CHADEMA YAPATA VIONGOZI WA KAMATI YA UTENDAJI

Kutoka kushoto ni Naibu Mkuu zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma, Katikati ni Naibu katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika na Kulia ni Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.
 Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa 
Naibu Katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KIBITI

 

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji katika Chanzo cha maji kwenye kijiji cha Muyuyu kata ya wilaya ya Rufiji wakati wa Ziara ya kiongozi huyo inayoendelea katika mkoa wa Pwani, ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa ilani  ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo Kinana anaongoza na Katibu wa NEC Siasa, Uenezi na Itikadi,(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-KIBITI)4 Mbunge wa jimbo la Kibiti . Mh. Abdul Marombwa akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa watumishi wa zahanati ya kijiji cha Muyuyu wakati ziara ya  katika mkoa wa Pwani7Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akipanda mti katika zahanati ya kijiji cha Nyamatanga wilayani Kibiti mkwani Pwani 8Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akishiriki  ujenzi katika zahanati ya kijiji cha Nyamatanga. 11Jengo la zahanati ya kijiji cha Nyamatanga 16Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizumza na wananchi wa kijiji Nyamatanga kata ya Nyamatanga 19Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akishiriki kupiga marimba katika kijiji cha Songa. 20Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akiweka jiwe la msingi  katika ofisi ya CCM  jimbo Kibiti. 21 Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM Kibiti 22Katibu Mkuu mahia kuc yindwa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akipata mahindi ya kuchoma mjini Kibiti. 23Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akikagua soko jipya mjini Kibiti. 24Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akikagua soko jipya mjini Kibiti. 25 MsKatibu wa CCM Mkoa wa Pwani mama Joyce Masunga akizungumza na waanchinchi wa Kibiti. 26Mkuu wa wilaya  ya Rufiji Bw. Nurdin Babu akiteta jammbo na Mbenge wa jimbo la Kibiti Mh. Abdul Marombwa huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mwisheshe Mlao.30Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akimsikiliza aliyekuwa Selemani Ndumbogani Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMa Kibiti mara baada ya kutangaza kurejea CCM. 31Selemani Ndumbogani Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMa Kibiti maraa  akikabidhi kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana baada ya kutangaza kurejea CCM. 32Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Andulrahmani Kinana akizungumza jambo na wazeee wa baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Kinyanya.

MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA AWATAKA BAADHI YA VIONGOZI KUTII SHERIA.

IMG_0010Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Hamad Rashid amewaomba viongozi  kuheshimu na kutii sheria.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Rashid wakati kikao cha Arobaini cha Bunge hilo, kinachoendelea  mjini  Dodoma cha kujadili sura zote 15 zilizobakia za Rasimu ya  Katiba Mpya, ikiwa ni mjadala wa mwisho.

“Hakuna dhambi mbaya ya kuamrisha mtu kuvunja sheria. Ninaomba sana ndugu zangu na viongozi wenzangu tutii sheria. Ndugu zangu tutulie tuendeshe nchi . Hii nchi ina bahati ya ajabu,” alisema Rashid huku akisisitiza kuwa ina Rais wa ajabu ambaye anaweza kumsikiliza mtu hata ambaye anampa amri.
Mhe. Hamad aliwataka watu wasicheze na dola, huku akitolea mfano yeye na wenzake 18 waliwahi kuwekwa ndani. Hivyo aliwaasa viongozi  wenzake wasicheze na Serikali, bali waitii.
Bunge hilo, ambalo linaendelea kwa mujibu wa sheria, ambapo baadhi ya wajumbe waliwataka wabunge wenzao kuendelea na kazi waliyotumwa na wananchi  ya kuhakikisha Katiba  inayopendekezwa inapatikana Oktoba 4,mwaka huu.

MNYAMA SIMBA ATUA ZANZIBAR KUANZA MAWINDO YA LIGI KUU

KIKOSI cha Simba kimewasili jioni ya leo visiwani Zanzibar na kesho kinaanza programu ya mwisho ya maandalizi ya kujiwinda na ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MTIBWA SUGAR WAIONYA YANGA SC, WASEMA AZAM WALIKUWA ‘WAGONJWA’ NGAO YA JAMII

Kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita

MTIBWA Sugar wamesema kitendo cha Yanga kuifunga Azam fc 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii jana uwanja wa Taifa si kigezo cha kuifunga klabu hiyo katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara, septemba 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

WABABE WA MBEYA CITY, VIPERS FC KUKIPIGA NA RUVU SHOOTING KESHO TAIFA

BAADA ya kuinyuka Mbeya City fc mabao 4-1 katika uwanja wa Sokoine jijni Mbeya mwishoni mwa wiki iliyopita, Vipers FC (zamani Bunamwaya) inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda, itashuka dimbani kucheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani .

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

NAUKALA NDIMA WALIPANIA TAMASHA LA HANDENI.

