All posts in SIASA

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia)
akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt Jojn Pombe Magufuli(kushoto)(leo) wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu
cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
unaoendelea mjini Dodoma.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Aggrey Mwanri  akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu  (leo) mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji
wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu
Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo  (leo) mjini Dodoma
katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira  akiwasilisha Bungeni  
(leo) mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na
mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim  Lipumba  akisikiliza
kwa makini taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na
mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13
iliwasilishwa jana (leo)  Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais   (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, MizengoPinda akizungumza na Mbunge wa Sengerema., William
Ngeleja kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 14, 2012.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza swali kutoka kwa  kiongozi wa
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14,
2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, wa zamzni , Edward lowassa  akisalimiana na Mbunge wa Vunjo.
Augustine Mrema kwenye viwanja vya  Bunge mjini Dodoma  Juni 14,2012.
Katikati ni Mbunge wa Simanjiro.  ChristopherOle Sendeka. (Picha na
Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo cha Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa cha Hombolo, Dodoma kwenye viwanja vya Bunge
Mjini Dodoma, Juni 14, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Kikwete aongoza kikao cha baraza la Mawaziri Dodoma

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Baraza la
Mawaziri mjini Dodoma leo mchana(picha na Fredddy Maro)

NAPE AANZA ZIARA MKONI IRINGA,KUFANYA MKUTANO MKUBWA LEO MJINI MAFINGA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye
ameanza ziara ya kikaz i ya siku nne mkoani Iringa, ambapo atakagua uhai
wa Chama na kukiimarisha katika wilaya mbali mbali mkoani humo.
Kufuatia ziara hiyo Nape leo amewasili mjini Mafinga katika wilaya ya
Mufindi kuanza ziara hiyo, Katika picha juu .Katibu Mwenezi wilaya ya Mafinga  Daudi Yassin akimtambulisha Nape kwa wenyeji


(Picha zote na Bashir Nkoromo wa BOFYA HAPA

Wanachama wa wapenzi wa CCM wakimsubiri Nape kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi, mjini Mafinga
Nape akivishwa skafu na Green Guard wa CCM, baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi iliyopo mjini Mafinga
Nape akisalimia wanafunzi wa Chuo cha Uhazili Mafinga, baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya Mafinga wilayani Mufindi

BAJETI YA SMZ YAWASILISHWA LEO MJINI ZANIZBAR

 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais anaeshughulikia Fedha na Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Zanzibar,Omar Yussuf Mzee akionesha mkoba wenye nyaraka za  Bajeti ya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 leo Nje
ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi(Picha na Yussuf Simai,MAELEZO
Zanzibar)
 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais anaeshughulikia Fedha na Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Zanzibar,Omar Yussuf Mzee akisoma bajeti ya SMZ
 
leokatika Baraza la Wawakilishi.(Picha na Yussuf Simai,MAELEZO
Zanzibar)
Baadhi ya wasikilizaji waliofika kusikiliza bajeti ya SMZ ya
mwaka 2012/2013 leo (Picha na Yussuf Simai,MAELEZO Zanzibar)

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho Ikulu.A pokea pia Salamu maalum Kutoka Sudan ya Kusini na DRC

Balozi wa Ukraine Volodymyr Butiaha akiwasilisha hati za Utambulisho
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za mabalozi
watano wanaoziwakilisha nchi zao hapa pamoja na kupokea wajumbe wawili maalum
waliotumwa na marais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mabalozi waliowasilisha hati za utambulisho
ikulu ni pamoja na Mhe.Domingo Lucenario wa Phillippines, Mhe.Volodymyr Butiaha
wa Ukraine,Mhe.Beyene Russom Habtai wa Eritrea, Mhe.Kingsley Saka Karimu wa
Ghana pamoja na Mhe.Gil Haskel wa Israel.
Wajumbe walioleta salamu maalum kutoka kwa marais wao ni
pamoja namhe.Raymond Tschibanda ambaye ni Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa DRC
na Mhe.Nhial Deng Nhial ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ya
Kusini. (picha zote na Freddy Maro)
 
Balozi wa Eritrea Mhe.Beyene Russom Habtai akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Ghana Mhe.Kingsley Saka Karimu akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Israel mhe. Gil Haskel akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Ghana Mhe.Kingsley Saka Karimu akiwasilisha hati za utambulisho
Mhe.Raymond Tschibanda akiwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Joseph kabila
Mhe.Nhial Deng Nhial akiwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Salva Kiir.

