All posts in JAMII

MATUKIO YA SEMINA YA SENSA MJINI DODOMA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa
Fedha Dr. William Mgimwa (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Naibu Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dr.
Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya
wakufunzi wa sensa ya watu na makazi ya 2012 kwa wakufunzi wa ngazi ya
kitaifa jana mjini Dodoma.
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa
akitoa neno la utanguzi wakati wa  ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa
sensa ya watu na makazi ya 2012 kwa wakufunzi wa ngazi ya kitaifa jana
mjini Dodoma.

 
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo
Pinda (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua mafunzo ya wakufunzi wa
sensa ya watu na makazi ya 2012 kwa wakufunzi wa ngazi ya kitaifa jana
mjini Dodoma.

PINDA AFUNGUA MAFUNZO YA SENSA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa
ya Wau na Makazi, Ngazi ya Taifa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini
Dodoma Juni 23,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya Watu na Makazi, Ngazi
ya Taifa  wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda wakati alipofungua Mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Chuo cha
Mipango Mjini Dodoma Juni 23, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiagana na Waziri wa Fedha, Dktwilliam
Mgimwa baada ya kufungua  Mafunzo wa Wakufunzi wa  wa Sensa ya Watu  na
Makazi ya Mwaka  2012 Ngazi ya Taifa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango
Mjini Dodoma Juni 23, 2012. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wazara ya
Fedha, Servacius Likwelile na Wapili kushoto ni Kamishina wa Sensa,
hajat Amina Mrisho  Said. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWENGE WA UHURU KUWASILI JIJINI DAR ES SALAAM, MKUU WA MKOA ATOA WITO KWA WANANCHI KUJITOKEZA KUUPOKEA, AWATAKA MADAKTARI KUSITISHA MGOMO WAO


Mkuu wa Mkoa wa Mkoa
wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari  ofisini kwake kuhusu mapokezi ya Mwenge wa
Uhuru utakaowasili jijini Dar es Salaam wiki ijayo ukitokea Mkoa wa Kusini
Pemba. Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa wanananchi wa mkoa wa Dar es
Salaam kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge huo.

Na. Adrophina Ndyeikiza na Aron
Msigwa – Ofisi ya RC -DSM
-  Dar es Salaam.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi
Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa
wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru utakaowasili  jijini Dar es salaam siku ya jumatatu ukitokea
mkoa wa Kusini Pemba.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utakabidhiwwa kwa
uongozi wa wilaya ya Temeke saa 4 asubuhi na kuanza mbio zake ukipita katika
wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kwa muda wa siku 3.
 
Amesema mbio za Mwenge wa uhuru
kwa mwaka huu zinaongozwa na Kauli Mbiu ya Shiriki Kikamilifu Katika zoezi la
Sensa ya Watu na Makazi na Mapambano dhidi ya Rushwa, Ukimwi na Dawa za
kulevya.
 
Ameto wito kwa waajiri na wakuu
wa taasisi zote za Serikali kushiriki kikamilifu katika maeneo yao ya kazi
kuulaki Mwenge huo.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam ametoa msimamo wa mkoa wa Dar es salaam kuhusu mgomo wa
madaktari kwa kuwataka madaktari hao kusitisha mgomo wao na kutoa huduma kwa
wananchi kama kawaida.
 
Amesema kufuatia Chama cha
Madaktari nchini  (MAT) kutangaza kuanza  mgomo wa madaktari nchi nzima mkoa wa Dar es
Salaam umefuatilia kwa karibu mgomo huo na kubaini kuwa hospitali zote za
Serikali za mkoa huo zimeendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida.
 
Bw. Meck  Sadiki ameeleza kuwa hakuna taarifa zozote za
kugoma kwa  madaktari waliopangiwa zamu
katika hospitali za Mwananyamala, Kinondoni na Temeke na Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
 
“ Ninachukua fursa hii
kuwapongeza madaktari wote wa hospitali za Serikkali za mkoa wa Dar es salaam
waliooendelea kutoa huduma kama kawaida licha kutangazwa kwa mgomo kwa
kuonyesha nia ya kugoma na kutii sheria”. Amesema.
 
Amewataka wale wote wanaoendesha
mikutano ya kuhamasisha migomo ndani ya maeneo ya hospitali za serikali kuacha
mara moja huku akisisitiza kuwa serikali haitawavumilia na watakaobainika
watachuliwa hatua za kisheria.
“ Ninatoa angalizo kwa wale wote wanaopenyeza
mikutano ndani ya maeneo ya hospitali za serikali waache mara moja kwa sababu
majengo yale ni kwa ajili ya matumizi ya huduma za afya tu”
 
Ameongeza kuwa tayari suala la
mgomo wa madaktari liko katika vyombo vya sheria na kufafanua kuwa tayari
mahakama ya kazi imeshabainisha wazi kuwa mgomo wa madaktari ni batili.
“ Kwa bahati nzuri suala hili
limepata nguvu kisheria kwa kuwa mahakama imeshabainisha wazi kuwa mgomo wa
madaktari hao kuwa  ni batili na kwa
yeyote yule atakekutwa ndani ya maeneo ya hospitali akiendesha mikutano sheria
itafuata mkondo wake” amesema.
 
