All posts in BIASHARA

NAPE AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KUBANGUA KOROSHO MTAMA NA KUFANYA MIKUTANO MIWILI YA HADHARA

 Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungmza na wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua Korosho cha Mtama ambapo wafanyakazi hao walitoa malalamiko mbali mbali ikiwemo kutokuwa na mikataba na vifaa vya kufanyia kazi.
 Mmoja kati ya vijana wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha kubangua akielezea matatizo yanayo wakuta kiwandani hapo.
  Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa kijiji cha Rondo Mnaramara baada ya kuwasili tayari kuwahutubia wakazi hao waliojitokeza kwa wingi.
 Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Rondo Mnara wakiwa tayari kumsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
  Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipitia moja ya jambo la msingi pamoja na diwani wa kata ya Rondo Mama Halima Mwambe muda mfupi kabla ya kuanza kuhutubia wakazi wa Rondo Mnara.

Continue reading →

Jukumu la kuwainua watoto wa kike ni la kila mmoja.Emma Oriyo

T1Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiongea na baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.

T2Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiwagawia kinywaji cha Grand Malt  baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.

T3Baadhi ya wanafunzi wa kike wakimsikiliza  Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo wakati wa maadhimisho hayo.

……………………………………………………………………………………………

Na Mwandish wetu

Meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya TBL Group,Emma Oriyo, amesema kuwa jukumu la kuwainua watoto wa kike nchini sio la serikali bali linamhusu kila mtanzania ikiwemo makampuni,taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani iliyoadhimishwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa siku hiyo ni muhimu kuadhimishwa kwa kuwa inatukumbusha watanzania kutofumbia matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu na kuangalia  namna ya kuyashughulikia.

“Hapa Tanzania Changamoto za hedhi kwa watoto wa kike ni kubwa wengi wakiwa wanakosa vifaa vya kuwaweka salama pia shule nyingi hazina miuondombinu rafiki kwa wasichana kujiweka salama wanapokuwa kwenye hedhi,matokeo yake wengi wanakuwa hawahudhuri masomo na kujikuta wamebaki nyuma ya wenzao wa kiume”.Alisema.

Amesema TBL Group katika miradi yake ya afya ya kusaidia jamii imeanza kuliangalia suala hili kwa undani ili kuweza kushirikiana na wadau wengine kukabiliana nalo “Leo kampuni yetu ni moja ya wadhamini wa tukio hili la siku ya hedhi ambalo lengo lake kubwa ni kuelimisha jamii umuhimu wa kuungana kuondoa changamoto na hedhi na tutaendelea na jitihada hizi na kutekeleza  miradi mingine ya kusaidia kuboresha afya  nchini”.Alisema.

Alisema  watanzania wakiungana na serikali katika  kukabiliana na changamoto hizi  hali itakuwa nzuri na watoto wa kike kusoma katika mazingira mazuri na itapelekea wafanye vizuri kwenye masomo yao sambamba na wenzao wa kiume.

Emma alisema kuwa hali ya kukosa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na miundombinu isiyo rafiki mashuleni mbali na utoro mashuleni pia inawasabishia watoto  wa kike kutojiamini na wakikua bila kujiamini wanakuwa hawawezi kutoa maamuzi sahihi.

“Wadau wote tukiungana katika suala hili tutaweza kutekeleza dira ya maendeleo ya taifa ambayo kwa upande wa elimu ina kauli mbiu isemayo Elimu Bora bila ubaguzi inawezekana.Timiza wajibu wako”

Waziri Mwijage kufungua maenesho ya Tanga Trad Fair

indexNa Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe.Charles. Mwijage anatarajia kufungua maonesho ya kibiashara ya Tanga (Tanga Trade Fair) kesho katika viwanja vya Chalinze vilivyoko Kijiji cha Mwahako, Mkoa wa Tanga.

Hayo yamesemwa leo  na Mwanakamati wa Maonesho hayo, Aisha Salim alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii  ambapo amesema kuwa maonesho hayo ya kibiashara ni fursa kwa wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali kuonyesha na kuuza  bidhaa zao  pamoja na kupata elimu.

“Maonesho haya ni ya kibiashara yanayojumuisha wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi kwahiyo, ni fursa kubwa kwao kuonyesha na kuuza bidhaa zao pamoja na kupata elimu kutoka kwa wenzao wa nchi zingine zitakazoshiriki kama  Syria, Kenya na Uganda”,alisema Aisha.

Aisha  aliongeza kuwa sio tu wafanyabiashara na wajasiariamali peke yao bali kuna baadhi ya Wizara, Mamlaka, Taasisi pamoja na Mifuko ya Kijamii ambazo wanashiriki katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyanyabiashara hao, baadhi ya washiriki hao ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Fedha, Mamlaka ya Bandari pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Alitoa rai kwa wakazi wa mkoani Tanga kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kuwaunga mkono wafanyabiashara hao kwani wana vitu ambavyo ni imara na vizuri pia wataweza kujifunza vitu mbalimbali ambavyo hawavijui au hawajawahi kuviona.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu amesema kuwa wamefurahi kuwa miongoni mwa washiriki katika maonesho hayo ambayo yatawasaidia wao kutoa elimu kwa wanachama wao pia watatoa bure baadhi ya huduma za vipimo kwa wakazi wa Tanga.

“Tutatoa elimu kwa umma kuhusu huduma za NHIF, elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kupima shinikizo la damu, kiwango cha sukari kwenye damu na uwiano wa uzito na urefu, pamoja na kutoa ushauri wa kidaktari,huduma hizi zinatolewa bure zikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuepukana na maradhi yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vingi”,alisema Singu.

Kwa upande wake Afisa Uanachama wa Mfuko huo, Miraji Kisile  ameeleza kuwa muitikio wa watu huenda ukawa mdogo kwa kuwa  maonesho hayo yanafanyika pembezoni mwa mji ambapo ni mbali na mjini kwahiyo ni changamoto kwa wakazi wa Mkoa huo kuja kwa wingi kwenye maonesho hayo,hivyo amewashauri waandaji wa maonesho hayo kuyasogeza karibu na watu wengi ili mwitikio uwe mkubwa.

Maonesho hayo yalianza mwaka 2013 na yanafanyika kila mwaka mkoani humo,yatafanyika kwa siku kumi kuanzia Mei 28 hadi Juni 6 mwaka huu yakijumuisha wafanyabiashara mbalimbali wakiwa na biashara za vipodozi,vifaa vya ujenzi,vitu vya asili,vyakula, samani za nyumba na maofisi  pamoja na maonesho ya wanyama.

Serikali yawatoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji mafuta ya ndege.

muh1Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

muh2Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

muh3Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaamWaziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam

muh4Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam eneo yalipo matanki ya mafuta ya kampuni ya GAPCO ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

muh6Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni wa Kampuni ya Oryx Energies Godifrey Fernandes akimuonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo baadhi ya maeneo yanapohifadhiwa mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.

muh7Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili mtasari wa kwanza kulia) akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta eneo la “Deport” ya PUMA wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta katika leo jijini Dar es salaam.

muh8Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya madereva wanaosafirisha mafuta ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

…………………………………………………………………………………………………………

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.

Hayo yamesememwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

“Mafuta ya ndege yapo na ndege zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.

Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya petroli.

Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

Imeonekana si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia hatua hiyo na hali ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza kwa wiki mbili kuanzia sasa.

Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika kwa matumizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam, Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi yanayoingia nchini.

Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com, TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies.

Mshindi wa bahati nasibu ya Taifa kupatikana kesho

1Mbunge wa zamani jimbo la Nanyumbu Dastan Mkapa (kulia) akipewa maelezo namna mshindi wa  bahati nasibu ya Taifa atakavyopatikana mara baada ya kukata tiketi ya mchezo huo katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma jana baada ya kuzinduliwa rasmi ukataji tiketi za mchezo.

2Mkurugenzi wa Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa ,Abbas Tarimba akiwaelekeza wananchi  jinsi mashine za mchezo huo zinavyofanya kazi.

3Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani akitoa maelezo ya mchezo huo kwa baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma.

4Wakala wa ukataji tiketi za mchezo wa bahati nasibu ya Taifa  mjini Dodoma Jamila Baduwel akitoa huduma hiyo kwa mmoja wa wananchi aliyetaka kununua tiketi za kushiriki.

