RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA PAMOJA NA KUFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA WODI YA WAZAZI YA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

2Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.

3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona wagonjwa wao.

4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili akitokea Dodoma.

5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero zao ndani ya muda mfupi ujao.

PICHA NA IKULU

…………………………………………………………………………………………….

IMG-20160210-WA0044

KPMG yawa kinara kundi lao katika michuano ya Awesome Bonanza 2016

Kikosi cha timu ya KPMG  Waliosimama kutoka kushoto ni
Isyaka,Bakari,Isaya, Nsanyiwa,Hamza(kocha),Getrude(kiongozi wa timu) na
Jovin.  Walioinama kutoka kushoto ni  Evans, Denis, Jamal, Thobias, Frank, Ahmed na Amiri.    Aliyelala ni Jim aka Messi wa
KPMG katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo
michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine

 

 Kikosi cha wachezaji wa Kampuni ya KPMG katika picha ya pamoja katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine

 

 Wachezaji wa timu ya KPMG wakiwa mapumziko kutoka kushoto walioangalia mbele Bakari , Dennis, hamza (kocha mchezaji) na isyaka katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine

 

Wachezaji wa timu ya KPMG wakishangilia Goli dhidi ya Timu ya Deloitte katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine

 

Wachezaji wa KPMG wakishangilia Goli lilifungwa na mshambuliaji wao machachari Daudi Mbaga dhidi ya  timu ya PWC katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine

 

 Kiungo wa Timu ya KPMG Bakari Mkupe akiwania mpira na wachezaji wa Timu ya PWC.katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
Wafanyakazi  wa kampuni ya KPMG waliokuja kushangilia wenzao  kutoka kushoto ni Asha, Mumtaz,Lilian, Witness, Getrude, patricia, desire na Grace.katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome
magazine

………………………………………………………………

                                     Na Krantz Mwantepele,Dar es salaam                                                                                              

Timu ya mpira wa miguu ya kampuni ya uhasibu ya KPMG ilishiriki michuano ya Awesome Bonanza siku ya
Jumamosi tarehe 6-Feb 2016 na kuibuka kinara katika kundi lao lililohusisha
timu nyingine za makampuni yanayohusika na uhasibu pia.
 Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na Jarida la
kila mwezi la Awesome magazine ilianza siku ya jumamosi tarehe 6 feb 2016
ikifanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Park vilivyopo maeneo ya Mnazi
Mmoja zamani kidongo chekundu kwa hatua za Makundi kwa kundi la timu kutoka
kampuni  za uhasibu.
Katika kundi hilo zilikuwepo timu kutoka kampuni za uhasibu za Deloitte, PWC na Innovex.
Timu ya kampuni ya  KPMG iliibuka kinara wa kundi hilo kwa kupata
ushindi katika mechi zao zote. KPMG ilipata matokeo yafuatayo: KPMG 3-1 PWC,
KPMG 4-1 Deloitte , KPMG 2-1 Innovex. Hivyo kuwafanya wasonge mbele katika
micuano hiyo itakayoendelea mwezi huu.
Wafungaji wa magoli ya
KPMG walikuwa
Jim Mwasigala (3)
Bakari Mkupe (2)
Frank Mboya (2)
Ahmed Mohammed
Daudi Mbaga
Akiongea baada ya mechi
hizo kocha mchezaji wa timu ya KPMG, Hamza Mzee amesema ya kwamba timu kampuni
ya KPMG imejiandaa vyema na wana uhakika wa kushinda michuano hiyo kwa kuwa
wanajali utamaduni wa kufanya mazoezi kupitia michezo kwa kuwa huboresha Afya
kwa ujumla.

TANZANIA KUANZA NA SHELISHELI U-17

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetoa ratiba ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Serengeti Boys) kuanza na Shelisheli.

Katika ratiba hiyo iliyotolewa makao makuu ya CAF, Cairo Misri na nakala yake kutumwa kwa TFF, Tanzania imepangwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Shelisheli kati ya Juni 24,25,26 nchini na marudaino kuchezwa Julai 01,02,03 nchini Shelisheli.

Mshindi kati ya mchezo huo namba 15 na16 atacheza dhdi ya timu ya Taifa ya  Afrika Kusini katika hatua inayofuata ya 16 bora, na kisha baadae kupata timu 8 zitakazofuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika nchini Madagascar mwakani.

Fainali za Kombe la Dunia (FIFA U17) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwezi Septemba waka 2017 nchini India.

HAICHOSHI MASIKIONI. HII NI NGOMA MPYA KUTOKA KWA MSANII BITTO KITUKUU.

Katika anga la Muziki wa Hip Hop nchini Tz, imedondoshwa ngoma mpya kutoka kwa Msanii Bitto Kitukuu. Ngoma inaitwa “Wapekee”. Ni ngoma tamu na isiyochosha kusikiliza masikioni.
 
