Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya TBS na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi Bahari Kuu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

TZTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.

Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu ambaye amemaliza muda wake.

Prof. Maboko ni Mhadhiri wa Jiolojia  katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza tarehe 21 Juni, 2016.

Utaratibu wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

23 Juni, 2016

JANNY SIKAZWE WA ZAMBIA KUAMUA MCHEZO WA YOUNG AFRICANS NA TP MAZEMBE

imagesMchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.

Sikazwe atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda. Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio Jose Mugadza.

Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limekataa ombi la Young Africans ya Dar es Salaam juu ya kubadili siku na muda wa mchezo dhidi ya T.P. Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa ya CAF iliyofika TFF imesema mchezo huo utafanyika Jumanne Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kama ulivyopangwa awali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Young Africans kwa upande wao waliomba mchezo huo ufanyike Juni 29, 2016 saa 1.30 usiku.

Kadhalika, kikao cha maandalizi katika mchezo huo kiliochofanyika leo Juni 23, 2016 kimeagiza uongozi wa Young Africans kuwaelimisha mashabiki wao kukaa katika eneo la mazoea tofauti na mipango yao ya kutaka kukaa eneo lote la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

SHELISHELI KUTUA USIKU HUU

IMATimu ya soka ya Vijana ya Shelisheli, inatarajiwa kuingia Dar es Salaam, Tanzania kesho saa 7.45 usiku (usiku wa kuamkia Ijumaa Juni 24, 2016), kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hiyo inaingia wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na itafikia hoteli ya Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.

Serengeti Boys ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2, 2016 huko Shelisheli.

Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WANASAYANSI

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.

S1Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.


  Baadhi ya Wasomi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)
uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.

 Sehemu ya walohudhuria wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam.

S2Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba mara baada ya kufungua  mkutano wa nne wa mwaka wa wanasayansi kutoka ndani na nje ya nchi ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa LAPF jijini Dar es salaam .

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Alex Msama: Amwangukia Mwakyembe, asema “Nakuomba radhi”

1aBw . Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari wakati alipomuomba Radhi Mh. Dk. Harisson Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba kutokana na Gazeti la Dira analomiliki kumuandika vibaya.

………………………………………………………………………………………………………..

 

Na Mwandishi Wetu

MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.

Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.

“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.

Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni  27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni  Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo  iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

BENKI YA BARCLAYS YAFUNGUA TAWI JIPYA LA CITY MALL JIJINI DAR ES SALAAM

1Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.

2Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross pamoja na viongozi wengine wakifurahia mara baada ya  kukata utepe kuashiria uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.

3Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.

5Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  na  Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross  wakifurahia jambo kwenye kaunta ya kuchukua na kuweka fedha mara baada ya uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo

6Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali vya benki ya Barclays Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo leo.

7Mtendaji Mkuu Benki ya Barclays Afrika na Mtendaji Mkuu wa wateja wa rejareja na bashara wa benki hiyo, Roy Ross akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini pamoja na wateja wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam. 8Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed  nakizungumza wakati wa uzinduzi wa kufunguliwa tawi la benki ya Barclays katika jengo la City Mall jijini Dar es Salaam leo.

10

Viongozi wa Benki hiyo Afrika na Tanzania wakiwa katika meza kuu.

11Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.

TUME YA UCHAGUZI YAKABIDHI TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015

IMG-20160623-WA0021 IMG-20160623-WA0022

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA AIRTEL

J1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano  na Uchukuzi, Edwin Ngonyani (kushoto)na Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Profesa  Faustine Kamuzora (kulia)  baada ya mazungumzo kati ya wizara hiyo na Viongozi wa  kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Sunil Colaso ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji  (wapili kushoto) na Beartice Singano.

(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAMILIKI HISA ZA TTCL KWA ASILIMIA 100

C1Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Afrika Bwana Christian Manuel De Faria (aliye kaa katikati)  na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina ( aliye kaa wa kwanza kushoto) wakiweka saini ya kuiwezesha Serikali kumiliki hisa za TTCL kwa asilimia 100.  Dkt. Injinia Maria Sasabo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (aliyesimama nyuma katikati), Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL (aliyesimama wa tatu kushoto) na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL (aliyesimama wa pili kushoto) wakishuhudia tukio hilo.

