All posts in MICHEZO

SIMBA YAPIGWA FAINI YA MILIONI 3

downloadBodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga klabu ya Simba faini ya sh. milioni tatu kutokana na timu yake kuvaa jezi ambazo hazikuwa na nembo ya mdhamini wa Ligi Kuu, kampuni ya Vodacom wakati wa mechi yao dhidi ya Kagera Sugar. Mechi hiyo namba 50 ya Ligi Kuu ya Vodacom ilichezwa Desemba 26 mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 13(7) ya Ligi Kuu inayotaka klabu kuheshimu masharti ya udhamini wa Ligi Kuu kwenye mechi zake.Nayo Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 28(4) kwa kusababisha mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati yake na Toto Africans iliyochezwa Januari 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuvurugika. Kutokana na mchezo huo kuvurugika, Toto Africans imepewa ushindi  wa pointi tatu na mabao matatu. Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia kanuni ya 28(1) inayotawala

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WAZIRI FENELLA MUKANGARA KUFUNGA MASHINDANO YA PROIN WOMEN TAIFA CUP KESHO

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara.
…………………………………………………………….
online casino mobile Hatimaye kesho fainali ya Proin Women Taifa Cup itafanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke huku Mshindi wa Kwanza katika Michuano hiyo ataondoka na Kitita cha Shilingi za Kitanzania Milioni 3 huku mshindi wa Pili akiondoka na Milioni 1 na Mshindi wa Tatu akiondoka na Kitita cha Milioni 1.
Mashindano ya Women Taifa Cup ni mashindano ya kwanza kufanyika Nchini Tanzania huku yakiwa yamedhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions na Azam.
Katika fainali hiyo mashabiki wataingia Bure huku mechi hiyo ikirushwa live na Azam TV.

Mgeni rasmi katika Fainali hiyo ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara ambae atafunga mashindano hayo katika dimba la Azam Complex ambapo mechi hiyo ya fainali itaanza kutimua vumbi saa 10:15 Jioni huku Jonesia Rukyaa refarii mwenye beji ya fifa ndiye atakepuliza kipenga akisaidiwa na Hellen Mduma, Agness Alphonce na Mwanahamisi Matiku huku kamisaa wa fainali hiyo anatarajiwa kuwa Ingridy Kimaro.
Katika Mechi ya Kumtafuta mshindi wa tatu timu ya Ilala itamenyana na Kigoma ambapo mchezo huo utaanza saa 8 Mchana. 

SIMBA YASHINDA BAO 2- 1 DHIDI YA JKT RUVU TAIFA

Kikosi cha timu ya Simba SCkilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa taifa na kushinda bao 2-1.
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kilichoanza leo.…
Kikosi cha timu ya Simba SCkilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa taifa na kushinda bao 2-1.
Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kilichoanza leo.
Makapteni wakisalimiana na marefa kabla ya mechi.
Mashabiki wa Simba wakishangilia.
Wachezaji wa Simba wakiwasalimia mashabiki baada ya mechi.
Timu ya Simba SC, imeshinda bao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu leo Uwanja wa Taifa, Dar. Sasa ina pointi 16.
Mfungaji kwa upande wa Simba ni Danny Sserunkuma kipindi cha kwanza na kipindi cha pili.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

18 zatinga hatua ya 18 bora ligi ya mkoa wa Dar es salaam

images
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimetangaza timu 18 zilizofanikiwa kutingia katika hatua ya 18 bora (raundi ya pili) ya michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam.
 
Timu hizo ni kutoka katika kundi (A) ambazo ni Red Coast,Yanga U20,Changanyikeni na Ukonga UTD,kundi (B) Simba U20,Stakishari,Zakhem na Beira Hotspurs,kundi (C) FFU,Sifa UTD,Pan Africa na Sinza Stars,huku  kundi (D) likitoa timu za Shababi,New Kunduchi,Ugimbi na Azania Ngano.
 
Timu mbili zilizopata nafasi ya kuongezwa kwenye hatua hiyo ya pili,ni Sifa Politan FC pamoja na Tuamoyo FC,zinazokamilisha idadi ya timu 18.
 
Makatibu wakuu wa timu zote 18,wanatakiwa kufika katika ofisi za DRFA zilizopo kwenye jengo la Machinga Complex Ilala (Ghorofa ya 3),siku ya jumatano 04/02/2015,saa 8 mchana,kukutana na kamati ya mshindano kwaajili ya kupata utaratibu.
 
Baada ya kikao hicho DRFA itapanga makundi na kutoa ratiba ya kuanza kwa patashika hiyo.

TIMU YA TASWA FC YATINGA NUSU FAINALI ASAS DAIRIES BONANZA

IMG_7675-1Mwandishi wetu.

Iringa. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imetinga kwa vishindo michuano ya soka ya Asas Dairies Limited inayoendelea mkoani Iringa baada ya kushinda mechi zake zote za hatua ya makundi.
Taswa FC ilichezo mechi yake ya kwanza dhidi ya Mkwawa Senior na kuicharaza kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kundi A. Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Samora, ulikuwa mkali na wa kusisimua na Taswa FC ilifunga mabao yake kupitia kwa Zahoro Mlanzi aliyefunga mabao matatu kutokana na pasi safi kutoka kwa Muhidin Sufiani, Ibrahim “Maestro”Masoud na Edo Kumwembe.
Mabao mengine ya Taswa yalifungwa na Ali Mkongwe baada ya pasi safi ya Mohamed Akida  na Nico Ndifwa baada ya pasi ndefu ya Elius Kambili. Mkwawa Senior ilishinda kuipita ngome ya Taswa FC chini ya Wilbert Molandi, Athuman Jabir na Mbozi Katala.
Katika mchezo wa pili, Taswa FC iliifunga Pawaga mabao 3-0 yaliyofungwa na Saidi Seif, Nico Ndifwa na  Athuman Jabir. Katika mchezo wa kundi B, Iringa Veteran ilifunga Mkwawa Junior mabao 6-1 yaliyofungwa na Lisa Mwalupindi aliyefunga mabao matatu, Mzee Mbata na Haji Mambo.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza timu yake kwa ushindi huo ten bila kufungwa na kuahidi kutwaa ubingwa huo. Kutokana na matokeo hayo, Taswa itacheza na Mkwawa Junior katika nusu fainali ya kwanza iliyopangwa kuanza saa 2.00 asubuhi kwenye uwanja huo huo.
 