Mimi binafsi nimebaini kwamba, ukianza kuisikiliza ngoma hiyo, huwa unatamani uirudie mara kwa mara na uzuri wake ni pale inaponoga zaidi ikifika mwishoni na hivyo kutamani kuisikiliza tena.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUISIKILIZA

Na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AZUNGUMZA NA WADAU WA SEKTA BINAFSI LEO MCHANA WIZARANI

ME1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Reginald Mengi (kulia), wakati akisisitiza jambo katika mkutano na  wadau wa Sekta Binafsi uliofanyika Wizarani hapo jijini Dar es Salaam.

ME2

Mdau wa sekta binafsi, Bw. Otieno Igogo (mwenye koti la mistari),  akisisitiza jambo wakati wa Mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta binafsi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

ME3

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa  akimsikiliza kwa makini Rais wa Wakala wa Forodha ya Tanzania (TAFFA), Bw. Steven Ngatunga wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Wadau wa sekta binafsi.

ME4

Wadau wa sekta binafsi wakijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika mkutano wao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

ME5

Mdau wa sekta binafsi Bw. Felix Mosha (wa kwanza kulia) akifafanua jambo katika mkutano wa wadau hao. (Kushoto) ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Reginald Mengi.

Wazazi Kisarawe wafunguka kuhusu adhabu kwa watoto

 Joseph Olowa akiiomba kampuni ya True Vision kusaidia kuelimisha watu wenye lugha za matusi hadharani  hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
  Mtoto akionesha jeraha alilopata baada ya kuchapwa na baba yake alipokuwa mdogo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Mkazi wa kisarawe  Juma Athumani akitoa ushuhuda wa adhabu ya kufukuza watoto nyumbani  hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.
Cornel Anatory akielezea alivyomwagiwa maji ya ugali utotoni   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Hamisi Idd akihamamisha wazazi kuwapa watoto elimu ya dini tangu utotoni ili kuepuka tabia mbaya hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Jamila Shabani akisema kuwa moja ya adhabu wanayopewa watoto ni kuchapwa fimbo    hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Kimela Billa Mtayarishaji wa vipindi vya Walinde Watoto akikabidhi Redio kwa Bi. Mwashamba Mrisho ambae ni mtendaji kata wa kata ya Kibo   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Kikundi cha Kisarawe Bomani maarufu kama Kibo katika picha ya pamoja baada ya kupata redio kutoka True Vision hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Kikundi cha Tushirikiane cha Kisarawe wakijadiliana baada ya kupewa Redio na True Vision ili kufuatilia vipindi vya Walinde Watoto hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Na Krantz Mwantepele , Kisarawe 

Watanzania wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga urafiki nao ili kuwawekea
misingi bora ya nidhamu na upendo. Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wazazi na
walezi kutoka wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani hivi karibuni wakati wa mdahalo
maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision
production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.
 
Katika mdahalo huo mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo athari za kuchapa watoto,
matusi pamoja na adhabu kali kwa watoto mfano kuwafukuza watoto nyumbani.
 
Aidha washiriki wa mdahalo huo walionyesha kusikitishwa na vitendo vya kuchapa watoto
fimbo kupita kiasi na wengine wakikemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi
kutukana watoto pasipo kuzingatia maadili huku wakiiomba serikali kuwawajibisha
wale wote wanaotukana hadharani bila kujali uwepo wa watoto.
 
Katika hatua nyingine, washiriki hao walikemea tabia ya kuwafukuza watoto nyumbani na
kudai kuwa huo ni mwanzo wa kuwaingiza watoto katika matatizo makubwa na
kuongeza idadi ya watoto wa mitaani aidha wamependekeza kuwa ni vyema watoto
wafanyiwe maombi mara kwa mara na kuwashirikisha katika Ibada ili kuwaepusha
kuwa na utovu wa nidhamu.
 Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Kibasila Kisarawe ambao walipata nafasi
ya kuongea na timu ya Walinde Watoto walionyesha kuchukizwa na tabia ya kupewa
adhabu kupita kiasi pamoja na kutukanwa tabia ambayo hufanywa na baadhi ya
walimu na wazazi.
 Naye mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibasila Kisarawe Debora Mbalilaki
alipendekeza kuangalia uwezekano wa kuwepo na adhabu mbadala badala ya fimbo
kwa wanafunzi.

Barabara ya Mugumu Serengeti kukamilika Mwezi Mei.

SE

Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO

………………………………………………………………

Barabara ya Mji wa Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara inatarajiwa kukamilika mwezi Mei baada ya kushindwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa.

Akiongea kwa njia ya simu leo,Afisa Habari Wilaya ya Serengeti Englibert Thomas Kayombo amesema kuwa, Barabara hiyo ilitakiwa kukamilika Januari 6 lakini kutokana na changamoto mbalimbali barabara hiyo haikuweza kukamilika kwa wakati.