…………………………………………………………………………………………………

Na Mwandishi wetu

Baada ya  kampuni ya Murhandizwa kutoka nchini Afrika ya Kusini ambayo ilipewa leseni ya kuendesha mchezo wa bahati nasibu ya taifa kuanza kuuza tiketi za mchezo huo wiki iliyopita ,leo (Jumamosi) ndio mchezo wa kwanza utafanyika na mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100  atatangazwa.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani International ambayo ni kampuni mama ya kampuni ya Murhandizwa,Prof .Bhongani Khumalo alisema kuwa michezo yote itaendeshwa kwa utaalamu  kwa kutumia teknolojia ya kisasa na kwa  uwazi vilevile  kuanza kwa mchezo huo hapa nchini ni mwendelezo wa michezo mingine mingi ya bahati nasibu itakayokuja baadaye.
“Kampuni yetu inao uzoefu wa muda mrefu kuendesha michezo ya Bahati Nasibu na tutahahakikisha watanzania  wananufaika na mchezo huu pia tutachangia pato la taifa kwa njia ya kodi kupitia mchezo huu.Aliongeza kuwa  uchezeshaji wa mchezo utakuwa wa wazi kupitia vyombo vya habari na mshindi atakuwa anatangazwa na kupatiwa fedha zake mara moja bila kuwepo urasimu wa aina yoyote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubatisha ya Taifa,Abbas Tarimba aliwataka watanzania kuchangamkia fursa hii kwa kununua tiketi za kushiriki katika mchezo kutoka kwa mawakala waliosambaa nchini kote ili waweze kujishindia zawadi ya mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.
Tarimba aliwataka wananchi wasiwe na hofu ya kushiriki kwenye mchezo kwa kuwa unafanyika kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali “Wananchi wasiwe na wasiwasi kushiriki kwenye mchezo huu kwa kuwa fedha zao na kanuni za uendeshaji wa mchezo vinasimamiwa na serikali.
Alisema ujio wa mchezo huu nchini mbali na kuwanufaisha  washindi binafsi utachangia kupanue wigo wa ajira kwa Watanzania wengi watakaosimamia zoezi la ukatishaji tiketi katika vituo zaidi 20,000 vitakavyofunguliwa Nchi nzima.
Tiketi za mchezo huu zimeanza kuuzwa nchi nzima na wakati wa uzinduzi wa huduma za kampuni mkoani Dodoma wananchi wengi walijitokeza kununua tiketi za kushiriki na walishauri mtandao wa kuuza tiketi ufanyike kupitia hata kwenye simu za mkononi ili kuwawezesha wananchi wengi kushiriki kununua tiketi ambayo kila moja inauzwa shilingi 500/-

Zawadi Azania Bank Kids Run zatajwa

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Runzitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kushoto ni Ofisa MasokoMwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea na kulia ni mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday. (Na Mpiga Picha Wetu)
 
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Run zitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo.
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
 
WADHAMINI wakuu wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, Benki ya
Azania, wametangaza zawadi za washindi wa mbio hizo zitakazofanyika viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Juni 5.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea,
alisema benki yake inajisikia fahari kuwekeza katika mbio hizo za watoto.
 
Alizitaja zawadi za mbio za kilomita 5 kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa
kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu,
wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na vya michezo.
 
Jibrea alibainisha kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za Kilomita 2
atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh.
50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
 
Katika mbio za Kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa
mshindi wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya
shule na michezo.
 
“Pia washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh.
15,000, begi lenye vifaa vya shule na michezo. Nia ni kuwafanya watoto
watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano, na zawadi zote za fedha
taslimu tutawawekea kwenye akaunti tutakazowafungulia katika Benki ya Azania,”
alisema Jibrea.
 
Ofisa huyo alifichua kilichowasukuma Azania Bank kudhamini mbio hizo kuwa
ni kurejesha sehemu ya pato lake kwa jamii, lakini pia kuwa sehemu ya
kuiwezesha jamii kujenga kizazi imara kinachoshiriki michezo kwa ustawi wa
taifa.
 
Kwa upande wake Mratibu wa Azania Bank Kids Run 2016, Wilhelm Gidabuday,
aliishukuru Azania Bank kwa kukubali kusapoti mbio hizo, na kuongeza kwamba kwa
kuwa msingi wa michezo yote ni mbio, basi anaamini Azania imewekeza mahali
sahihi.
 
“Hakuna mchezo duniani usiohusisha mazoezi ya kukimbia ama usiohitaji
mshiriki kuwa na mbio, iwe soka, ngumi, tenisi, nk. Ndiyo kusema Azania
imefanya uamuzi sahihi na tunawaomba wazazi na walezi wawasajili watoto wao kwa
ada ya Sh. 2,000,” alisema.
 
Alibainisha kuwa fomu za ushiriki zinapatikana katika matawi ya Azania Bank
popote jijini Dar es Salaam, ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.

TBL GROUP YALIPA KODI SHILINGI BILIONI 81

tb1Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.

tb2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.

tb3Mwandishi wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin  (hayupo pichani) kuhusiana na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa mkutano na wandishi wa habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya  mwaka  huu,mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016. \

tb4Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika  makao makuu  ya kampuni  hiyo Ilala jijini Dar es Salaam,  leo  Mei 26 2016.\

tb5Mtalamu wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi inavyozalishwa wakati walipotembelea kiwanda hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa  tathmini na waandishi hao

……………………………………………………………………………………………..

Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.

Akitoa  taarifa ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi  bilioni165 ikiwa ni kodi ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114   ikiwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo kodi ya PAYE.

TBL Group ni kampuni inayoongoza  kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.

TBL Group inajumuisha  makampuni ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited (TDL)  na  Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na vinywaji vya asili.. 

Jarrin alibainisha hayo wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia ya kisasa

Kampuni inavyo viwanda 10 nchini na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa ubora duniani.

Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza  mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni   – Konyagi, Valuer and Dodoma Wine –  Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba –   Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya  pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini ni asilimia 50%

 Jarrin aliendelea kueleza kuwa TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.

Pia imebainishwa kuwa zaidi ya wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya  Bihawana, Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia  mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.

Jarrin pia alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na  katika mazingira ya usafi yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.

Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.

Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza  kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili  ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha  vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin

Makandarasi 4572 wafutiwa leseni nchini

mg5Bodi ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya mwaka 1997.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bw. Nkhori amesema kuwa katika jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi 2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia 68.5 haikuwa na kasoro.

Ameongeza kuwa miradi mingine ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa, kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa sheria.

Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.

Licha ya mafanikio hayo CRD ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao, waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la ajira,”alisema Bi Ngimbwa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Mkutano huu pamoja na mamabo mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”

TTCL YAZINDUA NEMBO MPYA NA HUDUMA YA 4G LTE

FO1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na wadau wa Sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani), wakati uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO2Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE

FO3Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura akielezea mafanikio ya TTCL kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua nembo mpya ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salam.

FO5Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati wa halfla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO6Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakifatilia sherehe za uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

…………………………………………………………………………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya (TTCL), kuwa wabunifu ili kuhimili ushindani wa soko katika sekta ya mawasiliano na hivyo kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida.

Akizungumza wakati akizindua nembo mpya ya kampuni ya TTCL na huduma ya 4G LTE inayowezesha huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa haraka Prof. Mbarawa amesema huu ni wakati wa kubadili mtazamo na kufanya kazi kisasa ili kuvutia wananchi kutumia huduma za TTCL.

“TTCL lazima mubadilike ili muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amewataka TTCL kuhakikisha kituo mahiri cha kutunzia taarifa (Data Centre), kinaanza mapema mwezi Juni ili kuwezesha wadau wengi kunufaika na kituo hicho.

Prof. Mbarawa amesema Serikali inaunga mkono TTCL na imetenga masafa ya 800 MHZ ambayo yataiwezesha TTCL kushindana na makampuni mengine ya watoa huduma ya mawasiliano na kuwaunganisha wateja wengi kutumia huduma za mawasiliano na data.

“Uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL na huduma ya masafa ya 4G LTE uendane na ubunifu kwa wafanyakazi ili muwavutie watumiaji wengi wa simu na hivyo kupata soko kubwa na kuifanya TTCL kuchangia kikamilifu pato la taifa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema mawasiliano ni kiungo muhimu cha kufanikisha ukuaji wa sekta za kilimo, taasisi za fedha, uwekezaji, ujasiliamali na utendaji kazi wa Serikali na sekta binafsi hivyo ubunifu katika utendaji utaiwezesha TTCL mpya kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amewataka wananchi kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu namna ya kuzitambua simu na vifaa feki na hatua za kufuata ili ifikapo Juni 16 zoezi la kuzifunga simu feki litakapotekelezwa wasiathirike.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi. Edwina Lupembe amesisitiza kwamba TTCL imejipanga kuboresha huduma za fedha ili kuwezesha watumiaji wengi wa kampuni hiyo kunufaika na huduma ya kutuma na kupokea fedha.

“Tumekamilisha mradi mkubwa wa kusimika mitambo ya GSM, UMTS na LTE ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano 2G, 3G na 4G”, amesema Bi. Lupembe

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mabadiliko ya muonekano wa TTCL yataendana na mtazamo mpya wa wafanyakazi wenye lengo la kuiwezesha kampuni hiyo kuwa ya kisasa hapa nchini.

Amesema TTCL imejipanga kuboresha simu za mezani, mkononi, na huduma za intaneti ya haraka ili iweze kupata wateja wengi na hivyo kuongeza mapato yake.

“Teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE imeongeza nguvu kwa kampuni yetu kuleta ushindani katika soko la mawasiliano na zitaendelea kuongeza ufanisi na ubunifu wa huduma zetu kwa bei nafuu”, amesisitiza Dkt. Kazaura.

Tayari huduma ya 4G LTE inapatikana katika maeneo mengi ya Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.

RaisDk. John Pombe Magufuli akemea vitendo vya Rushwa kwa wakandarasi

MF01Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano  wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

MF1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam

MF2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.

MF3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.

MF4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.

MF5Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

………………………………………………………………………………………………………………….

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.

Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mnaweka viwango vikubwa vya fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya kutoa rushwa, kwa nini mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na kuwambia kuwa kama wapo watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili wapate kazi waitaarifu Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.

Mhe. Rais amewataka wakandarasi wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya wasiwe wanaweka viwango vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni.

 Akitoa mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati ya shilimgi milioni  670 na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa kazi.

Amesema serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.

Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo.

Kuhusu ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.

Amesema wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano  wako katika ujenzi wa mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye  uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi hawakosekani.

RAIS DKT. MAGUFULI AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUWA WAZALENDO

mg3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo vya rushwa katika maeneo ya Kazi.

mg1 Baadhi ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

mg4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

mg5Kaimu Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa kipaumbele makandarasi wazawa na kukabiliana na changamoto zinazowakabil.

mg6Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa akiongea na wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi wazawa kufanya kazi kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa makandarasi wenye nia ya kuwakwamisha.

mg7Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakandarasi  nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwaahidi makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi mbalimbali za ujenzi nchini.

mg8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

mg9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

mg10 mg11

Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Wakandarasi na viongozi wa mkoa wa Wizara ya Ujenzi wa mkoa wa Dar es salaam.

mg12Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).

mg13

WANAHISA WA BENKI YA POSTA TANZANIA, TPB, WAUPONGEZA UONGOZI WA BENKI HIYO KWA UENDESHAJI BORA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Be.Sabasaba Moshingi,(kushoto), akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo jijini Dar end Salaam Leo Mei 25, 2016. Wajumbe walipokea taarifa ya uendeshaji Benki hiyo kwa mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na mipango ya uendeshaji wa Benki kwa mwaka huu wa 2016. Pamoja na mambo mengine, Bw.Moshingi alisema benki inampango wa kuingia kwenye soko la his a(Dar es salaam stock exchange), sambamba na kuongeza Huduma za ATM kwenye matawi yake mbalimbali kote nchini. Katikati no Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, na kulia in Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki hiyo, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.Wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupokea taarifa ya mahesabu ya fedha iliyosomwa na Meneja wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Nexia SJ Tanzania, Bw.Fulgensio Mgaya, ambaye alisema mahesabu ya Benki hiyo hayakukutwa na dosari, wajumbe wa mkutano huo, Bi.Theresia A Chitumbi na Bw. James Sando, wameupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa usimamizi thabiti na uendeshaji mzuri wa Benki. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said). 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice
Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki
hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi
wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki,
upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa
wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence
Mafuru, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Hamisi Mussa Omar.

Mwenyekiti akiendesha kikao cha wanahisa wa TPB.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice
Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki
hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi
wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki,
upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa
wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence
Mafuru a
kizungumza kwenye mkutano huo

Wakurugenzi wa idara mbalimbali za TPB, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko
Katibu Mkuu wizara ya fedha serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar(kulia), na Mkurugenzi wa sheria na Katibu wa Bodi ya TPB, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.
 Picha ya pamoja ya uongozi wa TPB, na wanahisa waliohudhuria mkutano huo
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sa asaba Moshingi, akipitia makabrasha
 Katibu Mkuu wizara ya fedha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw.Hamisi Mussa Omar. (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Bw.James Sando wa TPC.
 Msajili wa Hazina kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Lawrence Mafuru, (kushoto), akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi
Mwenyekiti wa Bodi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (kulia), akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Bw. Sabasaba Moshingi

MAONYESHO YA BIDHAA ZA PLASTIKI, KUFANYIKA MEI 27-29 MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo jioni kuhusu maonyesho hayo.
Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi Hamza Mohamed Hamza akizungumza katika mkutano huo.
Taswira meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Africa-PPB Tanzania, Mohamed Sami akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Khaled Abu El M karem akizungumza kwenye mkutano huo.
………………………………………………………………………………..
Na Doto Mwaibale
 
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya kwanza  ya bidhaa za plastiki, mpira, kemikali za petrol na ujenzi  yanayotarajiwa kufanyika katika  Mei 27 hadi 29 mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Mlimani City jijiniDare s Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat,  alisema nchi zote za Afrika Mashariki na kati zitashiriki katika maonesho hayo.
Alisema Maonesho ya Afrika –PPB-EXPRO yatakuwa ni jukwaa la kipekee la bidhaa mpya  na yatatoa mwanya wa kuyaelewa  masoko yake ambayo hayafahamiki vizuri.
 “Maonesho haya yamebuniwa kwa lengo la  kukuza umoja miongoni mwa Waafrika kwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara  kati ya Misri na Tanzania na hali kadhalika  kuyaweka masoko yake kwenye ramani ya Afrika,kubainisha  kuwa Tanzania ni ya kwanza  katika orodha ya nchi za Afrika ambapo Africa-PBB-EXPO imepanga kushirikiana nayo.
“Aramex Africa ni mshirika rasmi wa usafirishaji wa Africa-PBB-EXPO na itakwua inatoa mchango mkubwa katika kutoa huduma za ugavi na usafirishaji  kutoka Misri hadi Tanzania,” alisema.
Alisema kupitia Aramex na kwa uratibu wa TanTrade na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Africa-PBB-EXPO  inatoa fursa ya kipekee kwa waoneshaji  walio na kanzidata za kina kusajiliwa mara zinapopokelewa.
Alieleza kwamba kanzidata hizo zinajumuisha hali ilivyo ndani ya soko la Tanzania na thamani yake pamoja na takwimu sahihi ya kuuza na kuagiza, hii inatoa  fursa ya uhakika kwa mikutano ya mkakati ya B2B pamoja na ufanisi unaohusiana pindi zinapofika.
Barakat alitoa wito kwa wafanyabiashara kushiriki katika maonesho hayo ili kuweza  ‘kubaini fursa za ushirikiano katika masoko haya mapya pamoja na mtandao ulio na wateja na wenza wa kibiashara. 
“Kwa kushiriki katika maonesho ya Africa-PPB-EXPO, pamoja na mambo mengine washiriki watajifunza jinsi maudhui ya kina ya sekta yanaweza kuathiri biashara zao,  umoja uliopo miongoni mwa viongozi wa sekta, kupata washirika wapya na kulinganisha kiwango chao katika mitazamo ya ubunifu.
“Kampuni ya EXPO ONE ambayo ni mwandaaji, ni taasisi ya kati ya  usimamizi wa mikutano na maonesho ambayo imejikita katika  kuandaa na kutoa huduma kwa maonesho ya  biashara ya kimataifa  pamoja na 
kuyatangaza mabanda ya Misri katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.
 Alisema kwamba maonesho mengine  ya Africa-PPB-EXPO yanatarajiwa kufanyika nchini Senegal na baadaye nchini Angola.

