All posts in SIASA

TAARIFA KWA WABUNGE NA WAGOMBEA WATARAJIWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2015 TANZANIA

Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Rais unataraji kufanyika hapo mwakani, Wabunge na wanaotaka kuwania Ubunge katika majimbo mbalimbali nchini hata urais mnakaribishwa kuandaa TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA VYAMA VYENU. Kitabu kama hicho kitakuwezesha wewe Mgombea kuto tumia nguvu kuubwa ya kujinadi badala yake utavigawa kwa wananchi mbalimbali jimboni kwako nawe kuelewa nini umewafanyia katika kipindi ambacho ulikuwa madarakani. 
 
Pia wagombea wapya pia wanaweza andaa vitabu kama hivi kuonesha yale ambayo wameshiriki kuyafanya na wanataraji kuyafanya chini ya ilani za vyama vyao husika. 
Mawasiliano zaidi kwa wenye uhitaji: Mroki Mroki (pichani juu) 
+255 717 002303/0755 373999/0788207274 
au barua pepe: mrokim@gmail.com

DK. EDMUND MNDOLWA: MSIWABUGHUDHI VIONGOZI WALIOPO MADARAKANI WAACHENI WACHAPE KAZI

Dotto Mwaibale

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametakiwa kuacha kuwabugudhi viongozi waliopo madarakani kwa kuchaguliwa waendelee kuchapa kazi badala ya kuanza kuzihitaji nafasi zao kabla ya wakati.

Mwito huo umetolewa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama hicho wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Dk.Edmund Mndolwa wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo.

“Wito wangu kwa wanachama wenzangu wenye lengo la kutaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chama chetu wasianze kutamka nia ya kuwania nafasi hizo kabla ya wakati kwani kufanya hivyo ni kuwapunguzia kasi ya utendaji viongozi waliopo madarakani.

Mndolwa alisema mtu anapotokea kuanza kuonesha nia kwa mfano wa kugombea ubunge katika eneo fulani kunamfanya mbunge aliopo katika eneo hilo kuacha kufanya shughuli za kuwatumikia wananchi badala yake anaanza kutumia muda mwingi wa kupambana na mtu huyo anayetaka kugombea kwenye jimbo husika.

Katika hatua nyingine Mndolwa amewataka watanzania kuendelea na mchakato wa Bunge la Katiba kwani ndio mahitaji yao badala ya kusitisha Bunge la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma.

“Kwa mtazamu wangu ni vizuri mchakato wa bunge hilo ukaendelea kwani ndio mahitaji ya watanzania waliowengi kukomea njiani ni kupoteza mabilioni ya fedha za wananchi kutoka na vikao vinavyoendelea kufanyika” alisema Mndolwa,.

Mndolwa alisema hivi sasa yupo katika ziara ya kutembelea mashina na matawi ya CCM wilayani humo kwa ajili ya kuimarisha uhai wa chama na kujua changamoto mbalimbali zilizopo ili kuziwasilisha ngazi ya juu kwa hatua ya utekelezaji.

LHRC, WASANII KUZINDUA FILAMU NA WIMBO WA KATIBA KWA AJILI YA KUHAMASISHA MCHAKATO WA KATIBA MPYA AGOSTI 9,2014

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Halord Sungusia (katikati), akionesha Rasimu ya Katiba Mpya wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa Filamu, Wimbo wa Katiba na mpango wa kugawa Rasimu ya pili ya Katiba katika mikoa 20 ya Tanzania. Kulia ni Msanii, Chrispiny Masele na Edson Kalokola. Wasanii hao wameshiriki katika Filamu hiyo ambayo inazinduliwa leo ukumbi wa Mlimani City.
Hapa Halord Sungusia akionesha Kadi zenye Filamu hiyo.
Msanii Edson Kalokola akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Msanii Edwardo Mwanisongole.
Wanahabari wakiangalia filamu hiyo wakati wa mkutano huo.
Wasanii walioshiriki kucheza filamu hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
WANATAALUMA na Wasanii wametakiwa kutumia ujuzi wao ili kuelimisha jamii katika uelewa wa mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea nchini.
Mwito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Halord Sungusia wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa Filamu, Wimbo wa Katiba na mpango wa kugawa Rasimu ya pili ya Katiba katika mikoa 20 ya Tanzania.
“Tunawaomba wanataaluma, wasanii watumie nafasi na vipaji walivyonavyo kuongeza hamasa ya wananchi ili washiriki kikamilifu katika mchakato wa kujipatia Katiba Mpya” alisema Sungusia.
Sungusia alisema LHRC kinaamini kuwa ni wajibu kwa vyombo vya habari kuhakikisha kwamba filamu na wimbo wa katiba vinatangazwa ili wananchi wapate elimu na taarifa sahihi ya katiba na hatimaye waweze kushiriki vyema wakati wa kupiga kura ya maoni.
Alisema hatua hiyo itahakikisha kuwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa watapata naaaaafasi ya kushiriki kikamilifu katika safari nzima ya kupata katiba mpya na iliyo bora.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na asasi mbalimbali pamoja na wasanii wameandaa Filamu na wimbo wa katika kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba mpya ambapo leo hii Filamu hiyo itazinduliwa ukumbi wa Mlima City jijini Dar es Salaam.

MAKATIBU UENEZI WA CCM WA KATA 90 MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATIWA SEMINA ELEKEZI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu waenezi 90 wa CCM wakati akifungua semina elekezi ya siku moja kwa makatibu hao kutoka Kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba na Katibu Muenezi Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Athuman Salum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu hao.
Makatibu Uenezi hao wakishangilia hutuba ya mgeni rasmi, Ramadhani Madabida.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Temeke wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Ilala wakipitia taarifa yao ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa chama chao.

Makatibu uenezi wa Wilaya ya Ilala wakiwa kwenye semina hiyo.

Hapa makatibu hao wakiwa kwenye majadiliano.
Makatibu hao kutoka Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hutuba ya mgeni Rasmi Ramadhani Madabida.
Makatibu uenezi hao wakiwa kwenye semina hiyo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 
Dotto Mwaibale
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amewataka makatibu waenezi wa chama hicho kumtetea Rais Jakaya Kikwete na chama hicho ili aendelee kuaminiwa na wananchi.
 
Madabida alitoa mwito huo wakati akifungua semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa mahususi kwa makatibu waenezi 90 wa chama hicho kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika leo ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala.
 
“Ninyi ni kama maofisa mawasiliano na masoko hivyo mnawajibu wa kukiuza na kukitangaza chama chetu kwa wananchi ili waendelee kuwa na imani nacho na serikali kwa ujumla” alisema Madabida.
 
Alisema kazi yenu kubwa ni kumtetea rais ambaye ni Mwenyekiti wetu wa chama taifa na ili aendelee kuheshimika kwa wananchi hasa pale anapochafuliwa na wapinzani.
 
Katika hatua nyingine Madabida aliwataka makatibu ueneze hao kuwa wamoja na kuacha kuwachukia viongozi waliopo madaraka baada ya chaguzi kuisha na akatoa onyo kuwa hata kuwa na mswalia mtume kwa mtu atakayebainika kuendeleza chuki hicho.
 
“Kumekuwa na tabia ya watu kuendeleza chuki baada ya kukosa nafasi katika uchaguzi hivyo kutufanya tushindwe kusonga mbele nasema katika hilo mtaniita majina mengi mabaya kwani siqwezi kumvumilia mtu” aliongeza Madabida.
 
Madabida aliwataka makatibu uenezi hao kufanya mikutano ya hadhara ili kukinadi chama chao kwani wenye wajibu wa kutekeleza ilani ya chama ni wao na si mtu mwingine.

Wazee wa Dar es salaam wawataka UKAWA kurudi Bungeni

WAZEE 02Mzee Alhaji Sheikh Bakari Chiwaka (kulia) akisisitiza umuhimu wa maridhiano katika mchakato wa Katiba Mpya na kuwa Katiba bora itapatikana kwa uongozi bora na wa kidemokrasia nchini. Kushoto ni Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora.
WAZEE 05Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamed Ligora akisisitiza (katikati) umuhimu wa kupata Katiba bora ya nchi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mzee Sheikh Yahaya Ngoma na kulia ni Mzee Alhaji Sheikh Bakari Chiwaka.