Aidha mkuu wa mkoa huyo
amebainisha kuwa maeneo yote ya hospitali ni maeneo ya kutolea huduma za afya
kwa wananchi na si mahala pa kuhamasisha mikutano ya kisiasa na kutoa onyo kwa
vikundi vyote vinavyojiita vikundi vya wanaharakati kutopenyeza harakati zao
katika maeneo hayo.

Pinda awaomba wananchi wote wajitokeza katika zoezi la sensa Agosti 26 mwaka huu.


Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dodoma
 
Serikali imewataka wananchi kujitokeza kwa wito katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayoanza tarehe 26 Agosti mwaka huu nchini kote na kuendelea katika kipindi cha siku saba(7) tangu siku ya zoezi hilo litakapoanza.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati anafungua mafunzo ya siku 10 ya wakufunzi wa sensa ya watu na makazi mjini Dodoma.

Alisema kuwa ili kufanikisha zoezi la sensa kwa mwaka huu ni  vema wananchi wakatunza kumbukumbu za taarifa za maswali yatakayoulizwa kwa watu wote watakaolala katika kaya zao usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti 2012.

Waziri Mkuu alisema kuwa kumbukumbu hizo ndio zitakazowasidia  kujibu maswali watakayoulizwa na makarani wa sensa katika siku watakapofika katika kaya zao kwenye kipindi cha siku saba za kuhesabu watu.

Alisema kuwa ili kufanikisha zoezi hilo ni vema viongozi wa vyama vyote vya siasa , wabunge , wawakilishi , viongozi wa madhehebu ya dini , watendaji wa kata, masheha, wenyeviti wa vijiji na watendaji wengine wakashirikiana katika kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kushirikiana na makarani , wasimamizi na watumishi wengine watakaofanya zoezi la sensa ili kufanikisha kazi hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha Waziri Mkuu alisema kuwa pamoja na kufanyika  zoezi la sensa hakusudii kusimamisha shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii kwani makarani wa sensa watapita kwenye kaya za wananchi katika muda wowote kuanzia usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti 2012 na kuendelea kwa siku saba.

Mheshimiwa Pinda alisema kuwa jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa kila mtu atakayekuwa nchini usiku wa kuamkia tarehe 26 Agosti mwaka huu anahesabiwa mara moja tu.

“Naomba wa wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sense kwa kutoa taarifa sahihi za kaya zao ili kupata takwimu sahihi kwa mipango ya maendeleo” alisisitiza Waziri Mkuu. Aliwahakikisha kuwa wananchi wasiogepe kutoa taarifa zote watakazoulizwa kwani kwa mujibu wa sheria ya sensa sura 351 taarifa zitakazokusanywa zitatumiwa kwa siri na zitatumika kwa shughuli za kitakwimu tu.

Aidha aliwataka wakufunzi wa sense ngazi ya kitaifa kujifunza kwa bidii kuwa mafanikio ya zoezi hilo yanategemea kwa kiwango kikubwa uelewa mpana na ushirikiano mkubwa wa viongozi na wakufunzi na makarani wa sense katika ngazi zote .

Sensa ya watu makazi hapa nchini ilifanyika mwaka 1910 na iliyofuata ilifanyika mwaka 1948 na 1957 kwa upande wa Tanzania bara na 1958 kwa Tanzania Visiwani.

Tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 sensa ya mwaka huu itakuwa ya tano ambapo zilifanyika mwaka 1967,1978,1988 na mwaka 2002.

Airtel yatoa vifaa vyamichezo kwa shule za Msingi Gongolamboto

Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa  Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi ya Maarifa Mwl Marietha Mulyalya wakati Airtel
ilipotembelea shule za  Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika
Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana
Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika
wakiteja jambo mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu
wa Taaluma na michezo wa shule ya msingi ya Gongolamboto Jaika Mwl Almasi
Shemdoe wakati Airtel ilipotembelea shule za msingi za Gongolamboto za
Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika na kugawa vifaa vya michezo hapo
Jana
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa  Mwalimu
wa Taaluma na michezo wa shule msingi ya Mwangaza  Mwl Abdul Mwarami wakati
Airtel ilipotembelea shule za  Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika
Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana

MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD WAWASILI MUGUMU SARENGETI KWA MAZISHI

Jeneza lenye mwili wa marehemu Willy Edward likiingizwa ndani baada ya
kuwasili nyumbani kwao Mugumu, wilayani Seerengeti jana  usiku PICHA NAKAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mdogo wa marehemu Willy Edward (kushoto) akilia huku akilakiwa na ndugu
yake baada ya mwili wa marehemu Willy Edward kuwasili nyumbani kwao
Baba mkubwa wa marehemu Willy Edward, Emmanuel Ongiri, akilia kwa
uchungu huku akiwa amelalia jeneza lenye mwili wa mwanawe ulipowasili
nyumbani kwao Mugumu, Serengeti usiku
Baadhi ndugu wa marehemu Willy Edward wakiangua kilio baada mwili kuwasili nyumbani kwao Mugumu, Serengeti

Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha mgomo wa Madaktari

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
      Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
      Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k
      Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
      Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
      Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

Waziri Celina Kombani akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani
akizungumza na waandishi wa habari  (leo) mjini Dodoma kuhusu
maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma ambayo yanaadhimisho kesho(leo)
tarehe 23.06.2012 kote duniani. Kuali mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu
ni kujenga uwezo wa utekelezaji wa mkataba wa misingi na kaununi za
utumishi wa umma na utawala ili kuwa nchi zinazojimudu kimaendeleo
katika Afrika.
 