“Ujenzi wa barabara una hatua mbali mbali ambazo zinafanywa kabla ya hatua ya mwisho ya kuweka lami, ikiwemo uchimbaji wa mitaro na kuondoa miundo mbinu yote iliyo katika barabara”Alisema Kayombo

Amezitaja baadhi ya changamoto hizo ni kuwepo mabomba ya maji na  nguzo za umeme yaliyopita katika barabara inayotarajiwa kuwekwa lami hivyo shughuli zilisimama ili kupisha zoezi la kuhamisha mabomba na nguzo hizo pia hali ya hewa, ya Mji wa Mugumu hupata mvua kubwa zinazonyesha kwa kipindi cha muda mrefu hivyo kupelekea zoezi la ujenzi wa barabara kwenda kwa taratibu.

Ameongeza kuwa,kutokana na changamoto hizo ujenzi wa barabara ya lami katika Mji wa Mugumu Serengeti ulisimama kwa muda hivyo mkandarasi ameongezewa muda hadi mwezi Mei 2016 ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo.

Katika mwaka wa fedha 2014/15 Serikali ilitenga bajeti ya ujenzi wa barabara ya Mji wa Mugumu yenye kilomita 3 kwa kiwango cha lami na kazi hiyo iko chini ya Kampuni ya SAMOTA Ltd.

KATIBU WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MANISPAA YA SONGEA (SUFA) KELVIN HAULE MBARONI KWA KUUZA TIKETI FEKI

Balozi wa Japan nchini Tanzania akabidhi gari ya huduma ya dharura kwa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu

1

Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakikata utepe  wakati balozi huyo alipokabidhi gari la Ambulance kwa Waziri Ummy Mwalimu  kwa ajili ya kituo hicho.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

2

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akijaribu kuwasha gari hilo la kubebea wagonjwa lililotolewa kwa kituo hicho.

3

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba kulia na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele.

4

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ,  Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba pamoja na viongozi mbalimbali wa Kituo cha kuratibu matukio ya Sumu  nchini na Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa makabidhiano hayo.

……………………………………………………………………………………………

Na Beatrice Lyimo-Maelezo

Dae es Salaam

Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba amekabidhi Gari la huduma ya dharura (AMBULANCE) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchini kilichopo chini ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Balozi huyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu sambamba na kuzindua Cheti cha Ithibati cha kuitambulisha Maabara hiyo kimataifa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo Balozi Yoshiba amesema kuwa Jumuiya ya Zimamoto ya nchini Japan imetoa magari 83 kwa Tanzania ikiwemo magari 10 ya huduma ya dharura kwa nia njema na pia kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Nchi ya Japani.

Amesema Jumuiya hiyo ilianza kutoa magari hayo tangu mwaka 2006 na kuahidi kuendeleza uhusiano huo wa kirafiki wenye manufaa kati ya Tanzania na Japani.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa makabidhiano ya gari hilo yameleta hamasa kwa upande wa Wakala na Wadau wengine katika kukabiliana na matukio ya Sumu nchini.

“Ili Taasisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi uwepo wa miundo mbinu kama vifaa ikiwemo mitambo, vitendea kazi kama vile magari na majengo bora ni suala ambalo halina budi kupewa kipaumbele”alisema Waziri Ummy.

Pia Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa majukumu yanayotekelezwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kulinda afya, mazingira  na usalama kwa watu na hivyo kuleta utengemano katika jamii.

Aidha, Waziri Ummy amezindua cheti cha Ithibati chenye namba ISO 1705:2005 kinachoitambulisha maabara ya Mkemia Mkuu kimataifa.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa agizo kwa Wakala wa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa kipaumbele suala la Madaya ya Kulevya kwa kuwapima watoto haswa wa shule za msingi na sekondari ili kuweza kupambana na janga hilo.

Serikali yabaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 ATCL

images (1)

Na Lorietha Laurence-Maelezo

……………………………..

Serikali imebaini wizi wa  takribani  shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa  wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali  imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi  cha polisi  kitengo cha usalama mtandaoni  ili kubaini mtandao mzima uliohusika  ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa  shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya  kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

 Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa  njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

