Archive for 2013

Mkapa atimiza miaka 75 ya kuzaliwa wake

mkapa+pxRais Mstaafu Benjamin Mkapa akipongezwa na Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo jana wakati misa ya jubilei ya miaka 75 ya kuzaliwa kwake. Picha na Fidelis Felix. 

Dar es Salaam.Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa jana aliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya Ibada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

Katika ibada hiyo ya shukrani iliyofanyika Kanisa Katoliki la Maria Imakulata, Upanga jijini Dar es Salaam, Mkapa aliwataka Watanzania kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Tunamshukuru Mungu kwa majaliwa aliyoipatia nchi yetu ya Tanzania na tunamwomba azidi kuijalia umoja katika yote tunayofanya na tunayokusudia kuyafanya,” alisema Mkapa.

Mkapa pia aliwashukuru waumini wenzake katika kanisa hilo, huku akifichua siri kwamba, Kadinali Pengo alimtaka ahamie Kanisa la Mtakatifu Joseph wakati alipokuwa rais, lakini hakukubali.

Kwa upande wake, Kardinali Pengo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

“Alichofanya Rais Mstaafu Mkapa ni cha kuigwa. Tunatakiwa kutambua kuwa hatuishi kwa nguvu zetu bali kwa uwezo wa Mungu hivyo ni lazima tumshukuru kama alivyofanya mwenzetu,” alisema Kardinali Pengo.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Edward Lowassa na Cleopa Msuya, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Wengine ni waziri wa zamani, Profesa Philemon Sarungi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa pamoja wakuu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Majenerali, Robert Mboma na George Waitara.

CHANZO: MWANANCHI

Dk Mvungi afariki dunia

mvungiDk Sengondo Mvungi.PICHA|MAKTABA 

Dar es Salaam.Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi (61) amefariki dunia katika Hospitali ya Millpark Netcare, Johanesburg, Afrika Kusini.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka Afrika Kusini na kuthibitishwa na Msemaji wa Hospitali ya Millpark, Tebogo Nyembezi zinasema Dk Mvungi alifariki dunia jana mchana. “Ni kweli tulimpokea mgonjwa huyo kutoka Tanzania na alifariki 6:00 mchana (saa 7:00 kwa saa za Afrika Mashariki),”alisema Nyembezi.

Nyembezi alisema kwamba walimpokea mgonjwa huyo akiwa na majeraha ya kichwa, lakini aliahidi kueleza sababu ya kifo chake leo baada ya kuzungumza na madaktari waliokuwa wakimtibu.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba pia alithibitisha kupokea taarifa za kifo hicho na kwamba walikuwa wakiendelea kuandaa taratibu za kuleta mwili wake nchini.

“Ni pigo kubwa kwetu, tunaangalia namna ya kuusafirisha kuja nchini na baadaye tutatoa taarifa rasmi,”alisema Jaji Warioba na kuongeza:

“Kwa kweli ni pigo kubwa siyo kwetu tu, lakini pigo kubwa kwa nchi yetu, tumepoteza mtu muhimu na kiungo muhimu sana. Dk Mvungi, wengine tulimfahamu tangu alipokuwa mwanafunzi, alikuwa mtu aliyesema kile alichokiamini, akikwambia kitu kilikuwa ni kile kilichopo moyoni mwake”.

Jaji Warioba alisema Dk Mvungi alikuwa msomi aliyebobea katika masuala ya sheria na kwamba alikuwa na mchango mkubwa katika tume. Pia alisema marehemu atakumbukwa kwa ushiriki wake wa dhati katika kupigania haki za binadamu, kazi aliyoifanya kwa moyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani alisema: “Dk Mvungi alikuwa mfanyakazi hodari, alikuwa hachoki na hata ulipotokea ubishi mkubwa katika majadiliano kiasi cha watu wengine ku-loose temper (kupandwa na jazba), yeye alibaki vilevile na alizungumza vilevile bila kubadilika. Kweli tumempoteza mtu muhimu sana maana alikuwa akifahamu vizuri sana sheria, hatuna jinsi maana tumempoteza, kwahiyo itabidi tuendelee na kazi hii. Hatuna namna nyingine ya kufanya,”alisema Jaji Ramadhani.

Jaji Ramadhani alisema taratibu nyingine zitatangazwa baadaye kwani lazima washirikiane na chama chake, NCCR- Mageuzi alikokuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji, familia yake na Chuo Kikuu cha Bagamoyo ambako alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliliambia gazeti hili kwamba walipokea taarifa ya kifo cha Dk Mvungi saa 9.30 alasiri jana. “Tumepokea taarifa hizo alasiri kwamba amefariki. Ni kweli na sasa ninaelekea nyumbani kwake ili kuitaarifu familia,”alisema Mbatia.

Taarifa ya Tume

Jana jioni, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa taarifa rasmi kuhusu kifo cha Dk Mvungi ikisema: “Kwa masikitiko makubwa, Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake Dk Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Millpark iliyopo jijini Johannesburg, Afrika Kusini amefariki dunia.”

Taarifa iliyotolewa Katibu wa tume hiyo, Assaa Rashid ilisema Dk Mvungi alifariki dunia saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini.

Iliendelea kusema taarifa hiyo kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini kuja nchini kwa maziko zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Dk Mvungi, alikuwa akitibiwa Afrika Kusini baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana walipovamiwa nyumbani kwake Kibamba, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Novemba 3 mwaka huu.

Alipelekwa nchini Afrika Kusini, Novemba 7, 2013 kwa matibabu zaidi baada ya kulazwa kwa siku tano kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (Moi) jijini Dar es Salaam.

Dk Mvungi, ambaye aligombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, alijeruhiwa vibaya kichwani na sehemu nyingine za mwili wake baada ya kukatwa mapanga na wavamizi hao.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Profesa Costa Mahalu alisema chuo hicho kimepoteza mtu muhimu sana, kwani ni mmoja wa waanzilishi waliokuwa wakifahamu vyema malengo na dira yake.

“Tumepata pigo kubwa sana kwani tumempoteza mtu ambaye tulishirikiana naye katika kuanzisha chuo hiki na aliyafahamu vyema malengo na dira yake, alikuwa ni mwalimu mzuri aliyebobea katika constitutional laws (sheria za Katiba) na wanafunzi walimpenda sana,”alisema Profesa Mahalu.

Profesa Mahalu alisema Dk Mvungi ambaye alikuwa naibu wake kabla ya kujiunga na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, walifahamiana naye siku nyingi na kwamba wakati marehemu alipokwenda kusoma Shahada ya Uzamivu nchini Ujerumani alifikia nyumbani kwake (kwa Mahalu).

“Wakati huo nilikuwa nikifundisha Ujerumani, alikuja kusoma PhD yake ya masuala ya sheria na alifikia nyumbani kwangu, tutamkumbuka kwa uhodari wake katika kuchapa kazi, kweli tumempoteza mtu mahiri sana,”alisema.

Chadema, CCM wamlilia

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amesikitishwa na taarifa za kifo cha Dk Mvungi na kwamba taifa limempoteza mwanzilishi wa mageuzi ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kudai Katiba Mpya.

“Tumepokea taarifa za kifo hiki kwa mshtuko mkubwa, tunamwomba Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya Dk Mvungi, tunatoa pole kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na uongozi wa NCCR-Mageuzi,” alisema Mbowe.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa (CCM), Mwigulu Nchemba alisema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa na kutoa pole kwa Watanzania wote kwa sababu Dk Mvungi alikuwa anafanya kazi muhimu ya kuwezesha kupatikana kwa Katiba Mpya.