Picha na tiganya Vincent-Dodoma

STIKA ZENYE NAMBA ZA VITUO VYA POLISI KUBANDIKWA KWENYE MABASI

 Kamanda Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani akizungumza na Waandishi
wa Habari Mara baada ya kuzindua kampeni ya kubandika stika zenye namba
za simu za vituo mbalimbali ambazo abiria watazitumia kwaajili ya kutoa
taarifa za usalama na matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani.
Kampeni hiyo inadhaminiwa na benki ya posta (TPB)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Moshingi  akibandika sitika hizo.
Mmoja wa Madereva waliokabidhiwa Stika hizo kwaajili ya kuzibandika kwenye magari
.

.

WAKAZI WA KILUVYA B. KISARAWE WAMTUHUMU DIWANI WAO KUJIPA TENDA


WAKAZI 
wa Kata ya Kiluvya B Kisarawe  Mkoani Pwani, wamemtuhumu Diwani wa Kata
hiyo Azamen Massawe, kwa tuhuma za kujipa tenda ya ujenzi ofisi ya kata
kinyume cha taratibu za tenda kinavyotakiwa.
Wakizungumza
na na Fullshangweblog kwa nyakati tofauti jana wakazi hao walidai kuwa, wanashangazwa
na hatua ya diwani huyo ya kujibebesha tenda kimya kimya bila
kuitangaza kwa wazabuni wengine jambo ambalo halikubaliki.

Walisema kuwa ujenzi wa ofisi hiyo, mbali na kufanyika kimya kimya lakini wanautilia 
shaka kutokana na utaratibu mbovu wa manunuzi ya vifaa vya ujenzi uliotumika kwani haukufuata sheria.

Walifafanua
kuwa ujenzi huo uligharimu shil. milioni 24 ambapo wakazi hao
wanapinga, kutokana na nguvu kubwa ya ujenzi huo imetokana na wananchi
wenyewe.

Wakazi hao
waliongeza kuwa licha ya ubadhilifu uliofanywa diwani huyo,bado vifaa
vingi vilivyotumika katika ujenzi huo vimetoka katika duka lake la vifaa
vya ujenzi.

“Awali
alituuzia matofali ambapo kila moja liligharimu shil. 2500 huku akidai
kuwa ofisi hiyo imetumia nondo 162 jambo ambalo si kweli, kwa sababu
mosi ofisi hiyo tumeijenga sisi wenyewe kuanzia msingi” walisema kwa
jazba wakazi hao.

Naye
diwani wa kata hiyo Massawe, alipotakiwa kutoa ufafanuazi juu ya sakata
hilo alisema hivi “ cha msingi mimi ni mfanyabiashara hivyo sikuona
vibaya kuchukua tenda hiyo, na gari langu ndilo lililotumika kupeleka
vifaa vya ujenzi katika ofisi hiyo bure bila malipo.

Vile vile
alidai kuwa kamati ya ofisi iliyoratibu shughuli zote za ujenzi ndio
inayoweza kuzungumzia suala hilo kwa kina kwa sababu ilihusika moja kwa
moja katika mchakato mzima wa ununuzi wa vifaa.

WANAFUNZI WA MUHIMBILI WACHANGIA DAMU KATIKA MPANGO WA DAMU SALAMA

Mtaalamu wa Maabara kutoka Mpango wa
Taifa wa Damu Salama Eliza Mgaya, akiweka vizuri mfuko wa damu kutoka
kwa mwanafunzi wa Chuo Cha Afya Muhimbili Paul Boniface, ambaye
ameshiriki kwenye zoezi la kujitolea damu linaloenda sambamba na
upimaji wa bure wa magonjwa mbalimbali, linaloratibiwa na Wanafunzi
wanao hitimu mafunzo ya Maabara kwenye Chuo cha Maabara Muhimbili
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakijiorodhesha Hospitali ya
taifa Muhimbili ili kuweza kupata huduma za bure za kupima afya zao,
zoezi hilo linaratibiwa na wanafunzi wa maabara wanao maliza kwenye chuo
cha maabara cha Muhimbili.
Wanafunzi wanaohitimu ngazi za
Astashada na Stashahada za Maabara kwenye Chuo cha Hospitali ya Taifa
Muhimbili, ambao ndio walioandaa zoezi la upimaji afya linaloendelea
hapa Muhimbili wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye hafla yao ya
kuhitimu masomo ambapo wanaelekea kuhitimisha masomo hayo.

TALISS YAITAKA SERIKALI KUSAIDIA KUTOA ELIMU YA UOKOAJI KATIKA AJALI ZA MAJI MASHULENI

TAASISI
isiyo ya kiserikali ya Tanzania Life Saving Society (TALISS), imeitaka
serikali kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali kutoa elimu kwa
walimu na wanafunzi shuleni, ili kupunguza ongezeko la vifo vitokanavyo
na maji.

Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dae es Salaam jana, Katibu  Mkuu wa
taasisisi hiyo, Alexander Mwaipasi alieleza kuwa vifo vingi vitokanavyo
na maji hutokea kutokana na wahusika kutokuwa na elimu ya kujiokoa.

Mwaipasi
alifafanua kuwa kutokana na ukosefu wa elimu ya uokoaji salama wa maji
watanzania wengi wamejikuta wakipoteza maisha kwa maji kutokana na
kushindwa kuogelea katika mabwawa, au baharini.