(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
 
 Na Immaculate Makilika –MAELEZO_DAR ES SALAAM
WAZEE  wa Mkoa wa Dar es salaam wamewaomba Umoja wa Katiba wa Wananchi (UKAWA) kurudi Bungeni ili kuendelea na mchakato wa majadiliano ya Rasimu ya Katiba Mpya yanayoendelea.
Wazee hao wamesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini pamoja na Bunge la Katiba Mpya linaloendelea mjini Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya  Wazee wenzake  Kepteni Mstaafu Alhaji Mohamedi Ligora , amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri na watu wake ni wazuri ni vema  UKAWA na wenzao  wakarudi Bungeni kujadiliana ili watimize matakwa ya kidemokrasia.
Amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawataki kufananishwa  na nchi zingine zilizofanya makosa na kupata matatizo kutokana na mambo kama haya ambayo yalisababisha wananchi wao kuzikimbia nchi zao kwa mambo ambayo wangeweza kukaa chini na kumaliza wenyewe kwa ajili ya maslahi ya umma.
Kapteni Mstaafu Alhaji  Ligora amesema kuwa suala la mchakato ni suala la kidemokrasia, hivyo ni vyema  UKAWA wakatumia fursa hiyo waliyonayo kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Rasimu ya Katiba hali itakayosaidia kupatikana kwa Katiba Mpya ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tanzania.
Aidha, amewaomba wajumbe walio Bungeni na wale walio nje ya Bunge kuacha kuwazomea UKAWA badala yake wawasihi warudi katika chombo rasmi cha kuboresha Rasimu ya Katiba Mpya.
 Naye Mzee Ali Bakari Muki, amewataka UKAWA kuheshimu misingi ya demokrasia lakini pia amewapongeza wabunge walioitikia wito wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kurudi Bungeni na kuendelea na majadiliano kuhusu Katiba kwani ndio Jukwaa pekee la kuwapatia wananchi Katiba bora.
Kwa upande wake  Mzee  Yahaya  Ngoma amewataka viongozi wote hasa UKAWA kuheshimu na kudumisha jitihada zilizofanywa na  waasisi wa Taifa hili akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuzingatia misingi na kanuni za uongozi bora kwa kutumia  njia ya majadiliano pale panapokuwa na mawazo tofauti baina yao.
Halikadhalika, Alhaji Sheikh Bakari Chikawa  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na kusisitiza ni moja ya tunda la uongozi bora na demokrasia nchini.
Aidha, ameongeza kuwa UKAWA ni vema wakatumia fursa hiyo ya demokrasia kwa kuwawakilisha vema wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha wanapata Katiba Bora.
Alhaji Chikawa amewaomba  UKAWA kurudi Bungeni kwani kunyume na hivyo ni watakua wametenda dhambi na madhara yake ni makubwa sana, na kusisitiza kuwa mazungumzo ni muhimu na  yakipuuzwa basi kuna madhara.

MBUNGE MSIGWA AENGULIWA KUGOMBEA UENYEKITI WA CHADEMA WILAYA KWA KUKOSA SIFA

mh Msigwa 
Mbunge Msigwa kulia akiwa na mbunge Chiku 
    mbunge mchungaji Msigwa kushoto akiwa na mbunge Chiku Abwao katika moja kati ya  vikao  vya baraza la madiwani Manispaa ya Iringa 
Na Francis GodwingaBlog
 
KAMATI ya uchaguzi  wa mkuu wa  wilaya ya Iringa mjini  kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemuengua katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa wilaya hiyo mbunge wa  jimbo la Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa ambae ndie alikuwa wenyekiti anayemaliza muda wake kwa  kukosa sifa ya kutetea tena nafasi hiyo.
 
Hatua  hiyo ya  kuenguliwa kwa Msigwa  imekuja baada ya  wajumbe  kulalamikia hatua ya chama kushindwa kulipa kodi ya ofisi ya kata na ile ya wilaya pia ugomvi mkubwa uliopo kati ya mbunge Msigwa na mbunge mwenzake wa  viti maalum mkoa Chiku Abwao aliyekuwa akigombea nafasi ya kiti mkoa wa Iringa nafasi ambayo msigwa pia alitangaza kugombea .
 
Hivyo  kutokana na mvutano huo kamati  hiyo  iliyoketi usiku wa  leo  ukumbi wa Sambala mjini hapa ililazimika  kuchukua uamuzi mgumu wa kufyeka majina ya wabunge hao kugombea nafasi hizo ili  kunusuru  chama.
 
Mmoja kati ya makada wa  ambae alishiriki kikao hicho cha kumuengua Msigwa na Chiku alisema kuwa chanzo cha msigwa kuenguliwa ni kutokana na kuendekeza kukuza makundi ndani ya chama na kuwa mbali na chama zaidi ya kufanya chama  kuendelea kukosa heshima.
 
Makundi hayo yanaelezwa kukiwekwa rehani chama hicho wakati kikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
Pamoja na Mchungaji Msigwa, taarifa hizo zimesema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Chiku Abwao (Chadema) naye ameenguliwa kuwani nafasi yoyote ya uongozi katika chama hicho mkoani hapa.
 
Hivikaribuni Abwao alinukuliwa akitangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa wa chama hicho unaotarajia kufanyika Jumapili keshokutwa.
 
Kuenguliwa kwa Msigwa katika uchaguzi huo kumeacha kampuni wagombea wawili wanaomenyana katika nafasi hiyo itakayosaidia kutoa picha ya jinsi mambo yatakavyokuwa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini mwaka 2015.
 
Wagombea hao ni Frank Nyalusi anayeelezwa kuwa ni mfuasi wa kufa na kupona wa Mchungaji Peter Msigwa na Mohamed Makuke ambaye ni mfuasi wa kundi la wengi linalodaiwa kumpinga Mchunngaji Msigwa.
 
Kundi linalojiita la wengi katika chama hicho limesikika likisema mara kwa mra kwamba tabia ya Mchungaji Msigwa ndani ya chama hicho inawaweka katika wakati mgumu wa kutetea nafasi ya ubunge mwaka 2015.
 
Mchungaji Msigwa ni kiongozi asiyeambilika, anayejua kila kitu, mbishi, kaidi, mwenye kiburi, asiyependa watu, mwenye visasi, majivuno na asiyetaka ushirikiano toka kwa wenzake, asiye na mikakati ya kujenga chama huku akiamini siasa za kitaifa pekee anazopenda zaidi zinaweza kulinusuru jimbo hili katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
 
Wakati Mchungaji Msigwa akirushiwa lawama zote hizo, taarifa za uhakika zimedai kwamba ofisi ya wilaya ya chama hicho imefungwa na wameamuliwa kuondoka baada ya uongozi wa mbunge huyo unaomaliza muda wake kushindwa kulipa kodi ya pango. Mchungaji Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Iringa Mjini anayemaliza muda wake hii leo.
 
Wanachama wa chama hicho wamechukizwa kwa hatua ya mbunge wao kuridhia kupoteza ofisi pekee ya chama hicho mjini Iringa kwasababu ya kushindwa kulipa Sh 540,000 walizokuwa wakidaiwa.
 
Kwa upande  wake  mbunge Msigwa alinukuliwa na mwandishi wa habari  hizi akimrushia maneno  mmoja kati ya  viongozi wa  chama  hicho  kuwa  watu  wanamchafua kwa suala la ofisi na  kuwa  ni ruksa kwa  wanachama ambao  wanapenda vyama vyenye ofisi  kuhama chadema na  kujiunga na vyama  hivyo .
 
Huku mbunge Chiku Abwao amethibitisha kuenguliwa  kwao katika  nafasi hizo japo amedai  kwa  upande  wake kaonewa na ataendelea  kutumia vikao kuomba  kurejeshwa kwa  jina lake.

OFISI YA CHADEMA KATA YA RUAHA JIMBO LA IRINGA MJINI YACHUKULIWA NA CCM BAADA YA CHADEMA KUSHINDWA KULIPA KODI

IMG_9966Katibu wa CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu ( wa  pili  kushoto ) na kada wa Chadema aliyehamia CCM Ibrahim Mmasi  pamoja na  wanachama  wengine wa CCM wakiwa  wameshika bendera ya CCM ambayo itapepea katika ofisi mpya ya kata ya Ruaha ,ofisi ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Chadema kabla ya  kufukuzwa kwa  kushindwa kulipa deni la kodi kiasi cha Tsh 540,000 , kushoto fundi rangi akiendelea  kupaka rangi ya CCM

IMG_9940Fundi akipaka rangi kuta za ofizi hiyo

 

………………………………………………………………..