Darbrew yapata tuzo ya uboreshaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller

1Mkurugenzi wa kampuni ya  Darbrew Limited inayotengeneza Chibuku,David Cason  akiongea na wafanyakazi wakati ya hafla ya kusherehekea kushinda  tuzo ya uendelezaji vinywaji vya asili kutoka SABMiller  iliyofanyika kiwandani hapo jana.

2Wafanyakazi wakifuatilia matukio

3Maofisa waandamizi wa kampuni wakati wa sherehe hiyo.

4 5Mkurugenzi na wafanyakazi wakifurahia tuzo.

6Wafanyakazi katika picha ya pamoja.

………………………………………………………………………….

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Darbrew inayotengeneza pombe ya Chibuku imetunukiwa  tuzo kutoka SABMiller  ya uendelezaji vinywaji vya asili nchini katika kongamano la masoko la viwanda  lililofanyika mjini Cape Town nchini Afrika ya Kusini.

Darbrew iliyopo chini ya TBL Group iliibuka kidedea baada ya kushindanishwa na viwanda vinavyotengeneza vinywaji vya kienyeji vilivyopo chini ya SABMiller vilivyopo katika nchi za Botswana,Malawi na Uganda.

Akitangaza mafanikio hayo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi Mkuu wa Darbrew, David Cason alisema kuwa tuzo hiyo ni mafanikio makubwa kwa kampuni na aliwapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma na kuhakikisha yanapatikana mafanikio siku hadi siku.

“Tuzo hii sio ya mtu mmoja imepatikana kutokana na mchango wa kila mfanyakazi wa DarBrew na inabidi kuongeza bidii zaidi katika kazi ili mafanikio zaidi yapatikane na kampuni izidi kusonga mbele na kuwa miongoni mwa makampuni makubwa ya vinywaji katika ukanda huu wa Afrika Mashariki”.Alisema Cason.

Alisema hatua ya kampuni kushindanishwa na viwanda vikubwa na kuibuka na tuzo ni jambo la kujivunia kila mfanyakazi  na aliwashukuru mawakala na wateja wote wa Chibuku kwa kuunga mkono biashara ya kampuni.

Kwa upande wake Meneja wa Mauzo wa DarBrew,Freddy Kazindongo alisema aliwapongeza wafanyakazi na kuwashukuru wateja kwa mafanikio yaliyopatikana na kuongeza kuwa kampuni imejizatiti kuongeza zaidi ubora wa huduma za uzalishaji na usambazaji na kuhakikisha kinywaji cha Chibuku kinawafikia wananchi popote walipo na wanakipata kulingana na kila mtu na uwezo wake .

Katika kuthibitisha hilo alisema wiki hii kampuni imezindua chibuku super ya mililita 750 ambayo itawawezesha wateja kupata  kinywaji  hicho kwa gharama nafuu.

Kazindogo alisema mkakati wa kampuni ni kuhakikisha  urasimishaji wa pombe za kienyeji unafanikiwa ambapo wananchi wataweza kupata kinywaji cha asili katika mazingira bora ya usafi wakati huohuo wakikinunua wanachanga pato la serikali kwa njia ya kodi kitu ambacho hakipo kwa pombe nyingine za asili.

Pia alisema kuwa kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja  ambazo zinawawezesha mawakala wakubwa na wadogo na akina mama wanaouza pombe za asili kujipatia mapato ya uendesha maisha vilevile kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na akina mama waliokuwa wanapika pombe za asili kwa kutumia kuni na mkaa watakuwa wanauza pombe ambayo tayari imetengenezwa badala ya kutumia muda mwingi kutengeneza pombe.

Serikali yawezesha vikundi 1,200 vya wakulima kupata masoko.

indexNa Raymond Mushumbusi MAELEZO

……………………………………………….

Serikali imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo wadogo nchini ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.

Akizungumza kuhusu mradi wa kuboresha miundombinu ya masoko,uongezaji wa thamani na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) Mratibu wa Taifa wa Mradi huo Bw. Walter Swai amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza kipato cha wakulima na uhakika wa chakula kwa kutengeneza miundombinu ya upatikanaji wa masoko kwa wakulima kwa kuboresha barabara za kutoka mashambani kuelekea sokoni na kuwapa taarifa sahihi kuhusu masoko na mahitaji yake.

Bw Walter Swai ameongeza kuwa lengo la mradi ni kufikia vikundi 1,600 kwa nchi nzima katika kutoa elimu ya kuwezesha wakulima kupata masoko ya mazao yao ikiwa ni jitihada za Serikali kuwawezesha wakulima hao kujikwamua kiuchumi.

“Nia yetu ni kufikia vikundi 1,600 katika mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na hadi sasa tumefika asilimia 75 ya lengo tulilojiwekea la kuwawezesha wakulima wadogo kupata masoko ya mazao yao” alisema Bw.Swai.

Naye Mtaalamu wa Masoko ya mazao ya kilimo wa MIVARF Bw. Muhoni Leonard amesema kuwa mradi huo utasaidia kuwapa wakulima taarifa sahihi juu ya masoko na mahitaji yake na kupunguza gharama ambazo zilikuwa zinatumika kwa ajili ya kupata taarifa hizo kutoka kwa madalali.

“Azma ya mradi huu ni kubadili muundo na utendaji wa wakulima wadogo kuongeza ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa masoko ya mazao husika” alisistiza Bw Leonard.

Aidha, mmoja wa wakulima na msindikaji wa mchele kutoka Wilaya ya Chato mkoani Geita Bw.Joseph Nchimani amesema kuwa elimu aliyoipata kutoka MIVARF imemuwezesha kuendesha kilimo cha mpunga kwa njia ya kisasa ambayo imemuwezesha kuongeza thamani ya mchele kwa kuufunga kwenye mifuko iliyo katika hali ya

ubora unaokubalika kwenye soko.

“Kabla ya kuanza kufunga mchele kwenye mifuko nilikuwa nauza jumla ya tani mbili mpaka kumi kwa mwaka ila baada ya MIVARF kuja na kunipa elimu hii nimeweza kuuza mpaka kufikia tani 50 kwa mwaka” alisistiza Bw.Nchimani.

Program hiyo ya MIVARF inajushughulisha pia na kutoa huduma za kifedha vijijini ambayo ni ya miaka saba inayotekelezwa kwa mikoa 30 ya Tanzania Bara na Visiwani na inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

AHADI YA RAIS JPM KUHUSU MAJI MJI WA ILULA KUTEKELEZWA -WAZIRI LWENGE

Bw Venance Mwamoto
…………………………………………………………………………………………..
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI  wa maji na  umwagiliaji mhadisi Geryson Lwenge amewaondoa  hofu   wananchi  wa  mji  wa Ilula  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa kuhusu  ahadi  ya Rais Dr John Magufuli ya  kumaliza kero ya  maji  katika  mji  huo  wa Ilula kuwa  itaanza kutekelezwa mwaka  huu.

Alisema  kuwa serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dr Magufuli  ni  serikali ya ukweli na  uwazi na ni  serikali ya  hapa  kazi Tu  hivyo kila ilichoahidi  kukifanya  itafanya kwa  wakati na  kuwataka  wananchi  kuendelea kujenga  imani  zaidi.
 
Waziri mhandisi  Lwenge aliyasema  hayo jana katika Mgahawa wa Bunge mjini  Dodoma , wakati  akizungumza katika  kikao chake na mbunge wa  jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mbunge wa viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati na wawakilishi   11 wa wananchi  wa mji  wa Ilula waliofika bungeni  mjini Dodoma kufuatilia ahadi ya maji  iliyotolewa na Rais Dr  Magufuli  wakati wa kampeni kwa wananchi  wa mji  wa Ilula .  