WAFNYABIASHARA WAULALAMIKIA UONGOZI WA KATA YAO

download

Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
………………………………………….
WAFANYABIASHARA katika eneo la soko mjinga jijini Arusha wameulalamikia uongozi wa kata yao ya Sinoni kwa kuwatelekeza na kuwasababishia hasara kutokana na kulipa michango isiyo na tija ambayo inawatia hasara mara kwa mara kutokana na kutopata faida yeyote.
Wameyasema hayo walipozungumza na Mwangaza FM leo hii kutokana na kukithira kwa michango mingi sokoni hapo ambayo imekuwa ni kero kubwa kwao na hasa ukizingatia wanalipa ushuru kama kawaida lakini wanadaiwa tena michango mingine.
Wameongeza kuwa wao wanalipa ushuru kama inavyotakiwa na serikali lakini kinachowashangaza ni pale wanapoambiwa wachange michango ya takataka na mlinzi wakati nyumbani wanapotoka wanalipia taka sasa wanajiuliza wanalipia taka mara ngapi? walihoji’
Kituo hiki kimemafuta Diwani wa kata ya Sinoni Godfrey Simbile ili ajibu tuhuma zinazomkabili yeye na uongozi wa kata hiyo lakini alidai yuko kwenye kikao na angeweza kutoa jibu la kueleweka kama atapata muda wa kutosha.
Pamoja na juhudi hizo lakini inasemekana Diwani huyo amekuwa akiwatelekeza wafanyabiashara hao kwani kila wanapomuhitaji afike sokoni hapo huwajibu hana nafasi ya kufanya hivyo na kusababisha wafanyabiashara hao kuwa na hasira na kuona viongozi wao hawawathamini.

MKURUGENZI MERU APIGA MARUFUKU UFUGAJI,ULIMAJI NA UTIRIRISHAJI WA MAJI MACHAFU KWENYE VYAZO VYA MAJI

images

Na Mahmoud Ahmad Arumeru

………………………………………….
MKURUGENZI wa halmashauri ya Meru, Bakari Sagini, amepiga marufuku
ulimaji, ufugaji na utiririshaji wa maji machafu kwenye vyanzo  vya
maji na atakayebainika atachukuliwa hatua kali.
Ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake na kuwataka wale wote wanaofanya shughuli hizo kuacha
mara moja
Alisema kumezuka tabia ya baadhi ya wananchi kuharibu vyanzo hivyo,
huku wakisingizia shughuli za kibinadamu, kwani  wanasababisha madhara kwa
maelfu ya watu bila wao kujua au kwa makusudi.
“Sasa kuanzia sasa atakayekamatwa akilima, kufuga au kutiririsha maji
machafu atakiona cha moto, kwani sheria ipo wazi na atachukuliwa hatua
kali, ili iwe fundisho kwa wengine,”alisema.
Aidha alisema suala la baadhi ya waalimu kuchangisha wazazi fedha
ambazo ni kero waache mara moja, kwani atakayekamatwa atakumbana na
mkono wa sheria ikiwemo kuachishwa kazi
.Ametoa  wito kwa wazazi kuhakikisha kila mtoto anyapaswa
kwenda shule ampeleke shulenina atakayebainika amemwachisha mtoto
shule au hajampeleka shule naye hataachwa.
Hata hivyo alitoa wito kwa wadau wa elimu kujitokeza kwa wingi
kusaidia wanafunzi wapate chakula mashuleni, kwani hali hiyo itapunguza utoro.

Pia Sagini aliomba Benki ya Dunia kuharakisha utoaji wa fedha za
miradi ya maji, kwani vijiji vingi vinakabiliwa na shida ya maji safi
na salama, kutokana na ucheleweshaji wa utolewaji fedha hizo ili
kukamilisha miradi.

KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

4

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania  Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar.

1Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.

5

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika  katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,

 

2

Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika  sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,3 Baadhi ya majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi  katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

6

Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman  Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

7

Kikundi cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,{Picha na Ikulu.]

Siku 100 za Rais John Magufuli, Wagonjwa Muhimbili Wapata Dawa kwa Asilimia 96

muh1

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

muh2

Waandishi wa habari  na Madaktari wakifuatilia mkutano huo leo.

muh3

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Museru akisisitiza jambo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali hiyo.

muh4

Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.

………………………………………………………………………………………………………………….

 Wagonjwa anaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi sasa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa yaliopo hospitali hapa.

Mafanikio hayo yamekuja baada ya uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa.

“Wagonjwa wanaokosa dawa kwenye maduka yetu, hospitali inanunua haraka ili mgonjwa apate dawa kwa wakati. Kwa sasa ukosekanaji wa dawa hospitalini umepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kuimarisha utendaji ndani ya hospitali,” amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.

Hayo yamesemwa leo na Profesa Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Profesa Museru amesema kwamba Katika muda wa kipindi cha miezi miwili Disemba 2015 na Januari 2016, hospitali imefanikiwa kulipa wafanyakazi malimbikizo ya madai yao ambayo walikuwa wakiidai hospitali hiyo kwa kipindi kirefu.

Malipo hayo ni malipo ya on call, malipo ya wauguzi ya usiku, malipo ya posho mbalimbali hasa kwa madaktari pamoja na kada nyingine za afya ambazo zinashughulika moja kwa moja na wagonjwa.

Amesema kwamba kutolipwa kwa malipo hayo kulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa na kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kukosekana kwa tija katika utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.