 

 

CHAMA  cha  demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Ruaha  jimbo la Iringa  mjini kimepata  pigo  kubwa baada ya kufukuzwa katika nyumba  waliyopanga kama ofisi  ya kata  hiyo baada ya  kushindwa  kulipa deni la  pango  kiasi cha Tsh 540,000 walizokuwa  wakidaiwa na mwenye nyumba  deni  ambalo limelipwa  na Chama  cha mapinduzi (CCM ) kata ya  Ruahakabla ya  kuichukua ofisi  hiyo .
 
Mmiliki  wa nyumba  hiyo iliyopo mtaa wa Ngeleli Ipogolo Bi  Neema Mwasika alifikia  hatua  hiyo ya  kuwataka  kuondoka katika  ofisi  hiyo baada ya  jitihada za  kudai  deni lake  kushindikana na  hivyo kulazimika  kupangisha nyumba   hiyo yenye  chumba  kimoja na sebure  kwa  mpangaji mpya ambae ni CCM kata ya Ruaha.
 
Akizungumza na waandishi  wa habari  leo katibu  wa  CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu alisema  kuwa  awali CCM  kilikuwa na ofisi  yake  eneo la Ruaha  jirani na mto hivyo  kutokana na mvua  kubwa  zilizonyesha mwaka jana  zilipelekea  ofisi hiyo  kuharibiwa  vibaya na  hivyo  kukosa kabisa  ofisi .
 
Alisema kuwa  kutokana na kutokuwa na ofisi  cham a kilikuwa  kikitumia nyumba ya mtu binafsi kama  ofisi  pale ilipohitajika  kukutana  viongozi ama wanachama  .
 
Shungu alisema  kuwa jitihada za  kutafuta  nyumba ya  kupanga  ili  kutumika kama  ofisi ya muda ya  CCM kata  hiyo ya  Ruaha  ziliendelea kufanyika  chini ya aliyekuwa kada wa Chadema kata  hiyo kabla ya  kujiunga na CCM Bw  Ibrahim Mmasi
 
Hata  hivyo  alisema ofisi  hiyo alisema kuwa baada ya  kuona  ofisi  hiyo imefungwa kwa  muda na kuwasiliana na mwenye nyumba alikubali  kuwapangisha kwa makubaliano ya  kulipa deni kwanza jambo ambalo  lilifanyika  hivyo na kulipia kodi ya miaka  miwili zaidi.
 
” Tumeipata  ofisi  hii kihalali na sio hujuma kwani  makubaliano  kati ya mmiliki wa nyumba na mpangaji yalifanyika na  hivyo kwa  kuwa  hitaji letu  nyumba ya kupanga  tuliona  hiyo  ina  sifa ambayo tuliitaka  hivyo  tunachofanya ni kufuta rangi na nembo  za Chadema na kuweka rangi ya CCM na nembo  zetu …..na tutaizindua rasmi jumapili  wiki  hii”
 
Kwa upande wake  kada   wa CCM aliyehama kutoka Chadema Bw Mmasi  alisema  kuwa ofisi hiyo  ilikuwa imezinduliwa na viongozi wa  kitaifa  kupitia zoezi la oparesheni Sangara tarehe 19 mey 2011 chini ya  naibu mkuu wa Chadema enzi hizo Zitto Kabwe na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na viongozi  wengine .

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la asema Katiba itakuwa ni ya Makundi yote.

imagesNa Magreth   Kinabo
 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewahakikishia Watanzania kwamba  Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa imezingatia matakwa ya makundi mbalimbali.
Mhe . Sitta aliyataja makundi hayo  baadhi ya  makundi hayo kuwa ni wafugaji, wakulima, wavuvi na wasanii.Huku akisema Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa ni bora kuliko iliyopo sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mhe . Sitta wakati akizungumza na wafugaji wapato 44 kutoka mikoa mbalimbali,ambao waliongozwa na Mwenyekiti wa ujumbe huo, Huruma Ole Kalaita na Mlezi wao, ambaye mjumbe wa Bunge hilo na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi(CHADEMA).
“Tunaamini ni wakati wa Katiba Mpya… lazima iweze kupatikana. Itakayozingatia Sheria bora na maslahi ya makundi mbalimbali  yatapatikana.
“ Utungaji wa Katiba ni suala la wananchi kutanguliza suala la muundo wa Serikali si haki. Ni muhimu kutanguliza haki za raia. Kinachotangulia ni haki za raia wetu na makundi mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Sitta.
Aidha Mhe. Sitta aliwakikishia wafugaji hao,kwamba Bunge hilo “ liko hapa kisheria kwa kanuni zake linaendelea na wale wanaopiga kelele hawalitakii mema taifa letu kwa sababu demokrasia  yoyote ni kupata kura ya walio wengiu,” alisema.   
 Kwa upande wake Mlezi wa wafugaji hao, Mhe. Shibuda alimpongeza Mhe. Sitta kwa jitihada zake za kuendeleza  vikao vya Bunge hilo, ambapo pia alimsihii kuwa asikatishwe tamaa kwa dhamira yake njema ya  kuendelea kuongoza vikao vya  Bunge hilo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya wafugaji hao na wakulima wa zao la pamba nchini, alisema kuwa wako pamoja  naye.
“ Hivi Serikali tatu au mbili inatiririsha nini kwa wakulima na wafugaji. Tunataka viongozi wa kukabiliana na matatizo ya  wananchi,” alisisitiza Shibuda.
Kwa upande  Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kalaita alipendekeza Katiba Mpya, itamke matumizi bora ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.
 Makamu wa Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kasundwa Wamalwa kutoka Kanda ya Magharibi akisoma mapaendekezo ya risala yao waliyoiwasilisha kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Sitta, ambapo walipendekeza Katiba Mpya itambue wafugaji wa asili.
 Aidha Makamu Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuwa na hofu ya  Mwenyezi Mungu wakati wanapoendelea na mchakato huo.
Miongoni mwa makundi mengine waliofika katika ofisi za Bunge mjini Dodoma ni Jukwaa la Katiba (JUWAKATA) na Jukwaa la Wahariri.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. STEPHEN MASELE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Picha Na  2

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (Kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam

Picha Na. 1

Rais Mstaafu wa Awamu ya  Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (kulia) akisisitiza jambo  wakati wa mazungumzo na  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (Kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake

MH. LOWASSA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada wakati alipo mtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na kufanya nae mazungumzo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada akifafanua jambo wakati wa Mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akimtambulisha Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada pamoja na Ujumbe wake alioambatana nao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akielezea jambo kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada na ujumbe wake alioambatana nao wakati wa kikao chao kilichofanyika leo ofisini kwake Mwenge,jijini Dar es saalam.Kulia ni Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) na Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Mh. Namelock Sokoine (kulia) wakimsikiliza Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada (wa pili kushoto) wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na namna Ubalozi huo utakavyoweza kufanisha Mradi wa Ujenzi wa Shule na Hospitali katika Wilaya ya Monduli.Wa pili kulia ni Katibu wa Balozi wa Japan,Bw. Sato Firgt.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada mara baada ya kufanya nae mazungumzo ofisini kwake Mwenge,Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada

MEMBE NA NAPE WAHANI MISIBA YA WALIOPATWA NA AJALI MTAMA NA KUTEMBELEA MAJERUHI

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akisalimiana na Salum Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo.
Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe
akititoa  mkono wa pole kwa Ndugu Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume
mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama karibu na stendi ya mabasi ya Masasi,Katikati ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye ambaye alitoa salaam za rambi rambi kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.

Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa
Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akiongozana na  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kwenda kutoa salaam za rambirambi kwa familia zilizopoteza jina wao kwenye agari ya gari iliyotokea Mtama,kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini,Richard Kasesela .

Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

Mbunge wa
Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe
pamoja na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimsikiliza Mzee Halfani Libaba ambaye ameondokewa na mtoto wake wa kiume Rajab Halfani kwenye ajali mbaya ya gari lililoacha njia wakati dereva akijaribu kumkwepa mbuzi na kusababisha vifo vya watu 8.

 Mbunge wa
Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe  na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa CCM Mkoa na Wilaya ya Lindi wakionyeshwa eneo ambalo ajali ilitokea.

 Mbunge wa
Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe
pamoja na
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimpa pole mpiga picha maarufu Mohamed Selemani ambaye amelazwa kwenye hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.

 Mbunge wa
Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe
akimjulia hali na kumpa pole Ndugu Shaaban Issa mmoja wa majeruhi watatu wa ajali ya a gari iliyotokea Mtama na kusababisha vifo vya watu 8.