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

Naibu Spika wa bunge la Tanzania Job
Ndugai(kushoto) akiwa na Mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu
Nchemba(kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya
kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa
Bunge kumalizika.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Emmanuel
Nchimbi(kushoto) , Naibu Waziri wa Habari, vijana ,Utamaduni na Michezo
Amos Makalla(katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Anna Abdallah
wakibadishana mawazo (leo) mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha
maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge
kumalizika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali
na pia Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo(kulia) ,Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  January
Makamba(katikati) na Andrew Chenge(kushoto) wakibadishana mawazo (leo) mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya
kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.
Mwenyekiti wa Simba Sport Club ambaye pia
ni Mbunge wa Tabora mjini Ismail Aden Rage(kushoto) akibadilishana
mawazo na Naibu Waziri wa Maji Dkt Binilith Satano Mahenge (kulia) leo
mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.
Waziri wa Nchi ofis ya Rais (Utawala Bora)
George Mkuchika(kulia) akijadiliana jambo  mjini Dodoma na Mbunge
wa Jimbo la Tanga mh. Omar Nundu (kushoto) mara baada ya kipindi cha
maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge
kumalizika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI) Hawa Ghasia (kushoto)
wakibadishana mawazo (leo) mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kazi na
Ajira Dkt. Milton Makongoro Mahanga(kulia)  mara baada ya kipindi cha maswali na majibu ya kikao cha pili cha Mkutano wa nane wa Bunge kumalizika.
Mwanasheria mkuu wa Serikali(AG) Jaji Frederick Mwita Werema(kulia) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Kigoma Kusini  David Kafulila(kushoto) wakibadilishana mawazo  mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu kumalizika.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo pinda  akizungumza na  Mbunge wa Viti Maalum
 Pauline Gekul na watoto wake Irene (kushoto)  na Inocentia kwenye
viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 12,2012. (Picha na Ofisi  ya Waziri
Mkuu) (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge Anne Makinda akimkabidhi kanuni za Bunge Mbunge wa
Kuteluliwa James Mbatia baada ya kumwapisha, Bungeni Mjini Dodoma, Juni
12,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Kuteuliwa Janet Zebedayo Mbene akiapa, Bungeni Mjini Dodoma  Juni 12, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge waKuteuliwa Saada  Mkuya  Salum akiapa Bungeni Mjini Dodoma Juni 12, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Mbunge wa Namtumbo Vita
Kawawa (kushoto) na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu  Nchemba kwenye
viwanja vya Bunge Mjini  Dodoma  Juni 12, 2012. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Mbunge wa Kuteuliwa, Sospeter  Mwijarubi Muhongo akiapa, Bungeni Mjini Dodoma, Juni 12, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Kikwete amwapisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Mpapi Bendeyeko na apokea vitabu vya hadhithi za Kikwele

 Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Ruvuma Bwana Hassan
Mpapi Bendeyeko akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu
jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili TATAKI
Dkt.Aldin Mutembei akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu cha kwanza
cha fasihi simulizi ya jamii ya Wakwere ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia
ni Mkuu wa Idara ya historia katika chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa
Kapepwa Tambila. Dkt.Mutembei ambaye pia ni mchapishaji na msimamizi wa tafiti
za Tamaduni lugha na fasihi za makabila ya Tanzania alikabidhi pia kamusi Asisi
ya Kiingereza-Kiswahili na Kiarabu(picha na Freddy Maro).