“Lengo la
taasisis ni kuzuia, kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na maji
kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kuishi salama karibu au ndani
ya maji pamoja na kusimamia suala la usalama kwa watumiaji wa maji ya
wazi na mabwawa”alichanganua Mwaipasi.


Aidha,
alisema kuwa kuna haja ya serikali kushirikiana na asasi nyingine kutoa
mafunzo na elimu kwa jamii ili itambue njia ya kujiokoa kabla na baada
ya  tatizo kujitokeza.

Hata hivyo
Katibu huyo, alitumia fursa hiyo kuieleza jamii kuwa taasisihiyo
itazindua wiki ya kuzuia vifo katika maji Kitaifa itakayofanyika jijini
hapa Juni 26 hadi 30 mwaka huu. 

“Katika
uzinduzi huo tutatoa semina na kufanya maonyesho mbalimbali kwa lengo la
kukuza na kueneza elimu ya uokoaji na usalama katika maji hapa
nchini”alisema Mwaipasi.

WAANDISHI WA HABARI KUUNDA MTANDAO UTAKAOWASIMAMIA

WAANDISHI wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekutana
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunda Mtandao utakaoweza kusimamia,
kupigania pamoja na kutetea haki zao.
 
Akizungumza katika kikao hicho juzi Katibu wa muda aliyeteuliwa
na waandishi hao, Eneza Mende alisema kuwa mtandao huo utajulikana kwa jilna la
‘Waandishi wa Habari Tanzania ‘ (TAJONET).

mtandao huo hutatumika kama chachu ya kusaidiana katika matatizo mbalimbali, ukiwa na sauti moja katika kutetea maslahi yao, huku ya habari ambayo yanadaiwa kuporomoka.

 Mende alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya wandishi wa
habari kujikuta wakikabiliwa na matatizo mbalimbali huku wakikosa msaada.
 Aidha, alibainisha kuwa TAJONET utakuwa bega kwa bega katika
kuangalia suala zima la afya ya wananchama kwa kuangazia ngazi ya chini kama
matibabu awapo hospitalini, pamoja na msiba.
 “Watu wengi wamekuwa wakichukulia matatizo ni kifo, bila kuangalia
mambo mengine kama ugonjwa, sisi hatutaki kujielekeza hivyo bali tunataka
ltatizo la ugonjwa lipewe 
kipaumbele  ili kuepusha
vifo visivyo na ulazima”alisema Mende.
 
Aidha, Mkutano huo umeteua viongozi wa muda  14, ambao kati yao wataunda kamati ya
rasimu ya upatikanaji wa katiba ya mtandao huo ambapo watakutana tena Julai 5 mwaka huu.

 


Walimu wanne wapandishwa mahakamani mkoani Arusha

Na Gladness Mushi wa Fulllshangwe-Arusha

Walimu wanne akiwemo mkuu wa shule ya Sekondari ya Moshono
Jijini Arusha wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuiba fedha za shule na
kusababisha hasara kubwa sana
Wakisomewa mashitaka mbele ya hakimu wa mahakama hiyo  Ngwanta Mwakunga  na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Rehema Mteta
washitakiwa hao walifanya makosa hayo kwa nyakati tofauti tofauti
Aidha ilisemekana kuwa Mshitakiwa wa kwanza ambaye alikuwa
ni mtumishi wa Serikali kati ya mwezi January na September aliiba kiasi cha
shilingi milioni 4.8 kutoka katika shule ya sekondari ya Moshono.
Mshitakiwa wa pili ambaye ni Dismas Lewigo naye aliiba kiasi
cha shilingi milioni 4 laki 6 ambapo ilikuwa ni kati ya June 2009 na 2010 hali
ambayo ilisababisha hasara kubwa sana
kwa Serikali
Mshitakiwa wa Tatu ambaye ni Lea Mwakenda aliiba kiasi cha
shilingi Milioni 2 laki 3 wakati mshitakiwa wa Nne Zinyangwa Mcharo naye aliiba
kiasi cha zaidi ya Milioni 11
Kesi hiyo itatajwa tena July 19 washitakiwa waliachiwa huru
kwa dhamana ya shilingi Milioni 5 wakati kwa mshitakiwa wa mwisho ni kiasi cha
shilingi million 4 pamoja na mali
isiyoamishika.

Mafunzo ya uokoaji kwenye maji kufanyika Juni 27-29 jijini Dar es salaam

Bwana Alex Mwaipasi katibu Mkuu wa chama cha kuogelea akizungumzia maonyesho yatakayokuwa maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya jinsi ya kutumia maji wakiwa salama ikiwa ni pamoja na kujua jinsi ya kujiokoa unapopata dharura ya kuzama kwenye maji kushoto ni John Belela Mwenyekiti wa (TALISS) , Maonyesho hayo yatafanyika kwenye viwanja vya Tanganyika International School Upanga jijini Dar es salaam  kuanzia Juni 27-29 