Balozi Mpya wa Ujerumani aonana na Rais Dk.Shein.

IMG_0488 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe,Egon Kochanke,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

IMG_0520

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi Mpya wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe,Egon Kochanke,baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

IMG_0542

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi Mpya wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe,Egon Kochanke,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana kujitambulisha.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 

MBUNGE WA CHADEMA AELEZA SABABU ZA KUREJEA BUNGENI

Arfi

Na Magreth Kinabo, Dodoma
 
Mjumbe wa Bunge  Maalum la Katiba Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda  Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya  Mwenyezi Mungu.
 
Aidha Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katikaBunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa Katiba mpya kwa amani na utulivu kwa kutumia kipaji chake na kuwatumikia Watanzania.
 
Kauli hiyo   imetolewa leo mjini Dodoma na mjumbe huyo, wakati akihojiwa na kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na  Shirika la Utangazaji la Tanzania(TBC).
Akizungumza katika kipindi hicho, huku akinukuu kitabu cha Nabii Musa,  Arfi alisema Mwenyezi Mungu hawapendezwi na mtu mwenye jeuri na anayejivuna.
 
“Nimejitathimini na kuona mimi mwenyewe ni nina nafasi gani… maaskofu, mapadre, wachungaji na masheikh. Viongozi wetu wametusii turudi turudi napata kiburi wapi cha kutokurudi,” alihoji Arfi.
 
Akirejea katika kitabu cha Qruan anasema Mwenyezi Mungu hapendezwi na mtu mwenye kiburi na anayejivuna. 
 
Aliongeza kuwa viongozi hao “ wana nafasi kubwa pia wanaheshima ndio maana nimeweza kurudi,””alisema.
 
Mjumbe huyo alisema  sasa ni wakati wa kila mtu kueleza ukweli, kwani amerejea katika Bunge hilo, amepata bahati ya kuchangia katika sura ya nne katika kifungu cha 43na 44 kinachohusu haki za msingi.
 
“Nimepata fursa ya kutoa mapendekezo ya haki za wazee nisingewezakuwasilisha kama ningekuwa nje. Pia haki za wafanyakazi,” alisema.
 
Akizungumzia kuhusu wajumbe wenzake waliosusia Bunge hilo, aliwataka kutanguliza maslahi ya taifa.Huku  akisisitiza kwamba atajitahidi kuwashawishi wajumbe walioko nje ya Bunge hilo ili waweze kurejea.
 
Arfi aliwahakikishia wananchi kuwa  wanawatengenezea  Katiba itakayowasaidia kubadilisha ya watu wote.

MAKAMANDA WA MATAWI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM KATA YA KIMANGA WALIVYOSIMIKWA

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akiwa kwenye hafla hiyo.

Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akifikwa skafu.Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akielekea meza kuu tayari kwa shughuli ya kusimika makamanda hao.Hapa Sadifa akisalimiana na wanachama wa CCM Kata ya Kimanga na vitongoji vyake.

Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kusimikwa kwa makamanda tisa wa vijana wa matawi katika Kata ya Kimanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tukiko.
Wanaccm wa Kata ya Kimanga wakiwa kwenye hafla hiyo.
Makamanda tisa wa Matawi Kata ya Kimanga wakila kiapo baada ya kusimikwa.
Vijana wa CCM Kata ya Kimanga wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi.
Wanaccm wakiwa kwenye hafla hiyo.
Akina mama wa CCM wakishangilia katika sherehe hiyo.
Sadifa akikabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi mbalimbali wa matawi wa Kata ya Kimanga.
Vijana wa CCM wa Kisukulu wakishangilia baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo.
Kamanda wa UVCCM Kata ya Kimanga, Scollastika Kevela (wa pili kulia), akiwa na makada wa CCM kwenye sherehe hiyo.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa (kulia), akihutubia kwenye hafla hiyo.

Makamanda wa matawi waliosimikwa wakisubiri kusimikwa.
Wanaccm wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Sadifa (katikati), akizungumza na makamanda hao baada ya kuwasimika.
Kamanda wa UVCCM Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (wa tatu kushoto) akiwa na makada wa chama hicho.Dotto Mwaibale

VIJANA nchini wametakiwa kuwa makini kwa kutumiwa na wanasiasa ili kuvuruga amani na usalama wa nchi uliodumu kwa muda mrefu.

Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Khamis Juma Sadifa wakati wa hafla ya kuwasimika makamanda tisa wa umoja huo wa matawi katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

“Ninyi vijana ndio walengwa wakubwa kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani na usalama wa nchi hivyo kuweni makini katika jambo hilo kwani tunachokihitaji ni amani na usalama wa nchi kwa watu wote na itikadi za vyama vyetu” alisema Sadifa

Sadifa alisema hata nchi hii ikitokea kuongozwa na chama kingine lakini bila ya kuwa na amani ni kazi bure hivyo ni vema kila mmoja wetu akatambua kuwa hana budi kuilinda amani iliyopo na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Sadifa alitoa baraka zake kwa Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, Scollastica Kevela kuendelea na utendaji kazi wake wa kuinua uhai wa chama katika kata yake kwa kuwatembea vijana na wanachama ili kujua changamoto zinazo wakabili.

“Nakuomba kamanda wangu Kevela endelea kufanya kazi yako ni kuimarisha chama katika matawi kwa kukukutana na vijana na si kukiuka sheria ya kuanza kufanya kampeni kama inavyodaiwa” Sadifa alitoa onyo.

Sadifa aliongeza kuwa kazi kubwa ya ukamanda wa vijana ni kuwakutanisha vijana na kusikia changamoto walizonazo na kuziwakilisha ngaji ya juu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Kevela alisema kazi ya kuwainua vijana kiuchumi ndio kipaumbele chake cha kwanza na atahakikisha anafanya hivyo kupitia vikoba ambako yeye ni Makamu wa Rais wa chama hicho nchini.

Alisema amekuwa akifanya ziara katika matawi mbalimbali kwenye kata yake ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kuimarisha chama hangamoto zinazowakabili vijana hao.

Katika hafla hiyo Sadifa alitoa vifaa vya michezo jezi na mipira kwa vilabu mbalimbali vya matawi katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa ofisi ya CCM katika eneo hilo ambapo zaidi ya sh. 500,000 zilipatikana.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA OFISI YA KATIBU WA BUNGE MAALUM.

sitta1(2)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM
BUNGE MAALUM LA KATIBA LIPEWE NAFASI YA KUFANYA KAZI ZAKE
Ofisi ya Bunge Maalum, imeshangazwa na kusikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari na makundi ya jamii yanayoeneza upotoshwaji mkubwa ambao umedakwa katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli aliyoitoa Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta (Mb) wakati wa mjadala wa kupitisha Kanuni tarehe 5 Agosti, 2014 kuhusu midahalo ya Katiba inayoendelea katika baadhi ya televisheni hapa Nchini.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mhe. Sitta hapo tarehe 5 Agosti 2014 alitahadharisha kuhusu baadhi ya midahalo hiyo inayoendeshwa ikiwa na mapungufu makubwa. Wanapangwa washiriki wenye mawazo na malengo ya upande mmoja na kutumia fursa hiyo kushambulia kwa lugha chafu makundi yenye mawazo tofauti ambayo kimsingi yalitakiwa yashirikishwe kwenye midahalo hiyo. Tumeshuhudia upotoshwaji mkubwa kuhusu kauli ya Mwenyekiti. Hali hii inadhihirisha jinsi maadili ya upashanaji habari yanavyotumiwa vibaya na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya makundi katika jamii.
Ifahamike wazi kuwa lengo la Mhe. Mwenyekiti lilikuwa ni kuwakumbusha wahusika na waandaji wa midahalo hii pamoja na Serikali kuwa utaratibu huu wa kualika kundi moja lenye mrengo mmoja na kuuita mkutano huo ni mdahalo si sahihi. Mdahalo kwa tafsiri yake, hauna budi kuwa na pande mbili au zaidi. Utaratibu wa uaandaji wa midahalo kote ulimwenguni msingi wake ni kutoa fursa kwa wasikilizaji/watazamaji kusikiliza pande zote zenye mawazo tofauti na kuwaachia wananchi kuchambua mawazo hayo na kuona yepi wayakubali au kuyakataa.
Inasikitisha pale ambapo baadhi ya watu wameamua kuitumia kauli ya Mwenyekiti, Mhe. Sitta kwa kupotosha umma na kujikita katika kuzua malumbano yasiyo na tija kwa Taifa hususan katika kipindi hiki ambacho wananchi wangependa kufuatilia mijadala kuhusu Katiba.
Baadhi ya vyombo vya habari, kwa makusudi vimeamua kubeba agenda tofauti na kuangukia katika mtego wa kuchochea uhasama. Matoleo yao wamekuwa na vichwa vya habari vilivyosomeka “Sitta Avaa Udikteta”Bunge lataka kina Warioba wadhibitiwe”, Sitta avunja nchi nk na hatimaye upotoshwaji wa aina hii kuenezwa katika mitandao ya kijamii ili kuuchafua mchakato wa Bunge Maalum kutunga Katiba na kumchafua Mwenyekiti.
 Ofisi ya Bunge Maalum inasisitiza na kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia maadili ya upashanaji habari kwa uadilifu, hususan katika kipindi hiki ambacho Nchi ipo katika mchakato ambao wananchi wangestahili kupata taarifa sahihi kuhusu utungaji wa Katiba. Bunge Maalum linakaribisha maoni ya wananchi yenye dhamira safi bila kuingiza chuki binafsi, uchochezi na upotoshaji habari wa makusudi.
Bunge Maalum linatoa rai kwa wote kwamba liachwe litimize wajibu wake.
      IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU WA BUNGE MAALUM
        7 Agosti, 2014