 Mwamoto  akishiriki na  wananchi wa mji wa Ilula  kukingas maji ambayo hutoka kwa mgao 
………………………………………………………………………………………………
Alisema  kuwa wizara  yake  imekwisha  ingiza  katika bajeti  yake ya mwaka 2016/2017 itakayosomwa mapema wiki  hii na  kuwa mbali ya  maeneo  mengine ambayo  yatapatiwa ufumbuzi  wa  kero ya maji mji  wa Ilula ni  miongoni mwa maeneo  hayo .

Waziri  huyo  alisema  kuwa lengo la  serikali ni  kuendelea  kusogeza  huduma ya  maji kwa  wananchi  wake na  kutekeleza ahadi  zake kupitia  ilani ya uchaguzi ya  chama tawala hivyo.

Hata  hivyo  waziri Lwenge  alimpongeza mbunge  wa Kilolo Bw Mwamoto na mbunge Kabati  kwa kuendelea  kupambana  bungeni kwa ajili ya kuwatumikia  wananchi  wao na  hata   kufuatilia baadhi ya ahadi  na  kuwa hatua hiyo ni nzuri na  inaonyesha  ni  kiasi gani wabunge  wao  walivyokaribu na changamoto  za  wananchi  wao.

Mbali ya waziri Lwenge  kuzungumza na  wananchi hao pia  mbunge  Mwamoto  aliwakutanisha  wananchi hao na  waziri  wa Kilimo ,mifugo na Uvuvi  Mwigulu Nchemba ambae katika  kikao  chake na  wananchi hao  alieleza mkakati wa   wizara yake  kushirikiana na  wizara ya viwanda na biashara pamoja na  wizara ya vijana na ajira ili  kuanzisha viwanda  vidogo vya  nyanya katika  mji  wa Ilula na  kuwa kazi ya  wizara  yake ni  kutoa mafunzo ya  kilimo cha  kisasa cha nyanya na  kuwawezesha  wakulima hao  wa mafano mpango ambao   utafanyika katika kanda mbali mbali ila kwa nyanda za juu  kusini  wanakusudia  kuufanya  wilaya ya Kilolo .

Kijana  wa Ilula  akichambua nyanya

Kwa  upande  wake waziri  wa vijana na ajira Antony Mavunde alisema  kuwa wizara  yake  ipo  tayari  kuwasaidia  vijana katika  wilaya ya  Kilolo kwani  tayari  wameonyesha  nia ya  kujikwamua  kiuchumi  kupitia  kilimo  cha nyanya na  kuwa kazi ambayo  mbunge na  viongozi wa wilaya ya  Kilolo wanapaswa  kuifanya ni kuwaunganisha  vijana  hao katika  vikundi na kuanzisha  Saccos zao  ili  pesa  itakapotolewa na  serikali  kupitia katika  saccos  hiyo .

Alisema  kuwa upo  uwezekano wa vijana hao  kuanzisha  kilimo  cha  nyanya  na  kuwa na  viwanda  vidogo  vya  kuchakata  nyanya na  kuziuza badala ya  sasa  kuuza kwa hasara.
Mbunge  wa Kilolo Bw.  Mwamoto aliwapongeza  mawaziri  hao  kwa kuonyesha  utayari  wao katika  kuwasaidia  wananchi  wa Kilolo na  kuwa kilio  kikubwa kwa  wananchi wa mji wa Ilula ni maji ,masoko ya uhakika  ya mazao na hivyo  kusaidiwa maji na vijana  kupata viwanda  vidogo  vidogo  wataweza  kukuza  kilimo cha  kisasa  zaidi.

 Katika ziara  yao  hiyo  bungeni wananchi  hao  ambao ni  wawakilishi  wa  wananchi wa Ilula  waliongozana na katibu  wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya ya  Kilolo Bw Clemence Mponzi na  aliyekuwa diwani wa Ilula Anna Msolla, Peter Mdanginyali , diwani wa kata ya Mlafu Bw  Isdori Kihenge , Vicent Gaifalo,Anna
Msolla, kada  wa hadema Bw Khalid  Muhel , Jocob Ngusulu
,Uzebeo Mhando  na katibu tarafa ya
Mazombe Bw. King’ung’e

MAKAMPUNI 52 YAJITOKEZA KUWEKEZA SEKTA YA UMEME

lu7Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………………………………………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi sasa Serikali imekwishapokea maombi 52 kutoka makampuni mbalimbali ambayo yanataka kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia.

“Haya maombi yamekwishapokelewa na wenye makampuni wamekwishahojiwa kuangalia uwezo walionao katika suala zima la uwekezaji wanaotaka kuufanya, na tukiwapata wenye uwezo na wenye nia ya dhati watapatiwa miradi ya kuiendesha,” alisema.

Aliwataka Watanzania hao waishio Zambia watumie fursa ya uwepo wao huko kutafuta marafiki ambao wanaweza kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali nchini kwani Serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu wakati wananchi wanahitaji kupatiwa huduma muhimu.

“Serikali peke yake haiwezi kufanya kazi ya uwekezaji kwa hiyo tunahitaji kushirikiana na sekta binafsi, taasisi za kifedha na washirika wa maendeleo na ndiyo maana kule kwenye mkutano nimewaeleza washiriki kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi.

Alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika kutawezesha wananchi wengi zaidi kujiingiza katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuinua uchumi wa nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Alisema malengo ya Serikali ya awamu ya tano ni kuona kuwa nchi inakuwa na mitambo mingi ya kuzalisha umeme na umeme wote unaozalishwa na mitambo hiyo inaunganishwa na gridi ya Taifa ili kuondokana na tatizo la mgao wa umeme nchini.

Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati vikiwemo gesi asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo, nishati ya joto kutoka ardhini (geothermal energy) na nishati inayotokana na vinyesi vya mifugo (biomass) ambayo alisema vinatumika kwa watu wachache (siyo kitaifa).

Alisema kupatikana kwa gesi asilia nchini kumeleta neema ambapo mabomba ya gesi yamekwishajengwa kutoka Mtwara hadi Kinyerezi na kutoka Kilwa-Songosongo hadi Dar es Salaam. “Sasa hivi kuna utafiti unaendelea juu ya uwezekano wa kusambaza gesi ya kupikia majumbani. Tumeanza pale Mikocheni (DSM) na sasa hivi wanafanya utafiti mwingine kule Mtwara ili wananchi waweze kutumia gesi hii kupikia badala ya mkaa,” alisema.

Akielezea kuhusu uwekezaji kwenye makaa ya mawe, Waziri Mkuu alisema Serikali imelenga kutumia makaa ya mawe ili kuendeshea mitambo ya kwenye viwanda vikubwa badala ya kutumia umeme au mafuta ya dizeli kama inavyofanyika sasa. “Baadhi ya wenye viwanda wanabadilisha mifumo ya kuendeshea mashine zao ili iweze kuendana na teknolojia ya makaa ya mawe pindi tu uchimbaji ukishika kasi,” alisema.

Akifafanua kuhusu juhudi za Serikali katika kusambaza nishati ya umeme, Waziri Mkuu alisema tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), vijiji zaidi ya 3,000 katika ya vijiji 12,000 vilivyopo nchini vimefikiwa na nishati ya umeme.

“Tulianza na REA awamu ya kwanza, awamu ya pili na sasa tunaenda awamu ya tatu. Hata mkipiga simu kwa ndugu zenu vijijini, mtakuta katika kila kata kuna vijiji kati ya vinne hadi vitano ambavyo vimefikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa REA,” alisema.

Waziri Mkuu amerejea nchini leo (Jumatano, Mei 25, 2016).

TANESCO yawataka wateja wake kuunganishiwa umeme na mafundi waliosajiliwa.

TAN1Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige  Mabulla.

………………………………………………………………………………………………..

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Shirika la Umeme Tanzania Nchini (TANESCO) limewataka wateja wake kuhakikisha wanaunganishiwa umeme na mafundi au wakandarasi waliosajiliwa na shirika hilo ili kupunguza ajali za moto.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Afya na Usalama kazini wa TANESCO, Mhandisi Majige  Mabulla alipokua akiongea na waandishi wa habari juu ya vyanzo vya ajali za moto vinavyosababishwa na umeme.