Spika wa Bunge akutana na Balozi wa marekani na Waziri wa Maji Ofisini kwake leo

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mazungumzo na balozi wa
Marekani hapa nchini Mhe. Alfonso Lenhardt alipo mtembelea Ofisini kwake
Dodoma leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikilza kwa Makini Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhe. Prof. Jumanne Maghembe alipo mtembelea Ofisini kwake
Dodoma leo
Naibu Spika wa Bunge akiwa katika amzungumzo na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Prof. Jumanne Maghembe alipo mtembelea Ofisini kwake
Dodoma leo.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete ashiriki kumuaga Muasisi wa CHADEMA Bob Makani katika viwanja vya Karimjee leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal
pamoja na Mama Salma Kikwete leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na
viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa
waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika
nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(picha zote na Freddy
Maro)
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani
Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob
Makani
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya
maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee
leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA
Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi
wa Chama hicho Bob Makani

Rais Kikwete awaapisha mabalozi Kumi Ikulu jijini Dar es Salaam leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo
amewaapisha mabalozi wapya kumi ambao wataongoza idara na kurugenzi mbalimbali
katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani Rais akiwa
katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha ikulu jijini Dar es
Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto walisimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha
Semu Somi,Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana,Balozi
Naimi Sweetie Hamza Aziz,Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari
Msechu.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji,Balozi
Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan
Muombwa Haji(picha na Freddy Maro)

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU BOB MAKANI

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wa Rais wa pili kutoka kushoto na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wa mwisho kushoto wakiongoza waombolezaji  kwenye viwanja vya Karimjee wakati Mwili wa muasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mzee Bob Makani ulipoagwa leo jijini Dar es salaam

(PICHA KWA HISANI YA MJENGWA BLOG)

Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiwa umewekwa eneo maalum tayari kwa kuaga mwili huo leo kwenye viwanja vya Karimjee.
Mwili wa Marehemu Bob Makani ukiteremshwa kwenyegari ili kuwekwa eneo hilo kwa ajili ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho.
Mwili ukiwekwa tayari kwa ajili ya waombolezaji kuuaga rasmi kabla ya kuzikwa huko Shinyanga.

Rais Kikwete na Mama Salma Wakagua mahindi Shambani kwao kijijini Msoga

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakikagua mahindi shambani kwao kijijini Msoga,Chalinze,wilayani Bagamoyo wakati wa mapumziko ya mwisho wa wiki(picha na Freddy Maro)

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSS:PROFESA GEORGE SAITOTI AFARIKI KATIKA AJALI YA HELIKOPTA NCHINI KENYA

 Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya Profesa George Saitoti amefariki dunia kwa ajali ya Helikopta iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Ngong Katika milima ya Magharibi mwa Nairobi nchini humo wakati akiwa katika safari ya kikazi akielekea Kisumu, Saitoti amefariki akiwa na Naibu Waziri wake Orwa Ojode.
Mbunge wa Kenya Najib Balala amethibitisha kutokea kwa kifo hicho katika mtandao wake wa Twitter, Serikali ya Kenya bado haijasema chochote kuhusu sababu za ajali hiyo iliyopoteza mawaziri hao pamoja na watu wengine wanne jumla yao wakiwa Sita, Profesa Saitoti alikuwa akitarajia kugombea urais katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika baadae mwaka huu

CCM WAZUNGUMZIA MIRADI YA MAENDELEA JANGWANI LEO

 Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli akihutubia katika
mkutano wa wachama wa CCM Jangwani leo jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mikakati ya chama kusikiliza
kero za wananchi pamoja na mfumuko wa bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea miradi mbalimbali inayoendelea nchini
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Waziri wa uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe akihutubia katika
mkutano wa wachama wa CCM jangwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mikakati ya chama  kusikiliza
kero za wananchi pamoja na mfumuko ya bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea wananchi miradi mbalimbali inayoendelea

 Katika picha kutoka kushoto ni mawaziri Prof Anna Tibaijuka, John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita.
 Abdulrahman Kinana (kulia) akipeana  mkono na waziri John Magufuli kushoto.