NAPE AZUNGUMZIA MIDAHALO INAYOENDELEA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na ambapo alisema kitendo cha Tume ya Katiba kukishambulia na kukisakama Chama Cha Mapinduzi haikuwa sawa na hakitovumilika, aliendelea kusema kuwa utaratibu huu wa baadhi ya wajumbe wa tume kumkejeli Mwenyekiti wa CCM Taifa hauvumiliki na haukubaliki hata kidogo.

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKIWA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE LA KATIBA

PG4A9093 PG4A9087Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Kamati mbalimbali za Bnge  Maalum la katiba kwenye viwanja  vya hoteli ya St. Gaspar mjini Dodoma Agosti 7, 2014   ambako  vikao vya kamati nne vinafanyika.   Kutoka kushoto ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utaala Bora, Capt George Mkuchika,  Faida Bakari na Dr. Ave Maria Semakafu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA PETER MUTHARIKA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

m2

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  aliyemtembelea kumjulia hali kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina  ya nchi hizo mbili.PICHA NA IKULU

m3

Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Mama Salma Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

m4

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe   kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao  walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

m5

Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  akiomngea na  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe   kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani,  alipomtembela kumjulia hali Rais Kikwete. Viongozi hao  walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

m6

Mke wa rais Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa furaha na mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

m7

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika,  wakiongea kwa furaha walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya  nchi hizo mbili.

m8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  na wake zao, Mama Salma Kikwete na Mama Getrude Mutharika,  wakiongea kwa furaha walipokutana  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani. Rais Kikwete na Rais Mutharika, ambao   walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya  nchi hizo mbili.

MO awashitaki CCM Singida kwa Kinana

kapambala

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Naomi Kapambala aaizungumza na waanndishi wa habari juu ya ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Na Hillary Shoo, Singida

Mbunge wa Jimbo la Singida mjini (CCM), Mohammed Dewji ameulalamikia uongozi wa Chama chake Mkoa wa Singida kwa kitendo cha kuchelewesha mchakato wa kumalizia ujenzi wa Uwanja wa michezo Namfua ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Kuchelewa huko kuanza kwa mchakato wa ukarabati na uwekaji wa nyasi za bandia kwenye uwanja huo imeelezwa ni kutokana na urasimu na maslahi binafsi miongozi mwa viongozi wa CCM Mkoa wa Singida.

Katika barua yake ya Julai 31 mwaka huu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Dewji amedai kuwa kwa kiasi kikubwa ameweza kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa vipindi vyote viwili pamoja na ahadi zake binafsi, isipokuwa ahadi ya kumalizia ujenzi wa michezo Namfua.

Katika barua hiyo, ambayo pia ameinakili kwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Baraza la wadhamini CCM Taifa, Katibu wa Uchumi na Fedha na Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Dewji amedai kuwa kila alipotaka kufanya hivyo alipata vikwazo kutoka kwa viongozi wa CCM mkoa wa Singida.

sehemu ya uwanja

Katikati ya kiwanja chenyewe.

Amesema kuwa matayarisho yote muhimu kuhusiana na ujenzi huo yapo tayari, ikiwa ni pamoja na kuwepo dola za kimarekani 880,000 (sawa na sh bilioni 1.46) ambazo kwa kushirikiana na Rais Kikwete aliweza kuzipata kutoka Makampuni ya Airtel Tanzania na Mohammed Ent (T) Ltd.

Dewji amesema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 yeye pamoja na Raisi Jakaya Kikwete walitoa ahadi ya kukarabati na kuweka nyasi za bandia kwenye uwanja huo unaomilikiwa na chama cha mapinduzi CCM.

uwanja

Hili ni jukwaa kuu la uwanja wa Namfua unaomilikiwa na CCM Mkoa wa Singida.

“Baada ya uchaguzi sote wawili tulishinda na sasa tunatumikia wananchi, na kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa vipindi vyote viwili, pamoja na ahadi zetu binafsi, lakini ahadi tuliyotoa ya ukarabati wa uwanja mpaka sasa hatujafanikiwa kuitekeleza. Alisem MO na kuongeza

Dewji amesema anasikitishwa na uongozi wa CCM Mkoa wa Singida bila sababu za msingi wanachelewesha kuanza kwa mchakato wa ukarabati wa uwanja huo.

Aidha amesema kuna vikao vingi viimefanyika na makampuni hayo bila mafanikio na hivyo anaomba CCM Makao makuu kuingilia kati ili kama kuna jambo linasababisha kusuasua kwa mchakato huo liweze kupatiwa ifumbuzi na ukarabati ufanyike haraka iwezekanavyo.

wakicheza

Vijana wakicheza mpira uwanjani humo.

Amesema suala la uchakavu wa uwanja wa Namfua imekuwa ni kero kubwa inayowakabili wananchi wa jimbo la singida mjini kwa sasa na hivyo kuwanyima vijana fursa za kutumia uwanja huo ili kupata ajira na kukuza vipaji kwa vijana.

Kutokana na ukweli kwamba muda wa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015 unayoyoma, Dewji maarufu kwa jina la “MO” amemwomba Katibu Mkuu wa CCM kuingilia kati urasimu huo usio wa lazima ili ujenzi uweze kufanyika mapema.

Akizungumzia madai hayo ya Mbunge Dewji, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Naomi Kapambala alikiri kupata nakala ya barua hiyo na kusema kuwa wamefanya matayarisho yote muhimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia Airtel makao makuu juu ya suala hilo.

Aidha Kapambala amesema kuwa kamati ya siasa imemaliza kazi na kupeleka baraza la wadhamini, na kinachosubiriwa na baraza kukaa ili kutoka majibu.

“Mi namshangaa ni kwa nini yeye mwenyewe Dewji hajafika hapa ofisini na kupata ufafanuzi juu ya hili matokeo yake analeta nakala ya barua kwetu, akamwulize katibu Mkuu ambaye amemwandikia hii barua.” Alisema Kapambala

Hata wakati katibu mkuu alipokuja hapa tulimweleza juu ya hilo , yeye kama anaonaje ni vyema akafika ofisini ili kujua inachoendelea.

jukwaa

Sehemu ya jukwaa la uwanja wa Namfua linalotumiwa na washabiki likiwa linaonekana kuchakaa.

Aidha Kapambala amesema Katibu mkuu msaidizi yuko jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamemwagiza kupitia baraza la wadhamini wa CCM ili kujua hatma ya suala hilo.

Pia Kapambala amesema pia ofisi yake imekwishatoa notisi kwa wafanyabiashara mbalimbali kuondoka kwenye eneo la uwanja ili kupisha ukarabati huo.

Mwenyekiti wa SIREFA Baltazari Kimario alisema anasikitishwa kuona maendeleo ya uwanja huo bado haujakamilika na hivyo kuathiri maendeleo ya soka katika mkoa wa singida.

Aidha wadau mbalimbali nao wametoa masikitiko yao kwa uongozi wa CCM Mkoa wa singida kuchelewesha mchakato huo kwa maslahi binafsi, huku Mbunge akiwa tayari kushughulikia kero hiyo.