Mhandisi Mabulla alisema kuwa matukio ya moto yanayosababishwa na umeme hutokea kutokana na kuzalishwa kwa joto kali ndani ya nyaya kunakosababishwa na umeme kuwa mkubwa kuliko uwezo, kulegea kwa maungio ya nyaya pamoja na radi au nyaya za umeme kuangukia juu ya paa la nyumba.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mabulla aliongeza kuwa ajali za moto zinazosababishwa na umeme huanza kama unavyoanza moto wa kiberiti au viwashio vinginevyo vya moto na husambaa haraka kwa kutegemea na aina ya vitu vilivyopo kwenye eneo husika kwa kuwa baadhi ya vitu hushika moto haraka na kuenea kwa kasi.

“Ajali za moto zinazosababishwa na umeme ni ngumu kutokea kama umeme utasukwa na mtaalam aliyebobea kwenye fani hiyo, TANESCO tunatoa wito kwa wateja wetu kuhakikisha wanafungiwa umeme na fundi au mkandarasi aliyesajiliwa na kampuni yetu,”alisema Mabulla.

Pia Mhandisi Mabulla alisema ili kuepukana na ajali za moto zinazotokana na hitilafu za umeme wateja wanapaswa ;kuepuka kupitisha nyaya za umeme juu ya paa za nyumba, kutokuunganisha umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine bila kupata maelekeza kutoka TANESCO.

Aidha Mhandisi Mabula alisema wateja pia wanapaswa kuhakikisha mfumo wa umeme unapitiwa upya kila baada ya miaka mitano pamoja na kuwa makini katika utumiaji wa vifaa vinavyotumia umeme kama vile pasi, hita za umeme.

MACHINGA, MFUPA ULIOISHINDIKA HALMASHAURI YA JIJI MWANZA.

Ipo kauli isemayo “Mfupa Uliomshinda Fisi” ikiashiria jambo gumu mithiri ya mfupa mgumu ambao umemshinda fisi ambae ni mnyama bingwa wa kutafuna mifupa ya kila aina.

Source http://binagimediagroup.blogspot.com

Ndivyo unaweza kusema ukiitazama picha hizi, kwani suala la kuzagaa ovyo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kwa jina la Machinga jijini Mwanza, ni mfano halisi wa mfupa ulioshindikana kutafunwa na halmashauri ya jiji la Mwanza.
 
Mara kadhaa juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kuwaweka wafanyabiashara hao katika mpangilio mzuri kwa ajili ya wao kufanya biashara katika maeneo rasmi yaliyotengwa lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwani mafanikio yake yakishindwa kuwa ya kudumu licha ya nguvu kubwa kutumika.
 
Kabla ya kipindi cha kampeni za Uchaguzi mkuu mwaka jana, halmashauri ya jiji la Mwanza ilifanikiwa kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi lakini baada ya kampeni kuanza, machinga walirejea mitaani kwa kasi ya ajabu na hakuna aliewagusa tena ambapo hivi sasa kila kona ya jiji la mwanza machinga wamezagaa ovyo.
 
Baadhi  ya Machinga jijini Mwanza wanaomba sekta hiyo kuboreshwa ili kuondokana na changamoto zinazowakabiri ikiwemo kukosa
maeneo maalumu kwa ajili ya wao kufanyia biashara hatua ambayo itasaidia
kuondokana na kadhia mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mgambo wa jiji wanaokuwa
wakiwaondoa katika maeneo yasiyo rasmi kufanyia biashara.

TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA – MAJALIWA

lu6WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa – Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema  upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Continue reading →

Kampuni ya TBL Group yaendesha zoezi la kutathmini wafanyakazi wake

index1 Afisa Rasilimali watu katika kiwanda cha TBL mkoani Mwanza, Dorah Nyambalya akifanya tathimini ya kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho jana.
index2Baadhi ya wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la tahmini kiwandani hapo leo
……………………………………………………………………………………………………….
Kampuni ya TBL Group kuanzia leo imeanza kuendesha zoezi la kutathmini wafanyakazi wote katika viwanda vyake vyote vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro.
Lengo kubwa la kuendesha zoezi hilo limeelezwa kuwa ni kujua changamoto wanazokabiliana nazo wafanyakazi katika majukumu yao ya kila siku ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuleta ufanisi wenye tija katika kazi.
Katika kutekeleza zoezi hilo wafanyakazi walijaza fomu maaalumu zenye maswali ya kiutendaji chini ya usimamizi wa watendaji wa idara ya Raslimali watu ambao yalihusu utendaji wao,changamoto wanazokutana nazo pia walipata fursa ya kutoa maoni yao ni jinsi gani ya kuboresha mazingira ya kazi na kuwaendeleza wao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Serikali kuboresha mazingira ya biashara ili kuongeza uwekezaji

tp1Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua(Kushoto) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara katikati ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.

tp2Wadau wa biashara kutoka sekta za umma na binafsi wakifatilia mkutano uliofanyika leo uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.

tp3Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi(Kulia) akijibu maswali toka kwa wadau wa bishara(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye. Picha zote na Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

……………………………………………………………………………………………………….

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuongeza uwekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua wakati akifungua mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara.

Dkt. Hamis Mwinyimvua amesema Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuandaa sera ambazo zitawasaidia wafanyabishara kuwekeza katika sekta mbalimbali.
“Tutahakikisha tunaboresha mazingira ya biashara kwani hakuna uwekezaji utakaowezekana kama mazingira ya ufanyaji wa biashara yatakuwa hayaridhishi.” Alisisitiza Dkt Mwinyimvua.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi amesema kuwa kuna haja ya Taasisi zote za umma na binafsi kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha mazingira ya biashara.
Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeanza kufanya maboresho katika mazingira ya uwekezaji.

Akifafanua kuhusu maboresho hayo Simbeye alisema kwasasa ujasili wa makampuni unafanyika kwa kutumia mfumo wa kieletroniki ambapo muombaji anaweza kusajili kampuni pasipo kufika katika Ofisi za BRELA katika kipindi cha muda mfupi.

Mkutano huu uliondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Baraza la Taifa la Biashara, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakishirikiana na taasisi za umma na binafsi umedhamiria kuwezesha wafanyabiashara na wawekezaji kuwa mazingira mazuri ya kufanya biashara

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM MKUTANO WA ADB – LUSAKA

lu1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

lu3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

lu4Rais wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

lu6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

lu8Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SHERIA MPYA YA USHIRIKA YAWANUFAISHA WAKULIMA WA TUMBAKU

indexNa Fatma Salum- MAELEZO, Dodoma.

Serikali imebainisha kuwa Sheria Mpya ya Ushirika (Sheria namba 6 ya mwaka 2013) imesaidia kupunguza changamoto za wanachama wa Vyama vya Ushirika pamoja na wakulima wa Tumbaku nchini.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Mhe. Tate William Ole-Nasha aliyasema hayo leo bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Mhe. Ole-Nasha alisema kuwa baadhi ya marekebisho ya Sheria hiyo yanayowanufaisha wanachama wa Vyama vya Ushirika wakiwemo wakulima wa tumbaku ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu wa vyama hivyo.

“ Katika maeneo yanayolima tumbaku viongozi wabadhirifu wa Vyama vya Ushirika 26 Mkoani Ruvuma  wakiwemo Maafisa Ushirika wawili wamesimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.” alisema Ole-Nasha.

Pia Mhe. Ole-Nasha alifafanua kuwa sheria ya sasa inakataza vyama kukopa zaidi ya asilimia 30 ya mali zake (Own Capital) ili kuzuia vyama hivyo kuingia kwenye madeni makubwa yasiyolipika  na hatimaye kusababisha migogoro ndani ya vyama.

Akizungumzia mafanikio upande wa tozo, Ole-Nasha lisema kuwa kuanzia sasa Mkutano Mkuu utakuwa chini ya uenyekiti huru utakaochaguliwa na wajumbe wa mkutano huo kinyume na awali ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu. 

“Lengo ni kulinda maslahi ya wakulima ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa tozo zote zinazoidhinishwa na Mkutano Mkuu zinakuwa na maslahi kwa wakulima wa Tumbaku.” Aliongeza Ole-Nasha.