C2Msajili wa Hazina Bwana Lawrence Mafuru akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utiaji saini na Bharti Airtel kwa niaba ya Serikali ili iweze kumiliki hisa 100 za TTCL

C3Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel ya kuuza hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha TTCL. Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto) wakifuatilia tukio hilo.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya makabidhiano ya hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za Kampuni ya TTCL kwa asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bharti Airtel.
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MASWALI KWA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

indexWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma juni 23, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

U1Afisa Malalamiko wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. James Katubuka (kulia) akihudumia mteja katika Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo.

U2Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Victor Gideon (kulia) akihudumia mteja katika Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo.

U3 U4Wateja wakihudumiwa katika Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

Picha na mpiga picha wetu

TBA yakusanya Bil. 2.6 kwa kipindi cha miezi mitatu.

K1Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Bw. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akiwaongoza wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya usafi jijini Dar es salaam katika kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.

K2Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) wakishiriki katika kufanya usafi jijini Dar es salaam ili kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.

————————————————————————

Na Ally Daud-Maelezo

Wakala wa Majengo nchini (TBA) wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 43 kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo wapangaji wa nyumba  hizo kushindwa kumalizia madeni wanayodaiwa

Akizungumza hayo katika kilele cha kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha kutoka kwa wateja wao waliowapangisha majengo na bado wanaendelea kukusanya mpaka watakapomaliza.

“Kutokana na mkakati wa kukusanya mapato na kutoa huduma bora kwa wateja wetu tumefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.6 katika kipindi cha miezi mitatu tuliyowapa wateja wetu  kuweza kukamilisha malipo hayo” alisema Bw. Mwakilinga

Mbali na hayo Bw. Mwakilinga amesema kuwa wameamua kutumia siku hiyo kufanya usafi kwenye makazi ya watumishi wa umma na wakazi wengine ili kuweka mazingira bora kwenye miradi yao na jamii nzima kwa ujumla.

“Siku ya leo tumeamua kuitumia kufanya usafi kwenye maeneo ambayo tumeweka miradi yetu kwa watumishi wa umma pamoja na mazingira mengine ili kuepuka na magonjwa yasababishwayo na uchafu” alisisitiza Bw. Mwakilinga.

Aidha Bw. Mwakilinga amesema wanampango wa kupanua wigo wa huduma yao kwa kuwapangisha watumishi  wa umma ambao wanastaafu waendelee kukaa kwenye nyumba hizo ili wasipate shida mara baada ya kustaafu.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo amesisistiza kuwa  wataendelea na utaratibu wao wa kukusanya kodi  na kuchukua nyumba zao kwa  wale ambao wamekaidi amri yao ya kutolipia kodi nyumba hizo ili wapewe wengine ambao wana huitaji .

Wiki ya utumishi wa Umma imeadhimshwa  kwa kila taasisi ya kiserikali kusikiliza na kutatua kero zinazowapata wateja wanaoutumia huduma za taasisi husika ili kuipeleka nchi katika utendaji bora na mafanikio kwa ujumla.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

R7Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akitoa hutuba yake mbele ya viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo

R4Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli akipokea Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) kutoka kwa Jaji Mstaafu wa Tume hiyo Mhe,Damian Lubuva mbele ya Viongozi mbali mbali na mabalozi wa nchi za nje  katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,[Picha na Ikulu.] 23/06/2016.

R5Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,Dkt.John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe,Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakionesha Ripoti ya Tume hiyo Juu baada ya kukabidhiwa rasmi leo katika ukumbi wa mikutano Ikulu ya Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.] 23/06/2016.

R6  Baadhi ya Mawaziri na Viongozi wengine wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Mkuungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli alipokuwa akitoa hutuba yake mbele ya viongozi hao na waalikwa wakiwepo mabalozi wa nchi za nje baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leoR8Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi (kushoto) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Nne Mhe,Jakaya Mrisho Kikwete(katikati)na Waziri Mkuu mstaafu Mhe,Ahmed Salum(kulia) wakiwa katika hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,

R9Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(NEC) katika ukumbi wa Mikutano Ikulu ya Dar es Salaam leo,