TAARIFA YA CHAMA CHA UOKOAJI

Tanzania Life Saving Society (TALISS) ni taasisi
ya kitaifa isiyo ya kiserikali ambayo jukumu lake kubwa ni kuzuia/kupunguza
idadi ya vifo vinavyosababishwa na maji, kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii
jinsi ya kuishi salama karibu/ndani ya maji, pamoja na kusimamia maswala ya
usalama kwa watumiaji wa maji ya wazi (Open water) na mabwawa (Swimming pools).
Katika kuendelea kutimiza wajibu wa kuelimisha
jamii,
Tanzania Life Saving Society (TALISS), kwa
mara ya kwanza inazindua Wiki ya Kuzuia Vifo Katika  Maji Kitaifa (NATIONAL DROWNING PREVENTION
WEEK) utakaofanyika katika shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST) iliyopo
upanga Dar es salaam, kuanzia tarehe 26 mpaka tarehe 30 Juni, 2012
kila siku saa 8:00 mchana mpaka saa 11:00 jioni, sambamba na hilo TALISS pia
itakuwa inaadhimisha miaka 20 ya kuzaliwa kwake.
Katika uzinduzi huo tutatoa semina na kufanya
maonesho mbalimbali, ambapo kusudi kuu la tukio hilo ni kukuza na kueneza elimu
ya uokoaji na usalama katika maji hapa nchini.
 
Tunatanguliza
shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu.
 Wako katika uokoaji wa maisha,
ALEXANDER H.
MWAIPASI
KATIBU MKUU

NHIF: WANANCHI JIUNGENI NA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF) KUEPUKA GHARAMA ZA PAPO KWA PAPO

WANANCHI
katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa
Afya ya Jamii (CHF) ili kuepuka gharama za papo kwa papo ambazo si
rahisi kuzimudu.
Rai hiyo imetolewa na Meneja Ofisi ya Kanda NHIF Moshi, Chris Mapunda  wakati
akizungumza na wananchi wa Kata ya Siha Kusini wakati wa zoezi la
Uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na CHF wilayani humo.
“Mfuko
wa Afya ya Jamii ni utaratibu wenye unafuu wa uchangiaji kabla ya
kuugua na unamwezesha mwananchi wa kawaida kumudu gharama za matibabu
pale anapougua nah ii inamsaidia mwanchi kumupunguzia gharama za
matibabu,” alisema Mapunda.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mfuko huo katika Wilaya ya Siha Bw. Amini
Lengati Munuo aliwasihi wananchi hao kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko
huo ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.
“Halmashauri
ya Wilaya ya Siha imepandisha gharama za papo kwa papo kitu ambacho
kitakuwa kigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kutoa fedha kila
anapofika kupata huduma na kwa maana hii ni vyema mkajiunga na Mfuko huu
ambao uchangiaji wake ni wa mara moja,” alisema.
Aidha
alisema kuwa dhamira ya Serikali kuanzisha Mfuko huo ni nzuri na
inayolenga kupunguza gharama za matibabu na hasa kwa wananchi wenye
vipato vya msimu ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za papo kwa papo
kila wanapougua. Halmashauri ya Wilaya ya Siha imepanga kiwango cha
mchango wa CHF kwa mwaka kuwa ni Shs 10,000 kwa Kaya ambayo ni baba,
mama, na watoto wane chini ya umri wa miaka 18.
la uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na mpango huu katika Wilaya ya Halmashauri ya Siha ni endelevu hivyo wananchi jitokezeni kwa wingi kujiandikisha katika Vituo vya Afya na Zahanati zilizopo karibu na maeneo mnayoishi ‘’ aliongeza Bw. Pita Kasaka ambaye ni mratibu wa Mfuko huo wa Wilaya.
Akitoa
shukrani, Mganga Mkuu wa Halmashuri ya Wilaya ya Siha Dr Best Magoma
ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Ofisi ya Kanda na Makao Makuu
kwa kushiriki kikamilifu katika Uhamasishaji kwa kutumia gari la
matangazo  la Mfuko huo. “Kwakweli tunawashukuru sana wenzetu wa NHIF kwa ushiriki wao, tunaamini ujumbe umewafikia wananchi, maana kwa muda mfupi tumeanza kuona mwamko wa wananchi wa kujitokeza na kuanza kujiandikisha” Amesema Dr Best Magoma

NAMSHUKURU MUNGU NIMEFIKA SALAMA JIJINI DAR, KESHO KIBARUANI

Namshukuru Mungu tuliondoka mjini Iringa leo mchana mishale ya saa nane mara baada ya kumaliza kazi ya uzinduzi wa mradi wa maji katika hospitali ya Wilaya ya Iringa, Tukiwa na Aunt T. na Familia yake tumefurahia sana safari yetu na ilikuwa ni nzuri ambapo tumeingia jijini Dar es salaam saa nne usiku, kutoka kulia  mstari wa mbele ni “Father Kidevu” Mroki Mroki, Naijo,Tevin na Nesto Mapunda na nyuma ni mimi John Bukuku (Mzee wa Fullshangwe) na Aunt T. mwenye miwani. tukipozi kwa picha mbelea ya mchuma huo V8, mara baada ya kumaliza mbuga ya Mikumi.