WAZIRI MUKANGARA MGENI RASMI KATIKA FAINALI YA MICHUANO YA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

images.....1Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara Anatajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Taifa Wanawake kati ya Pwani na Temeke itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni itachezeshwa na mwamuzi wa FIFA, Jonesia Rukyaa, na itaonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam. Waamuzi wasaidizi ni Hellen Mduma, Agnes Alphonce, na Mwanahamisi Matiku wakati Kamishna ni Ingridy Kimario.

Timu za Ilala na Kigoma zitacheza mechi ya utangulizi kutafuta mshindi wa tatu kuanzia saa 8.00 mchana. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin na kufanyika kwa mara ya kwanza nchini atapata kombe na sh. milioni tatu.

Makamu bingwa atapata sh. milioni mbili wakati mshindi wa tatu atapata sh. milioni moja. Kiingilio kwenye mechi hizo ni bure.

………………………………………………………….

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

FRIENDS RANGERS YAPOTEZA MECHI BAADA YA KUGOMA KUENDELEA NA MCHEZO

images.....1Mechi namba 120 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kundi A kati ya Majimaji na Friends Rangers iliyochezwa (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilivunjika dakika ya 38 baada ya Friends Rangers kugoma kuendelea na mchezo.

Kwa kitendo hicho, Friends Rangers imepoteza mchezo huo. Hatua nyingine za kikanuni zitafuata baada ya kamati inayohusika kukutana.

Wakati huo huo, mechi ya FDL kundi A iliyochezwa leo (Januari 30 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kati ya African Lyon na Ashanti United imemalizika kwa sare ya bao 1-1.

……………………………………..

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI TATU ZINAHITAJIKA ILI KUYAFANYA MAENEO YA KIHISTORIA KUWA NI KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII NCHINI.

imagesmNa Abdula Ali Maelezo-Zanzibar

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Said Ali Mbarouk amesema zaidi ya shilingi trilioni tatu zinahitajika ili kuyafanya maeneo ya kihistoria kuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii nchini.
Hayo ameyaeleza katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Saleh Nassor Juma.
Amesema hadi sasa Zanzibar ina maeneo ya kihistoria yapatayo 85 Unguja na Pemba, ambayo yatakuwa ni kivutio kikubwa cha Watalii na kuinua Uchumi wa Nchi ikiwa yatatunzwa, kuhifadhiwa na kutangazwa nje ya nchi.
Ametanabahisha kuwa kwa sasa Serikali inayashughulikia zaidi maeneo ya Ras Mkumbuu, Chwaka, Tumbe na Jambangome ambayo hayako katika uhifadhi mzuri na yameandaliwa mpango maalumu wa kuyashughulikia kwa kuwa kuna maeneo mengi ya kihistoria yanayohitaji kuhifadhiwa.
Amesema kuwa kwa mujibu wa mpango wa Maabara ya Utalii, Ras Mkumbuu imewekwa katika mpango wa mwaka wa fedha wa kujengwa ukuta wa kuzuia maji ya bahari yasiingie katika eneo hilo ili kuifanya Ras hiyo kubakia katika muonekano wake wa sasa na mandhari yaliyo mazuri yenye kuwavutia watalii .
Waziri Mbarouk amefafanua kuwa kuna maeneo mengi yaliyohifadhiwa katika kipindi cha hivi karibuni miongoni mwa maeneo hayo ni Kijichi, Kwa Bikhole, Maeneo ya Mahandaki yaliyotumika katika Vita vya Pili vya Dunia, Eneo la Pango la Watumwa na Mnara vyote vilivyoko Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo ujenzi wa Makumbusho kwenye Pango la Kumbi tayari umeshamalizika.
Waziri Mbarouk amesema ipo haja kwa Serikali kushirikiana na Kamati za Vijiji husika ili kuweza kuyahifadhi maeneo ya kihistoria kwa ajili ya vizazi vijavyo pamoja na kuzitaka kamati hizo za Vijiji kukarabati sehemu hizo pale wanapoona kuna maharibiko yamejitokeza.
Aidha Waziri Mbarouk amesema Serikali imekuwa ikichukua tahadhari kubwa kuona Kazi za Sanaa zikiwemo za Filamu na Muziki haziendi kinyume na Mila, Silka na Utamaduni wa Mzanzibari na badala yake ziwe ni zenye kutoa mafunzo pamoja na kuelimisha jamii.
Amesema katika kuhakikisha hayo Wizara yake inazingatia utekelezwaji wa Sheria Namba 1 ya Mwaka 2009 ya Bodi ya Sensa, Sheria hiyo iliundwa kwa lengo la kuhakikisha kazi zote za Sanaa na Utamaduni zinahakikiwa, ili kuhakikisha mafunzo yanayopatikana katika Sanaa hizo yanaenziwa, kulindwa, kukuzwa na kuendeleza Mila, Silka na Utamaduni wa Mzanzibari.
Amefafanua kwamba kwa kiwango kikubwa kazi hiyo imefanyika na hivi sasa Bodi ya Sensa ya Zanzibar inafanya kazi na Bodi ya Sensa ya Tanzania Bara katika kutekeleza jukumu la kuzuia uoneshwaji wa kazi za Sanaa zinazokwenda kinyume na Maadili ya Nchi yakiwemo Mavazi ya Wasanii yasiyokuwa na Stara na yanayokwenda kinyume na Utamaduni wa Mtanzania.
Waziri Mbarouk amewataka wasanii wa Filamu pamoja na Muziki kuwacha kuiga utamaduni wa Kimagharibi kwa kutoa kazi za sana ambazo zinahamasisha Ngono na kupelekea kumong’onyoka kwa Maadili ya Mtanzania.

WAANGALIZI WA SIRI KUSIMAMIA MECHI ZA MWISHO FDL

ZFA iliithibitishia TFF kuwa kesi hiyo imeondolewa kortini bila masharti, hivyo timu za Tanzania Bara kuruhusiwa kushiriki katika michuano ya Kombe la Mapinduzi. Ni muhimu suala hilo likashughulikiwa haraka ili kutohatarisha ushiriki wa timu za KMKM na Polisi kwenye michuano hiyo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

DRFA YAWAOMBA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUJITOKEZA KWA WINGI MICHEZO YA TAIFA CUP

 2
Uongozi wa chama  cha soka mkoa wa Dar es salaam,DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
 
Kesho (januari 28) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini.
Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda sare ya 1-1.
 
Katika michuano ya taifa Cup,Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali zilizopigwa leo (januari 27),ambapo Temeke imeiangamiza bila huruma Mbeya mabao 3-0,huku Ilala ikiizodoa Iringa kwa mabao 2-1.
 