 Wanachama wa CCM wakichambua baadhi ya kadi ya vyama pinzani zilizorudishwa na wanachama wao kama zinavyoonekana katika picha
 Waziri wa nyumba na maendeleo na makazi Profesa Anna Tibaijuka akifafanua jambo katika mkutano huo
Viongozi wa CCM pamoja na mawaziri wakiimba katika mkutano huo uliofanyika Jangwani jijini Dar es salaam leo

MKUTANO WA CCM DAR, JANGWANI YATAPIKA

Maelefu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM unaofanyika
 jioni hii kwenye VIwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam. Mkutano
huo ni wa kuwapongeza viongozi wa mashina na matawi waliochaguliwa
katika uchaguzi wa CCM ulifanyika kwa ngazi hizo mkoani Dar es Salaam.
(Picha na Bashir Nkoromo).
Maelefu wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM unaofanyika
 jioni hii kwenye VIwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam. Mkutano
huo ni wa kuwapongeza viongozi wa mashina na matawi waliochaguliwa
katika uchaguzi wa CCM ulifanyika kwa ngazi hizo mkoani Dar es Salaam.
(Picha na Bashir Nkoromo).

IPI MUHIMU: ‘VUA GWANDA VAA GAMBA’ YA CHADEMA NA ‘CHANA GAMBA NA GWANDA VAA UZALENDO’ YA CCM

Mfuasi wa Chadema akiwa na fulanaz yenye ujumbe ‘VUA GWANDA VAA GWANDA’
na wa CCM akiwa na fulanaz yenye umumbe ‘CHANA GWANDA NA GAMBA, VAA
UZALENDO’, Je nani zaidi?

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE Amtembelea Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Naibu
Waziri wa mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE) Mhe.Khalid Ghaanim Al
Ghaith wakati yeye na ujumbe wake walipowasili kwa mazungumzo ikulu jijini Dar
es Salaam leo asubuhi.Mhe.Ghaith anashughulikia pia masuala ya uchumi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
mazungumzo na ujumbe kutoka Umoja wa Falme za kiarabu(UAE) unaongozwa na Naibu
Waziri wa mambo ya nje wa Falme hizo mhe.Khalid Ghaanim Al Ghait (wapili
kulia) wakati ujumbe huo ulipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na
Freddy Maro)

MKATABA WA KIDIPLOMASIA KATI YA TANZANIA NA UJERUMANI WASAINIWA

NA MWANDISHI WETU
SERIKALI ya
Tanzania na Ujerumani zimetia saini mkataba ambao utaruhusu wenzi na
wategemezi wa kufanya kazi kwenye nchi hizo.
Mkataba huo
umesainiwa jijini Dar es Salaam jana,  na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa John Haule, akishirikiana na
Balozi wa nchi hiyo Klaus Peter Brandes. 
Haule alisema kuwa, Tanzania ni ya pili kusaini mkataba kama huo, ya kwanza ilikuwa ni nchi ya Zambia.
Vile vile
alifafanua kwamba ingawa Tanzania si mara yake ya kwanza kusaini mkataba
na nchi nyingine lakini inaonesha ni jinsi gani inatambulika ndani na
nje ya nchi hususan katika shughuli za maendeleo.
Aidha,
aliitaja moja ya faida ya mkataba huo ni kuwasaidia watu hao kuendeleza
taaluma zao sanjari na kupanua wigo wa kipato baina ya mtu  mmoja pamoja
na familia.
“Kwa sasa
Tanzania imeshaingia mkataba na nchi ya Canada, Marekani, pamoja na
Ujerumani kuna haja ya kushirikiana, ukichukulia kwamba nchi yetu ni
moja ya nchi yenye amani na inatambulika kwa sifa hiyo, hivyo muungano
huu utatuwezesha kufanya kazi kwa uhuru bila kujali huko nchi za
ugeni”alibainisha Haule.
Naye Balozi
wa nchi hiyo Klaus Peter Brandes alisema mkataba huo umeonyesha
ushirikiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili, na utaendelea kuleta
mafanikio makubwa kwa siku za mbele.