Continue reading →

MIAKA 10 YA UMOJA SWITCH WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi  Akizungumza na Vyombo vya Habari leo wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya UMOJASWITCH.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja Switch Bw Danford Mbilinyi Amezindua Amezindua Rasmi Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch..Katika Hotuba yake aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari Amesema Miaka  10 iliyopita Benki ndogo zilikuwana Changamoto Kubwa ya kuweza Kupatia Huduma za ATM wateja wao kwani Mitaji na Gharama za uwekezaji,Uendeshaji wa ATM na Wigo wao wa utoaji wa Huduma hii Uliwapa Changamoto kubwa.Kutokana na ChangamotoHizo  Mabenki Sita Yaliamua Kuanzisha Umoja wao ili Yaweze Kuweka ATM na Kuwezesha Benkihizo Kushirikiana katika Utoaji wa Huduma a ATMKWA Wateja wao,Umoja huo Ndio uliozaa UMOJASWITCH.
Akielezea Zaidi Bw Danford Mbilinyi Amesema kwa Sasa Umoja Switch Ina Jumla ya Mabenki 27 Yanayoshirikana katika Utoaji wa Huduma za Kibenki Kupitia ATMzaidi ya 250 Nchi nzima.Kupitia  Umojaswitch Mteja wa Benki Yenye Tawi Moja Inamwezesha Mteja wake Kupata Huduma Sehemu Yoyote Tanzania.
Mafanikio ya Umojaswitch ni Mafanikio ya Ushirikiano na Mabenki Pamoja na Mzingira Wezeshi yaliowekwa  na Serikali Kuptia Benki Kuu.Wakti Umoja Huo Ulioanzishwa na Kuanza kutoa Huduma zake Jumla ya Benki sita tu ndio walikuwa wanachama wa Umoja Swich Pamoja na ATM 27 tu.Tofauti na Ssas umoja huo una Wanachama 27 unaotoa Huduma kwa zaidi ya wateja Milionoi 2 kupitia Zaidi ya ATM 250.Mafanikio ya Umoja Huo yanachangiwa na Ubunifu na Huduma zitolewazo na Umojaswitch kama Kuhamisha Fedha Kutoka Benki moja kwenda Nyingine zilizopo ndani ya Umoja  huo Kupitia ATM Pamoja na Huduma za Kununua Luku Mpesa pamoja na Kulipia Huduma Mbalimbali Kupitia Hudama za Mobile Banking na zile za Uwakala.
Katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Umojaswitch ni Kutoa Elimu kwa Wananchi  Kuhusu Umuhimu wa Mtandao huu na Technolojia kwa Ujumla Katika Kukuza na Kuendeleza Sekta ya Kibenki na Mchango wake katika maendeleoa ya Maisha ya Kila siku, Pia katika Maadhimisho haya  Wanategemea Kufanya  Shuguli Mbalimbali ikiwemo kuchagiza Matumizi  ya Technolojia na Ubunifu Kwenye Vyuo vikuu hapa Nchini kwajili ya kuwa Kichocheo muhimu Katika Maendeleo ya Sekta ya Kibenki

ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WAMKUBALI RAIS MAGUFULI, AWAPIKU JK NA LOWASSA; UTAFITI WA CZI WABAINISHA

Mwanasheria msomi, kutoka taasisi huru inayojishughulisha na ushauri wa mambo ya habari, (CZI), David Saile Manoti, (katikati), akiwa na wasomi wenzake, Bi Dotto Nyirenda, (kushoto) na Juma George Chikawe, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Wanazuoni hao ambao ni wanachama wa CCM, wamesema utafitiunaonyesha Watanzania wengi wanaimani kubwa na Rais Magufuli katika mageuzi yake ya uchumi na nidhamu.

David Saile Mnoti, Mwanasheria, czi
 Dotto Nyirenda, Mwanadiplomasia, czi
 Juma George Chikawe, Mtaalamu wa Teknohama CZI
Continue reading →

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAKABIDHIWA MAGARI TISA

w1Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

w2Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatuma Mrisho akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kulia kwake ni Dkt. Michelle Roland Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention – CDC).

w3Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention – CDC) Dkt. Michelle Roland akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.

w4Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa pamoja na mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Claud Kumalija wakionyesha ufunguo wa gari mbele ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuashiria kupokea magari tisa yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.

w5Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasha gari kama ishara ya kupokea magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

Continue reading →

Watumishi wa Umma waaswa kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao

IMGS1319 Frank Mvungi – MAELEZO – Dodoma

—————————–
Watumishi wa Umma waaswa kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao hasa wanapowahudumia wananchi ili kuongeza tija.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Akifafanua Mhe. Majaliwa amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa watumishi wote wa Umma wanazingatia uadilifu, uchapakazi, sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia Utumishi wa Umma.
“Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaotumia madaraka yao vibaya bila kujali vyeo vyao” alisisitiza Mhe. Majaiwa.
Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali hivi karibuni itawasilisha Bungeni muswaada wa Sheria utakaosaidia kuanzishwa Kwa Divisheni ya kushughulikia Mafisadi katika Mahakama Kuu.
Lengo la Serikali ni Kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa vizuri pale wanapohitaji huduma mbalimbali ndio sababu tunaendelea kuimarisha vyombo vyetu kama Taasissi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili zitekeleze majukumu yake vizuri.
Katika kuimarisha maadili Mhe. Majaliwa amesema kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuanza kujumuisha masomo ya maadili katika mitaala ya Elimu hapa nchini ili kuongeza kasi ya kukuza na kujenga maadili miongoni mwa jamii.