Aidha DRFA imeipongeza timu ya Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya makundi.
 
Viongozi wa DRFA wamekuwa mfano kwa kujitokeza kushuhudia mechi hizo za Taifa Cup,Ligi kuu na zile za Daraja la kwanza,ili kuongeza chachu kwa timu za Dar es salaam kufanya vizuri.

KAMATI YA TUPA RUFANI YA MWANZA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

mmmmmmmmm   Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupa rufani ya timu ya Mwanza kupinga uhalali wa wachezaji wawili wa Kigoma kwenye mechi yao ya robo fainali iliyochezwa jana (Januari 26 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Mwanza iliyopoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1 iliwalalamikia wachezaji Neema Sanga na Vene Dickson wa Kigoma kuwa waliwahi kuchezea timu ya Taifa (Twiga Stars), hivyo kucheza mashindano ya Kombe la Taifa la Wanawake ni kinyume cha kanuni. Kamati baada ya kupitia rufani hiyo, imeitupa kwa vile timu ya Mwanza haikuwasilisha vielelezo vyovyote kuthibitisha madai hayo dhidi ya wachezaji hao. Pia Kamati yenyewe ilipitia taarifa za Twiga Stars ambapo haikupata kumbukumbu za wachezaji hao katika timu hiyo. Pia Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imesikitishwa na kitendo cha viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza kugomea uamuzi dhidi ya rufani yao, hivyo imependekeza Mwenyekiti wa TWFA Mwanza, Sophia Tigalyoma na Katibu wake Hawa Bajanguo wapelekwe Kamati ya Nidhamu kwa hatua za kinidhamu.

WASHINDI COPA COCA-COLA WAKABIDHIWA VITITA VYAO

Washindi wa Copa Coca-Cola 2014 wamekabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwa mdhamini wa michuano hiyo ya umri chini ya miaka 15 kwa wavulana na wasichana kampuni ya Coca-Cola. Fedha hizo kwa washindi mbalimbali tayari zimeingizwa kwenye akaunti zao.

Kwa upande wa wavulana; washindi na kiwango walichopata ni mabingwa Dodoma (sh. milioni nane), makamu bingwa Kinondoni (sh. milioni tano), mshindi wa tatu Kigoma (sh. milioni tatu) wakati timu yenye nidhamu Tanga (sh. milioni moja).

Mchezaji bora Mwami Ismail kutoka Kigoma (sh. 500,000), mfungaji bora Timoth Timoth wa Dodoma (sh. 500,000), kipa bora Kelvin Deogratia wa Geita (sh. 500,000) na mwamuzi bora Abdallah Mbarome kutoka Zanzibar sh. 500,000).

Kwa upande wa wasichana ni mabingwa Kinondoni (sh. milioni tano), makamu bingwa Ilala (sh. milioni tatu), mshindi wa watatu Temeke (sh. milioni mbili) wakati timu yenye nidhamu Mbeya imepata sh. milioni moja).

Zubeda Mohamed wa Kinondoni ambaye ndiye mchezaji bora amepata sh. 500,000, mfungaji bora Stumai Abdallah wa Temeke sh. 500,000 wakati kipa bora ni Suleta Saad wa Zanzibar sh. 500,000.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

NSSF, REAL MADRID KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA

3

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.

2 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.

1

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (kulia) wakibadilishana mikataba ya kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.

5

Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya timu yake  na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kitahusisha wanafunzi 108 watakaogawanywa kwenye timu za chini ya umri wa miaka 13, 15, 17, 19, kikosi cha pili na timu ya wakubwa.

…………………………………………………

Na Mwandishi wetu

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeingia mkataba na klabu maarufu duniani ya Real Madrid ya Hispania wa kujenga kituo cha michezo kwa ajili ya kuzalisha vipaji.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo wa miaka 18, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk Ramadhani Dau alisema ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 16 na unatarajiwa kuanza kujengwa Mei mwaka huu na kwamba utakamilika baada ya miezi 18.

Dk Dau alisema kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye kijiji cha michezo cha shirika hilo (NSSF Sports City), kitakuwa eneo la Mwasoga, Kigamboni, Dar es Salaam.

“Tuna eneo la zaidi ya ekari 400 ambapo tutajenga viwanja, shule ya michezo, nyumba za kuishi na maduka. Lengo letu tuzalishe na kuuza wachezaji. Tunakusudia kuwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 13, 18, 20, timu B na timu ya wakubwa,” alisema Dk Dau.

Alisema utekelezaji wa kituo hicho utaanza hivi karibuni kwa kutumia majengo ya kukodi wakati wakisubiri ujenzi kukamilika.

“Hivi hapa baada ya kusaini mkataba, utekelezaji utaanza kwa kutumia majengo ya kukodi ambayo tunadhani yatakuwa maeneo ya Temeke na tutakuwa tukitumia viwanja vya Karume na Uhuru,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF alisema katika kuendesha kituo hicho, kila kitu kitafanywa na Real Madrid kuanzia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.

“Sisi tunachukulia huu mradi ni uwekezaji na hatufanyi hisani, itazingatia misingi ya biashara na faida kubwa ni kwamba NSSF itaongeza kipato, lakini pia kituo kitatumika kuitangaza Tanzania kwa sababu yatakayofanyika yataoneshwa kwenye televisheni ya Real Madrid,” alifafanua Dk Dau.

“Lakini pia wakati umefika sasa kwa Tanzania kushiriki Kombe la Dunia Qatar 2022, kama unaandaa vizuri vijana wa miaka 13 sasa mpaka mwaka 2020 wanaweza kuwakilisha vizuri kwenye mechi za kufuzu na mwaka 2022 wakashiriki Kombe la Dunia, wakikosa la Qatar, basi hata hizo zinazokuja, hiyo pia ni moja ya madhumuni ya kituo hicho.”

Akizungumzia namna walivyofikia uamuzi wa kujenga kituo, Dk Dau alisema wazo hilo lilipatikana Agosti mwaka jana na kisha likapelekwa kwenye Mkutano wa Wanachama uliofanyika Arusha ambako waliazimia NSSF iwekeze rasmi kwenye michezo kabla ya kuwasilishwa kwenye bodi na utekelezaji kuanza kufanyika.

“Tulitembelea sehemu nyingi kuona wenzetu wanafanyaje. Binafsi nilitembelea nchi kadhaa za Ulaya, nilienda kituo cha Manchester United, Sunderland, Real Madrid kwa hapa Afrika nilikwenda Asec Mimosas (Ivory Coast) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC) kuona wanafanyaje, ziara ikazaa matunda kwani tulikubaliana na Madrid na ndio wamekuja kusaini mkataba leo (jana),” alifafanua Dk Dau.