Kwa mujibu wa Ole-Nasha Serikali inatambua uwepo wa kodi nyingi na tozo kwenye mazao mbalimbali ya chakula na biashara hivyo kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara katika sekta ya kilimo kwa kupitia upya taratibu, vibali, tozo, kodi, ushuru na ada nyingine zinazotozwa ili kutoa nafuu kwa wakulima.    

Kampuni ya Vision Investiments yatoa fursa kwa makampuni mengine.

indexMkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Vision Investiments  Ally Nchahaga (katikati) akifafanua juu ya fursa zitolewazo na Kampuni yao leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Aisha Mohammed na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Kampuni ya Mafuta ya Lake Oil  Aluwy Amar.

…………………………………………………………………………………………………………………..

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Kampuni ya Vision Investments imetoa fursa kwa makampuni mengine kushiriki kutoa huduma mbalimbali wakati wa makutano baina ya wanunuzi na wauzaji wa magari yanayoandaliwa na Kampuni hiyo yatakayofanyika Mei 29 mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni hiyo Ally Nchahaga ambaye amewaomba wauzaji na wanunuzi wa magari pamoja na makampuni mbalimbali kushiriki katika makutano hayo ili kutimiza mahitaji yao ya magari.

“Kama ilivyo ada kila Jumapili ya mwisho wa mwezi Kampuni yetu inawakutanisha wauzaji, wanunuzi wa magari pamoja na makampuni tofauti kutoa huduma shirikishi zinazokwenda sambamba na biashara hii ya magari ya watu binafsi” alisema Nchahaga.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Vision Investments makutano hayo yatafanyika nchini kwa mara ya sita ambapo mwaka huu yatafanyika katika viwanja vya Coco Mihogo kuanzia sa 4 asubuhi.

Nchahaga alizitaja baadhi ya kampuni zinazotoa huduma shirikishi zikiwemo Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), Kampuni ya Mafuta ya Lake Oli, Kampuni ya Coca cola, pamoja na Kampuni ya Simply Elegant ambazo zinatoa huduma za mikopo ya magari, mafuta ya magari, vinywaji pamoja na vilainishi vya magari kwa wateja watakaokuwepo katika makutano hayo.

Aidha, Nchahaga amesisitiza kuwa kampuni yao sio ya maonyesho ya magari wala wao sio madalali bali ni kampuni inayotoa fursa yenye gharama nafuu kwa wanachi kutimiza mahitaji yao ya magari.

Ameongeza kuwa elimu kuhusu magari na vifaa vyake itatolewa bure na mtu yeyote atakayehitaji kuuza gari lake atachangia shilingi elfu 50 ikiwa ni mchango wa kuweka gari lake katika viwanja hivyo pamoja na kufanyiwa matangazo katika mitandao ya kijamii kwa mwezi mzima.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mauzo cha Kampuni ya Mafuta ya Lake oil Aluwy Amar amesema kuwa Kampuni yao inatoa huduma mpya ya kulipa kwa kutumia kadi itakayomrahisishia mteja kupatiwa huduma za mahitaji ya mafuta ya magari yao kwa hiyo, watashiriki katika makutano hayo ili kutoa elimu kwa wateja hao kuhusu matumizi ya kadi hizo.

“Huduma hii tumeianza kuitoa kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huduma za kupatiwa kadi pamoja na kufanya miamala yote ni bure pia mwisho wa mwezi tutatoa huduma ya punguzo la bei kulingana na matumizi ya mteja”,alisema  Amar.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Aisha Mohammed amesema kuwa wamefurahi kupata fursa hii ya kushiriki katika makutano hayo kwakua anaamini ni njia moja wapo kwa benki hiyo kuwapa mikopo au kuwanunulia magari wateja wao ili kutimiza ndoto zao kwa muda muafaka.

 

SERIKALI KUZITAMBUA NA KUZIRASIMISHA BANDARI BUBU ZILIZOKIDHI VIGEZO KWA LENGO LA KUKUSANYA KODI.

Na.Aron Msimagesigwa – MAELEZO

.DODOMA.

Serikali imesema kuwa inaendelea na utaratibu wa kuzitambua na kuzirasimisha bandari Bubu zote zilizokidhi vigezo ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara kupitisha bidhaa mbalimbali ili ziweze kuchangia katika Pato la Taifa kulingana na  wingi wa bidhaa zinazopitishwa katika bandari hizo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu maswali ya Wabunge waliotaka kujua mkakati wa Serikali katika kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu kupitia bandari bubu hali inayoikosesha  serikali mapato.

Mhe. Ngonyani amekiri kuwepo kwa ongezeko la wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia bandari hizo katika maeneo mbalimbali nchini hasa ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na maeneo ya mipakani ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye makazi ya watu akieleza kuwa wengi wa wafanyabiashara wanakwepa kodi na kutafuta urahisi wa kupitisha mizigo yao.

Amesema maeneo hayo yamekuwa chanzo kikubwa cha upitishaji wa bidhaa zisizokidhi viwango, Silaha na Biashara haramu na kubainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa ndani wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na raia wa kigeni kuagiza na kuingiza bidhaa hizo kupitia bandari hizo kwa lengo la  kukwepa kodi.

Amesisitiza kuwa  Serikali ya Awamu ya tano inalishughulikia kwa nguvu zote suala hilo kupitia watendaji wake wakiwemo wakuu wa mikoa wa maeneo husika ambao hushirikiana na mamlaka zinazohusika vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti njia na maeneo yote yanayotumiwa na wafanyabiashara hao.

” Kama Serikali tunaendelea kufanya vikao kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kurasimisha bandari bubu zilizobaki ili tuweze kukusanya mapato ya Serikali yaliyokuwa yakipotea kutokana na wingi wa mizigo inayopitishwa” Amesema Mhandisi Ngonyani.

Amefafanua kuwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2015 na mwezi Januari,  2016, doria zilizofanyika katika maeneo yanayotumiwa na wafanyabishara hao zilifanikisha kukamatwa kwa wafanyabiashara 98 ambao wote walichukuliwa hatua za kisheria ikiwem mali zao kutaifishwa pamoja na  kuwafikisha mahakamani.

Kuhusu bandari bubu zilizotambuliwa na kuzirasimishwa na Serikali katika  Pwani ya Bahari ya Hindi ni  Mbweni ya jijini Dar es salaam, Mlingotini mkoani Pwani, Kisiju na Nyamisati mkoa wa Pwani na Bandari bubu ya Kilambo mkoani Mtwara.

Aidha, amesema Serikali inaendelea na utaratibu wa kurasimisha bandari binafsi umefanyika katika ziwa Victoria mkoani Mwanza na maeneo mengine ambayo serikali inaendelea kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni  amesema kuwa Serikali inaendelea kuvijengengea uwezo vikosi vyake vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea vifaa vya kisasa ili viweze kuimarisha doria nchi nzima ili kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi kukusanya taarifa za kiharifu ili kuwabaini na kuwakamata wafanyabishara wote wanaojihusisha na uagizaji na uingizaji wa bidhaa kupitia bandari bubu  ambaoumekua ukiisababishia serikali ikose mapato.

” Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaendelea kukusanya taarifa za kiharifu kutoka kwa wananchi ili kukabiliana na wimbi hili, pia tunaendelea kuviongezea nguvu vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kutimiza majukumu yao ipasavyo” Amesisitiza Mhe.Masauni.

JINSI TIGO MUSIC INAVYOBADILI MAISHA YA WANAMUZIKI WA KITANZANIA

New Picture (4)…………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MUZIKI wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo Flava’ ulikuwa haujulikani na pia haukuonekana kama ni sanaa halisi ya muziki;  hivi ndivyo ambavyo vizazi vilivyotanguliwa vlivyoutazama takribani miongo miwili iliyopita japo ni muziki wa kuburudisha watu wa rika zote wadogo kwa wakubwa.

Muziki wa ‘Bongo Flava’ umebadilisha himaya ya muziki hapa Tanzania ambao umepata sifa  katika nchi za Afrika mashariki, Afrika na Ulaya.

Ni ukweli usiofichika kuwa, sekta ya muziki wa kizazi kipya imekuwa kwa kasi na hata kuwapatia ajira vijana wengi wa kitanzania wenye vipaji ambao walikuwa hawana kazi hapa nchini kufuatia tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kwa vijana.