Fadhili Lugendo, ama Koka StarKUNDI la ngoma za asili lenye kupendwa na wengi jijini Dar es Salaam linalojulikana kama Naukala Ndima, limejipigia debe likisema lina hamu kubwa ya kufanya kazi ya maana katika tamasha la Handeni Kwetu, litakalofanyika Desemba 13, mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa matukio makubwa ya sanaa na burudani linafanyika kwa msimu wa pili, baada ya kuzinduliwa rasmi mwaka jana Desemba 14 na kuhudhuriwa na wengi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kundi hilo, ambaye ni miongoni mwa wasanii wa ngoma za asili, Fadhili Lugendo, maarufu kama ‘Koka Star’, alisema kuwa wamelipania tamasha hilo kwasababu wanafahamu linavyopendwa na wengi mkoani Tanga na Tanzania kwa ujumla kutokana na kuandaliwa vizuri.
Alisema kuwa tamasha la mwaka jana lilikuwa zuri na kuwapatia mafanikio makubwa kutokana na mikataba mingi waliyoipata, ukiwapo ule unaohusisha wao na televisheni ya CTN iliyowapa haki ya kurusha vipindi vya utamaduni wa Tanzania.
“Baada ya kusikia waandaaji wa tamasha hilo wamejipanga tena kufanya tukio hilo mwezi Desemba mwaka huu, tunapata shauku ya kuomba na sisi tuwe miongoni mwa makundi kutoka nje ya mkoa wa Tanga tutakaoshiriki.
“Nikiwa kama msanii wa ngoma za asili natambua matamasha makubwa kama haya ndio yanayoweza kutangaza sanaa yetu pamoja na kukuza utamaduni wa Mtanzania, hivyo endapo tutapewa mwaliko wa kuelekea Handeni, hakika tutafanya kazi ambayo haitasahaulika,” alisema.
Naukalanda Ndima ni miongoni mwa makundi kutoka nje ya Handeni, mkoani Tanga yaliyopata fursa ya kuonyesha sanaa yao mwaka jana kwenye tamasha hilo linaloandaliwa chini ya Mratibu wake Mkuu Kambi Mbwana. 

WAZUNGU WACHANJA MBUGA PEKUPEKU KATIKATI YA JIJI LA JIJI LA DAR ES SALAAM MAENEO YA POSTA

Licha ya kuwepo kwa madimbwi ya maji yaliyochanganyikana na maji taka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam , raia hao wa kigeni ambao hawakufahamika wanatoka taifa gani walinaswa na kamera ya mtandao wa habari za jamii.com wakipita maeneo ya posta mpya jirani na jengo la IPS wakiwa pekupeku jambo ambalo ni hatari kwa afya zao. 
 
Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja walikokuwa wakienda.
 
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na baadhi ya madhehebu kutoka nje ya nchi ambayo waumini wake hawavai viatu kutokana na imani zao. (Picha zote na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) 

 

Mhe. Nagu asisitiza suala la Muungano

 Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
MUUNGANO wa Tanzania ni muungano wa damu na wa watu, ambapo Ibara ya kwanza Sura ya kwanza inaeleza kuwa msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano pamoja na katiba iliyopo na inayopendekezwa ni haki ya makubaliaono ya mwaka 1964.
 
Hayo yamesemwa leo na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mary Nagu wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo kuhusu mambo mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.
 
Mhe. Nagu amesema kuwa Hati ya Makubaliano hayo imejengeka katika misingi ya utu, udugu na kuaminiana ambapo Waasisi wa muungano huo hawakupeleka maslahi yao wenyewe binafsi wala kuzingatia suala la mali, bali walizingatia umuhimu na mahitaji  ya muungano kutokana na mambo hayo makuu matatu.
 
Ameeleza kuwa mambo wanayoyajadili bungeni hapo kwa sasa ndiyo yatatokana na muungano ambao una mfumo bora na muundo bora.
 
Mhe. Nagu amebainisha kuwa wale viongozi wenye kutaka muungano wenye gharama kubwa watawafanya wengine washindwe hapo baadaye.
 
“Naomba sana tuendelee na kuona kuwa muungano huu ni muhimu nataka niwaambie kwamba Zanzibar ni lango kuu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na lango hili linatuhakikishia usalama wetu na ulinzi wetu kwahivyo na Wazanzibar nao wanufaike na rasilimali za Bara, kwahiyo muungano huu ni muhimu na utanufaisha pande zote mbili mimi sina wasi wasi”, alisema Mhe. Nagu.
 
Aidha, Mhe. Nagu amegusia suala la usawa wa jinsia kupitia hamsini kwa hamsini katika uwakilishi, ajira na maeneo mengine.
 