Alisema amekufa wakati mchango na mawazo yake yakiwa yanahitajika kwa kiasi kikubwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwamba CCM kinaendelea kuisisitizia Serikali iwasake wahalifu hao ili wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa alisema ameshtushwa na taarifa za kifo hicho ambacho kimetokea wakati Dk Mvungi akifanya kazi muhimu ya kuitafuta Katiba Mpya. “Naomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, amina,” alisema.

Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alisema taifa limepoteza mtu muhimu na kwamba hali ya ulinzi ni suala linalohitaji mjadala wa kitaifa.“Tunahitaji kuangalia kiini cha uhalifu hapa nchini, watu wanateswa na kujeruhiwa ovyo ni lazima tuchukue hatua,” alisema.

Mitandao ya kijamii

Muda mfupi baada ya taarifa za kifo chake, mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Jamii Forum ilikuwa ilitawaliwa na salamu za pole kutoka kwa watu mbalimbali.

Hussein Bashe kwenye ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa, “Dr Sengondo Mvungi Is No More (hatunaye tena), taarifa zilizonifikia kutoka Hospitali ya Millpark, ndugu yetu Mvungi amefariki, mnamo saa tisa na nusu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Wahalifu wamekatisha uhai wake wakati akifanya jukumu zito kwa ajili ya taifa letu. Jambo hili linaumiza sana Mungu atalipia uhalifu huu, poleni Tume ya Katiba, Poleni Familia, poleni NCCR-Mageuzi.”

Mtu mwingine aliyechangia suala hilo kwenye mtandao wa Jamiiforum ni yule aliyejitambulisha kwa jina la Ta Muganyizi aliyeandika kuwa, RIP Dr. Mvungi… Mungu akulaze mahala pema peponi. Japo umeondoka kivuli chako kitaishi… Naipa pole familia yako, maisha yetu kwa sasa nchini ni kudra za Mwenyezi Mungu. Ni kwamba tupigwe… wengine wamepona lakini wewe umeondoka.”

CHANZO: MWANANCHI

JK akataa zawadi ya pande la dhahabu

 

jk+mkonoRais Jakaya Kikwete.PICHA|MAKTABA 

Geita.Rais Jakaya Kikwete jana aligoma kupokea zawadi ya dhahabu kutoka Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya mkoani Geita.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana ilisema viongozi wa kampuni hiyo walitaka kumkabidhi Rais Kikwete gramu 227 za dhahabu safi wakati alipotembelea mgodi huo.

Rais Kikwete badala yake aliwaelekeza waiuze dhahabu na fedha zitakazopatikana zitumike kuwasaidia watoto yatima.

Alikabidhiwa zawadi hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambao ni makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale, Geita.

Gramu hizo 227 zina thamani ya Sh16 milioni kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete aliuliza: “Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”

Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete aliupongeza uongozi wa mgodi huo akisema umeongeza thamani ya dhahabu na maisha ya wananchi katika eneo hilo… “Mmefanya vizuri na mgodi huu, ni mradi wa maana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifu huu unastahili pongezi,” alisema Rais Kikwete.

Mgodi wa Nyamigogo ni wa marudio kwani unazalisha dhahabu kutokana na mchanga ambao awali ulishafuliwa na kutoa dhahabu. Ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa kiasi cha Sh 1.6 bilioni kimewekezwa kuuendeleza.

Uongozi wa mgodi huo ulisema mgodi huo unaozalisha kiasi cha gramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi, na unaajiri watu 45 kati yao wanawake 10.

Rais Kikwete alizindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake Geita ambao ni moja ya mikoa minne aliyoianzisha mwaka jana. Mikoa mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.

Amtetea Magufuli

Rais Kikwete amewataka viongozi wa CCM kuacha kulalamikia utendaji wa viongozi na badala yake kuelimisha wananchi juu ya utendaji wa Serikali.

Akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani Geita, Rais Kikwete alisema viongozi hao walimpinga Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wakati akiwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alipokuwa akipambana na uvuvi haramu.

“Walimwona mbaya, tena hata wazee wa CCM walilalamika na kupiga kelele… anatuharibia kura, sasa hayupo, samaki wamekwisha ziwani. Watu wenu wamebaki kuwa maskini na hakuna samaki,” alisema.

Aliwahimiza viongozi wa Mkoa wa Geita kufikiria mpango wa kufuga samaki akitoa mfano wa Vietnam ambayo sasa inafuga sato na sangara kwa kiasi kikubwa.

CHANZO: MWANANCHI

TBL YATOA MSAADA WA SH. MILIONI 38 ZA KUCHIMBA KISIMA ZAHANATI YA NBC TABATA DAR

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) eneo la Tabata, Joseph Nicholous (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 38, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji visima ya Basic Co. Ltd, Deo Bishubo kwa ajili ya gharama ya kuchimba kisima cha kina kirefu katika Zahanati ya NBC Tabata, Dar es Salaam juzi.Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Muuguzi Kiongozi wa Zahanati hiyo, Semeni Mtauka.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Baadhi ya wakazi wa Tabata miongoni mwao wakiwemo wagonjwa akishuhudia makabadhiano ya msaada huo
Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu (kushoto) akielezea mikakati ya TBL ya kusaidia upatikanaji wa maji katika baadhi ya vituo vya afya na zahanati nchini.
Muuguzi kiongozi wa zahanati hiyo, Mtauka akitoa shukurani kwa TBL kuwapatia msaada wa kisima hicho kitakachosaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la maji.
Mkazi mmoja wa Tabata akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo
Zahanati ya NBC Tabata

Rais Dk.Shein azungumza na Vyombo vya habari

TA1A1237Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na
Wahariri na Waandishi wa habari Waandamizi wa Vyombo mbali mbali vya Bara na Visiwani,mkutano huo uligusia masuala ya kiuchumi na kijamii katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
TA1A1214Baadhi ya Wahariri habari wa Vyombo mbali mbali na Waandishi  Waandamizi wa bara na Viwani wakiwa katika
mkutano na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) uliogusia masuala mbali mbali ya kiuchumi na kijamii katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

WANANCHI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA ELIMU

Rc Dsm

Na Aron Msigwa – MAELEZO,  Dar es salaam.
Serikali imewataka wananchi kuzitumia ipasavyo fursa za elimu zinazotolewa kupitia programu mbalimbali za ikiwemo Elimu ya Watu Wazima (EWW) na ile ya Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (ENMRA) ili kupunguza tatizo la umasikini, maradhi na ujinga.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadiki wakati akitoa taarifa kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi yatakayofanyika jijini Dar es salaam kuanzia Novemba 13, 2013 yakiongozwa na kauli mbiu “Kisomo kwa ajili ya Karne ya 21”
 
Amesema  serikali imeanzisha programu mbalimbali za elimu kuanzia msingi mpaka sekondari kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata fursa hiyo na kuondokana na tatizo Umaskini, maradhi na ujinga na kuwawezesha kujikwamua  kiuchumi, Kijamii, Kisiasa na Kiutamaduni.
Ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaam kwa sasa unaratibu program mbalimbali zikiwemo Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA) unaowahusisha wanafunzi wenye umri kati ya miaka 9 hadi 18 ambao husoma katika mfumo wa makundi rika.
Amesema  jumla ya wanafunzi 1,846 wamejiunga na program hiyo kwa mwaka 2013 wakihusiha wale wenye umri wa miaka 9 mpaka 13 na 14 mpaka 18.
Bw. Meck Sadiki ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaam pia unasimamia Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii (MUKEJA) unaohusu utoaji wa Elimu kupitia kisomo cha kujiendeleza na kisomo chenye manufaa kinachowahusisha watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 18 wapatao 1,678 waliojiunga kwa mwaka 2013.
Ameongeza kuwa wanafunzi wapatao 2,309 wamejiunga na programu ya Elimu ya Sekondari Huria (PESH) ambayo huendeshwa kwa wanafunzi ambao wamekosa sifa za kuchaguliwa kujiunga na shule za sekondari kupitia chaguo la mfumo rasmi.
“Wanafunzi wanaosoma katika mpango wa PESH serikali imewawekea utaratibu wa kusoma katika shule za msingi na sekondari ambazo hazina utaratibu wa awamu mbili za kusoma, wao husoma jioni baada ya muda wa kawaida wa masomo”
Aidha amezitaja programu nyingine za elimu zinazowahusisha watu wazima  na vijana kuwa ni pamoja na Elimu ya Masafa na Ana kwa Ana (ODL) ambayo ina jumla ya wanafunzi 335 wanaoendelea na masomo na Elimu Changamani (IPPE) ambayo inawahusisha vijana 112 waliomaliza elimu ya msingi na kukosa nafasi ya kujiunga na sekondari ambao hujengewa uwezo katika masomo ya maarifa, ufundi, afya, maktaba na mazingira.  