DIWANI WA CHADEMA AWATAKA VIONGOZI WA MANISPAA YA KINONDONI KUACHA VITISHO

NA MWANDISHI WETU
DIWANI
wa Kata ya Saranga (Chadema),   amewataka baadhi ya viongozi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kuacha
vitisho na ubabe kwa kuwafukuza kazi baadhi ya wafanyakazi pindi
wanapodai haki zao za msingi.
Akizungumza
na Fullshangweblog  jijini leo, Efraim Kinyafu alisema kuna baadhi ya wafanyakazi
katika Manispaa hiyo, wamekuwa wakiishi maisha ya kubahatisha kutokana
na malipo madogo yasiolingana na kazi wanazofanya.
Kinyafu
alisema viongozi wanaotumia njia kama hizo, watambuwe kuwa huo ni
ukiukaji wa sheria za kazi na kuwa yuko tayari kutofautiana nao na na
kuahidi kusimamia haki ya kila mfanyakazi katika Manispaa hiyo.
 “Haipendezi
kuona mfanyakazi  anaishi kwa kutegemea posho kitendo ambacho kimekuwa
kikiwashangaza baadhi ya watumishi wengine, kwani huwezi kupata posho
bila kuwa na mshahara”alisma kinyafu.
Aidha,
anasikitishwa na vitendo wanavyofanyiwa baadhi ya madereva  wa Manispaa
hiyo kwa kulipwa shilingi 2000 kwa siku ambapo kwa mwezi anapokea
shilingi 72000 pesa ambayo haimsaidii kifamilia.
“Unajua
hii hali ni kero kubwa kwa wafanyakazi hao ambao hadi sasa wamekuwa
wakisikitika kwa kukosa mtetezi ambapo wamekuwa wakindelea kuheshimu
kazi zao kwa lengo la kujenga taifa”alisema Kinyafu.
Alisema
kutokana unyanyasaji huo ameamua kujitolea kuundikia barua inayoutaka
uongozi wa manispaa hiyo kufuatilia madai ya wafanyakazi wote
wanaokoseshwa haki zao kwa lengo la kuwarekebishia haki hizo bila
kutumia vitisho kwa wale wanaotoa sauti.  

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAWILI NA KAMISHNA WA MAHAKAMA LEO.

Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa
jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya
uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu
kanda ya Dar es salaam.
ais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifuarahia
Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa
(wa tatu kutoka kulia)  mara baada ya kumwapisha leo Ikulu
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya
Rufani Mussa Kipenka na Jaji  Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh.
Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria hafla
fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu jijini
Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam.

Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo
vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza majukumu
yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha
kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais  Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

Rais Dk. Shein akutana na Balozi wa Msumbiji na Sweden

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali
Mohamed Shein,akisalimiana  na  Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali

Mohamed Shein,akizungumza na  Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour

Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda

wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa  Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa  Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA CANADA

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo Juni 7, 2012 katika Ikulu ya Dar es salaam
amekutana na kuagana na Bw Robert J. Orr,  Balozi wa Canada nchini,  anayemaliza muda wake wa uwakilishi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Bw Robert J. Orr,  Balozi wa Canada nchini,  anayemaliza muda wake wa uwakilishi.

ZIARA YA NAPE NJOMBE NA MKUTANO WA MAKAMBAKO

.Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni jana, Juni,6, 2012 kwenye uwanja wa Polisi, mji wa Makambako, wilaya ya
Njombe mkoa mpya wa Njombe.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ,
akizindua tawi la CCM, Ubena Makambako, akiwa katika ziara ya
kuimarisha uhai wa chama mkoani Njombe.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 
akisakata muziki na kijana Kata ya Ilembula, kabla ya kuhutubia mkutano
wa hadhara kwenye Kata hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
akizungumza na wazee wa Kata ya Ilembula wilaya ya Wanging’ombea akiwa
katika ziara ya kikazi mkoani Njombe.
Vijana wakionyesha umahiri wa kucheza sarakasi walipotumbuiza wakati wa mkutano wa CCM kwenye uwanja wa Polisi Makambako.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipiga ngoma.