Watanzania Kumiliki hisa Katika Kampuni za Mawasiliano Hapa Nchini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano Bungeni mjini Dodoma jana. (Picha na Robert Okanda).Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  —————————-
Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Kieletroniki ili kuwezesha watanzania kumiliki hisa zitakazouzwa na Kampuni za Mawasiliano kupitia soko la hisa.
Hayo yamesemwa leo Bungeni  Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bungeni  muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.
“Mhe. Naibu Spika, sehemu ya nne inapendekeza marekebisho katika sheria ya Posta na   Mawasiliano ya Kielektroniki, sura 306 kama ifuatavyo, kufuta kifungu cha 6(2d) na kukiandika upya ili kuweka sharti kwa kampuni za mawasiliano kuwasilisha Katiba ya Kampuni itakayothibitisha muundo wa umiliki wa hisa kama mojawapo ya taarifa zinazopaswa kuwasilishwa wakati wakuomba leseni,” alifafanua Mhe. Mpango.
Aidha Mhe. Mpango aliendelea kwa kusema kwamba, watoa huduma za Mawasiliano ya Kielektroniki watawekewa sharti la kuuza hisa zao kwa Umma na kusajili hisa zao katika soko la hisa Nchini Tanzania ili kutoa fursa kwa watanzaniai kununua hisa na kumiliki asilimia 25 ya Kampuni hizo.
Kutokana na marekebisho ya sheria hiyo, kampuni za huduma za Mawasiliano ya kielektroniki ambazo tayari zimesajiliwa hapa Nchini zitawajibika kujioredhesha katika soko la hisa na kuuza hisa zao ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 01, 2016.
Vile vile kampuni ambazo zitasajiliwa baada ya Julai 01, 2016 zitawajibika kuuza hisa zao na kujioredheshsha katika soko la hisa ndani ya kipindi cha Miaka miwili kuanzia Julai 01, 2016.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti  Mhe. Hawa Ghasia amesema kwamba kamati imekubaliana na marekebisho hayo aidha kamati inaishauri Serikali  kuweka tafsiri ya watanzania ili kuwezesha hisa hizo kuuzwa kwa watanzania  pekee na pia kuangalia suala la miezi sita kwa makampuni yaliyosajiliwa lisilete utata kwenye utekelezaji wake.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AKUTANA NA BODI YA MRADI WA MENEJIMEN TI YA MAAFA DAR ES SALAAM.

T1Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Bodi ya Mradi ya Menejimenti ya Maafa kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 23, 2016.

T2Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi huo Juni 23, 2016.

T3Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya akizungumza jambo katika kikao cha Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam, tarehe 23 Juni, 2016.

T4Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (mwenye suti) akimsikiliza Mtaalam wa Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Kimataifa Bw. Godfrey Mulisa wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi huo kilichofanyika  katika Ukumbi Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam, Juni 23, 2016.

T5Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akisalimiana na Mchambuzi wa masuala ya mipango wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Kimataifa Bw. Mads Hove wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa mradi wa Menejimenti wa  Maafa.

T6Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Menejimenti ya Maafa mara baada ya kumaliza kikao chao kilichofanyika Ofisini hapo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QURAAN TUKUFU KUFANYIKA DIAMOND JUBILEE JUMAPILI HII

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan Tukufu, Sheikh Othman Ally Kaporo (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam Juni 23, 2016. Mashindano hayo yatafanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Sheikh Mohammed Ally Hassan(kulia) na Sheikh AllySendo
Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID MASHINDANO

ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Quraan, yanatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 26, 2016 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO leo Juni 23, 2016, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo, Sheikh Othman Ally Kaporo, amesema, mashindano hayo ambayo ni sehemu ya kutekeleza ibadaya funga
ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, yatashirikisha wanazuoni kutoka mataifambalimbali Duniani.