Naye Mkuu wa Vituo vya Michezo wa Real Madrid, Rayco Garcia aliishukuru NSSF wa kuwa na mpango huo na kuahidi kufanya kazi ili kuipatia Tanzania mafanikio.

“Tukifanikiwa kuwatoa vijana hao, Tanzania itaweza kushiriki kwenye michuano mikubwa kama alivyosema Dk Dau, inabidi tufanye kazi ili vijana wafanikiwe, wafike mbali,” alisema Garcia.

Mbali na Garcia ambaye pia ni kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Madrid, wengine walioambatana kwenye msafara huo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, Ruben de la Red, Kocha Mkuu wa timu za vijana, Francisco Martin Ramos na Juan Jose San Roman Milla. Mwaka jana, wachezaji wa zamani wa Real Madrid walifanya ziara nchini.

PANAMA FC,BOOM FC,KUANIKA 18 BORA LIGI YA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mechi ya kiporo katika michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam kati ya klabu za Panama FC dhidi ya Boom FC, itapigwa kesho kwenye uwanja wa Airwing,ukiwa ni mchezo ambao utatoa fursa kwa DRFA kutangaza timu 18 zilizofanikiwa kutinga katika hatua ya 18 bora ya michuano hiyo.

Michuano hiyo ya ligi mkoa wa Dar es salaam iliyokuwa na jumla ya timu 36,inaingia katika hatua ya mwisho katika hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa Dar es salaam katika ligi ya mabingwa wa mikoa ya TFF.

Kivumbi cha hatua ya 18 bora,kitaanza kutimka tarehe 4 /02/2015.

……………………………………………………………………………………………………………

LIGI YA WANAWAKE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Ligi ya soka la wanawake kwa mkoa wa Dar es salaam inataraji kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao kwa kushirikisha jumla ya timu 12,zitakazoumana kuwania ubingwa huo.

Itakumbukwa kwamba DRFA iliamua kusogeza mbele mashindano hayo ambayo yalikuwa yaanze januari 16/2015,kutokana na upungufu wa wachezaji kwa timu husika ambao wengi wao wanashiriki mashindano ya kuwania kombe la Taifa Wanawake,ambayo sasa imeingia katika hatua ya robo fainali.

Timu zote 12 zitakazoshiriki ligi hiyo ya mkoa wa Dar es salaam,zitawekwa hadharani hapo baadaye.

IMETOLEWA NA AFISA HABARI DRFA- OMARY KATANGA

ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE KUANZA KESHO

miguuHatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa kesho (Januari 26 mwaka huu) na Januari 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kila siku.

Mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Televisheni itaanza saa 9 alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo fainali ya pili ambayo ni kati ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.

Ilala na Iringa watacheza robo fainali ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9 kamili alasiri, na kufuatiwa na robo fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.

Nusu fainali za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari 29 mwaka huu wakati Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15 jioni ambapo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).

Timu zote zilizoingia hatua hiyo ya nane bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini zimefikia hosteli ya Msimbazi.

Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

 

Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa watakiwa kujenga utamaduni wa kutekeleza wajibu wao kwa kujitolea zaidi.

unnamed

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) mara baada ya kuzindua Balaza la 13 la Michezo leo jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Michezo Zanzibar, Naibu Kaibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Mwenyekiti wa BMT Bw. Dioniz Malinzi na mjumbe wa BMT Mhe. Zainab Vulu (MB).

Picha zote na Frank Shija, WHVUM.

unnamed2Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akitoa nasaha kwa wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati akizindua Balaza la 13 la Michezo leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo. Wajumbe waliohudhuria hafla hizo ni pamoja na ,Mkurugenzi wa PSPF Adam Mayingu, Zacharia Hans Pope, Jamal Rwambow, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF Crescentius Magori ,wajumbe wengine ni Alex Mgongolwa, Jennifer Mmasi Shang’a, Mhe. Zainabu Vulu (MB), Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro. unnamed3Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi akitoa neno lashukrani mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Baraza la 13 la Michezo leo jinini Dar es Salam. Pembeni ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.

unnamed4Baadhi ya wajumbe wa Barala la Michezo la Taifa (BMT) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri wakati wa hafla ya uzinduzi wa baraza hilo leo(jana) jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Zacharia Hanspope, Crescentius Magori ambaye, Adam Mayingu ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro

unnamed5Baadhi ya wajumbe wa Barala la Michezo la Taifa (BMT) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri wakati wa hafla ya uzinduzi wa baraza hilo leo(jana) jijini Dar es Salaam Kutoka kulia ni Mhe. Zainabu Matitu Vulu(MB), Jamal Rwambow (SACP msataafu) na Mwl. Zaynab Mbiro.

unnamed6Baadhi ya wajumbe wa Barala la Michezo la Taifa (BMT) wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri wakati wa hafla ya uzinduzi wa baraza hilo leo jijini Dar es SalaamKutoka kulia ni Mhe. Zainabu Matitu Vulu(MB), Jamal Rwambow (SACP msataafu) na Mwl. Zaynab Mbiro.

TAARIFA MBALIMBALI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

index6 ZAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

Timu za mikoa sita tayari imepata tiketi za kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake itakayoanza Januari 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati nyingine mbili zinajulikana leo (Januari 23 mwaka huu).

Mikoa ambayo timu zake tayari zina tiketi za robo fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin ni Ilala, Kigoma, Mwanza, Pwani, Tanga na Temeke.

Matokeo ya mechi za leo kati ya Iringa na Ruvuma, na ile kati ya Mbeya na Katavi ndiyo yatakayoamua ni timu zipi mbili kati ya hizo zinakwenda Dar es Salaam kucheza robo fainali.

Timu zote zilizofuzu hatua ya robo fainali zinatakiwa kuripoti Dar es Salaam keshokutwa (Januari 25 mwaka huu). Fainali ya michuano hiyo itachezwa Februari Mosi mwaka huu.

TIMU YA BEACH SOCCER ZANZBAR YAWASILI DAR

Timu ya beach soccer ya Zanzibar imewasili Dar es Salaam leo mchana, tayari kwa kambi ya pamoja na Tanzania Bara kwa ajili ya kuunda kikosi cha Tanzania kitakashiriki mechi za mchujo za michuano ya Afrika.