Kuhusu  maadhimisho ya mwaka huu Bw. Mecki Sadiki ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine yatakuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu kusikiliza, kusoma na kutoa maoni ya upatikanaji wa katiba mpya nchini, kuongeza mwamko kwa jamii katika masuala ya elimu, kutathmini utekelezaji wa azimio la ulimwengu kuhusu utoaji wa elimu kwa wote na kutathmini mafanikio na mapungufu ya utekelezaji wa Elimu ya Watu Wazima (EWW) na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi (ENMRA).

MHE. UMMY MWALIMU AFUNGUA KIKAO KUJADILI MATOKEO YA UTAFITI WA HALI YA DEMOKRASIA KATIKA NGAZI ZA CHINI KWA MTIZAMO WA KIJINSIA

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifungua kikao cha majadiliano ya taarifa juu ya Utafiti Kuhusu Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa kijinsiaNaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifungua kikao cha majadiliano ya taarifa juu ya Utafiti Kuhusu Hali ya Demokrasia katika ngazi za chini kwa mtizamo wa kijinsia Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Ibrahimu Lipumba akitoa taarifa za Awali za Matokeo ya Utafiti huo. Mhe.Lipumba amesema Utafiti huo ulihusisha madodoso mia sita(600) kutoka katika Mikoa minane nchini.Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Ibrahimu Lipumba akitoa taarifa za Awali za Matokeo ya Utafiti huo. Mhe.Lipumba amesema Utafiti huo ulihusisha madodoso mia sita(600) kutoka katika Mikoa minane nchini Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano (2)Baadhi ya Washiriki wa kikao wakati wa majadiliano

Naibu Waziri wa Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amefungua kikao cha Kujadili Matokeo ya Utafiti wa Hali ya Demokrasia
katika ngazi za chini kwa mtizamo wa Kijinsia.

Kikao kimeandaliwa na Kituo cha Demokrasia nchini kwa ushirikiano wa Shirika la Kimataifa la IDEA, na kuvishirikisha  Vyama
vya siasa, Wizara, Halmashauri na  Baadhi ya Taasisi Zisizo za Kiserikali.Kuijadili taarifa hiyo.

 Wakati akifungua kikao Mhe.Ummy amesisisitiza kuwa, Demokrasia kamili haiwezi kupatikana bila ushiriki sawa wa wanaume na wanawake na kuongeza kuwa, Serikali za mitaa ni wadau wakubwa wa kuleta usawa wa demokrasia.
                 (Picha zote na Asteria Muhozya- MWJJW)

TANZANIA YAONGOZA KWA VIVUTIO VYA UTALII AFRIKA

06 TembeaNa Jovina Bujulu-Maelezo

Tanzania inaongoza kwa kuwa na vivutio bora vya utalii barani Afrika,utafiti uliondeshwa na mtandao wa safaribookings.com wa nchini uholanzi umebainisha.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) bw.Allan Kijazi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam.

Bw. Kijazi alibainisha kuwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilikuwa ya kwanza kati ya vivutio 50 bora Barani Afrika ambapo vivutio 10 kati ya hivyo viko Tanzania.

Alivitaja vivutio vilivyoongoza kuwa ni Ruaha,Mahale,Gombe,Katavi,Tarangire,ziwa Manyara na Arusha,Vingine ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la akiba la selous.

Akizungumzia faida za kuwa na vivutio bora ,ndugu kijazi alisema kwamba wingi na ubora wa vivutio hivyo umetoa fursa ya pekee kwa wawekezaji kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali katika hifadhi hizo hivyo kuongeza pato la Taifa.

Aidha ndugu Kijazi aliongeza kwamba TANAPA imetenga maeneo 34 kwa ajili ya kupanua wigo wa huduma za malazi katika hifadhi  za Taifa ambapo kipaumbele ni kwenye hifadhi za kusini na magharibi ya nchi ambazo zina uhaba wa malazi na hivyo kusababisha idadi ndogo ya watalii kutembelea maeneo hayo.

Bw. Kijazi alimaliazia kwa kusema kwamba wanategemea kuongeza idadi ya watalii kutokana na maboresho hayo na hivyo kukuza pato la Taifa kutokana na sekta ya utalii.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO PLC JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Afisa Utawala wa Benki ya Maendeleo, Rose Mushi, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa  kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013. Wa pili (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene (kulia) ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa kadi ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account katika benki hiyo, Elianasa Marco Njiu,mkazi wa jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Nov 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa kwanza kupata mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa bemki hiyo,leo.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.

BODI YA LIGI YAFUNGIA VIWANJA SABA, FUTURE TAIFA STARS vs TAIFA STARS UWANJANI KARUME!!

tff_LOGO11

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) imefungia viwanja saba vilivyokuwa vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya mechi za mpira wa miguu.

Uamuzi huo umefikiwa na TPL Board katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL katika mzunguko wa kwanza.

Viwanja vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza ili viruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa yake yamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo (dressing rooms) havina hadhi).

 

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitch ni mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha (pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea (pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).

Klabu ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu ya uamuzi huo ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja hivyo ili wafanye marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea mechi zao.

Kwa upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza mechi ya utangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa gharama za uharibifu baada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga baada ya gharama hizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.

Pia Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kushambulia basi la wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi dhidi yao, na kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya Ligi.

Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo mwamuzi msaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi na kichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.

Beki wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam. Kitendo hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa mechi tatu zinazofuata za timu yake.

Mchezaji Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na kukataa kupeana mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers, hivyo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.

Mtunza vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenye benchi la ufundi wakati wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoa lugha chafu kwa refa, hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.

Kocha Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechi yao dhidi ya Ashanti United. Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas Justin amepelekwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya nguoni.

Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.

Katika FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000 na kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti wa mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.

Kamishna Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa Squad na Transit Camp kwa kutokuwa makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa Transit Camp ilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda gani.

Kocha wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na Meneja wa timu hiyo Mrimi Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi tatu kila mmoja kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidi ya Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.

Pia Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakati waamuzi wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa wakati.

Kocha wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia kuhamamisha washabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa Squad.

Naye Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi kwa mwamuzi wa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.

Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi imeahirisha kufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa Uwanja wa Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo haikumalizika. Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka huu).

FUTURE TAIFA STARS vs TAIFA STARS UWANJANI KARUME

Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho (Novemba 13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mechi hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kim Poulsen kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa Stars watakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.

Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo (Novemba 12 mwaka huu). Miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.

Boniface Wambura Mgoyo

Kaimu Katibu Mkuu

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania

ANAMTAFUTA BABA YAKE MZAZI WALIYEPOTEZANA NAYE MUSOMA

Jina langu ni Cosmas Hans Moses (22) na dada yangu anaitwa Aneth Hans Moses(24), kwa sasa naishi mwanza..