Kwa wale watakaojaaliwa, wanaweza kufika kwenye msikiti wa Mtoro ulioko
Kariakoo, na kujionea jinsi vijana wadodo wanavyosoma Quraan, kila siku usiku, na Jumapili ndio mashindano yenyewe haswaa.’Alisema.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, washindani watatu waliwaonyesha waandishi umahiri wao wa kuhifadhi Quraan, miongoni mwao ni wanafunzi wawili wenye umri wa miaka kati ya 8 na 10, Abuzar Kholidi kutoka Tajikistan, na Ahmed Abdallah
kutoka Bangladesh. Kijana mwingine aliyeonyesha ufundiwa kuhifadhi Quraan Tukufu ni Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia.
 
 Ahmed Abdallah kutoka Bangladesh
 Gadzhimurad Magomedov, kutoka Russia

Continue reading →

watumishi wizara ya mambo ya ndani watakiwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi

N1Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bi. Lilian Mapfa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo juu ya masuala mbalimbali ya kiutendaji na uboreshaji mazingira ya kazi kwa watumishi  hao katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwa ni sehemu ya  Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma.

N2Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Berious Nyasebwa  akieleza changamoto kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria  kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo wizarani hapo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kilele chake ni leo.

N3Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Bw. Shomari  akieleza changamoto kadhaa zinazoikabili Idara ya Huduma za Sheria  kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali (Hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo wizarani hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kilele chake ni leo.

N4Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na  watumishi mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano wao uliofanyika wizarani hapo katika kuadhimisha kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma.

———————————————————————

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bi. Lilian Mapfa amewataka watumishi wote wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma ili kuleta ufanisi wa kiutendaji katika kuhudumia wananchi. 

Mkurugenzi Mapfa ameyasema hayo leo wakati akipokea changamoto mbalimbali za kiutumishi kutoka kwa watumishi wa ngazi tofauti wanaofanya kazi katika wizara hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kilele chake ni leo.

Bi. Mapfa amesema kuwa ni muhimu watumishi wakafanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa ndio nguzo kubwa inayoleta ufanisi wa kiutendaji mahali pa kazi na hivyo kufanikisha majukumu ya  wizara.

Katika kikao hicho ambacho ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo vya wizara hiyo pia walishiriki na kupokea kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wao.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na malipo ya fedha za likizo, malipo ya kazi kwa muda wa ziada pamoja na vitendea kazi.

Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na watumishi hao Bibi. Mapfa amesema kuwa ofisi yake imepokea changamoto na kero mbalimbali zilizotolewa na hivyo zitafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya Utumishi wa Umma. 

Aidha Bibi Mafpa amewataka watumishi wote kuimarisha upendo na amani miongoni mwao kwani ndio nguzo pekee inayochangia kuleta maendeleo ya kweli ya wizara na ya mtumishi mmoja mmoja. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Wabunge kushiriki harambee ya Media Car Wash

02Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso

0`3Msanii wa Bongo Fleva Inspekta Harun akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam kuhusu harambee ya kuosha magari itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni mjini Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari Bw. Peter Nyanje. Kushoto ni Mratibu wa Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso.

01Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Wajumbe wa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Picha na: Frank Shija, Maelezo

————————————————————————–

Na: Frank Shija, MAELEZO

Zaidi ya waandishi wa Habari 1000 kutoka vyombo mbalimbali kunufaika na Mfuko wa Bima ya Afya kupitia msaada kutoka kwa Kamati ya Okoa Maisha ya Waandishi wa habari.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mjumbe  wa kamati hiyo Peter Nyanje wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambe ya maalum ya kuosha magari Media Car Wash for health itakayofanyika tarehe 25 Juni mjini Dodoma.

“Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya fedha takribani shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi zaidi ya 1000 hapa nchini.”Alisema Nyanje.

Nyanje amesema kuwa harambe hiyo itakuwa ni yapili ikitanguliwa na ile iliyofanyika katika viwanja vya Leaders jijni Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidai kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa taabani.

Aliongeza kuwa  na harambee hiyo imekusudia kuhakikisha waandishi wengi zaidi wanakatiwa Bima ya Afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi.

Kwa upande wake Mratibu wa Media Car Wash Grace Nacksso ametoa rai kwa Wabunge, viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika katika viwanja vya Jamhuri ili kushiriki katika zoezi hilo ambapo watu wataoshewa magari yao na watu maarufu wakiwemo wasanii wa Bongo fleva ,Bongo Movie na Miss Tanzania Lilian Kamazima.