Katika hatua nyingine, Profesa Museru amesema kwamba mapato kwenye hospitali hiyo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 baada ya Disemba hospitali hiyo kuzalisha Shilingi bilioni 3.3 kutoka wastani wa shilingi 2.7 zilizokusanywa miezi mitano (Julai 2015 hadi Novemba 2015)

“Mwezi  Disemba mwaka jana  tulizalisha shilingi bilioni 3.3 na Januari 2016 tulizalisha shilingi bilioni 4.3,” amesema mkurugenzi huyo.

Akizungumzia mashine za CT-Scan na MRI, Profesa Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli ilinunulia Hospitali hiyo mashine mpya ya CT-Scan yenye uwezo wa 126 slices.

“Uwapo wa mashine hii mpya umeongeza uwezo kwa kiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwa wakati mmoja. Sasa tunaweza  kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde sita. Awali  tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakini sasa tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa 24.

“Baada ya kuwapo kwa mashine hizi mbili za CT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwa vipimo vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hii mpya ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye nguvu kubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamu zaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kama moyo, utumbo, ubongo na hivyo kupata majibu sahihi ya chunguzi na uhakika zaidi. Mashine hii mpya tangu ilipofungwa Novemba 26, 2015 hadi Februari 9, 2016 imepima wagonjwa 863,” amesema Profesa Museru.

Amesema kwamba baada ya mashine ya MRI kutengenezwa wagonjwa zaidi ya 2,200 wamepimwa na kwamba baada ya mashine ya CT-SCAN kutengenezwa wagonjwa zaidi 1,000 wamepatiwa vipimo.

Benki ya Dunia kutengeneza miundo mbinu imara Temeke

msuNa Jacquiline Mrisho -MAELEZO

…………………………………………………………………………

Serikali kushirikiana na Benki ya Dunia inategemea kuanza ukarabati wa Miundo Mbinu mibovu hususani  ya mitaro inayosababisha maafa wilayani Temeke kuanzia mwezi Mei mwaka huu.

 Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wilaya ya Tem
eke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama  ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.

Hili limetokea baada ya uchunguzi uliofanyika jana ambapo Mhandisi wa Wilaya, Bwana Afya pamoja na Afisa Habari wa Wilaya walifika eneo la tukio na kuona hali halisi.

‘’Ni kweli maafa hayo yametokea na sababu hasa ni miundo mbinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika maeneo ya makazi ya watu,kwahiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi yanapostahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu’’Alisema Msumba.

Aliongeza kuwa ukarabati huo wa mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Aidha, Joyce Msumba amesema kuwa endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza watatumia njia ya kuyanyonya maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea.

Mradi huu unalenga kuhamisha njia za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende moja kwa moja baharini.

HILARY CLINTON “APIGWA”, TAJIRI DONALD TRUMP ASHINDA KURA ZA MCHUJO

NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya Habari
………………………………………………………………………………………

HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti
charais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo,
ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.

Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye
mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne
usiku.

Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutokaNew York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo”
nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich
aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted
Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.

Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari
wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo. Clinton ambaye aliwahi
kuwa Waziri wa Mamboya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari
amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye
kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic. 

Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

KOMBE LA SHIRIKISHO RAUNDI YA 16

Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16 bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.

Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.

Ijumaa tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Jumamosi, Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex – Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Februari 28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Raundi hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Young Africans watawakaribisha JKT Mlale katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.

UJUE MTUNGI WA FAYA ULIOJAZWA NA ULIOTUPU/AMBAO GESI IMEKWISHA

Mtungi uliojaa kwa kuzima Moto

Mtungi uliotupu kwa maana ya kwamba mshale wake umerudi kushoto kama
unao kwenye gari lako,ofisini au nyumbani ujue hilo ni kopo tu hautakusaidia chochote kuzima
moto. Sana sana utautumia kuwadanganya askari na wakaguzi wasiojua tu. Kwa ufupi
unajidanganywa wewe mwenyewe.
Mtungi ulioactive kwaajili ya kuzima
moto mshale wake utakuwa kwenye green (kijani). Ikiwa mshale utakuwa
kulia mwa alama ya kijani mtungi huu umejazwa kupita kiasi na ni hatari.Imeandaliwa na RSA na Dj Sek Blog

Huu ni mtungi ambao hauna ujazo wowote na hauwezi kuzima moto kwa namna yoyote ile

 

Serikali yasisitiza kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi nchini.

ngo1

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.

ngo2

Nibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.

ngo3

Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte  (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.

ngo4

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.

ngo5

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.

ngo6

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi  wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

…………………………………………………………………………………………………………

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imesema dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia maeneo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam.

Dkt. Mpango aliyaeleza maeneo hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo ni pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.

Maeneo mengine ni miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili kuweza kupata matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo maeneo maalum ya kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na Mtwara kutokana na maliasili iliyopo hapo.

Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia malighafi inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa ni msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.

Katika suala la ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji ndani na nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mataifa mengine.

Mafanikio ya ujenzi wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria kushirikiana na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana na maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.

Aidha, ili kujenga uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi ambayo ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha ambapo wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika mkutana huo, Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara yao ili kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza wafanyabiashara wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia wanapouza bidhaa zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine hizo, Serikali inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.

Vile vile, Dkt. Mpango ametoa namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi nzima kwa namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.

Aidha, Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache kufanyabiashara za magendo ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati na Sera TPSF Felix Mosha  amesema kuwa Sekta binafsi itaendelea kushirikiana na Serikali katika mpango wa kukuza uchumi wa nchi na kumhakikishia  Waziri wa Fedha na Mipango kuwa watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini wanakwenda pamoja na Sera ya “Hapa Kazi Tu”.

 

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA UTURUKI NA CUBA

 

IMG-20160209-WA0010

Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

IMG-20160209-WA0011

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akirekodi mambo muhimu kwenye ‘diary’ yake wakati wa mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

IMG-20160209-WA0012

Balozi wa Uturuki nchini, Bi. Yasemin Fralp akifurahi jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki.

IMG-20160209-WA0009

MWANAHARAKATI KHADIJA LIGANGA ANUIA KUKUSANYA PEDI KWA AJILI YA MABINTI WANAOSOMA.

Kutokana na Wasichana wengi walio
Mashuleni kulazimika kukosa Masomo yao katika Kipindi cha hedhi, Mwanaharakati
wa Kutetea haki za Wanawake na Wasichana nchini Khadija Liganga, amelazimika
kuanzisha kampeni ya kukusanya pedi 3,000 ndani ya mwezi huu ili kuwasaidia wahitaji.
 

Akizungumza jana katika Kipindi cha Passion Break Fast kinachorushwa na Radio Passion Fm ya
Jijini Mwanza, Liganga alibainisha kwamba ameamua kukusanya pedi hizo kutoka
kwa wadau mbalimbali ili kuziwasilisha katika Shule 10 za Msingi na Sekondari zilizo katika Mikoa ya Mwanza na Mara hii ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wasichana wanafunzi ambao
hawana uwezo wa kumudu kununua pedi hizo.
 

“Tarehe Moja mwezi wa Kwanza mwaka huu, wanawake tulikutana Jijini Mwanza chini ya mpango
tuliouita Women Round Table kwa ajili ya kupanga mikakati mbalimbali ya
kimaendeleo kwa mwaka huu 2016. Moja ya mikakati niliyoipanga ni pamoja kuanzisha
mradi uitwao Binti Box ambao umelenga kusaidia uchangiaji na upatikanaji wa
pedi kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji mashuleni pamoja na kuwapa elimu ya
namna ya kujiweka katika hali ya usafi wawapo katika kipindi cha hedhi”.
Alisema Liganga na kuongeza kuwa mpango huo utakuwa endelevu.
 

Kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wasichana katika maeneo mbalimbali nchini kukosa masomo
yao katika kipindi cha hedhi huku baadhi yao wakilazimika kuacha shule kutokana
na aibu wanayokumbana nayo wawapo shuleni hii ikiwa ni kutokana na kukosa elimu
ya kutosha pindi waingiapo katika kipindi cha hedhi.

Unaweza kuungana na mwanaharaki huyo kwa kuchangia pedi ambapo anapatikana kwa nambari 0713 093 801 hiyo ikiwa ni kwa wale walio mbali na Jijini Mwanza ama waweza kutembelea ofisi
za Dida Vitenge Wear zilizopo Nganza Sekondari barabara ya kwenda Chuo Kikuu
cha SAUT jirani na ghorofa upande wa kushoto hapo.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

 

BONDIA IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KUMKABILI JOSEPH SINKALA MARCH 12 DAR LIVE

Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana umwamba wa kurushiana makonde na Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ Maokola anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa atakapozipiga na Joseph Sinkala March 12 katika ukumbi wa Dar live katikati ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘super D’ Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa jinsi ya kupiga ngumi kali za mkunjo wa chini ‘Upcut’  na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘super D’  jana wakati wa kujiandaa na mpambano wake na Joseph Sinkala March 12 mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Dar Live Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa jinsi ya kupiga ngumi kali za mkunjo wa chini ‘Upcut’  na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’  jana wakati wa kujiandaa na mpambano wake na Joseph Sinkala march 12 mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Dar Live Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

SERA YA ELIMU YATAJWA KUCHANGIA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

IMG_2472Balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely Mattli akitoa neno la ufunguzi katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijana

IMG_2469

IMG_2480

703IMG_2572Washiriki wa mdahalo wakiwa katika makundi kujadili mada zilizotolewa.

………………………………………..