Mhe. Nagu ameleza kuwa usawa wa jinsia utajenga jamii nzuri ya Tanzania ikiwemo kuleta heshima pamoja na haki katika jamii hiyo kwani kwa mila na desturi za Waafrika na Watanzania, wanaume hawakupaswa kuwa wamiliki wa kila kitu.
 
“Akina baba ni Custodians lakini  wakajigeuza wamiliki, tunachotaka waendelee kuwa Custodians na sisi watuone ni wenzao, kwahivyo suala la jinsia halina mjadala, kupitia uwakilishi teundelee na hamsini kwa hamsini na Katiba iseme wazi, mengine yatajitokeza kwenye Sheria ya uchaguzi”. Alisisitiza Mhe. Nagu.
 
Kuhusiana na suala la ajira na uongozi Mhe. Nagu ameeleza kuwa wanawake zaidi ya asilimia 52% wangepaswa kuwa katika kila eneo lakini hawapo na suala hilo linaleta tofauti isipokuwa mashambani ambapo chakula chote kinachotoka kwa kiasi kikubwa wanaolima ni wanawake.

ZNZ KUFANYA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KATIKA KAYA ZAKE

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  15/09/2014

Serikali ya Mapiduzi Zanzibar inatarajia kufanya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya kwa Mwaka 2014/15 ambao utasaidia kutoa viashiria mbali mbali kwa ajili ya kutathmini Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).

Utafiti huo utazishirikisha Kaya 4,560 katika maeneo 380 ya kuhesabiwa Watu yaliyochaguliwa kitaalamu katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mafunzo ya Wadadisi, Wasimamizi na Wahariri wa Utafiti huo yaliyofanyika Ukumbi wa Kwawazee Sebleni Mjini Zanzibar.

Amesema Utafiti huo utakaoendeshwa kitaalamu utaanza rasmi Octoba 6 mwaka huu na kuchukua miezi 12 kumalizika kwake.

Mkuu huyo wa Mkoa amefahamisha kuwa hakuna lengo binafsi la kuwachunguza Wananchi hali zao za maisha katika utafiti huo badala yake unakusudia kukusanya Takwimu sahihi za Mapato na Matumizi ya Kaya husika ili kutathimi hali halisi kwa Maendeleo ya Taifa.  

Abdallah amesema dhamana ya Mafanikio ya utafiti huo ipo Mikononi mwa Washiriki hao hivyo wanapaswa kujitahidi katika mafunzo hayo ili lengo lililokusudiwa liweze kutimia.

Ametoa Wito kwa Masheha wa Shehia na watendaji wengine katika maeneno yatakayohusika na Utafiti huo kutoa mashirikiano kwa Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti huo ili kutimiza lengo.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mohamed Hafidh Rajab amefahamisha kuwa Utafiti huo utasaidia kupata Takwimu zitakazosaidia kupata Mchanganuo na kadirio la Pato la Taifa sambamba na kujua Mfumuko wa Bei unavyoenda nchini.

Mafunzo hayo ya Watafiti yanayodhaminiwa na Benki ya Dunia kupitia Mpango mkuu wa kuimarisha Takwimu Tanzania yanawashirikisha Wadadisi na Wasimamizi 217 Unguja na Pemba,ambapo yatachukua jumla ya siku 18 kumalizika kwake.

Utafiti wa Mwaka 2014/15 ni wa mara ya Tano kufanyika tokea Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ambapo Utafiti wa mwaka 2009/10 ulionesha kuwa Asilimia 44 ya Wazanzibari hawamudu Mahitaji yao ya Chakula na mambo mengine.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZNZ

TANZANIA KINARA KATIKA KUTAMBUA MCHANGO WA MWANAMKE NA KUTHAMINI JITIHADA ZAKE

PIX 1-3
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwahutubia baadhi ya Wabunge Wanawake na Wanaume wakati wa Warsha ya Waheshimiwa Wabunge iliyohusu Kuimarisha Uongozi na kuleta Amani katika Uchaguzi iliyofanyika tarehe 13-14 Septemba 2014 mjini Dodoma.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-DSM.
 
Tanzania imekuwa miongoni mwa Mataifa yaliyoko mstari wa mbele katika kutambua mchango wa mwanamke na kuthamini jitihada zake katika kuleta mafanikio na kuhamasisha mabadiliko ya jamii nzima ili kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unakuwepo.
 
Kutokana na sifa hiyo, Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa Barani Afrika na dunia nzima kwani katika juhudi za kuleta usawa wa kijinsia na kuinua hadhi ya wanawake imefanya jitihada mbalimbali katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
 

Continue reading →

Tanzania kuungana na Jumuiya ya Kimataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni.

 
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
Tarehe 16 Septemba, mwaka huu Tanzania itaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994.
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Mwandisi Dkt. Binilith Mahenge wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari 15 Septemba, 2014 kwa lengo la kuongelea juu ya Maadhimisho hayo linalofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.
 