Grace amesema kuwa wao kama waratibu wa harambee hiyo wamejidhatiti kuhakikisha harambee hiyo inafanyikiwa ili kutimiza azma ya kusaidiana miongoni mwa wanataaluma ya habari nchini.

Harambe ya Media Car Wash itakayofanyika mjini Dodoma inatahudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wasanii Joh Makini, Inspekta Haroun, Nikki Wa Pili, G. Nako, Aunt Ezekiel,Kajala Masanja, Ray Kigosi, Jacob Steven (JB) pamoja na Miss Tanzania Lilian Kamazima

TOVUTI YA WANANCHI INAVYOTATUA KERO ZA WANANCHI

indexNa. Immaculate Makilika -MAELEZO

Ni ukweli usiopingika kwamba dunia imeingia katika maendeleo ya teknolojia yanayopelekea matumizi ya vifaa vya kisasa na vyenye utaalamu wa hali ya juu katika kufanya shughuli mbalimbali, ambazo hapo awali zilifanywa kwa kutumia nguvu kubwa na idadi kubwa ya watu na kwa muda mrefu.

Maendeleo hayo ya teknolojia yamejidhihirisha katika nyanja nyingi mojawapo ni hii ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano umerahisisha mawasiliano na unatoa fursa kwa jamii kwa ujumla kuwa huru zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

Serikali inatoa fursa kwa wananchi kutoa hoja na kero zao popote pale walipo kwa kuanzisha tovuti katika wizara, taasisi na ofisi zake ambazo zinawezesha wananchi kupata tarifa muhimu na kwa urahisi kuhusu wizara, ofisi ama taasisi husika na serikali kwa ujumla.

Katika kuzingatia maendeleo hayo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, mwaka 2006 Rais wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, aliitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati huo chini ya Idara ya Habari  -MAELEZO kuanzisha, kuratibu na kusimamia Tovuti ya Wananchi.

Dhamira kubwa ya kuanzishwa kwa tovuti hii ni kutokana na matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara ya 18 toleo la mwaka 2005, maagizo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya mwaka 2003; na dhana ya Serikali inayozingatia Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 19 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Aidha, tovuti hii inatoa fursa kwa wananchi kuwasiliana moja kwa moja na Serikali yao, kuwawezesha watanzania popote walipo duniani kuweza kuwasilisha hoja zao, maoni na malalamiko serikalini kwa kutumia mtandao wa intaneti .

Continue reading →

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUSIKILI KERO NA MAONI TOKA KWA WATUMISHIWA OFISI HIYO

mao1Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Eva Mbigi akimkaribisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (katikati)  ili kuongea na Watumishi wa Ofisi hiyo. aliyekaa kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

mao2Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil akiongea na kutolea ufafanuzi kero mbalimbali toka kwa  Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.  

mao3Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mbarak Abdulwakil alipokua akitoa ufanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyakazi wa Ofisi .

HARAMBEE YA OKOA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIKA JUMAMOSI JUNI 25 MKOANI DODOMA

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR.
Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.
Mkutano ukiendelea kuhusiana na harambe hiyo.
 
======  ======  ======  ======
Kamati ya Maandalizi ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. 
 
Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge. Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-, zilichangishwa.
 
Fedha hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili. 
 
Pia tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja kushiriki zoezi hilo. 
 
Wasanii hao ni kundi la Weusi ambalo linajumuisha John Simon Makini a.k.a Joh Makini, Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili na George Sixtus Mdemu a.k.a G Nako, wenye asili ya Arusha na wanafanya shughuli zao za kimuziki Jijini Dar es Salaam pamoja na Haruna Kahena a.k.a Inspekta Haruni. Wasanii wa Bongo Movies ni pamoja na Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Ray Kigosi na Jacob Stephen a.k.a JB. Na pia kutoka Orijino Komedi tumepewa mwakilishi Isaya Mwakilasa ambaye zaidi anajulikana kwa jina la Wakuvanga na maarufu zaidi kama Mama Bele. Asanteni kwa Kunisikiliza Judicate Shoo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee

Jeshi la Polisi nchini kuzinduzi mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao

indexJeshi la Polisi nchini, linatarajia kufanya  uzinduzi wa mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao, ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu nchini. Mpango huu utaanza kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kuanzia mwezi wa Julai mwaka huu na baadaye kuufikisha katika mikoa yote nchini mwanzoni mwa mwaka 2017.