Katika kuadhimisha miaka 50 ya mahusiano na ushirikiano baina ya Uswisi na Tanzania, ubalozi wa Uswisi nchini umefanya mdahalo wa wazi kuhusu ajira kwa vijana ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana mawazo jinsi wao wanavyofanya ili kupambana na tatizo la ajira.

Mdahalo huo ambao ulifanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam ulijadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha kuwepo kwa ajira chache lakini pia uwezo wa vijana wa kuingia katika soko la ushindani la ajira.

Aidha mdahalo huo uliweza kujadili kuhusu changamoto iliyopo ya ajira kwa vijana na kuependekeza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaonekana kukua kwa jinsi siku zinavyokwenda.

Wakizungumza na Mo Dewji Blog baada ya kumalizika kwa mdahalo huo wadau mbalimbali ambalo walihudhuria walisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaanzia katika aina ya sera ambazo serikali inazitumia katika sekta ya elimu kushindwa kufanya kazi katika soko la ajira la sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa ili serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana inatakiwa kuhakikisha inaimarisha uchumi wa nchi lakini ambao unatoa nafasi za ajira zaidi.

Alisema mbali na kuimarisha uchumi pia inatakiwa kuwatengenezea wananchi wake mazingira mazuri ambayo yatawashawishi kujiajiri bila kutegemea ajira ya serikali au makampuni binafsi ambayo kwa sasa ndiyo yanaonekana kutoa nafasi nyingi za ajira.

“Vijana wengi kwa sasa wakimaliza vyuo wanajiajiri na hata kama wanauza barabarani korosho huko nako ni kujiajiri … serikali inatakiwa kuimarisha uchumi wa nchi na sio kukuza tu lakini ukue na utoe fursa za ajira kwa wazawa,” alisema Eyakuze.

Aidha aliwataka vijana kuacha tabia ya kutegemea ajira za serikali na sekta binafsi kwani ushindani katika soko la ajira ni mkubwa na kama wanakuwa hawajajiandaa kwa kiasi kinachohitajika sasa katika soko la ajira basi inaweza kuwa ngumu kwao kupata nafasi.

Nae Amabalis Batamula kutoka Femina alisema sera ambazo zinatumika nchini hazitekelezwi kama zinavyopangwa na serikali na pia hazina faida kwa soko la ajira la sasa kutokana na kubadilika kwa jinsi miaka inavyozidi kwenda.

Alisema ni jambo la ajabu baadhi ya sera za elimu ni kuendelea kutumika hadi sasa licha ya soko la ajira kubadilika na hivyo kuhitaji sera mpya ambazo zinakwenda na wakati lakini pia kuwashauri vijana wanaohitimu kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe wakijiajiri ili kuepuka tatizo la ukosefu wa ajira.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), inaonyesha kuwa zaidi ya vijana 800,000 humaliza chuo kila mwaka na wanaokadiriwa kupata ajira rasmi ni 40,000 pekee hivyo kuonyesha ni jinsi gani kuna upungufu mkubwa wa ajira nchini.

AJALI ILIYOTOKEA MWENGE DAR ES SALAAM

DSC00421

DSC00429Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakishuhudia Gari lenye namba za usajili T 838  CJC  aina ya Benz baada kupata ajali barabara ya  Samjoma Mwenge Dar es salaam chanzo cha ajali hiyo kinasemekana ni mwendo kasi ambapo dereva wa gari hilo alishindwa kulimudu gari na kugonga ukuta wa barabara.hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.

DSC00420

DSC00426  Askari wa usalama barabarani akichukua maelezo kutoka kwa dereva aliekuwa akiendesha gari hilo ambaye jina alikuweza kufaamika mara moja.DSC00430Gari la break down likivuta gari hilo baada ya kupata ajali.

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG

ELIMU BORA ITOKANE NA WALIMU BORA – MELISA

Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo

Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila , katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow (TFFT)N,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo naMzawadi mbalimbali.

washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la
The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .
,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la
The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .
,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo

………………………………………………………………………………………………………………………

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
 
Serikali imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango
cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa
kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa
Watanzania.
Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow  (TFFT) ,Melissa
Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule
za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu
nchini na ustawi bora wa jamii .
 
Melisa alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu
waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu
ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda
kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.
 
“Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua
kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao
,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na
washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa
 
Afisa Elimu wa Shule za Msingi  Wilaya ya Meru  Tumsifu Mushi
amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku
wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa
na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.
 
Kwa upande wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli
Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua
likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari  na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.
 
“Kazi ya ualimu unapaswa uwe unapenda watoto unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim

MWIGULU ATUA MVOMERO KUJIONEA HALI HALISI ,ZAIDI YA MBUZI 70 WAKATWAKATWA MAPANGA

Mh:Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.

Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.

Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.

Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.

Mh:Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.

Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.

Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.

 

Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga  na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda.

Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.

Mwigulu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.

Waziri wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.