MGOMBEA AWAASA WANACHAMA WA KLABU YA YANGA KUCHANGA 5000 KILA SIKU

Mgombea wa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya yanga Bw, Ayubu Nyenzi
katikati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokutana wakati alipokutana nao na kuelezea nia yake ya kugombea kiti hicho
ambapo alisema kuwa anataka agombee ili awaase wanachama wa Yanga
kuchanga kufunga mkanda na kuchangia klabu hiyo shilingi 5000 kila siku kwa ajili ya kumaliza matatizo yaliyopo klabuni
hapo na sio kutegemea misaada kutoka kwa wafadhili. Alisema kuwa endapo
wanachama watatoa Sh, 5000 kila mmoja  zitapatikana kiasi cha sh,
milioni 70 kwa mwezi.


(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AAGANA NA BALOZI WA MSUMBIJI ANAYEMALIZA MDA WAKE

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini Balozi wa
Msumbiji hapa Nchini Mhe. Amour Zacarias Kupela, wakati alipofika Ofisini kwake
jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake
nchini.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akutana na viongozi wa Kampuni ya Kilimo ya YARA ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika
mazungumzo na viongozi wa kampuni ya kilimo ya YARA  ya nchini Norway inayoshughulika na
uzalishaji wa mbolea wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam
leo.Kampuni hiyo ina andaa mipango ya kuzalisha mbolea nchini.
(PICHA NA IKULU)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa kampuni ya Kilimo ya YARA ya nchini Norway wakati
alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

NAPE:ARDHI IKIMILIKIWA NA WATU BINAFSI WANYONGE WATATAABIKA

NA BASHIR NKOROMO, NJOMBE
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kusiistiza juu ya msimamo wake wa
ardhi kuendeleakumilikiwa na serikali kwa maslahi ya taifa zima.

Msimamo
huo ulielezwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Turbo mjini
Njombe.

Nape alisema, tofauti na mapendekezo ya baadhi ya vyama vya siasa
kwamba ardhi imilikiwe na wananchi, CCM inaona kwamba bado kuna ulazima
wa ardhi kuwa chini ya miliki ya Serikali, kwa sababu kuwafanya hivyo
kuna faida kubwa zaidi.

“Sisi Chama Cha Mapinduzi, baada ya kutafakari kwa kina, katika
rasimu yetu kuhusu katiba mpya ya Tanzania tumependekeza pamoja na mambo
mengine, kwamba ardhi iendelee kumilikiwa na serikali kwa sababu
tunaona kwamba utaratibu huu ndiyo unaifanya ardhi kuwa mali ya wanancho
wote”, alisema Nape.

Alisema, madhara ya ardhi kumilikiwa na watu binafsi katika nchi ni
jambo la hatari sana, kwa sababu inaweza kumilikiwa na mabepari wachache
hata wasiozidi wanne nchi nzima kama ilivyo katika baadhi ya nchi
jirani hatua inayowafanya raia kulazimika kuwapigia magoti mapepari
wanapohitaji hata eneo dogo tu kufanyia shughuli zao.

Nape aliwataka Watanzania kuunga mkono hoja ya CCM ya  kuendelea
kuifanya ardhi kuwa chini ya miliki ya watu binafsi na kuachana na ile
ya Chadema inayosisitiza kutaka ardhi imilikiwe na watu binafsi.

“Hawa
Chadema wanatetea umiliki wa ardhi kuwa chini ya watu binafsi kwa
sababu wana maslahi nalo, maana tunajua mwanzilishi wa chama chao ni
mmoja wa matajiri wanaomiliki ardhi kubwa sana hapa nchini, sasa
wanapendekeza hivyo ili mwanzilishi huyo wa chama chao asije akapokwa
eneo hilo baada ya katiba mpya kutoa maelekezo kwamba ardhi ni mali ya
umma kupitia umiliki wa serikali”, alisema.