Uzinduzi huo utafanyika  siku ya Jumamosi, tarehe 25 Juni, 2016 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam, kuanzia saa tatu asubuhi, ambapo Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dr John Joseph Pombe Magufuli. Sambamba na uzinduzi huo wa mpango, Mhe. Rais ataanza kuzindua kituo cha Mawasiliano ya simu za dharura za Polisi 111, na 112 (Police Call Centre) na kituo cha Polisi cha kuhamishika kilichopo maeneo ya Coco beach mkabala na jengo la Coco Plaza, ambacho ni miongoni mwa vituo 13 vitakavyowekwa kwenye maeneo tete kiuhalifu yaliyoainishwa katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni.

Lengo la Mpango huu ni kuimarisha usalama wa wananchi katika jamii na mali zao. Huu ni ubunifu wa Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ambapo Jeshi la Polisi limeamua kuondokana na utendaji wa kimazoea  kwa kuanzisha mikakati mikuu minne ambayo ni  kuongeza ufanisi katika shughuli za kipolisi, kuongeza ubora katika utoaji wa huduma za kipolisi, kuimarisha mawasiliano na ushiriki wa wadau pamoja na kubuni  vyanzo mbalimbali katika kutafuta rasilimali fedha.

Kupitia mikakati hiyo, Jeshi la Polisi litaanzisha mpangilio mpya wa ulinzi na doria katika  maeneo yaliyokithiri kwa uhalifu, litaboresha Vituo vya Polisi kuwa katika muonekano bora na wa aina moja nchi nzima, litaimarisha ubia na sekta binafsi za ulinzi, litaongeza uharaka wa kufika kwenye matukio ya uhalifu yanayoripotiwa, litaimarisha na kudumisha misingi ya maadili, litaweka mifumo thabiti ya kusimamia rasilimali watu, litaimarisha mawasiliano ya ndani na nje ya Jeshi, na mwisho litatafuta vyanzo mbadala vya fedha zinazohitajika ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake. Vyanzo mbadala vitaongeza wigo wa kutafuta rasilimali fedha kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Serikali ambayo Jeshi la Polisi limekuwa likipata kila mwaka.

Aidha, uzinduzi huo utasindikizwa na Wasanii mbalimbali wa Muziki wakiwemo, Bendi ya Polisi, ya Moto Band, Manfongo, Ndolela, Man Prince pamoja na wasanii wengine na burudani mbalimbali zitakuwepo.

Wananchi  wote  kwa ujumla wanakaribishwa ili kupata maelezo ya kina na uelewa juu ya mkakati huu mpya wa kimageuzi ulioandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau-PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Asanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na:

Advera J. Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)

Msemaji wa Jeshi la Polisi,

Watumishi wa Umma watahadharishwa kutosambaza Nyaraka za Serikali katika mitandao ya kijamii

wt1Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Eliakim Maswi akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

wt2Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dkt. Joel Bendera akizungumza na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Manyara katika kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

wt3Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa Watumishi wa Umma wa mkoa wa Manyara kuhusu hoja mbalimbali alizozipokea wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

wt4Afisa Muuguzi Msaidizi, Mkoa wa Manyara,Bi. Josephine Mosha akiwasilisha maoni kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki wakati wa kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

wt5Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb), akikabidhiwa ripoti kuhusu kero na maoni kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Mkoa (CWT)-Manyara Bw. Qambos Michael Sulle ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016.

…………………………………………………………………………………………………..

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewataka Watumishi wa Umma kuacha tabia ya kusambaza Nyaraka za Siri za Serikali katika Mitandao ya Kijamii.

Waziri Kairuki aliyasema hayo katika kikao kazi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mkoani Manyara.

Waziri Kairuki alisema serikali inao utaratibu wake wa kusambaza nyaraka kwa waajiri, na taarifa kumfikia kila mhusika na sio kupitia mitandao ya kijamii.

“Nawakumbusha kuhusu Kanuni za maadili katika Utumishi wa Umma ambazo  kila mtumishi anapaswa kuzingatia na kuelewa na endapo kama huelewi uliza ueleweshwe” Waziri Kairuki alisema na kuongeza Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma lazima zifuatwe.

Aliongeza, hatua zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kusambaza nyaraka kinyume na taratibu, kupitia namba zao za simu.