Picha na Sanga Festo Jr.

 

Serikali kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

MABONDIA FRANCIS MIYEYUSHO NA NASSIBU RAMADHANI KUZIPIGA SIKU YA PASAKA UWANJA WA TAIFA

Mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Francis Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Christopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS   

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Francis Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

Akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kuwa amewasainisha mabondia hao kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano mkali utakaokuwa  wa kufungua mwaka 2016

Aliongeza kwa kusema mbali na mpambano huo siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku hiyo.

Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba.

Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kujitokeza kwa wingi ili kushudia mpambano huo ambao unatarajiwa kuwa  na msisimko wa aina yake,  vilevile mabondia hao wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wafurahie mchezo huo mapema na  kurudi majumbani  na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati  muafaka na kumalizika mapema.

TFF yaipongeza SHIWATA kumpatie eneo Samatta

shv

Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Michael Kagondela (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi eneo ambalo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta atapimiwa ekari tano na kukabidhiwa na mtandao huo kwa ajili ya kujenga chuo cha wanamichezo, Mkuranga mkoani Pwani. Picha na Mpiga picha Wetu.
……………………………………………………………………………………………… 

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga

MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ameupongeza uongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA)kumpatia uanachama wa heshima na kumzawadia ekari tano za eneo la ardhi mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta ili ajenge kituo cha kuendeleza michezo nchini.

Akizungumza na Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael Kagondela katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi, Madadi ambaye pia ni mwanachama wa SHIWATA alisema huo ni motisha mzuri utakaowavutia wachezaji wengine kujibidiisha kuiga nyayo za Samatta.

Alisema Samatta amefungua njia kwa wachezaji wengine ambao kuanzia sasa watajitahidi kuonesha vipaji vyao binafsi ambavyo matokeo yake vinageuka kuwa lulu katika sura ya Afrika na dunia.

Naye Katibu Mkuu wa SHIWATA, Kagondela alisema mtandao huo unaomiliki ekari 300 kwa ajili ya kujenga makazi na viwanja vya burudani na kumbi za starehe inatarajia kupata wawekezaji kuwekeza katika fani mbalimbali za michezo.

Alisema kutoka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anna Wambura alipotembelea kijiji cha wasanii Mkuranga hivi karibuni ahadi zake za kuwapatia huduma za jamii za umeme, barabara na maji zimekuw2a kichocheo kwa wasanii kujenga nyumba zao kwa kasi.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema wameanza kutekeleza rai ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga aliyoitoa hivi karibuni akiwataka SHIWATA kuandaa tamasha kubwa mwaka huu litakalowakutanisha wasanii wa fani zote nchini.

BARABARA ZA MZUNGUKO JIJINI DAR ES SALAAM KUMALIZIKA MWEZI JUNI

ra1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa tatu kulia), huku Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akifatatilia maelezo hayo.

ra2

Muonekano wa Barabara ya Tankibovu-Goba inayojengwa kwa kiwango cha Lami kama ilivyokutwa leo mchana.

ra3

Muonekano wa daraja la kinyerezi lenye urefu wa mita 40 ambao ujenzi wake umekamilika

ra4

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kimara – Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa Km 2.6.

ra5

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua hatua za Serikali za kuhakikisha ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam unakamilika mwezi juni mwaka huu.

………………………………………………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara za mzunguko (ring roads) zenye lengo la kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam utakamilika baadae Mwezi Juni mwaka huu.

Amesema kufuatia Serikali kuanza kulipa madeni ya makandarasi amewataka makandarasi wote kurudi kazini ili kufikia lengo la Serikali la kukamilisha barabara hizo mwezi juni sambamba na ulipaji wa madeni yote.

“Tunawaomba wale wenye nyumba pembeni mwa barabara za mzunguko ambao wapo kwenye orodha ya kulipwa fidia waondoke maeneo hayo ili kuruhusu kazi ya ujenzi wa barabara kuendelea”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara za Tankibovu – Goba (km9), Goba – Mbezi Mwisho (Km7), Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu (km2.6), Mbezi Mwisho – Malambamawili – Kifuru – Kinyerezi (km14), na Tabata Dampo – Kigogo (km1.6).

Barabara hizo zenye urefu wa Km 27.2 zimejengwa kwa gharama ya takriban sh. bilioni 56.3 ikiwa ni gharama za ujenzi na fidia ambazo zote zinalipwa na fedha za mfuko wa barabara.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amewataka madereva kulinda barabara hizo kwa kutoegesha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa na kukemea vitendo vya uchimbaji mchanga pembeni mwa madaraja.

Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40 lililojengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 2.3 ambao ujenzi wake umekamilika.

Barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuvutia magari mengi kutumia barabara hizo na kupunguza msongamano katikati ya jiji ambapo hadi sasa Km 27 zimekamilika na Km 28 zinaedelea kujengwa.