ROLI LA MCHANGA LAVAMIA BAR NA KUUA TEGETA

 Roli aina ya SICANIA lililokuwa limebeba mchanga likiwa limeacha njia
na kuingia kwenye kwenye Bar ijulikanoyo kama Kmm maeneo ya Tegeta Kibaoni jijini Dar es salaam leo kwenye ajali hiyo mtu mmoja amefariki
hapohapo na wengine wawili majeruhi.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
Mabaki ya vifaa mbalimbali vilivyoharibiwa kwenye bar hiyo baada ya kutokea kwa ajali hiyo leo maeneo ya Tegeta.
Jeshi la polisi likiimarisha ulinzi katika ajali hiyoiliyotokea leo maeneo ya Tegeta Kibaoni

SERENGETI YAZINDUA MRADI WA UVUNAJI MAJI HOSPITALI YA WILAYA IRINGA MJINI

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba akifungua maji kwenye bomba mara baada ya kuzindua mradi wa kuvuna maji katika hospitali ya wilaya ya Iringa, iliyopo Frelimo Kata ya Mwangata Iringa mjini, mradi huo utasaidia zaidi ya wakazi 100.00 wamaeneo ya karibu na hospitali hiyo, mradi huo umegarimu jumla ya shilingi milioni 50,000 za kitanzania na umegharimiwa kwa ufadhili wa kampuni ya mbia ya Serengeti (SBL), kushoto katika picha ni Malala Paulo Kamimu Mkurugenzi Manispaa ya Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba akifunguapazia wakati akizindua  mradi wa kuvuna maji katika hospitali ya wilaya
ya Iringa, iliyopo Frelimo Kata ya Mwangata Iringa mjini, kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Wakazi wa Iringa na wageni mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Srengeti Teddy Mapunda  katikati wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi mbalimbali wa hospitali hiyo na manispaa ya Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba akimtwisha ndoo ya maji BAgusta Mtemi Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Iringa mara baada ya kuzindua mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba akizungumza katika uzinduzi huo, kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti na kushoto ni Mh. Amani Mwamwindi Meya wa Manispaa ya Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Leticia Warioba akimsikiliza Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengetiwakati akisoma risala yake
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Sewrengeti kutoka kushoto ni Bw. Philip Ghucha, David Shayo, Imani Lwinga na mdauGerson Malisa wa kampuni ya TKA wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akimuonyesha Dr. Leticia Warioba  Mkuu wa Wilaya ya Iringa jinsi matanki ya maji yalivyojengewa katika eneo maalum kwa ajili ya uvunaji maji katika mradi huo.

Wakufunzi wa sensa wakiwa katika mafunzo mkoani Dodoma

Makundi mbalimbali ya wakufunzi wa Sensa kwa ngazi ya kitaifa
wakiwa katika mafunzo kwa njia ya vitendo jana katika Kijiji cha Nala
mkoani Dodoma jinsi ya kutumia ramani katika zoezi la sensa ya watu
ambayo inatarajia kufanyika nchini kote tarehe 26.08.2012. Wakufunzi hao
wako mkoani Dodoma kwa ajili ya mafunzo ya kuwawezesha ili nao waende
kutoa elimu hiyo katika ngazi za mikoa.
 
Picha zote na Tiganya Vincent- MAELEZO-Dodoma

TANGAZO KWA WANAFUNZI WALIOHITIMU VYUO VYA AFYA MACHI , 2012


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kuwajulisha 
wanafunzi wote waliohitimu  vyuo vya afya nchini mwezi Machi 2012,
kufika Wizarani ili waweze kuchukua barua za kupangiwa vituo vya kazi
kabla ya tarehe 30 June,2012.
Pia waombaji wengine waangalie majina yao kwenye
website ya Wizara
www.moh.go.tz
Imetolewa na:

Regina L. Kikuli
Kaimu Katibu Mkuu
21/06/2012

Over 150,000 to benefit from SBL/EABL Foundation sponsored rain water harvesting project in Iringa, Tanzania

Thousands of
people being served by Frelimo District Hospital in Iringa have reasons to
smile after a state of the art rain water harvesting facility was commissioned
in the area.
The model
facility costing approximately Tzs 50 Million has been constructed through
funding of EABL Foundation and Serengeti Breweries Limited (SBL) and will
benefit over 100,000 area residents.
Speaking when she
commissioned the facility, Iringa District Commissioner, Dr. Leticia Wariobaa expressed
her gratitude to SBL for guaranteeing availability of water at the hospital,
saying this was one of the key elements for a sustainable community.
“I am glad that
this facility will provide the community with the much-needed resource and wish
to thank SBL and EABL Foundation  for
their efforts”, she acknowledged.
She further
revealed that the project would go a long way in reducing the impact of water
borne diseases which was prevalent in the fast expanding area.
The rainwater
harvesting facility project was launched during the climax of world water day
that was nationally commemorated at Samaora Memorial Stadium in Iringa.
SBL was the
official sponsor of the water week whose climax was graced by the President of
the United Republic of Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
This year alone
Serengeti Breweries Limited has allocated more 300,000,000 shillings on water;
of which 100,000,000 million for the water week sponsorship of media and
communication, branding material, t-shirts, caps, brochures, booklets,
certificates, posters and fliers.
And the remaining
200,000,000 shillings were set aside for water and sanitation projects in
Iringa , Mwanza, Moshi and Dar es salaam.
Also present
during the commissioning ceremony was SBL’s Corporate Relations Director, Teddy
Mapunda who revealed that the business was committed to working with
communities in providing long term solutions through provision of clean,
sustainable water.
“As a company, SBL
recognizes that water is a basic need and an important catalyst for both
economic and social development of the country. Finding sustainable solutions
to the problems of our people underscores our commitment to the communities in
which we operate”. Temeke and Mawenzi hospitals would certainly be commissioned
soon as constructions are being finalised. 
Last year, SBL/EABL
Foundation commissioned water and sanitation project in Mkuranga and was part
of corporate companies and NGO’s that came together to improve water at Amana
hospital in Dar es salaam.
Serengeti
Breweries Limited and EABL foundation invested 384.6 Million on Mkuranga Water
project to benefit more than 250,000 people.