Uwanja huo hivi sasa umebaki kuwa kama eneo maarufu la vijana kuvuta bangi na wengine kujisaidia hovyo kwenye vyoo na hivyo kutapakaa kwa vinyesi kila mahali ndani ya uwanja huo.

Ujenzi wa Uwanja wa Namfua,ambao ulikuwa ukienda sambamba na Jengo la CCM mkoa, ulisimama miaka ya 1990 na tangu wakati huo uwanja huo umebakia gofu na kugeuka maficho ya wahalifu mbalimbali na eneo la choo cha jumuiya.

Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Singida wakipiga picha jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.

bangi

Vijana hawa walikutwa wakivuta bangi kwenye majukwaa ya uwanja wa Namfua.

jengo la ccm

Hapa ndio makao makuu ya CCM Mkoa wa Singida.(Picha zote na Hillary Shoo).

RAIS KIKWETE AJIUNGA NA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WA AFRIKA NA MAREKANI JIJINI WASHINGTON DC LEO

w1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Ikulu ya Marekani (White House) jijini Washington DC kwa dhifa ya Kitaifa waliyoandaliwa viongozi wa Afrika na mwenyeji wao Rais Barak Obama Julai 5, 2014

w2

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Afrika katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani  ambao umefunguliwa na Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC  leo Julai 6, 2014

w3

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wa Afrika katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Marekani  ambao umefunguliwa na Rais Barak Obama katika ukumbi wa State Department jijini Washington DC  leo Julai 6, 2014

w4

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Bernald Membe akiongea na baadhi ya viongozikatika mkutano huo.

w5 w6 w8

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry anaelekeza namna ya kutumia kipaza sauti baada ya Rais Obama kufungua mkutano huo, wakati  mwenyekiti wa Umoja wa Afrika  Rais  Mohamed Ould Abdel Aziz alipoongea kwa niaba ya Viongozi wa Afrika

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI KWA NCHI ZA AFRIKA NA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA, JIJINI ARUSHA.

1

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa  Chuo cha Nelson Mandela cha jijini Arusha wakati alipowasili kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR

2

Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha Nelson Mandela, Bernard Mussa, aliyetafiti kuhusu kuongeza joto katika Majiko kwa kutumia mwanga wa jua, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR

3

Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa mradi wa Masai Stove’s & Solar, Kisioki Moitiko aliyetafiti kuhusu mzunguko wau meme wa Jua kutumika katika nyumba za kabila la kimasai (Maboma) wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR

4

Makamu wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Hassna Founoune, kutoka Taasisi ya Tafiti ya Kilimo ya Senegal, wakati Dkt. Bilal alipofika chuoni hapo kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la siku tatu lenye lengo la kujenga nguvu ya pamoja katika ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR.

5.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR

6

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo katika Screen na Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela, Prof. Bulton Mwamila, wakati wakiangalia mjadala uliokuwa ukiendelea kupitia ‘Video Conference’ kati ya Marekani na Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa Tafiti za Kisayansi kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la sahara. Picha na OMR

7

Makamu wa Rais Dkt. Bilal katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi.

………………………………………………………………………………..

Kongamano hilo la siku tatu limefanyika katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Jijini Arusha jana Agosti 5, 2014, na kushirikisha mabingwa mbalimbali wa tafiti ndani ya Afrika na nchi za ukanda wa Jangwa la Sahara. 

Kongamano hilo ambalo limedhaminiwa na Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) linalenga kukuza tafiti za kisayansi na kutanua maendeleo ya tafiti hizo ili yasaidie wananchi wa nchi za ukanda huu hasa vijana ambao wanaelezwa kuwa na idadi kubwa kulinganisha na wazee na akina mama.

Katika Hotuba ya mgeni rasmi Makamu wa rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alisema kuwa, dhana ya umuhimu katika uwekezaji na utanuaji wa sayansi katika Afrika, inahitaji kutazama kundi la vijana na kulihamasisha kushiriki katika masomo ya sayansi ili kuharakisha maendeleo kwa Bara la Afrika.

Bunge Maalum la Katiba lapitisha Azimio la Mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni.

sp
Na Magreth Kinabo
Bunge  Maalum la Katiba limepitisha azimio la mapendekezo marekebisho ya baadhi ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ili kuwezesha ili kuwezesha kijadili  Rasimu ya Katiba kwa muda  siku 60 za nyongeza  na tatu zilizobakia.
Marekebisho hayo yamepitishwa  kufuatia  Mwenyekiti wa   Kanuni na Haki za Bunge Maalum  la Katiba, Mhe. Pandu Ameir Kificho  kuwasilisha  mapendekezo ya kanuni hizo mapema leo asubuhi  katika  Bunge hilo mjini Dodoma mara baada ya kuanza kikao cha 30.
Azimio hilo,limepitishwa baada ya baadhi ya wajumbe kuchangia hoja hiyo na kuungwa mkono, ambapo uamuzi huo ulitangaza na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta.
 Mhe . Sitta alisema Bunge hilo ,litaanza kujadili rasimu ya Katiba Mpya katika kamati 12 kuanzia kesho tarehe 6 Agosti, mwaka huu kwa muda wa siku 15  yaani hadi  Agosti 27, mwaka huu.
“ Hivi sasa watumishi wa Bunge  na Sekretarieti  wanaweka nyezo zote za kupitia , ambapo pia Katibu wa Bunge Maalum la Katiba yupo nao anashughulikia suala hili pamoja na kamati ndogo ili kuwezesha kazi hii kufanyika bila buguza,” alisema Mhe. Sitta.
Aliongeza kwamba baada ya hapo kutakuwa na siku tatu  kwa kamati kukamilisha Rasimu zao za Katiba.
“ Kamati zinatakiwa kutumia sekretarieti ndogo kuandika sura wasisubiri hadi Agosti 28,mwaka huu. Tumeongeza Idadi ya wataalamu katika kila sekretarieti ndogo,” alisisitiza.
 Aidha Mhe. Sitta alisema kutokana na marekebisho ya Kanuni  ya 32 kifungu cha 2  kinachosema kamati kubadilisha sura za rasimu  na sura, hivyo zinatakiwa  kutumia muda wa siku saba kupendekeza sura mpya kuanzia Agosti  6,mwaka huu hadi Agosti 13,mwaka huu.
 Akizungumzia kuhusu maudhurio ya wajumbe wa Bunge hilo, alisema watakiwa kutia saini kwenye maudhurio hayo na hakuna kusainiana kila mtu atatia saini mwenyewe.
Mhe .Sitta akifafanua kuhusu utaratibu wa kutoa taarifa za kamati kwa vyombo vya habari alisema utatolewa.
 Alisema Bunge hilo litarejea Septemba 2, mwaka huu baada ya kukamilisha kazi za kamati.
Bunge hilo limeanza vikao vyake kwa mara nyingine  leo, baada ya kuairishwa Aprili 25, mwaka huu.

TSNPmyatoa tamko kuhusu mwenendo wa katiba

MTANDAO wa wanafunzi nchini (TSNP) Umetoa tamko dhidi ya mwenendo wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa wanafunzi Bwana Alphonce Lusako ametoa tamko hilo katika mkutano ulioudhuriwa na  waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Lusako ametoa ombi kwa vyama vyote vya siasa kurudi bungeni na kufanya maridhiano ili tuweze kupata katiba mpya ambayo itasaidia kuokoa mabilioni ya fedha za watanzania ambazo zimekwisha tumika katika mchakato wa kutafuta katiba mpya.
“Tunawaomba CCM,UKAWA,TANZANIA ONE na wajumbe wa Bunge Maaalum la Katiba kujua kuwa kushindwa kwa mchakato huu siyo kushindwa kwa  kwa chama chochote ila ni kushindwa kwa Watanzania,”alisema Lusako.
Viongozi wa mtandao wa wanafunzi nchini, umewaomba UKAWA, CCM na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wafikie muafaka na watambue kuwa sheria kuu ya wao ndani ya bunge ni kuboresha Katiba ya wananchi na siyo kupindua maamuzi ya wananchi.
Wajumbe  wa Bunge Maalum la Katiba  wanatakiwa wajue kuwa hawapo kwa ajili ya kutafuta na kutambua mshindi na mshindwa, bali upo kwa ajili ya ushindi wa watanzania ambao pesa zao nyingi zimetumika.
Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa, mchakato haupo kwa ajili ya kutambua nani anamsimamo huu na msimamo ule,bali upo kwa ajili ya kutambua msimamo wa watanzania juu ya namna gani taifa lao litaongozwa na katiba iliyotokana na mawazo yao.
Mtandao wa wanafunzi nchini uliitisha kongamano rasmi la wanafunzi wa Vyuo Vikuu na sekondari kwa ajili ya kujadili mchakato mzima wa kupata Katiba mpya ndani ya Taifa letu ambao uliwapa wanafunzi fursa ya kupaza sauti zao juu ya mchakato mzima wa katiba.