Tanzania imepangwa kucheza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayofanyika kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu jijini Mombasa. Mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye nchini.

Zanzibar imewasili na kikosi cha wachezaji 14 na viongozi watatu ambacho kitaungana na kile cha Tanzania Bara. Timu hizo zitacheza jumla ya mechi nane kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam.

Mechi hizo zitachezwa mbili asubuhi na mbili jioni kesho (Januari 24 mwaka huu), na nyingine nne kwa utaratibu huo huo keshokutwa (Januari 25 mwaka huu) kabla ya Kocha John Mwansasu kutaja kikosi cha mwisho Januari 26 mwaka huu.

VPL KUTIMUA VUMBI WIKIENDI

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 12 wikiendi hii kwa mechi saba. Kesho (Januari 24 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Morogoro na Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mechi za Jumapili ni kati ya Azam na Simba (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar na Ndanda (Uwanja wa CCM Kirumba), Stand United na Coastal Union (Uwanja wa Kambarage),, Mbeya City na Tanzania Prisons (Uwanja wa Sokoine), Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar (uwanja wa Mabatini), na JKT Ruvu na Mgambo Shooting (Uwanja wa Azam Complex).

KLABU KUJIGHARAMIA HOTELI MICHUANO YA CAF

index

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini.

Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa kuziweka timu ngeni.

Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.

Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana. Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

HABARI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

tff_LOGO1

WACHEZAJI WAWILI VPL, FDL WAPIGWA FAINI
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imewapiga faini na kuwafungia mechi wachezaji wawili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa kufanya vitendo kinyume na kanuni zinazotawala ligi hizo.

Mshambuliaji Haruna Chanongo wa Stand United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga teke mwamuzi wa mechi dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa Januari 3 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu.

Kipa Amani Simba wa Oljoro JKT amepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kukataa kupeana mkono na viongozi wakati wa kusalimia kabla ya kuanza mechi kati ya timu yake na Toto Africans iliyofanyika jijini Mwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 14 ya FDL.

Timu ya Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi ya FDL dhidi ya Mwadui ya Shinyanga iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Pia Polisi Tabora imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 40 dhidi ya Geita Gold, adhabu ambazo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41.

12 WAPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapeleka wanamichezo 12 wakiwemo viongozi, makocha na wachezaji kwenye Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na matukio mbalimbali kwenye Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake.

Wachezaji Dihe Makonga, Swalehe Idd Hussein, Ramadhan Mwinyimbegu na Shaibu Nayopa wa Oljoro JKT, na Nassib Lugusha wa Polisi Dodoma wanalalmikiwa katika Kamati ya Nidhamu kwa kushambulia waamuzi na kufanya vurugu kwenye benchi la timu pinzani katika mechi zao za FDL.

Mtunza Vifaa (Kit Manager) wa Polisi Mara, Clement Kajeri analalamikiwa kwa kuongoza mashambulizi dhidi ya waamuzi kwenye mechi kati ya timu yake na Mwadui iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Naye Mtunza Vifaa (Kit Manager) wa Rhino Rangers, Albert Mbunji anapelekwa katika Kamati hiyo kwa kupinga maamuzi na kuwatukana waamuzi kwenye mechi dhidi ya Polisi Dodoma iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Pia Mtunza Vifaa (Kit Manager) wa Oljoro JKT, Eliud Justine Mjarifu analalamikiwa kwa matukio mawili; alimpiga Kocha wa Burkina Faso, CR Mwakambaya kwenye mechi ya FDL iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Pia alimtukana mwamuzi akiba (fouth official) Mussa Magogo kwenye mechi dhidi ya Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kocha wa Polisi Tabora, Kim Christopher analalamikiwa kwa kumtolea mlugha chafu mwamuzi wa mechi kati ya timu yake na Panone FC iliyochezwa Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Msimamizi wa Kituo cha Musoma, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona naye anapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kwa tuhuma za kutotoa ushirikiano kwa maofisa wa mechi na kuchochea maofisa hao (waamuzi) kupigwa.

Kwa upande wake, Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imependekeza Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Sologo, na Kaimu Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Singida (SIREFA), Gabriel Gunda kupelekwa kwenye kamati ya Nidhamu kwa matukio mbalimbali yaliyojitokeza kwenye mechi za Kombe la Taifa la Wanawake.

Sologo anatuhumiwa kumpiga kibao mwamuzi wa mechi ya marudiano kati ya timu yake ya Simiyu na Shinyanga iliyochezwa mjini Shinyanga, tukio ambalo lilimfanya mwamuzi huyo avunje mchezo.

Naye Gunda analalamikiwa kwa kushindwa kuhakikisha timu yake ya Singida inaingia uwanjani kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Dodoma iliyokuwa ifanyike kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

SDL KUANZA MZUNGUKO WA PILI JANUARI 31
Mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Pili (SDL) sasa utaanza Januari 31 mwaka huu, badala ya Januari 24 mwaka huu kama ilivyopangwa awali ili kutoa fursa kwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia usajili wa dirisha dogo.

Timu zinazocheza ligi hiyo katika makundi manne tofauti ni; Milambo FC, Mji Mkuu FC (CDA), Mvuvumwa FC, Singida United, na Ujenzi Rukwa (Kundi A), Arusha FC, Bulyanhulu FC, JKT Rwamkoma FC, Mbao FC, na Pamba SC (Kundi B).
Nyingine ni Abajalo FC, Cosmopolitan, Kariakoo Lindi, Kiluvya United, Mshikamano FC, na Transit Camp (Kundi C), wakati Kundi D ni Magereza Iringa, Mji Njombe, Mkamba Rangers, Town Small Boys, Volcano FC, na Wenda FC.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

indexMICHUANO YA KOMBE LA TAIFA YAINGIA RAUNDI YA PILI

Michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inaingia raundi ya pili kesho (Januari 17 mwaka huu) kwa mechi za kwanza za raundi hiyo zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Arusha, Mlandizi, Dar es Salaam na Katavi.

Jijini Dar es Salaam kutakuwa na mechi mbili ambapo mkoa wa kisoka wa Ilala utacheza na Mtwara kwenye Uwanja wa Karume, wakati Uwanja wa Chuo cha Bandari uliopo Tandika utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Temeke na Dodoma.

Mechi nyingine za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitakuwa kati ya Kagera na Mwanza itakayochezwa mjini Bukoba, Arusha na Tanga (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid), Pwani na Kinondoni (Uwanja Mabatini, Mlandizi), na Katavi na Mbeya zitakazoonesha kazi kwenye Uwanja wa Azimio.