Waziri Kairuki, pamoja na mengine alisisitiza waajiri kuwashirikisha Watumishi katika bajeti kupitia baraza la wafanyakazi ili wajue mambo ya msingi watakayotekeleza na kuweza kuhoji pale itakapolazimu kufanya hivyo na kwa Waajiri ambao hawajaunda mabaraza ya wafanyakazi wameelekezwa kuunda mabaraza hayo.

Pia, Waziri Kairuki alikumbusha kuwa uhamisho usifanyike kiholela, bali kwa sababu za msingi na pale kibali cha ajira kinapotolewa utekelezaji ufanyike mapema ili huduma ziendelee kutolewa.

Aidha, watumishi wanaoteuliwa katika nafasi za madaraka wathibitishwe katika kipindi cha miezi sita.

Pamoja na kupata fursa ya kuongea, na kushauri, Watumishi wa Umma waliandika kero na maoni ambayo yalichukuliwa ili kufanyiwa kazi.

Kikao hicho kilikua na lengo la kupokea maoni na kero za watumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2016 na kilihudhuriwa na watumishi wote wa mkoa wa Manyara, kupitia uwakilishi.

Wiki ya Utumishi wa Umma ni moja ya tukio muhimu katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU), ambayo huadhimishwa kutambua mchango wa watumishi wa Umma barani Afrika katika kuleta maendeleo, ikiwamo kutatua changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu. Wiki hii huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa wakati mmoja.

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAMU 7 WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOMALIZA MUDA WA KUTOA HUDUMA NCHINI

utm1Mtaalamu wa kujitolea kutoka nchini Japan, Bi.Yuka ITO, akielezea namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

utm2Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Kosuke MATSUDA aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

utm3Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba ( wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine ni watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na  wawakilishi kutoka JICA.

utm4Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Bw.Mick Kiliba (kulia) akifuatilia maelezo ya Bi. Yuka ITO ya namna alivyofanya kazi katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika  ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

utm5Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Yuka ITO aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi mapema leo.

SHIRIKA LA I,H,H INSANI YARDIM VAKFI KWA KUSHIRIANA NA JUMUIYA YA MUZDALIFA ZANZIBAR YATOA MSAADA WA FEDHA KWA MAYATIMA ZANZIBAR

va1Wafanya kazi wa Jumuia ya Muzdalifat wakitayarisha malipo ya Msaada kwa ajili ya Watoto Mayatima wanaosaidiwa na Shirika la Misaada la I,H,H,INSANI YARDIM VAFKI kutoka Uturuki, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile selasi mjini Unguja.

va2Baadhi ya Watoto mayatima wanaopatiwa Fedha za Msaada na I,H,H,INSANI YARDIM VAFKI kutoka Uturuki,wakishirikiana na Jumuiya ya Muzdalifat wakiongozana na walezi wao kuchukua fedha zao.Zaidi ya watoto 800,wamepatiwa fedha hizo katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi mjini Unguja.

va3Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk akizungumza machache katika hafla ya kuwa kabidhi Fedha  Watoto Mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,katika ukumbi wa  Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja.

va4Mfanyakazi wa Jumuiya ya Muzdalifat akiwakabidhi Watoto mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,Fedha taslim za msaada katika ukumbi wa  Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

MBUNGE WA JIMBON LA KIKWAJUNI MHANDISI HAMAD MASAUNIN AKABIDHI JEZI ZA MASHINDANO

SAUN1Muonekane wa nyuma wa moja ya jezi zitakazotumiwa katika mashindano ya kombe la Masauni/Jazeera ,  kutoka maeneo mbalimbali katika Jimbo la Kikwajuni kama inavyoonekana.

SAUN2Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi nahodha wa timu ya Mkunazini, Ahmed Omari Haji ,  jezi zitakazotumiwa na timu yake wakati wa Kombe la Masauni -Jazeera, linaloanza kutimua vumbi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Zanzibar. Wapili kulia ni Diwani wa kata ya Miembeni, Mbaruku Abdallah Hanga.

SAUN3Nahodha wa timu ya Kikwajuni Bondeni, Salum Said (kushoto),  akipokea jezi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).

SAUN4Nahodha wa timu ya Kikwajuni Bondeni, Salum Said (kushoto),  akipokea jezi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).

SAUN5Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto), akiwa na baadhi ya viongozi na makocha  wa timu zinazotarajiwa kuanza kumenyana katika mashindano ya Kombe la Masauni-Jazeera, muda mfupi baada ya kukagua Uwanja wa Mnazi Mmoja utakaotumika kwa mashindano hayo.(Picha  na  Mpiga Picha Wetu)