Katika hatua nyingine, Nape amewataka watendaji wa mkoa mpya wa
Njombe wanaohusika na upimaji viwanja, kuhakikisha wanafanya kazi
hiyokwa kuzingatia haki ili kusitokee malalamiko kwa yeyote kunyimwa
eneo kwa hila yoyote.

Nape alisema, kupima vbiwanja kwa kuzingatia haki kutawezesha kila
mwananchi kupata eneo analohitaji kulingana na sheria, lakini
isipozingatiwa hivyo, wanyonge hawatapa ardhi kwa kuwa haki
isipozingatiwa ni matajiri tu ndio watakaopata maeneo tena makubwa sana.

“Mimi kama msemaji wa Chama Cha Mapinduzi kilichiunda serikali
iliyopo madarakani, nawaagiza viongozi wa mkoa huu mpya tangu wa
serikali na wa CCM ngazi zote, kuwa makini na hili kwa sababu ardhi ni
miongoni mwa mambo ambayo huzusha sana migogoro jambo ambalo hatutaki
kabisa litokee hapa”, alisema.

Akizungumzia uhai wa Chama Cha Mapinduzi, Nape alisema, CCM bado ni
imara kutokana nna misingi yake, na itanedelea kutawala tangu jana, leo
na kesho kwa sababu ya misingi hiyo, hivyo wana-CCM waendelee kutembea
kifua mbele.

Nape aliwataka wana CCM nchini kote, kupuuza propaganda za baadhi ya
vyama vya siasa za kujaribu kuonyesha kwamba CCM imechoka kuwatumikia
wananchi.

“Si kweli kwamba CCM imechoka, bado ni imara na ndiyo
maana kila mara tumekuwa tukifanya mageuzi kuhakikisha kinaenda na
wakati, na kutokana na mageuzi tuliyomo sasa nawahakikishieni kwamba
baada ya uchaguzi ndani ya chama mwaka huu, CCM itakuwa chama bora zaidi
kuliko chama chochote cha siasa Tanzania na duniani kote”, alisema na
kuongeza;

“Katika uchaguzi huo, CCM itahakikisha mafisadi na wala rushwa na
wasio na uzalendo kwa nchi hii, hawapenyi  na kujiingiza katika uongozi,
kwa sababu atakayebainika kujaribu kutumia rushwa kujipenyeza ili apate
uongozi wakati si msafi na hana sifa tunazotaka tutamshughulikia kwa
nguvu zote.

Aliwataka wana CCM kuhakikisha fursa ya uchaguzi ndani ya Chama
unaofanyika mwaka huu, kuitumia vizuri ili kukifanya chama kiwe imara
zaidi kwa manufaa ya taifa akinukuu kali ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere kwamba “Bila CCM Makini Nchiye Itayumba’.

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

By Zitto Kabwe

Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:

1.    Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%

2.    Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei

3.    Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).

4.     Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya  elimu ya juu.

Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti
kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2)
Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi
lilikubaliwa  lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la
kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

Kambi Rasmi ya
Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa
kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi
itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya
Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao
(sitting allowances).

Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs.
15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba
Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali
ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?

Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na
kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.


1. Kuendelea kushinikiza
kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa
misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03
trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.

2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.

3. Kuelekeza fedha za kutosha  kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.

4.
Kuongeza wigo wa kutoza  tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo
sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia
kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi
na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa
wanafunzi.

5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE)
mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za
kutumia na kukuza
uchumi.

6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya
kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la
taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato
zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini,
mafuta na gesi.

7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.

8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.

9.
Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa
elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa
Elimu(Regulatory authority)

10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya
kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za
kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.

Kambi
ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa
deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi
maalum kuhusu
akaunti ya Deni la Taifa.

Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia
kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye 
magari na posho mbalimbali na Kwamba  fedha nyingi zitumike kwa miradi 
mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta
fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano

Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.