Ninayemtafuta ni Baba yetu mzazi anaitwa Hans Moses
Mwakyusa, zamani alikua anaishi Kiabakari Musoma vijijini na huko ndiko tulikopotezana mimi nikiwa mdogo kabisa kwa hiyo simfaham hata nikimuona… Kwa sasa nasikia
anaishi Kyela Mbeya pia ni mfanya biashara ila sijui anafanya biashara gani.

Naomba msaada wenu ili niweze kuonana tena na baba yangu mzazi mawasiliano yangu ni 0765-684572

KINANA KUFANYA ZIARA MIKOA YA MBEYA NA RUVUMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari  kwenye ukumbi wa Sekretarieti ,Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba (Picha na Bashiri Nkoromo)
………………………………………………………………………………………………………

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana ataanza ziara ya siku 22 kwenye mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanzia tarehe 15/11/2013 mpaka mwanzoni mwa mwezi wa Desemba 2013. Huu ni mwendelezo wa ziara za kichama katika kuimarisha chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,  kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kushirikiana nao kuzitafutia ufumbuzi.


Katika ziara zilizopita na vikao kadhaa vya chama  Serikali iliagizwa kushughulikia baadhi ya kero, na tumeshuhudia baadhi ya hoja hizo zikichukuliwa hatua. Baadhi ya hoja zilizoanza kushughulikiwa na Serikali ni pamoja na:-

 

1)         Hoja ya kufufua viwanda nchini.

Baada ya ziara kadhaa za Katibu Mkuu, uchambuzi na vikao kadhaa vya CCM, Chama kiligundua kuwa viwanda vingi vilivyo binafsishwa havifanyi kazi kama ilivyokusudiwa na vingine kufungwa kabisa na kugeuzwa magodauni.
Pamoja na athari kubwa kwa uchumi wa nchi yetu, kufungwa na kutofanya vizuri kwa viwanda hivyo kumechangia sana tatizo la ajira nchini kuwa kubwa. Hivyo Chama kiliagiza Serikali kufanya tathmini ya viwanda vyote vilivyo binafsishwa na hali yake kwa sasa na vile visivyofanya kazi kama ilivyokusudiwa vichukuliwe na Serikali na kutafuta njia sahihi ya kuvifufua upya.

Serikali imechukua hatua kadhaa katika hili, ikiwemo kufanya tathmini na mapendekezo kadhaa yamewasilishwa na timu iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kufanyia uamuzi na kuchukua hatua.

Tunajua zipo hatua kadhaa zimechukuliwa katika jitihada za kufufua viwanda vya kubangua korosho kama sehemu ya utatuzi wa tatizo la soko na zao la korosho. Pia Serikali ipo katika hatua kadhaa za kushughulikia viwanda vingine nchini.


Tunaipongeza serikali kwa hatua hii muhimu ya kutekeleza agizo la chama. Tunaitaka serikali ikamilishe zoezi hili mapema iwezekanavyo ili nchi ifaidike na ufufuaji huu wa viwanda nchini.

 

2)         Changamoto kwa wakulima wa pamba


Katika ziara ya Katibu Mkuu mikoa kadhaa ya Kanda ya Ziwa, alitumia muda mrefu kujifunza na kuzungumza na wakulima wa zao la pamba wa mikoa hiyo. Pamoja na tatizo kubwa la soko na bei ya pamba, pamekuwa  na changamoto kubwa ya mfumo unaosimamia zao la pamba ikiwemo upatikanaji wa pembejeo.


Hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya kutengeneza nyuzi, nguo na kukamua mafuta ya pamba. Tulishuhudia ujenzi wa viwanda kadhaa mjini Shinyanga, vingi vikijengwa na wawekezaji kutoka China.

Lakini wakati wa Bunge la juzi, Serikali imeamua kutoa ruzuku ya asilimia hamsini kwa mbegu bora za pamba ili kuwawezesha wakulima kumudu bei ya mbegu hizo na hivyo kuboresha zao la pamba nchini na maisha ya wakulima kuwa bora zaidi.(bei ya dukani kwa kilo moja ni Sh. 1,200/=; Serikali italipia

Sh.600/=).

Katika hili la mbegu bora na kilimo cha mkataba tunaitaka Serikali na hasa wakuu wa wilaya na mkoa kuacha mara moja kutumia nguvu kuwalazimisha wakulima kulima kwa mkataba na kutumia mbegu bora badala yake wawaelimishe na kuwashawishi badala ya kutumia nguvu.

Tunaipongeza Serikali kwa kuanza kuchukua hatua za kutekeleza baadhi ya mapendekezo ya CCM ya namna ya kutatua matatizo yanayowakabili wakulima wa pamba nchini. Tunaitaka Serikali kuongeza kasi ya utatuaji wa changamoto hizo ili wakulima wa pamba wafaidike na uchumi wa nchi kukua kwa kasi nzuri.

3).        Migogoro kati ya wakulima, wafugaji na hifadhi juu ya matumizi ya   

ardhi

Katika ziara mbalimbali za Katibu Mkuu kwenye mikoa kama ya Morogoro, Njombe, Simiyu, Mara n.k. alishuhudia migogoro mingi sana juu ya wakulima, wafugaji na hifadhi  mbalimbali nchini. Hakuna shaka migogoro hiyo imegharimu sana maisha ya watu na mali zao na hata uchumi wa nchi yetu.

Chama kiliagiza migogoro hiyo kushughulikiwa mapema na kupata ufumbuzi wa kudumu. Chama kinalipongeza Bunge na hasa Wabunge wa CCM na Serikali yake kwa uamuzi wa kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza na kutoa

mapendekezo ya hatua kadhaa za kuchukuliwa katika kufikia suluhisho la kudumu kwa migogoro hii.


Tunawaomba wananchi watoe ushirikiano wa kutosha kwa kamati teule ya Bunge ili kazi hii ya kamati iwe na matokeo mazuri yatakayosaidia kumaliza tatizo hili nchini. Wakati Kamati teule ya Bunge ikifanya kazi yake, tunawaomba wakulima na wafugaji kote nchini kutulia kusubiri matokeo ya kamati hii teule ya Bunge.

Hivyo basi,  ziara hii ya Katibu Mkuu imelenga pamoja na mambo mengine kuimarisha Chama, kukagua Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kusikiliza kero za wananchi. Tumeona jinsi ziara zilizotangulia zilivyokuwa na matokeo mazuri, tunaamini ziara hii pia itakua na matokeo mazuri.

Imetolewa na:-

(Sgd.)
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

ITIKADI NA UENEZI

12/11/2013

Upendo Kilahiro ajinafasi Tamasha la Krismas!!

Upendo-Kilahiro

Na Mwandishi Wetu
BAADA ya msanii Upendo Nkone kuthibitisha kushiriki Tamasha la Krismas litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, msanii Upendo Kilahiro naye amejitosa kushiriki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamefikia makubaliano na msanii huyo na wanafurahi kwamba tamasha litaenda vile wanavyotaka.

“Kilahiro tutakuwa naye, naamini mwaka huu tamasha hili litakuwa bora zaidi kutokana na kushirikisha waimbaji wengi wakali.

“Mpaka sasa Watanzania wawili tumeshakubaliana nao, yaani Kilahiro na Upendo Nkone,” alisema Msama na kuongeza kuwa bado wanaendelea na mazungumzo na wasanii wengine wa nje na ndani ya nchi.
Baadhi ya nyimbo za msanii huyo ni Zindonga alioimba kwa Kizulu), Unajibu Maombi na Ni Salama Rohoni. Pia anatamba na albamu mbalimbali ikiwemo Ficho Langu.

Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.