Mwandisi Mahenge ameeleza kuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
 
Ameendelea kwa kusema kuwa Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
 
“Punguzo hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani”, alisema Dkt. Mahenge.
 
Akizungumzia kuhusu mikakati ya kitaifa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Mkataba huo, Dkt. Mahenge alisema kuwa 1996 Serikali iliandaa na kutekeleza Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Ozoni, mikakati hiyo ni pamoja kujenga uwezo wa Taasisi zinazosimamia utekelezaji wa Mkataba, kuweka takwimu za kemikali hizo, kutoa elimu kwa wadau na kwa umma kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili, kusambaza habari kuhusu kemikali na teknolojia mbadala na mikakati mingineyo.
 
“Hatua hizi zimewezesha Tanzania kuondosha kemikali hizi kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Mkataba”, alisema Mhe. Mwandisi Mahenge.
 
Chini ya Programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu, serikali iliandaa Mpango wa Usimamizi wa Vipodozi yaani (Refrigerant Management Plan) na katika utekelezaji wake, mambo kadhaa yamefanyika ikiwemo kuandaa Kanuni za Usimamizi wa kemikali zinazomong’onyoa tabaka la hewa ya Ozoni ambazo zilianza kutumika tarehe 7 Desemba mwaka 2007, kusambaza kwa Vitambuzi vya kemikali hizo vipatavyo 18 kwa ajili ya vituo vilivyo mipakani mwa Tanzania, pia kusambaza mitambo na zana za kuhudumia majokofu na viyoyozi kama vile mashine za kunasa na kurejeleza gesi chakavu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya fani ya kuhudumia majokofu na viyoyozi hapa nchini.
 
Aliongeza kuwa hadi sasa, Tanzania imeweza kupunguza zaidi ya tani 216 sawa na asilimia 86% ya kiasi cha matumizi ya kemikali hizo, mwaka 1999.
 
Hapa nchini maadhimisho haya yatafanyika kwa njia ya uelimishaji umma kuhusu Tabaka la Ozoni, faida zake, madhara ya kuharibika kwa Tabaka hilo na matumizi salama ya bidhaa zenye kemikali rafiki kwa tabaka la ozone.

RAIS DKT. SHEIN APOKELEWA COMORO

IMG_4092RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN AKISALIMIAANA NA BALOZI COMORO NCHINI TANZANIA ALIPOWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA COMORO AKIWA KATIKA ZIARA YA KISERIKALI AKIWA AMEFUATANA NA MKEWE MAMA MWANAMWEMA SHEIN NA VIONGOZI MBALI MBALI [PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]
IMG_4102RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN  AKIWA NA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA COMORO MOAMED  ALI SOILIHI WAKATI WIMBO WA TAIFA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAA TANZANIA NAWIMBO WA MUUNGANO WA COMORO UKIPIGWA [PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]

BENKI YA DUNIA NA SERIKALI IKISHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI WAKUBWA WA MADINI WAZINDUA MRADI WA UCHIMBAJI MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO WADOGO MKOANI GEITA


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh,Stephen Masele akizungumza kwenye uzinduzi huo uliovuta hisia za wanakijiji wengi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Wananchi

Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine,Michael Van Anen

Mwakilishi Mwandamizi kutoka Benki ya Dunia ambaye pia ni mtaalamu wa madini kutoka idara ya nishati endelevu nchini Marekani,Bwa.Mamadou Barry akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo wadogo katika kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele.Mradi huo Umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali kwa kushirikiana na Wawekezaji wakubwa wakiwemo Geita Gold Mine na African Barrick Gold

Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mh.Omary Mangochie akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo.

VIDEO CLIP NA MICHUZI JR-LWAMGASA-GEITA

DK. SHEIN AWASILI COMORO KWA ZIARA RASMI YA SIKU NNE

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

    Zanzibar                                                             15 Septemba, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewasili visiwa vya Comoro leo mchana kuanza ziara ya kikazi ya siku nne kufuatia mwaliko wa Rais wa Muungano wa Comoro Mheshimiwa Ikililou Dhoinine. 

Katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Prince Said Ibrahim mjini Moroni, Dk. Shein alipokelewa na mamia ya wananchi wa mji wa Moroni na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano wa Comoro Mheshimiwa Mohamed Ali Soilihi pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Mheshimiwa Balozi Chabaka Kilumanga.

Mara baada ya kuwasili Dk. Shein alikaribishwa kwa kupigiwa wimbo wa Taifa na kuvishwa shada la maua kulingana na utamaduni wa watu wa Comoro baadae kusalimiana na viongozi wa Serikali na kidini waliofika kumlaki.

Katika mazungumzo mafupi kiwanjani hapo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano wa Comoro,viongozi hao wawili walieleza haja ya kuimarisha ushirikiano wa kindugu na wa damu uliopo kati ya Visiwa vya Comoro na Zanzibar.