 

HOTUBA YA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA MHE. SAMUEL SITTA KATIKA UFUNGUZI WA AWAMU YA PILI YA BUNGE HILO, DODOMA TAREHE 5 AGOSTI 2014  

Karibuni tena Dodoma Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la kutunga Katiba ya nchi yetu. Sote tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu wetu kwa kuendelea kutupa uhai na afya hadi leo kutuwezesha kuwepo ndani ya ukumbi huu. Tupo humu ili tuitekeleze kazi waliyotukabidhi Watanzania wenzetu milioni arobaini na sita (46) ya kuwapatia Katiba mpya. Dhamana hii ni nzito na haistahili kufanyiwa ajizi.

Tunaendelea na shughuli zetu za Bunge Maalum kwa kuzingatia Kanuni ya 30 (1) inayosema

Akidi kwa kila kikao cha Bunge Maalum isipokuwa wakati wa kupitisha uamuzi wa Bunge Maalum itakuwa ni nusu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum“.

Nimetaarifiwa na Katibu kwamba wajumbe waliokuja Dodoma kuhudhuria ni zaidi ya robo tatu ya Wajumbe wote wa Bunge Maalum. Nawashukuruni nyote kwa kuja hapa Dodoma ili kutimiza wajibu wenu.

Kwa niaba yenu, nawashukuru Watanzania wenzetu wote ambao kwa mamilioni wamedhihirisha utashi mwema wa kisiasa kwa kuunga mkono hatua ya Bunge Maalum kuendelea na kazi zake hadi tuipate Katiba inayopendekezwa ambayo wataipigia kura ya maoni. Kipekee na kwa niaba yenu, nawashukuru kwa dhati viongozi wetu wa dini wa madhehebu yote wanaloliombea Taifa hili mafanikio Bunge Maalum, wakitanguliza utaifa pamoja na amani ya nchi na umoja ndani ya nchi na siyo ubinafsi na maslahi ya makundi.

 Kwa leo sikupenda sana kuzungumzia hoja mbali mbali zinazotawala magumzo ya mchakato wa Katiba mpya hapa nchini, magumzo yanayoendeshwa na makundi maalum kwa jazba na hata matusi. Hata hivyo nalazimika kutoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu upotoshaji mkubwa unaoendeshwa na baadhi ya watu kuhusu Bunge Maalum. Nikiwa Mwenyekiti wenu ninao wajibu wa kuwafafanulia wananchi kuhusu uhalali wa shughuli za Bunge Maalum linaloendelea na utaratibu wa shughuli zetu.

Ni Rasimu ya Tume au la

Wapo wanaodai kuwa eti hapa Bungeni hatujadili Rasimu ya Tume. Tuhuma hii haina ukweli hata kidogo. Msingi wa majadiliano yote tangu tumeanza ni Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Katiba. Utaratibu ni kwamba pale ambapo wajumbe wanaona panafaa kurekebishwa wanafanya hivyo. Maana ya rasimu ni andiko ambalo halijajitosheleza bila kupata ithibati ya taasisi ya juu zaidi. Anayekabidhiwa rasimu anayo haki na mamlaka ya kuirekebisha. Vinginevyo kujadili rasimu hakuna sababu. Itakuwa ni jambo la ajabu na lisilo na mantiki yoyote kuwa taasisi iliyopewa mamlaka ya kujadili Rasimu ikishaijadili iiache ibaki kama ilivyokuwa wakati ilipowasilishwa!

 Je suala ni muundo wa Muungano tu?

Maudhui ya Rasimu yanajumuisha baadhi ya masuala muhimu yafuatayo:

-      Kuimarisha Muungano wetu kwa kuleta uwiano     bora zaidi wa mamlaka ya Zanzibar na Tanzania      Bara ndani ya Muungano

-      Kuimarisha haki za binadamu ili kuwawezesha      raia wa kawaida kufaidi uhuru wa demokrasia     bila ubabe na dhuluma

-      Kuzuia wachache kufuja rasilimali za taifa bila       kujali maslahi ya wengi na ya vizazi vijavyo.

-      Kujenga uwiano sahihi na wenye haki baina ya      wanawake na wanaume katika nafasi za uongozi.

-      Kubainisha hatua zenye kuleta matumaini mapya ya maendeleo kwa makundi maalum ya vijana     wakulima wadogo, wafugaji, wafanyakazi wa ngazi   za kawaida, walemavu, wafanya biashara wadogo   na wajasiriamali wengine.

-      Kuweka msingi imara wa kutungwa kwa sheria      kakamavu za kuzuia ukandamizaji wa raia,        unyonyaji, wizi wa mali ya umma, rushwa,    hujuma dhidi ya uchumi na kuzuia mapato        haramu na fedha chafu.

-      Kutambua haki za ardhi kwa wakulima, wafugaji    na wajasiriamali wengine ili kupunguza migongano na migogoro.

-      Kuweka Misingi ya utawala bora inayozingatia        uadilifu, sifa stahiki na ufanisi.

-      Kuwezesha kutungwa kwa sheria bora zaidi     zitakazosimamia chaguzi zilizo za haki na huru    zaidi pamoja na kuwepo Tume za Uchaguzi       zilizoboreshwa.

Zaidi ya hivyo, yapo mapungufu katika Rasimu iliyopo kwa kuachwa masuala ya kuwezesha Serikali za mitaa; kutoa maelekezo kuhusu masuala ya matumizi ya ardhi na rasilimali nyingine za Taifa. Nini kinatuzuia kuiboresha Rasimu kwa kuyaongeza mambo haya ndani ya Katiba kwa faida ya Taifa? Continue reading →

PRESIDENT KIKWETE ATTENDS CIVIL SOCIETY TOWN HALL MEETING ON OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP

b1

President Jakaya Mrisho Kikwete with the US Secretary of State John Kerry exchange views before the start of a Civil Society Town Hall Meeting on Open Government Partnership (OGP) at the National Academy for Sciences in Washington DC. President Kikwete and President John Dramani Mahama of Ghana served as panelists during the session which was moderated by VOA’s Straight Talk Afrika  presenter  Shaka Ssali

b2

  President Jakaya Mrisho Kikwete applauds as the US Secretary of State John Kerry takes a sip of water after addressing  a Civil Society Town Hall Meeting on Open Government Partnership (OGP) at the National Academy for Sciences in Washington DC. President Kikwete and President John Dramani Mahama of Ghana served as panelists during the session which was moderated by VOA’s Straight Talk Afrika  presenter  Shaka Ssali.

b3

  President Jakaya Mrisho Kikwete applauds as the US Secretary of State John Kerry takes a sip of water after addressing  a Civil Society Town Hall Meeting on Open Government Partnership (OGP) at the National Academy for Sciences in Washington DC. President Kikwete and President John Dramani Mahama of Ghana served as panelists during the session which was moderated by VOA’s Straight Talk Afrika  presenter  Shaka Ssali.

b4

 US Secretary of State John Kerry takes a sip of water after addresses a Civil Society Town Hall Meeting on Open Government Partnership (OGP) at the National Academy for Sciences in Washington DC as  President Kikwete and President John Dramani Mahama of Ghana who served as panelists listen. The session was moderated by VOA’s Straight Talk Afrika  presenter  Shaka Ssali.

b5

 President Jakaya Mrisho Kikwete and President John Dramani Mahama of Ghana take part in a Civil Society Town Hall Meeting on Open Government Partnership (OGP) at the National Academy for Sciences in Washington DC as  President Kikwete and President John Dramani Mahama served as panelists during the  session was moderated by VOA’s Straight Talk Afrika  presenter  Shaka Ssali (right).
STATE HOUSE PHOTOS

BALOZI WA UJERUMANI NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE D’SALAAM

PIX 1 (5)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke alipokuwa akimfafanulia jambo wakati Balozi huyo na Naibu wake walipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

PIX 2 (3)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimfafanulia jambo Balozi wa Ujerumani nchini, Egon Kochanke wakati Balozi huyo na Naibu wake, John Reyels (kulia) walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

PIX 3 (3)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiagana na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, John Reyels wakati Naibu huyo na Balozi wake, Egon Kochanke (katikati) walipomaliza mazungumzo na Waziri Chikawe ofisini kwake Dar es Salaam baada ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi huo na Wizara yake. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Neno La Leo: Mkwamo Wa Katiba Na Msafara Wa Tembo..