Waandaaji hao wamepanga tamasha hilo lifanyike Desemba 25 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na siku inayofuata Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

DR.MVUNGI AFARIKI DUNIA LEO NCHINI AFRIKA KUSINI

RAISKIKWETERais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia na daktari wa zamu wakimwangalia Mjumbe wa Tume ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI)  Oktoba 3, 2013 kufuatia kujeruhiwa kwake na watu wanaosadikiwa ni majambazi usiku wa Jumamosi Oktoba 2, 2013.

(PICHA NA IKULU)

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA KITENGO CHA HABARI KATIKA MTANDAO WAKO WA www.fullshangweblog.com INADAIWA KUWA MJUMBE WA TUME YA KATIBA ALIYEJERUHIWA NA WATU WANAOSADIKIKA NI MAJAMBAZI USIKU WA JUMAMOSI OKTOBA 2 MWAKA HUU, DKT. SENGONDO MVUNGI , AMEFARIKI DUNIA LEO ALASIRI NCHINI AFRIKA KUSINI ALIPOKUWA AKITIBIWA.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI NA MBUNGE WA KUTEULIWA MHE. JAMES MBATIA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA KIFO HICHO CHA DKT. MVUNGI ALIYEWAHI KUWA KIONGOZI MKUBWA WA CHAMA HICHO.

KITENGO CHA HABARI KINAFUATILIA KWA KINA TAARIFA HIZO, TAFADHALI ENDELEA KUWA NASI.

CREW NZIMA YA MTANDAO HUU INATOA POLE KWA WATANZANIA WOTE WAKATI HUU WA MAJONZI.

MWENYEZI MUNGU AWAPE NGUVU.

AMINA

ITS YOUR GOLDEN CHANCE, DON`T PLAN TO MISS

NEW Prof_Dev_Centre logo

International Night

16th November 2013 at IIS grounds in Gangilonga, Iringa

entrance: 18,000 in advance; 20,000 at gate

children aged 3-12 8,000 in advance; 10,000 at gate

Music, Entertainment, International Foods, School Tours

Iringa International School is an authorized IB World School in the primary (IBPYP) and a Cambridge International School in the secondary, offering IGCSE and International A levels.

Limited spaces available for boarding/day students.

PO Box 912, Lumumba Street, Iringa

tel: 255 26 270-2018

email: iringainternational@gmail.com

website: iis.ac.tz

MKUTANO WA WADAU KUHUSU MIKATABA YA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA WAFANYIKA DAR ES SALAAM LEO

IMG_4175Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano wa wadau kuhusu mikataba ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma uliowahusisha watendaji wakuu wa taasisi za serikali ili kupata maoni yao jijini Dar es salaam leo. IMG_4206Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, na Mwenyekiti wa mkutano Bw. HAB Mkwizu akisikiliza mada wakati wa mkutano kuhusu mikataba ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma. IMG_4208Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Hassan Kitenge akiwasilisha mada wakati wa mkutano  wa wadau kuhusu mikataba ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma uliowahusisha watendaji wakuu wa taasisi za serikali ili kupata maoni yao jijini Dar es salaam leo. IMG_4185Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na sekretariati ya mkutano wa wadau kuhusu mikataba ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM NDUGU PHILIP MANGULA ZIARANI MKOANI RUKWA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Philip Mangula akifurahia jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kuwasili Mkoani Rukwa akitokea Katavi kwa ziara ya kichama hivi karibuni. Mheshimiwa Mangula atamaliza ziara yake leo tarehe 12 Novemba 2013 Mkoani Rukwa ambapo amefanya mikutano mbalimbali ya nje na ya ndani pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayoendeshwa na Chama cha Mapinduzi na Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta alipowasili Wilayani hapo hivi karibuni kwa ziara ya kichama ya siku nne Mkoani Rukwa.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula akipeana mikono na Mbunge wa Nkasi Kusini Ali Kessy maarufu kama Ali Mabodi katika ziara yake Wilayani Nkasi hivi karibuni.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa watatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Hiporatus Matete wa pili kushoto na Katibu wa CCM Mkoa wa rukwa wakifurahia mapokezi ya wananchi wa kijiji cha Kizi kilichopo Wilayani Nkasi waliokuwa wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula kwa ujio wake Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe wa pili kushoto na msafara wa viongozi wa Chama Tawala kutoka Mkoa wa Katavi wakiondoka katika viwanja vya Kizi baada ya kumuaga na kumkabidhi Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula kwa viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya ziara ya kichama Mkoani humo.

(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2014 IPUNGUZE VIFO VYA WAJAWAZITO

Baadhi ya wajawazito wakiwa wamepumzika wodini.ZAIDI ya Wanawake 8,700 hufariki duni kila mwaka nchini Tanzania kutokana na matatizo ya ujauzito na hasa wakati wa kujifungua. Takwimu hizi zinaonesha takribani wanawake 24 hupoteza maisha kila siku huku ikikadiriwa mmoja kufa kila baada ya saa moja.

Hata hivyo wataalamu wa afya wanasema moja kati ya sababu zinazochangia vifo hivi  ni kukosekana kwa huduma za dharura katika Vituo vya Afya wakati wa kujifungua. Hata hivyo Serikali ya Tanzania mwaka uliopita katika ahadi zake imeahidi kupunguza vifo hivi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015.

“Si sahihi mama mjamzito kufa wakati wa kujifungua au si sahihi mama huyu kupoteza uhai wake kwa kuugawa kwa kiumbe anachokileta duniani, hii haiwezi kukubalika. Na inasikitisha zaidi pale maisha ya mama huyu yanapotea hata kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika,” anasema Rais Kikwete katika hotuba yake mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (U.N) Ban Ki-moon.

Wewe pia unaweza kushiriki katika kupigania kutokomeza vifo hivi kwa akina mama wajawazito pamoja na watoto. Je, unataka kushiriki? Tafadhali fuata kielelezo/link hii hapa chini:-

http://www.change.org/petitions/the-government-of-the-republic-of-tanzania-save-women-and-newborns-lives-during-childbirth-by-properly-funding-emergency-obstetric-care-in-2014-budget-3?share_id=VqZSinjvFV&utm_source=share_petition&utm_medium=email&utm_campaign=petition_invitation 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index

WILAYA YA  MBEYA MJINI – AJALI YA  PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.

 

MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 10:45HRS HUKO  KATIKA ENEO LA SOKOMATOLA, KATA  YA  SOKOMATOLA,   TARAFA YA  SISIMBA,  JIJI NA MKOA WA MBEYA, BARABARA YA  SOKOMATOLA/STENDI KUU.  PIKIPIKI T.542 CLY AINA YA  SUNLG IKIENDESHWA NA FRANK S/O TEGETE, MIAKA 25, MNGONI, MKAZI WA MTAA WA MAJENGO, ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  ROMANUS S/O KYANDO, MIAKA 34,MKINGA,MKULIMA, MKAZI WA SOKOMATOLA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA  KUFIKISHWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA KWA MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  AJALI NA KUITELEKEZA PIKIPIKI  ENEO LA TUKIO.  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   MADEREVA KUWA MAKINI  WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

WILAYA YA  RUNGWE – TAARIFA YA  KIFO.

MNAMO TAREHE 11.11.2013  MAJIRA YA  SAA 18:45HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KILELO, KIJIJI CHA MASEBE,TARAFA YA  UKUKWE, WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA, ANYIMIKE S/O MWAKYAMBO,MIAKA 54,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA KALALO ALIKUTWA AMEFARIKI DUNIA NDANI YA  NYUMBA YAKE. CHANZO NI KUNYWA POMBE KUPITA KIASI NA KUTOKULA CHAKULA. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA TABIA YA  KUNYWA POMBE KUPITA KIASI KWANI  NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

Signed By:

[DIWANI ATHUMANI- ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Kizungumkuti cha amani kati ya M23 na DRC

DRC ilisusuia shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kutokana na maandiko yake

Shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu , iligonga mwamba.

Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.

Mpatanishi wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.