Nazo Ruvuma na Iringa zitacheza Januari 19 mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji. Mechi hiyo itachezwa tarehe hiyo ili kusubiri matokeo ya mechi ya marudiano kati ya Shinyanga na Simiyu.

Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Januari 15 mwaka huu) kupitia ripoti ya mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza kati ya Shinyanga na Simiyu ambayo ilivunjwa na mwamuzi katika daika ya 70.

Baada ya kupitia ripoti, Kamati imebaini kuwa licha ya vurugu alizofanyiwa mwamuzi, bado mechi hiyo ingeweza kuendelea kwa kuchezeshwa na mwamuzi wa akiba kwa vile usalama ulikuwepo baada ya yeye kupigwa.

Pia Kamati imeagiza Katiba wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Sologo aliyeripotiwa kumpiga mwamuzi suala lake lipelekwe kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi, wakati Kocha wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye naye alishiriki kumpiga mwamuzi amesimamishwa wakati akisubiri kuchukua hatua zaidi.

Continue reading →

Waziri Mukangara azindua mfumo wa kununua filamu kwa njia ya mtandao

unnamed

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapo nchini Lu Youqing na Mwakilishi Mkuu wa Wafanyabiashara kutoka China waishio nchini Lin Zhiyong. Jumla ya vifaa kumi na nne vimetolewa ambavyo ni Roboti ya kujifunzia mpira wa Meza, Kifaa cha kupimia upepo kwa ajili ya Riadha,Nyavu ya mpira wa Meza, Mashine ya kupimia Uzito,Ulingo wa Ngumi,Kompyuta,Printa, Radio Call, mashine ya kutafsirina kuhesabu matokeo katika riadha na nyaya za umeme vyenye thamani zaidi ya 200.

unnamed2

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akicheza Mpira wa Meza na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

unnamed3

Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akielezea namna mmtambo wa Radio Call unavyofanya kazi, katika mwenye blauzi ya kitenge Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda

unnamed4

Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akielezea namna mmtambo wa Radio Call unavyofanya kazi, katika mwenye blauzi ya kitenge Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda

unnamed5

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija

………………………………………………………………………………………………..

Na. Benjamin Sawe

WHVUM

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara amewasihi wadau wa filamu kuongeza ujuzi na kubadilika ili kuendana na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni katika masuala yanayohusu tasnia hiyo hasa katika suala zima la teknolojia ya uandaaji na usambazaji wa filamu.

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa filamu za Kitanzania kwa njia ya mtandao ambao mfumo huo umebuniwa na kampuni ya Proin Promotion Limited ya nchi.

Dr. Mukangara alisema hatua hiyo ni fursa muhimu katika kupanua wigo wa soko na kuendana na mabadiliko yanayotokea duniani katika kila nyanja ikiwemo mauzo ya filamu kwa nja ya mtandao.

“Ipo aja kwa wadau wetu kupanua eneo la mauzo ya kazi za filamu kwa kutumia mifumo ya kisasa katika usambazaji na uuzaji wa kazi ikiwemo mauzo na manunuzi kwa njia ya mtandao”.Alisema Dr. Mukangara

Alisema njia hiyo ikitumiwa vizuri itakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wadau kuongeza idadi ya wanunuzi wa kazi za filamu kwani zitaweza kuwafikia watu sehemu mbalimbali ulimweguni kwa urahisi pamoja na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kushindana na wafanyabiashara wakubwa kupitia kazi watakazozizalisha.

Alizitaja faida nyingine nia pamoja na kupata wafadhili na misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wa filamu ulimwenguni ikiwa ni pamoja na kupata faida zaidi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanunuzi wa kazi zao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion Bw. Johnson Lukaza alisema kunachangamoto ya jinsi ya kudhibiti maharamia wanaoiba kazi za wasanii amabazo wanazifanya kwa jasho na manufaa wanayopata huwa finyu.

“Tunatumaini njia hii huenda ikaleta nafuu ya kipato zaidi kulingana na hali ilivyo sasa kwa kuongeza wigo wa mauzo ambao kwa sasa utakuwa ni wa urahisi duniani kote”.Alisema Bw. Lukaza.

Alisema kampuni yake hainunui haki za msanii bali inampa mrahaba wa kila nakala ambayo inauzwa ambapo mfumo huo unaongeza kila nakala ambayo itakuwa imenunuliwa hivyo kumfanya msanii kufaidika kwa kila nakala inayouzwa na kwa wakati wowote

“Sasa hivi wasanii watapata fursa ya kuuza kazi zao kupitia mtandaoni hata kaziwalizofanya miaka ya nyuma na kuanza kufaidika tena pamoja na vizazi vyao.”Alisema Bw. Johson.

DStv SUBSCRIBERS SCORE WITH A SPECIAL AFCON CHANNEL

images (1)Africa’s biggest sporting spectacle, the 2015 Africa Cup of Nations (Afcon) is coming to DStv.

From the 17th of January until the 8th of February, all Compact, Compact Plus package subscribers will get special access to an Afcon-dedicated channel, SuperSport 5 (SS5). Furthermore, SS9 East Africa will now also be available on the Family bouquet, further making the tournament available to more subscribers. The channels will only be available on the bouquets for the duration of the Afcon tournament.

The activation of the channels on the lower tier bouquets forms part of MultiChoice’s continued efforts to give subscribers access to our exciting range of entertainment content via our different technological platforms while putting a spotlight on the abundance of sports talent on the continent.

DStv Premium and Compact Plus subscribers will also have access to view all 32 matches from the tournament in both HD and SD across three other SuperSport channels: SS7 which will act as the overflow channel for SS5 at the playoff stage where matches will kick off simultaneously, SuperSport Select and Maximo (where available).

 “Afcon is Africa’s biggest football event and we are delighted to offer it to our subscribers on our multiple channels and platforms,” said Peter Fauel, General Manager MultiChoice Tanzania. “The channel that has been dedicated to Afcon will bring our subscribers closer to the soccer action and convey the excitement of the Afcon taking place in Equatorial Guinea.”

The live Afcon coverage will feature expert analysis from some of the most recognisable faces in the football industry like Ghanaian-born, former France football star Marcel Desailly, former South African national team player Neil Tovey, Ghanaian former international player Samuel Kuffour and the South Africa’s former striker, Benni McCarthy.

To add to the Afcon excitement, DStv and SuperSport have launched the #AfricaShowYourLove campaign to encourage subscribers to show their support for their favourite teams by uploading pictures of themselves dressed up in their football fan regalia onto the DStv Facebook page to win great prizes.