Ingawaje fani ya muziki imwekuwa ikionekana kuwa na maendeleo yanayosuasua kwa kipindi cha muongo mmoja hivi, wasanii wa muziki bado wanakumbana na changamoto nyingi.

Wameeleza changamoto hizo kuwa ni mapungufu ya kuwezeshwa kitaifa na kimataifa na kuwepo kwa ujuzi mdogo miongoni mwa wanamuziki.

Kuna baadhi ya makampuni, mashirika na hata watu binafsi ambao wameona umuhimu wa kutatua matatizo kama haya yanayowakabili wasanii na wanamuziki hapa nchini, na badala yake wamegundua mikakati ya kuwawezesha ili kutimiza malengo na ndoto zao kwa ujumla.

Tigo Tanzania ni moja ya makampuni hayo, na kwa kuwa ni kampuni ya kidijitali inayobadili maisha ya
watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’
ambayo inalengo la kuwawezesha wasanii wa muziki hapa nchini na kufanya kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.

Continue reading →

Mhandisi ashauri kufanyike uwekezaji wenye kuleta mapinduzi nchini

 Mhandisi Richmond Raymond.
 Mhandisi Richmond Raymond akiangalia pumba za mpunga ambazo ni malighafi katika kiwanda cha Mwanza.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL wakishiriki shughuli za kijamii za kusafisha mazingira.
…………………………………………………………
 Na Mwandishi wetu-
Meneja wa kiwanda cha Bia ya bia cha TBL cha mjini
Mwanza,Mhandisi Richmond Raymond ameshauri kuwa ili taifa la Tanzania
liondokane na tatizo la umaskini kwa haraka wawekezaji katika sekta zote
wanapaswa kulenga pia kusaidia jamii zilizowazunguka na kuwa na mtazamo wa
kunufaisha watu wengi zaidi kutokana na uwekezaji huo.
Katika mada yake aliyoitoa hivi karibuni katika mkutano wa
masuala ya  Uwekezaji wa kustawisha na
kubadilisha jamii uliofanyika jijini Dar es Salaam,Richmond alisema kuwa tatizo
la  kuondokana na umaskini halihusu
serikali peke yake bali linahusu sekta zote zikiwemo  zisizo za kiserikali ambazo zinajumuisha
viwanda na makampuni mbalimbali yanayofanya

biashara nchini.
Mhandisi Richmond alitoa mfano wa kampuni ya TBL Group ambayo
ni mwajiri wake kuwa imeweka mifumo na miongozo inayoelekeza kuipa kipaumbele
miradi ya kijamii na alidai kuwa tayari imeanza kuleta mabadiliko chanya na
kubadilisha maisha ya watanzania wengi.
Aliitaja baadhi ya miradi ambayo imeonyesha mafanikio kuwa ni
mradi wa kilimo shirikishi wa Go farming ambao kampuni inawasaidia wakulima kwa
kuwapatia pembejeo,utaalamu na kuhakikishia uhakika wa soko la mazao yao ,mradi
ambao umewanufaisha wakulima wa zao la Shahiri kwenye mikoa ya kanda ya
Kaskazini mwa Tanzania na kuongeza ajira ya wafanyakazi wa mashambani ambao
alidai utaanza kutekelezwa katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini.
Miradi mingine aliitaja kuwa ni kusaidia miradi ya
maji,kusaidia miradi ya Afya hususani ya kupambana na ugonjwa wa
Malaria,kuwezesha akina mama wanaouza pembe ya chibuku kupitia vikundi
vinavyojulikana kama Chibuku Mamas,kutoa elimu ya biashara kwa wafanyabiashara
wadogowadogo wanaoendesha biashara ya vinywaji , kusaidia kutoa elimu ya
Usalama barabarani na kuhamasisa wafanyakazi wake kutenga muda wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii.
Pia Richmond alisema kuwa kampuni imeanza kutumia teknolojia
za kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kutumia mtambo wa uzalishaji usiotumia
nishati ya mafuta kama ilivyozeleka katika uzalishaji wa viwandani bali
inatumia pumba za mpunga.
“Teknolojia hii ya aina yake barani Afrika ambayo imeanza
kutumika kwenye kiwanda cha TBL Mwanza ninachokiongoza ni muhimu kuanzishwa
katika viwanda mbalimbali kwa kuwa inasaidia katika  utunzaji wa mazingira”.Alisema
Aliongeza
kuwa mbali na kutunza mazingira imewezesha wakulima wa zao la mpunga kunufaika
kwa kuuza pumba za mpunga ambazo zamani zilikuwa zinatupwa sasa ni malighafi
kubwa ambayo imeanza kubadilisha uchumi wa wananchi “Huu ndio uwekezaji wenye
ubunifu unaobadilisha maisha ya wananchi na kutoa mchango katika kupunguza
umaskini nchini”Alisema

SERIKALI YAFAFANUA KUHUSU NDEGE NDOGO ZINAZOENDESHWA NA RUBANI MMOJA

imagesNa Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI imesema kuwa, hakuna kiwango kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria kumi au zaidi ni sharti iendeshwe na marubani wawili.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tambwe, Mhe. Khalifa Issa aliyetaka kujua kuhusu Sheria za nchi na za Kimataifa zisemavyo kuhusu ndege za namna hiyo kurushwa na rubani mmoja.
Eng. Ngonyani amesema kwamba, taratibu zinazoongoza fani ya kuendesha ndege nchini huongozwa na miongozo inayokubalika Kimataifa na ambayo imeridhiwa hapa nchini na Bunge.
Amefafanua kuwa, Katika taratibu hizo, kuna matakwa ya kisheria na kiufundi ambayo yakifuatwa yanawezesha kuwa na uwezekano mdogo sana wa kukumbwa na athari ya kiafya na kushindwa kumudu kuendesha ndege.
Ameeleza kuwa, Marubani hupimwa afya zao na madaktari bingwa kila muda maalum kulingana na umri kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 140 mpaka 177 ya The Civil Aviation (Personnel Licensing) Regulations, 2012.
“Serikali inaruhusu ndege kuendeshwa na rubani mmoja kwa kuzingatia taratibu hizo, Aidha, Kanuni 32(5) inasema kwamba ndege iliyoandikishwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruka kwa shughuli za kibiashara yenye uzito unaozidi kilo 5,700 itakuwa na marubani wasiopungua wawili”, alisema Eng. Ngonyani.
Pia amefafanua kuwa, shughuli za Usalama wa Anga nchini zinaongozwa na Sheria Namba 80 “Cvil Aviation Act. 80” na Kanuni zilizotengenezwa chini yake, ambapo urushaji wa ndege yenye abiria tisa au zaidi unaongozwa na Kanuni ziitwazo “The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations, 2012” ambapo ndege inayotimiza vigezo vilivyowekwa kwenye vifungu (2), (3) na (4) vya Kanuni ya 32 kuwa na uzito wa chini ya kilo 5,700 inaruhusu kuendeshwa na rubani mmoja.
Ameongeza kuwa, katika viwango vinavyotolewa na Shirika la Kimataiaf la Usafiri wa Anga (ICAO) kwenye kiambatanisho namba 19, chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Usafiri wa Anga (Chicago Convention) hakuna kiwango chochote kinachobainisha wazi kuwa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 10 au zaidi ni sharti iendeshwe na marubani wawili.
“Pia hakuna hata mapendekezo ya kiutekelezaji kwenye suala hilo, na hata katika Kiambatanisho cha 6 chenye sehemu tatu kianchohusiana na uendeshaji wa ndege ambacho ndicho kinachozungumzia idadi ya marubani katika uendeshaji wa ndege hakina katazo hilo”, alisisitiza Eng. Ngonyani.

BENKI YA CRDB YAFANYA MKUTANO MKUU WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari akihutubia mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICC Arusha. 
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akijibu maswali ya wanahisa.
 Manaibu Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka na Saugata Bandyopadhyay wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo.
Mwanahisa akiuliza swali.
Wanahisa wakiwa katika mkuano.
Mwenyekiti Abeid Mwasajone akiongoza mkutano wa wanahisa. Katikati ni Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo na Makamu Mwenyekiti, Steven Mashishanga.

Continue reading →