Dk.Shein alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano wa Comoro kuwa ziara yake hiyo ya siku nne itasaidia kuimarisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungua milango zaidi ya ushirikiano kati ya  nchi hiyo na Zanzibar.  

Kabla ya kuondoka kwenda mjini Moroni, Dk. Shein alikagua vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni na kusalimiana na wananchi wengine walioshiriki mapokezi yake. 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa hapa, baadae leo jioni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Muungano wa Comoro Mheshimiwa Ikililou Dhoinine.

Mazungumzo hayo na Rais Dhoinine yanatarajiwa kuwa juu ya kukuza uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Muungano wa Comoro na pia kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na nchi hiyo.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais amefuatana na mke wake Mama Mwanamwema, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, Naibu wa Waziri wa Kilimo na Maliasili  Bibi Mtumwa Kheir Mbarak na Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa, Uwezeshaji na Uchumi Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.

Wengine ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Bwana Ali Saleh Mwinyikai, Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Bibi Asha Ali Abdulla na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Bwana Kombo Abdulhamid Khamis. 

KATIBU MKUU UTUMISHI ATOA SOMO KWA WATUMISHI RS MWANZA

1.KATIBU MKUU UTUMISHI GEORGE YAMBESHI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA RS MWANZA(PICHA NA AFISA HABARI WA RS MWANZA)
Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.  
Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao. 
Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu ” kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza” alisema na kuongeza.  kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri. 
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi” Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.
Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.
Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.
Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana.
Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania.

 

MKUTANO WA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUFANYIKA DAR E S SALAAM SEPTEMBA 18-2014 UKUMBI WA MIKUTANO WA BENKI KUU YA TANZANIA BoT

Dotto Mwaibale 
 
 BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasa

imezifungia kampuni 86 kufanyakazi ya ukandarasi baada ya

kushindwa kufuata sheria za ujenzi. 

 
 Hayo yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakatiakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,

kuhusu mkutano wa usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Septemba 18, 2014 jijini Dar es Salaam. 

 
 “Kazi yetu kubwa ni kusimamia sheria ya shughuli za ujenzi na kama tukibaini kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifungia kufanyakazi” alisema Jehad. 
 
 Alisema lengo mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta ya ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma hiyo. 
 
 Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa ambayo yanabomoka hapa nchini.Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti na ilivyosasa.
 

Dk.Mwakyusa alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepowataalamu wa majengo wanapotumia vifaa vya ujenzi

ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa hawana hatia. 

 
“Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwaujumla kama ikiwepo sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya kutumia

vifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiwa

zitumike aina gani kwenye jengo husika ,”alisema

Dk.Mwakyusa.

Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo. 
 Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad akizungumza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu mkutano huo.  
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (katikati), akiwa na viongozi wenzake wa bodi hiyo. Kutoka kulia ni Kaimu Msajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala, Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad, Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Mwanasheria wa Bodi, Ibrahim Mohamed.
 Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 
Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

TUTENGENEZE KATIBA INAYOLENGA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI WETU KWA MIAKA 50 IJAYO. Prof:Mwandosya.

Mwandosya akizungumza 1MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
 Prof. Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
 Mhe. Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.
 Ili kufanikisha nchi inapiga hatua baada ya kuwa na Katiba bora, Mhe. Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi wote wa Umma hawana budi kuliletea tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa ndani ya rasimu ya katiba  na kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma sio mtawala na mambo yanayohusu miiko na maadili ya mtumishi huyo yenye kumtumikia mwananchi serikali Katiba imeweza kuyazungumzia.
 
“Tumezungumzia kuhusu rushwa ambaye ni adui wa haki, kwamba hili tulitambue katika Katiba ili katika Sheria likasimamiwe vilivyo na pia tumezungumzia pia wale wanaouhujumu uchumi”, alisema Mhe. Mwandosya.
 Kuhusu haki za vijana, Mhe. Mwandosya ameeleza kuwa katika Rasimu ya Katiba wamezungumzia juu ya haki za vijana, haki za walemavu, haki za wazee, pamoja na haki za watoto, huku akiwashangaa baadhi ya wajumbe walioko nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa wanapoteza wakati kana kwamba hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
 “Nawaomba wananchi watusikilize na wayazingatie haya tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
 Akizungumzia kuhusu Vyombo vya Usalama, amesema kuwa Katiba inawalinda na kuwatambua viongozi wa usalama, ambapo sheria inawapa haki hata baada ya kustaafu ili wakaweze kuishi maisha bora kwa kuchukua dhamana kubwa, hivyo kwa dhamana hiyo viongozi hao wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha na masuala ya kisiasa kwasababu.
 “Usalama wa Taifa, Jeshi, Polisi, Magereza na Uhamiaji, hawa tunawatengezea mambo mazuri sana wanapostaafu, kwahiyo tafadhari sana mkishatoka tusaidieni, toeni ushauri lakini mkijiingiza katika siasa na mafaili yetu huku mmeyashika hamtutendei haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
 Aidha, ameomba kuwepo na Randama kwani hiyo inaandikwa katika lugha ambayo mwananchi anaweza kuisoma tofauti na katiba kwani hiyo inaandikwa kwa lugha ya kisheria, kwahiyo amependekezo kuwepo na randama kwa ajili ya wananchi.
 Mwandosya ameongezea juu ya suala la amani kuwa ni jambo kubwa sana, amewananga watu wenye tabia ya kutaka wananchi kuandamana wakapigwe risasi hao ni watu wasioitakia mema nchi, hivyo amewaasa wananchi walipinge kwa nguvu zao zote kuhusu suala hilo.
 “Nina ushauri kwa viongozi wenye kutaka wananchi wakapigwe risasi na Polisi, naomba watangulie wao wajipige risasi, unapotaka kuwa Shujaa anzia kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke vijana ambao ni matumaini ya nchi yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara hata kidogo na wananchi mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini? Kwasababu gani? Na kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya maswali kwakweli mtaona nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchi ya amani”, alisisitiza Mhe. Mwandosya. 