TAARIFA KUTOKA KWA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI TFF

indexPOLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matukio ya vurugu na uvunjifu wa amani ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za FDL zinazochezwa kwenye uwanja huo, ikiwemo ile ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui ya Shinyanga ambapo waamuzi walipigwa.

Kamati zinazohusika zitakutakana hivi karibuni kupitia matukio yote ya utovu wa nidhamu kwenye FDL, na hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ikiwemo na viwanja ambavyo vimekuwa na sifa ya vurugu.

Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vina wajibu wa kutoa ulinzi wa kutosha viwanjani wakati wa mechi.

RAUNDI YA PILI TAIFA CUP WANAWAKE JUMAMOSI

Mechi za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17 mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.

Timu tisa zilizofuzu kutoka raundi ya kwanza baada ya mechi za nyumbani na ugenini akiwemo mshindwa bora (best loser) zitaungana na Ilala, Kinondoni na Temeke kucheza raundi ya pili. Mechi za marudiano za raundi hiyo zitachezwa Januari 21 mwaka huu.

Hatua ya robo fainali itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu fainali na fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions itafanyikia jijini Dar es Salaam.  

KOCHA NOOIJ KUTAJA STARS MABORESHO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij anatarajia kutaja kikosi cha Maboresho kitakachoingia kambini Januari 18 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu jijini Mwanza.

Nooij atataja kikosi hicho kwenye mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Januari 15 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Uwanja wa Karume.

RAMBIRAMBI MSIBA WA STEPHEN NSOLO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) uliotokea jana (Januari 13 mwaka huu) jijini Mwanza.

Msiba huo ni pigo kwa wadau wa mpira wa mpira wa miguu kwani wakati wa uhai wake, Nsolo alitoa mchango mkubwa akiwa kiongozi. Aliongoza SHIREFA akiwa Katibu kuanzia mwaka 1975 hadi 1994.

Kabla ya hapo alikuwa Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha miaka kumi. Pia aliwahi kuwa mwamuzi wa daraja la kwanza na kamishna wa mpira wa miguu kwa muda mrefu.

TFF inatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, SHIREFA na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwa msiba huo.

Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo (Januari 14 mwaka huu) katika makaburi ya Shinyanga Mjini. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

 

KOMBE LA MAPINDUZI CUP UWANJA WA AMANI

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Simba kabla ya mpambano wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa Sugar katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar mchezo uliofanyika jana Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

unnamed1Kikosi kamili cha Timu ya Simba kikiwa katika picha ya pamoja Uwanja wa Amaan Studium jana wakati wa Mpambano wa mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup na Timu ya Mtibwa Sugar mchezo huo ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein [Picha na Ikulu.]

unnamed3Wananchi na Mashabiki wa timu ya Simba wakifuatilia kwa makini mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3, [Picha na Ikulu.]

unnamed4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Izhaka baada ya kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi uliofanyika jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan Studium,[Picha na Ikulu.]

unnamed5Wachezaji wa Timu ya Simba wakisherehekea ushindi wao baada ya kuwafunga kwa matuta timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi 4-3 katika uwanja wa Amaan studium Mjini Unguja jana katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

unnamed6Mashabiki wa Timu ya  Simba Wengundu wa Msimbazi walipokuwa katika jukwa la   Saa katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja wakishangilia timu yao ilipocheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali ya kombe la Mapinduzi,Timu hiyo ya Simba ilishinda kwa matuta 4-3ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]

unnamed2Bendera ya Shirikisho la mchezo wa Mpira wa Miguu FIFA iliyobebwa na Vijana wakiwepo na waamuzi wa Mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Timu ya Mtibwa Sugar na Simba katika Uwanja wa Amaan Studium katika kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika mchezo huo Simba iliibuka kwa ushindi wa matuta 4-3 dhidi ya Mtibwa, [Picha na Ikulu.]

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto) wakiangalia mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi Cup kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliochezwa jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ikiwa ni katika kusherehekea miaka 51 ya mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambapo simba iliweza kutokakifua mbele kwa kuwafunga Mtibwa matuta 4-3 , [Picha na Ikulu.]

MIKANDA MIWILI YA UBINGWA WA TAIFA WA NGUMI KUGOMBANIWA MANYARA PARK JANUARY 30

Na Mwandishi Wetuindex
BONDIA Ibrahimu Tamba ambaye ni bingwa wa uzito wa kg 72 ambaye ni bingwa wa TPBO anatarajia kuvaana na Baraka Mwakansope wa Mbeya mpambano wa ubingwa wa raundi kumi utakaofanyika january 30 katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM
akizungumzia mpambano huo promota Jafari Ndame amesema siku hiyo kutakuwa na mipambano miwili ya ubingwa yote yakiwa na raundi kumi kila moja mpambano mwingine utawakutanisha Azizi Abdallah akatakaekabiliana na Selemani Zugo pia kutakuwa na mipambano mingine mikali ya utangulizi ambapo
bondiaTasha Mjuaji atapambana na Bakari Dunda na Jems Kibazange atacheza na Stivin Kobelo wakati Julius Kisarawe atapambana na Jems Martin na shomali Mirundi atakabiliana na Shedrack Ignas na Twaha Issa atakutana na Kassim Gamboo uku Husein Gobos akicheza na Samweli Stopa wakati Iddi Mgodomi atapambana na Shomari Punzi

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

indexSTARS MABORESHO, RWANDA KUCHEZA MWANZA JAN 22

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN). Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda jijini Mwanza.

TAIFA CUP WANAWAKE KUPIGWA JUMAMOSI

Mechi za kwanza za raundi ya kwanza za mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa kesho (Januari 10 mwaka huu) kwenye miji 11 tofauti nchini.

Katika mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin, Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora itacheza na Kigoma kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Simiyu na Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha na Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro na Tanga (Uwanja wa Ushirika).

Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma na Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya na Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi na Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma na Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.

Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwaka huu, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.

Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwaka huu wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwaka huu.

Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.

KILUVYA UTD, NJOMBE BADO ZAKIMBIZA SDL

Kiluvya United ya Pwani na Njombe Mji ya mkoani Njombe ndizo timu pekee zilizomaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa kushinda mechi zote katika makundi yao, hivyo kujipatia pointi 15 kila moja.

Njombe Mji imeongoza kundi D lenye timu za Mkamba Rangers ya Morogoro iliyofikisha pointi nane, Wenda ya Mbeya pointi sita, Volcano FC ya Morogoro pointi sita, Town Small Boys ya Ruvuma pointi tano na Magereza ya Iringa yenye pointi moja.