MISA YA MAZISHI YA MAREHEMU PETER MWENGUO KUFANYIKA SAA SABA MCHANA KARIMJEE

Mkurugenzi mtendaji mstaafu wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Marehemu Peter Mwenguo itafanyika leo saa saba mchana tarehe 21/06/2012,  katika ukimbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, baada ya misa kutakuwa na kutoa heshima za mwisho hapohapo Karimjee na baadaye msafara utaelekea katika makaburi ya Kinondoni kwa mazishi

LEO NIKO MKOANI IRINGA KWA KAZI ZA KIJAMII

 
 Ni asubuhi mapema na hii ni stendi kuu ya mabasi mjini Iringa hii ni taswira niliyoichukua asubuhi hii nikiwa katika hoteli niliyofikia ya Kalenga West Park Motel,Namshukuru Mungu nilifika salama mkoani hapa jana mida ya saa nane mchana hali ni shwari kabisa na nimeamka salama nikijiandaa kwa majukumu yangu ya kijamii ambapo nitakuwa nikiripoti tukio la kuzindua mradi wa maji katika hospitali ya wilaya ya Iringa iliyoko Frerimo kata ya Mwangata mjini Iringa , mradi ambao unazinduliwa leo na mkuu wa wilaya ya Iringa.

Jana nilitamani sana kumuaga ndugu yangu, rafiki yangu na mpiganajiwa wangu Marehemu Willy Edward aliyekuwa mhariri wa Gazeti la Jambo Leo, lakini jukumu hili ndilo lililonifanya nikashindwa kumuaga, hata hivyo kiroho niko pamoja naye na mazuri yote aliyoniachia nitayaenzi na kuyafanyia kazi
MUNGU AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU WILLY EDWARD OGUNDE “MZEE WA MOROCCO”  Kama tulivyokuwa tumezoea kuitana tukikutana.

MPANGO WA NMB FINANCIAL FITNESS WAENDELEA KATIKA SHULE MBALIMBALI

 Dotto Mbwana, mfanyakazi wa NMB Muhimbili akigawa
vijarida vya NMB Financial Fitness kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi
Muhimbili mpango huo ni kwa ajili ya kuwaandaa wanafuzi kupata uelewa wa masuala ya kibenki mashuleni
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakijisomea kijarida
cha NMB Financial Fitness wakati wafanyakazi wa NMB Turiani walipotembelea
shule yao
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida
cha NMB Financial Fitness
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida
cha NMB Financial Fitness
Meneja wa NMB Muhimbili Janeth Shango akiwasisitizia
wanafunzi juu wa kuweka fedha wakiwa na umri mdogo

Mkuu wa wilaya Meru atoa wito kwa halmashauri kuanzisha stesheni za Televisheni

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha

MKUU wa wilaya ya Arumeru Bw Nyerembe Munasa ametoa changamoto kwa halimashauri ya Meru na  manispaa  ya Arusha kuanzisha television za halimashauri ambazo zitawawezesha kuandaa program ambazo zitawaelekeza wananchi wao kutambua mambo muhimu yanayoendela katika halimashauri zao pindi wawapo kwenye vikao

Bw. Nyerembe aliyasema hayo alipokuwa akiongea katika semina ya wadau wa hlimashuri hizo ya  kuelimisha umma kuhusiana na mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analojia kwenda digital iliyofanyika mjini hapa. Bw. Nyerembe amesema kuwa  kutokana mabadiliko ya mafumo wa utangazaji halimashauri zinapaswa kuhakikisha kuwa zinaanzisha television ambapo kupitia mfumo huo zitawawezesha wananchi kuelewa mambo yanayoendelea katika halimashauri zao pindi wawapo kwenye shughuli zao.

Aidha amewataka madiwani  wa halmashauri hizo kuhakkisha kuwa wanasimamia kikamilifu miradi ya wananchi hao na kuhakikisha kuwa wanawapa taarifa sahihi za mabadiliko ya mfumo wa utangazaji .

Mbali na hayo bw Nyerembe amewataka wananhabari kuanzisha vituo vya utangazaji hasa kwa kipindi hiki cha mabadiliko ili waweze kujiajiri wenyewe kwa kuwa waandishi  wao ndio mhimili wa nne wa dunia .

Pia ameeleza kuwa  waandishi wanapaswa kufanya utafiti kwa jamii juu ya habari za kisayansi  na kuzitengenezea mkakati ya vipindi vitakavyoleta mabadilikokwa jamii

WENGI WAMUAGA MAREHEMU WILLY EDWARD KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

 Prof. Ibrahim  Lipumba kushoto Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF, Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi wakijumuika pamoja na viongozi wengeni, ndugu jamaa na marafiki pamoja na waombolezaqji wengine walioudhuria katika ibada ya 
kuaga mwili wa marehemu Willy Edward Ogunde aliyekuwa mhariri mkuu wa Gazeti la  Jambo leo katika viwanja vya
mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

Mwili wa marehemu Willy Edward Ogunde aliyekuwa mhariri mkuu wa Gazeti la  Jambo leo ukiwasili  katika viwanja vya
mnazi mmoja jijini Dar es salaam jana.