1 (7)

Ndugu zangu,

Msafara wa tembo huwa na kawaida ya kutokurudi nyuma,ndio maana porini huzioni nyayo za tembo zenye kwenda mbele na kurudi nyuma.

Ni ukweli, kuwa tembo ndiye mnyama mkubwa porini, na ni mfalme wa pori. Lakini tembo hufika mahali akasumbuliwa na siafu kiasi cha kuweweseka na hata kutamani kulihama pori. Ni kwa kosa la tembo kukanyaga kichuguu cha siafu. Naam, siafu mia tano ni wengi kuliko tembo mmoja, pamoja na ukubwa wa tembo.

Na adili ya jambo hilo ni ukweli kuwa duniani hapa mkubwa anapaswa kumuheshimu mdogo, na mdogo pia kumuheshimu mkubwa.Hivyo, wanadamu tunapaswa kuheshimiana.

Kwenye hili la hofu ya mkwamo wa mchakato wa Katiba nayaona mapungufu mawili kwa pande zinazohusika; KUTOHESHIMIANA na KUTOAMINIANA.

Kwenye awamu ya kwanza ya Bunge Maalum la Katiba mawili hayo yalijidhihiri. Hakika UKAWA na CCM kwa pamoja wamebeba dhamana kubwa ya hatma ya nchi yetu. Kuna makosa yameshafanyika tangu kuanza kwa mchakato huu. Hatupaswi kama taifa kuwa kama tembo kwenye msafara wao, kwamba hawarudi nyuma.

Kabla ya kuendelea na mchakato huu wa Katiba, kama taifa, na kwa kupitia viongozi wakuu wa UKAWA na CCM. Viongozi hao, kwa namna yeyote ile, wana lazima ya kujiandalia au kuandaliwa mazingira ya kukaa meza moja kama Watanzania. Kuendelea kufanya vikao vya siri na kuyapitia mapungufu yaliyojitokeza kwenye Awamu ya kwanza, kisha watoke kwa pamoja na kwa kauli moja ya namna ya kwenda mbele.

Wakishindwa kukaa meza moja,basi,ni heri mchakato mzima ukahairishwa kusubiri wakati muafaka, kuliko kusonga mbele kwa staili ya msafara wa tembo, maana, huko njiani kutakuwa na vichuguu vingi vya siafu vitakavyokanyagwa, na tembo pamoja ukubwa wao, wataweweseka sana porini, na hata kusababisha pori lichafuke. Pori kukosa amani. Continue reading →

KONGAMANO LA MARIDHIANO YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUFANYIKA DODOMA.

peter20mziray20

 

Na  Magreth Kinabo- MAELEZO
2/08/2014
Baraza la Vyama vya Siasa nchini  limeamua mazungumzo  ya maridhiano  kati ya pande zinazokizana kuhusu kuendelea kwa  Bunge Maalum la  Katiba  kutokana na mvutano  ya kutaka serikali mbili au tatu  yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa.
Aidha baraza hilo,limeamua kufanyike kongamano Agosti 9 na 10 mwaka huu mjini Dodoma kwa  ajili  ya kuangalia maslahi mapana  ya taifa.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa baraza hilo, Peter  Kuga  Mziray, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo, na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa,akiwemo Msajili  wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kilichofanyika kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dares Salaam.
Alisema katika mkutano huo,  baraza hilo limepokea ripoti ya mkutano wa  Msajili wa Vyama Vya  Siasa nchini na baadhi viongozi wa vyama vya siasa, pia limepokea ripoti ya chama kimoja kimoja, ambavyo ni Chama cha Demokrasia  na Maendeleo ( CHADEMA), Chama  cha Wananchi (CUF)  Chama cha NCCR – MAGEUZI na Chama cha Mapinduzi (CCM).
 Aidha  Mziray  amesema  kwamba  katika mkutano huo, kuna mambo ambayo wamekubaliana na mengine hawakuafikiana.
 “Baraza limeamua mazungumzo ya mariadhiano yaendelee kupitia kamati zitakazoundwa ,ambazo zitakuwa na wajumbe wachache. Baraza linawashauri wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba warudi Bungeni  kwa kuwa ndio mahali pekee pa kutoa hoja na wala si sehemu nyingine,” alisema Mziray.
 Aliongeza kuwa anavipongeza vyama hivyo kwa kuonesha nia ya kuendelea kwa mazungumzo hayo na  wameonesha imani na baraza hilo, ambapo wametaka majadiliano  kupitia kamati yafanyike.
 Mwenyekiti huyo akizungumzia kuhusu kongamano hilo ,ambalo litamhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya  Kikwete,ambaye atakayelifungua, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Mohammed Gharib Bilal, Marais wastaafu,wabunge,majaji, maspika, viongozi wote waliowahi kushika madaraka, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini zote.
“Lengo la kongamano hili ni kujadili hali ya kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya. Kongamano hili ndio njia ya kutafuta maridhiano  katika suala hili. Tunategemea busara za viongozi hawa zitatubadilkisha  na kutuweka pamoja  kwa maslahi ya taifa na kuachana na mambo ya kivyama,” alisisitiza.
Aliyataja mambo ambayo, wamekubaliana kuwa yasiwepo wakati wa kuendelea kwa Bunge hilo ni kutumia lugha za matusi na kejeli.
Katika  mazungumzo hayo, “Baraza limeona   si rahisi kufikia muafaka kwani kila upande  ulionesha kuwa Bunge hilo halina mamlaka ya kubadilisha Rasimu ya  Katiba Mpya, na mwingine unadai Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha na kuboresha rasimu hiyo kwa vile  suala hilo lipo kisheria kulingana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kifungu cha 25 na kanuni zinaruhusu,” alisema Mziray.
 
Kwa upande mwingine Mziray  alisema kuwa jambo lingine lilionesha ugumu ni mvutano uliopo wa kuhusu wa kuwepo kwa Serikali mbili au tatu kwa sababu ni  suala la kisera za vyama na sera haibadilishwi mpaka mkutano mkuu wa chama.
 
KWA MAWASIALIANO ZAIDI 
NAMBA YA MWENYEKITI WA BARAZA HILO NI O715665506.

 

CCM YASTUKIA USANII WA UKAWA

     Chama Cha Mapinduzi kimewastukia Ukawa na kusema wanachofanya
ni Usanii usiokuwa na tija mbele ya mambo ya msingi kwa Taifa la Tanzania,
akizungumza na mwaandishi wa habari hizi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM
Nape Nnauye alisema hoja zote zinazotolewa na UKAWA zina majibu kwenye Sheria na
Kanuni zinazoendesha Bunge la Katiba ,CCM pia imewashukia  UKAWA kwa kuwatukana na kuwadhalilisha
viongozi wa dini ambao wamekuwa wakisisitiza UKAWA kurudi Bungeni.
     CCM yawaomba wabunge wa bunge la Katiba wanaotaka Katiba
mpya waendelee na bunge  litakapoitishwa
tarehe 5/8/2014.
Kwa taarifa za ndani ya kikao hicho ,kikao kimeisha kwa
kukubalina kutokubaliana ,pande mbili hizi zimekutana zaidi ya mara nne pamoja
na kikao cha leo kilichoanza tangia asubuhi saa nne mpaka jioni lakini hakuna
hata pande mmoja uliokubalina na mwenzake.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani Msajili wa vyama vya
Siasa  nchini anatarajiwa kuzungumza na
waandishi wa habari kesho jijini Dar es Salaam.

UKAWA wakutana na waandhishi wa habari jijini Dar

Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Profesa Ibrahim Lipumba (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa Tamko kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na wa pili kulia ni Mwenyeti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa.
Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono kuashiria umoja mara baada ya kuongea na wandishi wa habari kutoa Tamko la Ukawa kuhusu Wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi,Mosena Nyambabe,Mwenyekiti wa Chadema,Mh.Freeman Mbowe ,Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahim Lipumba,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Mh. James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt. Wilbrod Slaa wakiwa nje ya makao makuu ya cuf.