LAPF YATENGA BILIONI 3 KATIKA MIKOPO YA ELIMU MWAKA HUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

“PIGA KITABU NA LAPF”

WANACHAMA WA LAPF KUNUFAIKA NA FAO LA ELIMU

 Bilioni 3 kutumika mwaka wa masomo 2014 – 2015 kutoka mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wake.

 15 Septemba 2014, Dodoma: Wanachama wa mfuko wa penseni wa LAPF kunufaika na fao jipya lilozinduliwa hivi karibuni nchini kwa Baraka zake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia. Fao hilo lijulikanalo kama ‘Piga Kitabu na LAPF’ limelenga kuwakopesha wanachama wa LAPF mikopo ya elimu ya juu kwani ni ombi la muda mrefu kutoka kwa wanachama wa mfuko huo. Hivyo kwa kuthamini na kuona umuhimu wa elimu Mfuko wa Penseni wa LAPF umjibu kiu yao ya muda mrefu ili kumpunguzia mzigo mwajiri.

 Akiongea kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bwana Eliud Sanga alieleza kuwa  mfuko wa Pensheni wa LAPF una huduma nyingi na ambazo zimelengwa kwa ajili ya jamii na hususani zinazochangia sana kwenye maendeleo. “Huduma hii mpya ya Fao la Elimu imetengewa shilingi Bilioni Tatu (3) kwa mwaka huu wa fedha ikiwa ni kianzio cha mfuko huu, tunaahidi mwaka unaofuata fao hili litatengewa bajeti kubwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika nchi yetu, wanachama wengi wameshanufaika mpaka sasa na wengine wengi zaidi wanazidi kutuma maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu. Fao hili litawanufaisha wanachama maelfu na maelfu, wanachama wengi watume maombi kunufaika na huduma hii”

 “Mwanachama anatakiwa kujaza fomu ya mkopo wa elimu LAPF/LON.2, ambayo hupatikana katika ofisi zote za LAPF pamoja na ofisi za waajiri wachangiaji na pia kwenye tovuti ya LAPF www.lapf.or.tz. Baada ya kukamilisha fomu na kuambatisha vielelezo vinavyotakiwa atawasilisha fomu hiyo kwenye ofisi za LAPF au atatuma kwa njia ya posta. Fao hili la Mkopo wa Elimu kwa mwanachama utalipwa moja kwa moja chuoni kila mwaka wa masomo kwa taratibu za chuo husika na urejeshaji wake utakuwa kwa muda wa miaka mitano tangu ulipoanza kutolewa” Aliongeza Bwana Sanga.

 ‘Piga Kitabu na LAPF’ ni fao la elimu litakalotolewa kwa  mwanachama yoyote wa lapf ambaye amekidhi vigezo kama kupata kibali cha kusoma toka kwa mwajiri wake, barua (admission letter) ya kukubalika kujiunga na chuo cha hapa nchini kilichosajiliwa na nacte au tcu na awa na michango inayozidi kiasi cha mkopo unachoombwa kwa asilimia 25.

PINDA ASHIRIKI KIKAO CHA PPP DIALOGUE./ PINDA AKUTANA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA SHIMITOMO

PG4A5452Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Bw. Lord Hollick ambaye ni  Mjumbe wa Masuala ya Biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza nchini  Tanzania katika majadiliano  kuhusu  ushirikiano baina ya serikali na Sekta Binafsi  (PPP Dialogue) kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam Sept. 15, 2-14. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5470Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa  wa Kampuni ya Japani ya  SUMITOMO baada ya kuzungumza nao ofisini kwake jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014.Kulia kwake ni Rais wa kampuni hiyo, Nakamura Kumharu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI, OKWI MWENDO MDUNDO, LOGA AIBUA JAMBO MSIMBAZI!