Hata hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi za upatanishi.

Kundi la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na Uganda.

Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo yatasainiwa. Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.

Serikali ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.

Duru zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.

MZIZIMA ROTARY CLUB YAMPA TUZO MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA (NHC)KWA UTENDAJI ULIOTUKUKA

1aRais wa Mzizima Rotary Club Bw. Ambrose Ntageki Nshala akikabidhi cheti maalum cha kutambua utendakazi na mchango wa Nehemia Mchechu Kyando Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) wakati Club hiyo ilipomkabidhi cheti na tuzo maalum katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam. 2aRais wa Mzizima Rotary Club Bw. Ambrose Ntageki Nshala akikabidhi tuzo  maalum ya kutambua utendakazi na mchango wa Nehemia Mchechu Kyando Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) wakati Club hiyo ilipomkabidhi cheti na tuzo maalum katika hafla iliyofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam. 3aKushoto ni Paul Mashauri na na wajumbe wengine wa Rotary Club wakimpigia makofi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando hayupo pichani mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo 4a Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando akitoa shukurani zake kwa Rais wa Rotary Club na wajumbe wake mara baada ya kukabidhiwa tuzio hiyo. kulia ni Rais wa Mzizima Rotary Club Bw. Ambrose Ntageki Nshala. 5aMkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando akizungumza jambo na Paul Mashauri Mwenyekiti wa  East Africa Speakers Bureau (EASB) na katikati ni Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC , Muungano Kasibi Saguya 6aMkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Mzizima Rotary Club Bw. Ambrose Ntageki Nshala mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo jana 7aMkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu kushoto  akiwa katika picha ya pamoja na Paul Mashauri Mwenyekiti wa  East Africa Speakers Bureau (EASB) 8aBaadhi ya wajumbe wa Rotary Club Mzizima wakiwa katika hafla hiyo 9aBaadhi ya wajumbe wa Rotary Club Mzizima wakiwa katika hafla hiyo 10aBaadhi ya wajumbe wa Rotary Club Mzizima wakiwa katika hafla hiyo 11a Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC , Muungano Kasibi Saguya kushoto akiwa na
Yahya Charahani ambaye ni Meneja Mawasiliano wa NHC wakiwa katika hafla hiyo jana

12aMzee Method Kashonda mmoja wa viongozi wa Mzizima Rotary Club akikaa kwenye kiti chake mara baada ya kusoma wasifu wa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Bw. Nehemia Kyando Mchechu jana kabla ya kumkabidhi tuzo yake aliyokabidhiwa na taasisi hiyo kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam jana.

VIJANA MKOANI KILIMANJARO WAHIMIZWA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MILENIA

IMG_3534Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungmza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro juu ya umuhimu wa kujihusisha na kazi za Umoja wa Mataifa wakati wa ziara za kutembelea shule mbalimbali za mkoa huo.

Na. Mwandishi wetu.

Vijana wa shule za sekondari nchini wameaswa kuwa mabalozi wazuri pindi watakapomaliza masomo yao juu ya kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya milenia kwa sababu ni dira ya maendelo ya taifa na dunia kwa ujumla.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho, Lyamungo na Umbwe sekondari hivi karibuni, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema malengo ya milenia yanagusa Nyanja zote za maendelo kwa vijana walio na wasio mashuleni.

Bi. Nkhoma amewataka wanafunzi wafanye kazi za kujitolea na kuhakikisha wanapeleka elimu waliopata kupitia vilabu vya Umoja wa Mataifa kwa jamii na kuhamasisha dhana ya kujitolea kwa maslahi ya nchi.

“kila ndani ya saa moja tuna vijana 50 ambao wanapata maambukizi ya VVU kati ya miaka 14-24 ambao wengi kati ya hao ni Wasichana, hivyo msijihusishe na masuala ya mapenzi mnapokuwa mashuleni”, amesema Bi. Nkhoma.

IMG_3558Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha takwimu za Mimba za Utotoni zilizotolewa hivi karibuni (“Young People Today. Time to Act Now”) ambapo asilimia 25 ya watoto wa kike chini ya miaka 14 wanapata wakiwa mashuleni.

IMG_3550Pichani juu na chini ni vijana wa shule ya Sekondari Umbwe wakifuatilia kwa umakini mjadala wa masuala ya Umoja wa Mataifa uliiongozwa na Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).

IMG_3544

IMG_3574Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser akifafanua jambo kwa vijana waliojiunga na klabu za Umoja wa Mataifa shuleni hapo juu ya umuhimu wa kuwa na cheti cha klabu ya Umoja wa Mataifa

IMG_3586Msafara wa wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakitazama baadhi ya kazi mbalimbali zinazofanywa na klabu ya Umoja wa Mataifa katika shule ya sekondari Umbwe ikiwemo shughuli za kuchangia damu, kusafisha mazingira na mengineyo yajihusishayo moja kwa moja na shughuli za jamii.

IMG_3630“Ubovu wa miundombinu ni changamoto kubwa kwa ziara yetu lakini ujumbe wa shughuli za Umoja wa Mataifa lazima ziwafikie walengwa”.

IMG_3679Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifurahia uwepo wake mbele ya wanafunzi wa Kibosho Girls shule ambayo binafsi alisoma miaka 20 iliyopita, ambapo pia ujio wake ulikuwa chachu na hamasa kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.

IMG_3666Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibosho wakimsikiliza kwa makini Bi. Usia Nkhoma Ledama.

IMG_3692Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwasisitizia wasichana wa shule ya Kibosho juu ya umuhimu wa kujiamini na kujitambua wakati wa maamuzi yao binafsi.

IMG_3738Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa.

KIUNGO MATATA STEVEN MAZANDA: MAANDALIZI YA MAPEMA YAMETUPA MAFANIKIO, NAPENDA VIJANA WANAVYOCHEZA SOKA KWA SASA!!

kikosiKiungo jembe wa Mbeya City FC, Steven Mazanda (waliosimama, wapili kulia) amesema hawana presha na kasi ya timu pinzani, mzunguko wa pili wako fiti balaa!

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam

Kiungo wa Mbeya City, Steven Mazanda, amesema siri ya mafanikio ya kikosi chao katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika novemba 7 mwa huu na klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tatu kwa pointi 27 sawa na Azam fc katika nafasi ya pili ni maandalizi ya mapema waliyofanya pamoja na nidhamu kubwa ya wachezaji kuanzia uwanjani na nje ya uwanja.

“Unajua sisi tulijiandaa mapema sana, na ndio maana unaona kikosi kinacheza kitimu na kila mtu anavutiwa. Kiukweli kumekuwepo na changamoto za ushindani, lakini tunaingia katka kila mechi kuhitaji ushindi”. Alisema Mazanda.

Mazanda ambaye  amewahi kuzichezea timu za Tukuyu, Simba, Mtibwa na Kagera Sugar, kabla ya kuisaidia Mbeya City kupanda daraja ameongeza kuwa mzunguko wa pili hakika utakuwa mgumu kwao kwani timu nyingi zinajipanga kujiweka sawa katika msimamo.

“Kuna timu zitakuwa zinawania nafasi ya ubingwa, nyingine nafasi za katikati, wakati hatari zaidi itakuwa mkiani ambao klabu zitakuwa zinawania kukwepa mkasi wa kushuka daraja. Sisi tuko tayari kwa kupambana na hiyo ndiyo kazi yetu”. Alisema Mazanda.

 Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba, kupanda na kushambulia pia, ni mpigaji faulo mzuri amekiri kuwa vijana wamekuwa wakicheza soka safi sana na kuonesha juhudi zao, lakini kwa yeye aliyecheza soka kwa muda mrefu huwa hawampi  presha akiwa dimbani.

