana 56 waliohitimu mafunzo ya Ulinzi Shirikishi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alikikabidhi pia kikundi hicho cha Ulinzi Shirikishi sh. 500,000 za kuanzishia Saccos yao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamis Mzuzuri.
Jumanne Jumbe naye akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mama Mkazi wa Kata ya Azimio akilalamika mbele ya Mtemvu, kuhusu mchezo wa Kangha Mbendembende au kangamoko unavyowadhalilidha wanawake ambapo aliomba upigwe marufuku kwa vile auendani na maadili ya kitanmzania.
Mgambo Said Amiri akilalamikia kitendo cha mabosi wake wa Kituo cha Polisi cha Tambuka Reli kinavyowalea vibaka na majambazi katika eneo hilo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WAALGERIA KUCHEZESHA TAIFA STARS VS TEMBO WA AFRIKA MAGHARIBI, IVORY COAST

04

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika Jumapili saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.

 Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.

 Kamishna wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).