Na Boniface Wambura, Dar es salaam

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

Serikali imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s)

IMG_0214

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bw. Marcel Katemba akiongea na waandishi wa habari( Hawapo pichani)kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuyajengea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo katika  jamii, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro.

 PICHA NA GEORGINA MISAMA

  Na Jovina Bujulu-MAELEZO

Serikali kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam.

Mercel alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2005.

“Sera hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na ushirikano” Alisema Marcel.

Marcel aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea kusimamia sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta hiyo.

Aidha Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za maadili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala, kutandaa na kuboresha huduma zinazotolewa na mashirika hayo.

Akifafanua zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s umeimarika kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo yakiserikali.

Pia Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Juhudi za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa wananchi kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya wananchi 35,000 ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679 kote nchini.

 

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL AKUTANA NA MBUNGE SHIRIKISHO LA UJERUMANI

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Mhe. Charles M. Huber (wa pili kushoto) ambaye ni Mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo na Mambo ya Nje ya Bunge la Shirikisho la Ujerumani wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Septemba 15, 2014.4.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Charles M. Huber (kulia kwa Makamu wa Rais), Stefan Reith Mwakilishi wa Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kushoto, Naibu Balozi wa Ujeruman nchini John Reyels (wa pili kulia) na Richard Shaba baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam Septemba 15, 2014.

JENGO LA GHOROFA MOJA LINAPANGISHWA MKOANI DODOMA, LIPO KATIKATI YA MJI.KWA MAWASILIANO ZAIDI 0787 970 072

Muonekano wa Jengo hilo ambalo lipo Katikati ya Mji wa Dodoma, lenye Ghorofa moja linakodishwa tunapenda kuwakaribisha Mtu binafsi, makampuni, shirika au taasisi ambayo inataka kufungua ofisi au imekuwa ikihitaji jengo kwaajili ya Ofisi sasa Jengo Zuri tu lenye huduma zote muhimu lipo na Nafasi pia Zipo Karibu Kwa Mawasiliano Zaidi 

Piga namba hii 0787 970 072
 Korido Kama inavyoonekana 
 Vyumba vyake ni Vikubwa na Unaweza kufanya Ofisi kama inavyoonekana kwenye picha.
 Sehemu ya Kupandia Kwenda kwenye ghorofa ya Kwanza

NI Jengo la Ghorofa 1 ambalo hapo awali lilikuwa ni hotel lakini kwasasa linapagishwa kwaajili ya Makampuni, Maofisi na Mashirika mbalimbali au Watu binafsi ambao wanahitaji Ofisi Mkoani Dodoma, Jengo Hilo linapatikana Mkoani Dodoma na Lipo Katikakati ya Mjini Kabisa huku likiwa na Huduma Zote Muhimu za Kijamii.

Kama Kampuni, Shirika, au Taasisi inataka kupanga au Mtu Binafsi basi asisite kuwasiliana na Sisi kupitia namba hii 0787 970 072

Simba Chawene awataka Watanzania kuachwa kuingia barabarani kufanya maandamano ya kupinga mchakato  wa Katiba

PIX 1-1Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Simba Chawene akichangia mada bungeni mjini Dodoma.

 (Picha na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma)

Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. George Simba Chawene amesikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya Wajumbe walioko nje ya bunge hilo kuhusiana na uhalali wa bunge hilo lililoko Kisheria.
 
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo huku akisisitiza kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa na watu hao wanapaswa kuangaliwa kuhusu uzalendo wao.
 
Mhe. Chawene ameeleza kuwa inasikitisha zaidi hasa pale shutuma zinapoelekezwa kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta, kuwa bunge hilo sasa linaonekana ni mali ya Mwenyekiti wa bunge hilo wakati si kweli.
 
“Gazeti linachukua kurasa tatu hadi nne kuzungumzia habari Sitta king’ang’anizi, hivi hili bunge lipo kama liliitishwa na Sitta ama na Rais wa nchi?, hili bunge liko kisheria”, alisema Mhe. Chawene.
 
Aliongeza kuwa kwa niaba ya Watanzania wanafanya kazi ya bunge hilo kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza kuwa wajumbe waliotoka nje ya bunge hilo wamevunja sheria na kwamba hawawezi kutafuta uhalali nje ya sheria.
 
“Wanamlazimisha Rais avunje bunge hili, Rais wa kufuata utawala bora anavunja kwa mamlaka yapi? Mamlaka ya Rais yako kwa mujibu wa sheria”, alisema Mhe. Chawene.
 