“Nafurahi sana kuona changamoto kubwa ya vijana wakiwa uwanjani, timu zote zinazotumia damu changa zinafanya vizuri sana, kiukweli hawa makinda wapewe nafasi ili sisi wakongwe tuwaoneshe jinsi mpira unavyochezwa”. Alisema Mazanda.

Mazanda alisema kwa sasa kazi yao ni moja tu ambayo ni kujiandaa kwa mzunguko wa pili na lazima kieleweke.

“Tulivyoanza, watu walisema nguvu ya soda, nadhani hata wewe mwenyewe ulisikia, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele, tulipata nguvu zaidi. Sasa ahadi yetu ni kuonesha soka la uhakika”. Alisema Mazanda.

Ingawa umri umeenda lakini uzoefu unaonesha kuwa  viungo huwa bora kwa jinsi umri unavyoenda.

Hatua hii ya Kenya itaiimarisha EAC

membe_aminaWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bernard Membe akimsindikiza  mgeni wake Waziri mwenza wa Kenya, Amina Mohammed baada ya waziri huyo kumaliza  kuzungumza na waandishi wa habari Dar Salaam.

PICHA|EMMANUEL HERMAN 

Bila shaka hakuna Mtanzania hata mmoja ambaye hakuipongeza hatua ya Serikali ya Kenya kutuma ujumbe wa kuunga mkono msimamo wa Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), licha ya nchi za Uganda, Kenya na Rwanda kufanya mikutano kujadili mipango na masuala yanayohusu jumuiya hiyo pasipo kuihusisha Tanzania, kinyume kabisa na Mkataba wa Jumuiya hiyo.

Tanzania ilipinga kwa nguvu zote hatua ya nchi hizo kuitenga hata katika masuala yaliyo chini ya jumuiya hiyo, ambayo kwa mujibu wa mkataba huo yanapaswa kujadiliwa na kutekelezwa kwa pamoja na nchi zote wanachama. Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulihutubia Bunge wiki iliyopita na kuelezea kwa kirefu ukiukwaji wa mkataba huo na athari za kuzitenga Burundi na Tanzania katika mikutano inayojadili masuala ya EAC.

Pamoja na kuzikosoa na kuzilaumu vikali nchi hizo tatu kwa kukiuka mkataba huo pamoja na itifaki zake mbalimbali, Rais Kikwete aliweka wazi msimamo kwamba Tanzania kamwe haitajitoa katika Jumuiya hiyo na itaendelea kuwa mshirika mwaminifu wa Jumuiya hiyo pasipo kutetereka. Msimamo huo bila shaka uliondoa hofu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wananchi katika nchi zote wanachama wa EAC, kwamba Tanzania ingejitoa katika Jumuiya hiyo kutokana na kutengwa na nchi hizo tatu zilizokuwa zikiunda kile kilichoitwa ‘Coalition of the willing’ (Ushirikiano wa wenye hiari).

Hotuba ya Rais Kikwete ilifikisha ujumbe kule kulikotarajiwa. Ikiwa ni siku nne baada ya Rais kulihutubia Bunge akilalamikia nchi hizo kuitenga Tanzania, Kenya imemtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, Amina Mohamed kuja hapa nchini kuwasilisha ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta kwamba nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania kwa kutambua umuhimu wake kama moja ya waanzilishi wa Jumuiya hiyo. Waziri huyo alisema kuwa, kuja kwake hapa nchini kunafuatia Serikali ya Kenya kusoma kwa undani hotuba ya Rais Kikwete ambayo alisema, ilikuwa nzuri na ilitolewa kwa nia njema tu ya kuimarisha Jumuiya hiyo na siyo kuidhoofisha.

Sisi tunadhani hatua ya Kenya ya kutafuta maridhiano na Tanzania ni ya kupongeza, hasa tukitilia maanani ukweli kwamba moja ya sababu kubwa zilizosababisha kuvunjika kwa EAC mwaka 1977 ilikuwa ni kutokuwapo utamaduni wa nchi wanachama kujikosoa na kuona umuhimu wa kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo. Hatua hiyo ya Kenya yafaa iwe mfano kwa nchi nyingine ndani ya Jumuiya hiyo, kwamba zijisahihishe pale zinapojiridhisha kwamba zimekosea hapa au pale.

Hapa hatuna maana kwamba Tanzania haikuchangia lolote katika kufikiwa kwa hali hiyo ya kutengwa. Kwa mfano, mbali na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi imekuwa ikilalamikiwa na nchi nyingi jirani zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam. Yamekuwapo malalamiko mengi na ya muda mrefu kuhusu ucheleweshaji wa kupakua na kupakia shehena za mizigo, ukubwa wa tozo za bandari na barabara pamoja na uchakachuaji wa mafuta. Ndiyo maana baadhi ya nchi hizo zimeamua kutumia Bandari ya Mombasa.

Ni matumaini yetu kwamba nchi wanachama wa EAC zitachukulia mvutano uliokuwapo kati yao na Tanzania kama changamoto ya kuzisukuma kushirikiana zaidi ili kujenga Jumuiya yenye nguvu kubwa kiuchumi. Wakati huohuo, hatua hiyo ya Kenya ni ya kijasiri, siyo udhaifu.

CHANZO: MWANANCHI

CP SULEIMAN KOVA AKIONESHA MAPANGA YALIYOTUMIKA KUMSHAMBULIA DR. MVUNGI

SONY DSCKamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna (CP), Suleiman Kova (kulia), akionesha mapanga kwa waandishi wa habari na mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto), Dar es Salaam jana, yaliyotumika kumshambulia Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Dk.Sengondo Mvungi wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa tisa walioshiriki katika tukio hilo.

(Picha na Philemon Solomon wa Fullshangwe Dar es Salaam)

MASHINDANO YA VIJANA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KURINDIMA DEC 13 JIJINI ARUSHA!!

_MG_3798

Mahmoud Ahmad Arusha
Mashindano ya vijana waliochini ya miaka 18 kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki yanatarajiwa kuanza kurindima kwenye viwanja vinne jijini hapa kuanzia desemba 13 hadi 15 na kuzishirikisha zaidi ya timu 30 zitakazoumana kwenye mashiondano hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mratibu wa mashindano hayo kutoka Future Stars, Alfred Itael alisema mashindano hayo yajulikanayo kama Chipukizi Cup na kuzishirikisha nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki za Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi na wenyeji Tanzania.
Itael alisema kuwa hadi sasa ni nchi tatu zimethibitisha kushiriki mashindano hayo kwa kuleta vilabu vya vijana kuja kushiriki na kuzitaja nchi hizo kuwa ni wenyeji Tanzania,Uganda na Kenya na mashindano hayo yanatajiwa kuanza kutimua vumbi Tarehe 13 mwezi December.
Alifafanua kuwa timu shiriki zitakuwa na vijana kuanzia miaka 10-18 huku akiwataka nchi ambazo hazijatihitisha kufanya hivyo kabla ya November 20 Huku akibainisha kuwa timu za wanawake zitakuwa na vijana kuanzia umri wa miaka 14-18.
Aidha alisema Itael kuwa mashindano hayo yatakuwa ya mzunguko katika hatua ya awali na hatua ya pili itakuwa ni mtoano hadi kumpata mshindi atakayepewa kombe na huku mchezaji bora na mfungaji wakipata Medali.
Itael alitoa wito kwa wadau na watototo hasa vijana kujitokeza kuja kuonyesha vipaji na kujionea vipaji vya soka na kuwataka wadhamini mbalimbali kutoka katika mashirika mbali mbali kujitokeza kudhamini michezo hiyo ilikuweza kufanikisha kwani michezo inagharama nyingi na zinahitaji kusaidiana.
Mgeni rasmi kwenye mashindano hayo atakuwa Kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa Stars ambaye ni balozi wa Future Stars Kim Poulsen ambaye pia atakuja kuangalia vipaji mbali mbali vya vijana watakaojitokeza kwenye mashindano hayo huku akiwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ya kuonyesha vipaji ili waweze kupata nafasi ya kuitumikia timu zao za taifa.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAJAMBAZI 8

[DIWANI ATHUMANI- ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

 “PRESS RELEASE” TAREHE 11.11. 2013.