Katika kundi C, Kiluvya United inafuatiwa na Mshikamano ya Dar es Salaam yenye pointi kumi, Abajalo pia ya Dar es Salaam pointi saba, Cosmopolitan na Transit Camp za Dar es Salaam ambazo kila moja imemaliza mzunguko huo ikiwa na pointi tano. Kariakoo ya Lindi haina pointi.

Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma na Singida United ya Singida ndizo zinazochuana katika kundi A kila moja ikiwa na pointi nane. Mvuvuma FC ya Kigoma yenye pointi tano ndiyo inayofuatia, wakati Milambo ya Tabora ina pointi nne huku Ujenzi Rukwa ikikamata mkia kwa pointi moja.

Pia mchuano mkali uko katika kundi B ambapo JKT Rwamkoma ya Mara na Mbao FC ya Mwanza ziko kileleni kila moja ikiwa na pointi tisa. AFC ya Arusha inafuatia kwa pointi sita, Bulyanhulu FC ya Shinyanga ina pointi nne wakati Pamba FC ya Mwanza iko mkiani kwa pointi moja.

Mzunguko wa pili wa ligi hiyo itakayotoa timu nne zitakazopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao (2015/2016) utaanza kutimua vumbi Januari 24 mwaka huu.

YAYA TOURE MWANASOKA BORA WA AFRIKA KWA MIAKA MINNE MFULULIZO

article-2077899-0F42D59700000578-75_306x480

Kiungo mchezeshaji wa Manchester City, Yaya Toure ameibuka na kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2014

Ushindi huo wa Toure unamfanya awe amechukua tuzo hiyo mara nne mfululizo.

Toure, 31, ameibuka mshindi katika sherehe za tuzo hiyo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Lagos Nigeria.

Raia huyo wa Ivory Coast amewashinda mshambuliaji wa Borussia Dortimund raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.

Toure ameingoza Man City kubeba ubingwa wa England huku yeye akiwa amepachika mabao 20 na kuwa kiungo mwenye mabao mengi zaidi England.

Bondia mtanzania Omari Kimweri anayetesa Australia kutoa sapoti ya mafunzo ya ndondi Dar

Kutua Februari, apania kuzalisha akina Mayweather kibao nchini
NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.
Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Kwa hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Michael Yombayomba, Stanley Mabesi ‘Ninja’ Rashid Matumla, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’  na wengineo wengi.
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant.
Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu kwa sasa.
Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.
Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo, zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia mafanikioi ya akina Mayweather.
Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.
Bondia huyu wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia nyota.
Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchiniDeer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanamasumbwi wa Tanzania.
Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.
Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.
“Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya,  Hispania,” anasema Super D.
Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.
Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia, lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.
“Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,” anasema.
Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion, umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.
Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa hapa nchini kama Mbwana Matumla, FrancisMiyeyusho,Ibrahimu Class’ King Class Mawe’ ambaye ni bingwa
wa WPBF Africa na wengineo.

 

Chamijata kuenda China Machi 28

indexMwandishi Maalum

CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) kimesema kimepata mwaliko kushiriki mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika nchini China kuanzia Machi 28 hadi 20 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chamijata Tanzania Mohammed Kazingumbe wakati akizungumza na Fullshangwe katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.

Alisema Chamijata imekuwaikipata mialiko mara kwa mara katika nchi za China na Korea Kusini hivyo kwa mwaka huu mwaliko wa kwanza ni kutoka China na mialiko mingine ipo ambayo ni kwenda Korea Kusini mwezi Septemba.

Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa wanahangaika kutafuta wafadhili ili waweze kupeleka timu na viongozi wa Chamijata wakati huo ukifika.

“Tumepata mwaliko wa kwenda China katika mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika Machi 28 hadi 30 hivyo jithada na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunashiriki,” alisema Kazingumbe.

Kazingumbe alisema Chamijata ina imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kuwa michezo ya jadi inarejea katika hadhi yake ya awali ambapo amewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha hilo.

Mwenyekiti huyo alisema Chamijata katika kuhakikisha kuwa inakuza mchezo huo itatumia kitabu ambacho wamekiandika chenye maelezo kwakina kuhusu mchezo wa bao.

Chamijata yapata msaada wa mabao kutoka kwa Diwani

indexMwandishi Maalum

DIWANI wa Kata ya Msongola Angelina Malembeka ametoa msaada wa mabao matatu kwa Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) ikiwa ni jitihada zake za kuendeleza mchezo huo.

Malembeka ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Manispaa ya Ilala alikabidhi mabao hayo jana katika ofisi za Chamijata zilizipo Temeke jijini Dar es Salaam.

Alisema ameamua kutoa msaada huo kwa Chamijata kutokana na kuona kwa muda mrefu mchezo huo umeshindwa kuvuma hivyo kwa kuanzia mabao hayo yatawasaidia.

Diwani huyo alisema pia katika kuendeleza mchezo huo amegawa mabao katika mitaa tisa ya Kata yake lengo likiwa ni kuendeleza mchezo huo kuanzia Mitaa hadi ngazi ya Taifa.

“Jamani naomba mpokee mabao haya ila naahidi kuendelea kuwasaidia pale msaada utakapo hitajika kwani mimi ni mdau  wa michezo hasa michezo ya jadi,” alisema Malembeka.

Malembeka alisema iwapo michezo ya jadi itapewa kipaumbele ni dhahiri kuwa jamii itadumisha tamaduni zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chamijata Gamaliel Mhanga alimshukuru Diwani huyo kwa msaada wa mabao hayo ambapo aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia chama hicho.

Mhanga alisema Chamijata imejipanga kutekeleza mipango yake mbalimbali ya kuboresha na kuendeleza michezo ya jadi kwa kushirikiana na wadau kama Diwani Malembeka.

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE KATIKA KIPINDI CHA KRISMAS NA MWAKA MPYA

Bondia Jacobo Maganga kushoto akipambana na Shabani Kaoneka wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa sare Picha na SUPER D BOXING NEWS

 

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS

 

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ katikati akiwa na mabondia Shomari nMirundi kushoto na Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28

 

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ kushoto akiwa na mabondia Shomari Mirundi katikati na Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28
Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akipambana na moro best wakati wa mbambano wao kumbele alishinda kwa pointi mpambani huo wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Jacobo Maganga kushoto akipambana na Shabani Kaoneka wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa sare katika mpambano huo uliovuta isia za watu wengi Picha na SUPER D BOXING NEWS