Aidha, ameeleza kuwa Sheria inayoendesha mchakato wa Katiba ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imetungwa kutoka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye hatua tatu zikiwemo hatua ya kukusanya maoni ambayo Tume ya Warioba ilifanya kazi hiyo na kumaliza, hatua ya Pili ni bunge hilo kujadili kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa uwakilishi uliopo ndani ya bunge hilo na hatua ya tatu ni wananchi kwenda kutunga Katiba.
 
“Sisi hapa tunatoa Katiba inayopendekezwa, inayofuata ni Watanzania kwenda kutunga Katiba kwa kutunga kwa kupiga kura ya kusema ndiyo au hapana yale tuliyoyajadili na kuletwa na Tume”, alisisitiza Mhe. Chawene.
 
Aidha, amewataka watanzania kuwaona watu hao kuwa ni watu wabaya na wasio na nia nzuri na nchi na kuepuka kuingia barabarani kufanya maandamano ya kuipinga Katiba hiyo.

AIRTEL YAZINDUA EXPRESS SHOP DODOMA.

 

pic 1Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikatata utepe
kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya
Mkuu mkoani humo,  anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel
huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel
Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa
duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine  katika mikoa ya Dar
es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya  Morogoro,
Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu
pic 2 Anaezungumza ni Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw
Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa
maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi kuhusiana
na muonekano wa duka jipya la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu
muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa huyo kuzindua duka hilo jana.
pic 3Kati kati ni Mkuuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema nchimbi akiwa
na Mkurugenzia wa huduma kwa Mteja Airtel Bi Adriana Lyamba  (shoto)
na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki
iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel
mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
pic 4Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi
na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la
Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana, Airtel ilizindua duka hilo
kwa dhumuni la kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchinipic 6Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya
pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa
Mkuu jana, picha na mpigapicha wetu

Airtel yazindua Xpress shop Dodoma
       wateja wa Airtel kupata huduma bora na za uhakika
Dodoma, Tanzania Septemba 12, 2014. Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia ukarabati uliokuwa
unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza
kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi
Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na  mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema
Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa  kuboresha
maduka yake nchini  pamoja na duka la Dodoma
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja Bi Adriana Lyamba alisema,”Leo tunazindua rasmi duka hili lenye
muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja
kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu
na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma
mbalimbali. Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu
za pesa mkononi za Airtel Money ,internet na kuweza  kununua muda wa
maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za
mawasiliano na huduma nyingine nyingi.
Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora  kwa haraka zaidi
kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika
na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea
zaidi nchini. Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu
tofauti katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema”
nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma
za mawasiliano kwa watumiaji nchini. Sote tunatambua mawasiliano ni
nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za
kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma
watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha
uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku”.
“Serikali inaunga mkono juhudi  zinazofanywa na Airtel na kuwaomba
waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za
mawasilaino nchini.  tuko tayari kushirikiana Airtel katika
kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili
kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za  mawasiliano na
hatimaye kuwa maisha bora.”
Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni
imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha
Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya  Morogoro, Bukoba na
Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa
septemba.

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA RASMI TOVUTI YA JESHI LA MAGEREZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza tayari kwa uzinduzi rasmi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mhe. Waziri(wa pili kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
2Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(aliyesimama) akitoa maelezo mafupi kabla ya uzinduzi rasmi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza leo Septemba 15, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akitoa hotuba kwenye hafla ya uzinduzi wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza, leo Septemba 15, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akikata utepe kabla ya kuzindua rasmi TOVUTI ya Jeshi la Magereza inayopatikana kupitia annuani ya www.magereza.go.tz(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
5Muonekano wa Mwanzo wa TOVUTI ya Jeshi la Magereza inayopatikana kupitia annuani ya www.magereza.go.tz(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WAKIBADILISHANA MAWAZO LEO MJINI DODOMA.

 

5(1)Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba  Ally Kessy(kulia) na Mohammed Raza (kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha arobaini cha Bunge hilo.

2(1)Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba  wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wakielekea kuhudhuria  kikao cha arobaini cha Bunge hilo.

KAMPUNI YA ABOOD YAINGIZA MABASI MAPYA.

Kampuni ya mabasi ya Abood yenye maskani Mkoani Morogoro imeingiza Mabasi Mapya na ya
kisasa nchini kwa lengo la kutoa huduma za usafiri kaika mikoa
mbalimbali ya nchini Tanzania.

Continue reading →

MH FREEMAN AIKAEL MBOWE ASHINDA NAFASI YA MWENYEKITI CHADEMA TAIFA

Hatimaye Mhe Freeman Aikael Mbowe Amechaguliwa Tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kupata kura 789 sawa na asilimia 97.3 ya kura zote. Aliyeshinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Bara ni Profesa Abdallah Safari kwa kupata kura 775 sawa a asillimia 95 na nafasi ya Makamu mwenyekiti Zanzibar ameshinda Mh Saidi Issa Mohamedi kwa kupata kura 645 sawa na asilimia 79.