      WILAYA YA MBEYA MJINI – MWILI WA MTUHUMIWA  ALIYEFARIKI DUNIA
AKIWA NA MADAWA YADHANIWAYO   

                                                          KUWA  YA  KULEVYA WATAMBULIWA                                 

                                                         NA KUKABIDHIWA  KWA NDUGU.

§  MNAMO TAREHE 11.11.2013 MAJIRA YA  SAA 14:10HRS HUKO KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA. JESHI LA POLISI LILIWAKABIDHI MWILI WA MAREHEMU KASSIM S/O SAIDI MBOYA NDUGU ZAKE WAWILI AMBAO NI BABA WA MAREHEMU AITWAE SAID S/O ATHUMANI MBOYA, MIAKA 60, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA – MCHANGANI – DSM NA MDOGO WAKE NA MAREHEMU AITWAE HASSAN S/O SAID MBOYA, MIAKA 28, MPOGORO, TINGO KAMPUNI YA  MOHAMED ENTERPRISES DSM, MKAZI WA MWANANYAMALA MCHANGANI –DSM.

§  BAADA YA UTAMBUZI NDUGU HAO WA MAREHEMU WAMEMUELEZEA MAREHEMU NDUGU YAO KUWA  ALIKUWA  ANAITWA KASSIM S/O SAIDI MBOYA, MIAKA 36, MPOGORO, MKULIMA, MKAZI WA MWANANYAMALA-MCHANGANI –DSM. 

§  AWALI MNAMO TAREHE 07.11.2013 MAJIRA YA SAA 11: 00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. KASSIM S/O SAIDI MBOYA, ALIFARIKI DUNIA AKIWA KATIKA TARATIBU ZA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.

§  MAREHEMU ALIKUWA ANASAFIRI KUTOKA DSM KUELEKEA LILONGWE NCHINI MALAWI AKIWA KATIKAM BASI LA TAQWA LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.319 BLZ AINA YA NISSAN AKIWA NA HATI YA KUSAFIRIA NAMBA – AB 051010 PIA AKIWA NA BEGI DOGO LENYE SURUALI MOJA AINA YA JEANS, T-SHIRT MOJA NYEUSI, RABA JOZI MOJA RANGI NYEKUNDU, MKATE MMOJA, MKOBA MDOGO WA KIUNONI, VACCINATION CARD MBILI ZA KINGA YA UGONJWA WA MANJANO, RAND MBILI SARAFU ZA AFRIKA YA KUSINI NA MIFUKO SITA [06] YA RAMBO RANGI NYEUSI.

§   BASI HILO BAADA YA  KUFIKA MPAKANI KASUMULU NA ABIRIA KUSHUKA KUTOKA KWENYE GARI HILO NA KUANZA KUFANYA TARATIBU ZA  KUVUKA MPAKA KUINGIA NCHINI MALAWI, MAREHEMU ALIBAKI NDANI YA  GARI HUKU HALI YAKE YA  KIAFYA IKIZIDI KUDHOOFIKA. 

§  WAHUSIKA WA GARI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI AMBAPO MAREHEMU ALICHUKULIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA  WILAYA YA  KYELA KWA MATIBABU. HATA HIVYO KABLA HAJAPATA MATIBABU ALIFARIKI DUNIA. 

§  MWILI WA MAREHEMU ULISAFIRISHWA HADI HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA NA KUFANYIWA UPASUAJI AMBAPO ZILIPATIKANA PIPI 65 ZA DAWA ZIDHANIWAZO KUWA ZA KULEVYA ZIKIWA TUMBONI KWA MAREHEMU NA MOJA KATI YA  PIPI HIZO IKIWA IMEPASUKA,  PIPI HIZO ZINA UZITO WA KILO 1 NA GRAM 140.TARATIBU ZINAFANYWA ILI DAWA HIZO ZIPELEKWE OFISI YA  MKEMIA MKUU WA SERIKALI KWA UCHUNGUZI WA KITAALAM IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA AINA YA MADAWA HAYO.

§  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI  KINYUME CHA SHERIA, NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI PIA INAPUNGUZA NGUVU KAZI YA TAIFA.

Signed by:

[DIWANI ATHUMANI- ACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

DCI Robert Manumba amestaafu kwa mujibu wa sheria

 

Advera-SensoTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

DAR ES SALAAM NOVEMBER 11, 2013.

  Jeshi la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa  Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa kustaafu kisheria  ambao ni miaka sitini (60) katika utendani wake wa kazi.

Aidha, katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka (1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam, (1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam   (1987 – 1993),

Pia, amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995),  Mkufunzi mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 – 2001) na kuwa  msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini (2001 – 2006). Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu, alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.

Aidha, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na kumpongeza (DCI) Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa weledi na uwaminifu mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.

  Pia, amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza kusaidia kupunguza uhalifu hapa nchini kwasababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.

  Hata hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa upulelezi ukiendelea,  mkuu wa ufuatiliaji na tathimini CID makao makuu,  kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo.  

Imetolewa na:-

Advera Senso – SSP

Msemaji wa Jeshi la Polisi.

KATIBU MKUU WA NISHATI NA MADINI ELIAKIM MASWI AFANYA ZIARA KWENYE MRADI WA BOMBA LA GESI MKOANI LINDI

Picha Na. 1Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akisalimiana na wafanyakazi wa mradi wa bomba la gesi huko Kilwa.Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Eliakim Maswi alifanya ziara kwenye mradi wa bomba la gesi katika mikoa ya Lindi na Mtwara  mwishoni mwa wiki. Picha Na. 2Mtaalamu mwelekezi kutoka katika kampuni ya Worley Parsons,  Pieter Erasmus akitoa maelezo  kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na M adini, Eliakim Maswi jinsi uunganishaji wa bomba la gesi unavyofanyika. Picha Na. 3Wafanyakazi  wakiendelea na kazi ya uchomeaji wa bomba la gesi. Picha Na. 4Kazi ya uunganishaji wa bomba la gesi  ikiendelea Picha Na. 5Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa bomba la gesi ikiwa ni pamoja na ukamilishwaji wake

CECAFA Challenge Cup Referees named

images

The Council of East and Central Africa Football Associations (CECAFA) has this Monday released a list of 18 referees who will travel to Nairobi to handle this year’s Challenge Cup matches.

The list released by the CECAFA Secretary General Nicholas Musonye has nine (9) referees and nine (9) assistants. All these referees will however be subjected to fitness and medical tests on arrival in Nairobi before the tournament officially kicks off, November 27.

The Referees are:

 1. Anthony Okwayo-Kenya
 2. Denis Batte-Uganda
 3. Wish Yabarow– Somalia
 4. Israel Mujuni– Tanzania
 5. Louis Hakizimana– Rwanda
 6. ThieryNkurunziza– Burundi
 7. WaziriSheha– Zanzibar
 8. GebremichaelLuleseged– Eritrea
 9. KheiralaMurtaz – Sudan

Assistant Referees

 1. Gilbert Cheruiyot– Kenya
 2. TonnyKidiya– Kenya
 3. Mark sonko– Uganda
 4. FedinardChacha– Tanzania
 5. Suleiman Bashir- Somalia
 6. Fraser Zakara-South Sudan
 7. SimbaHonore-Rwanda
 8. Hamid Idam– Sudan
 9. KinfeYimla-Ethiopia

Regards

ROGERS MULINDWA

CECAFA MEDIA MANAGER