Mjane wa Marehemu Willy Edward Bi Rehema akifarijiwa na ndugu huku akilia kwa uchungu kwa kumpoteza mume wake mpendwa marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti wa IPP Reginald Abraham Mengi, Akimfariji Athumani Hamisi katika msiba huo
Mwenyekiti wa makampuni ya  IPP Reginald Abraham Mengi, Akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Willy Edward wanaofuatia nyuma yake ni Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye
Baadhi ya waombolezaji walioudhuri katika kuuaga mwiliwa marehemu Willy Edward wakiwa katika mstari tayari kwa kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.

MISA YA MAREHEMU PETER MWENGUO ITAFANYIKA LEO KWENYE UKUMBI WA KARIMJEE

Taarifa zaidi kuhusu Misa ya mazishi  ya aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji mstaafu wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Marehemu Peter Mwenguo itafanyika leo saa saba mchana tarehe 21/06/2012, 
katika ukimbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, baada ya misa kutakuwa na
kutoa heshima za mwisho hapohapo Karimjee na baadaye msafara utaelekea
katika makaburi ya Kinondoni kwa mazishi

WADAU ARUSHA WALIMLILIA MAREHEMU WILLY

NA GLADNESS MUSHI   WA FULLSHANGWE-ARUSHA
 
JIJI la Arusha ni moja ya mji ambao umepokea kwa masikitiko makubwa
kifo cha aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la jambo leo marehemu Willy
Edward (38) aliyefariki usiku wa juni 16 ghafla kwa kusababishwa na
mshutuko wa moyo.

Kifo hiki kimesitisha wadau mbali mbali wa mtandao huu ambao walikuwawapenzi watembeleaji  na pia hata wawakilishi wa mtandao huu kwa kuwakifo hicho kimetokea ghafla kwani amefariki dunia akiwa bado kijanaangali anahitajika kutoa mchango wake katika tasnia nzima yauahandishi wa habari.

Wakielezea kwa nyakati tofauti baadhi ya wadau mbali mbali mkoani hapawa jambo leo Bw. Adamu Aly alieleza kuwa kamwe hataweza kumsahaumarehemu kwa mchango wake katika tasnia ya habari kwa kuwa alikuwakijana mwadilifu na aliyekuwa anafanya kazi yake kwa umahiri ambapoalikuwa hata ameipa tasnia ya uhabari sifa mbali mbali kutokana namawazo aliyokuwa akiyatoa.

“Marehemu Willy ni mmoja wa wahariri ambao alifanya kazi yake kwaumakini ambapo kwa kweli inasikitisha sana kwani nimepokea msiba huukwa mshutuko mkubwa na huzuni nyingi kwani alikuwa kijana na badoalikuwa anahitajika sana hasa katika kuendelea na umahiri wake wakazi lakini basi tu kazi ya Mungu haina makosa”alisema Adamu

Nae Qeen Lema mwandishi wa habari aliyefanya kazi na marehemu kwakipindi akiwa majira jioni akielezea kwa undani alivyomfahamu marehemualisema kuwa hatua aliyo kwa sasa amefika ni kwa ajili ya mharirihuyo makini ambaye kila mara alikuwa akimpachangamoto na miongozo mbalimbali kwa ajili ya kuweza kusonga mbelezaidi kiuhandishiAidha bi Queen aliongeza kuwa ingawa kwa sasa hatuna tena MhaririWilly lakini jamii inapswa kufanya na kuenzi kazi zake hasa zakusaidiajamii za waandishi wa habari ambao ni wachanga sana na kwahali hiyo wahariri waliobaki wanatakiwa kuiga na kufuata hilo ilikuimarisha tasnia ya habari hapa nchini

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa marehemu alikuwa ni mpenda watu naalikuwa hasiti hata siku moja kutoa ushauri kwa maelekezo palepalipoonekana makosa alimradi tu kuhakikisha kuwa tasnia ya habariinasonga mbele.

Nao mawakala wasambazaji wa gazeti hili mjini hapa wameungana kwapamoja kumwombolezea mhariri huyo ambaye wamedai kuwa kila marawalikuwa wanawasiliana ili kihakikisha kuwa gazeti hilo limefikiawalengwa ambapo wamesema kuwa wamebaki na pengo kubwa ambalo halitaalisahulike daima.

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la nyumba mjini Dodma leo

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
mkutano na viongozi wa mifuko ya hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la taifa
ikulu mjini Dodoma leo.Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto
viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni
mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi. PICHA NA FREDDY MARO
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo
wakati akiongea na mkurugenzi mkuu wa PPF Bwana William Eriyo mjini Dodoma leo
baada ya kikao maalumu na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la
Nyumba .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba la Taifa
mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo. viongozi Wengine
waandamizi w aliohudhuria kikao hicho Naibu Waziri wa Ardhi Goodluck ole
Medeye(watatu kushoto),Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wanne kushoto),Gavana
wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu(kulia) na naibu katibu Mkuu Hazina Dr.Servacius
Likwelile(kushoto). Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto
viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni
mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemiah  Mchechu mara baada ya kikao maalumu
kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr.Ramadhani Dau akiteta
Jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu mjini Dodoma leo.